FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM SPORTS HD SASA JUNI 11
Fainali
za kuwania Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama
Azam Sports Federation Cup (ASFC) sasa zitafanyika Juni 11, 2016.
Mchezo huo wa fainali utakaozikutanisha timu za soka ya Young Africans na Azam FC utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Rais
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema leo Mei 9,
2016 kuwa tarehe hiyo ni mwafaka kulingana na kalenda ya shughuli
mbalimbali za soka.
“Ratiba inaonyesha hivyo,” amesema Malinzi alipozungumza ofisini TFF, Dar es Salaam.
Alichambua
ratiba na kalenda hiyo kuwa Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kufikia
kikomo Mei 21, 2016 kabla ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kuitwa kwa
ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya ‘Harambee Stars’
unaotarajiwa kufanyika Mei 29, mwaka huu.
Taifa
Stars itacheza mechi hiyo ikiwa ni maandalizi ya mchezo wake dhidi ya
Misri unaotarajiwa kufanyika Juni 4, 2016 jijini Dar es Salaam kuwania
kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Tayari
TFF imefafanua iwapo Bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa
msimu 2015/16 inayoendelea atashinda pia taji katika fainali za Kombe la
Shirikisho la ASFC, ndiye atayeiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi
ya mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.
Kwa
msingi huo, timu itayopoteza fungwa katika fainali hizo za Kombe la
Shirikisho –ASFC linalodhaminiwa na kituo cha Televisheni cha Azam,
ndiyo itakayowakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho
Barani Afrika katika msimu wa 2016/17
Fainali
za Kombe la Shirikisho zinakuja baada ya mchuano ulioshindanisha timu
64 za Ligi Kuu Tanzania Bara - VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL
(24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).
Post a Comment