Hadithi: Weapons of mass destruction (Mwanzo mpaka mwisho)

UTANGULIZI
Ulimwengu umegubikwa na matatizo mengi mbali ya njaa na ugonjwa wa UKIMWI, lakini matatizo makubwa yanayoufanya uduwae ni yale ya ugaidi. Marekani, baada ya kudaiwa kwamba kikundi cha ugaidi cha Al Qaeda kinachoongozwa na Osama bin Laden ndicho kilichohusika na milipuko ya Balozi zake mjini Dar es Salaam, Tanzani na Nairobi, Kenya Agosti , 1998, Septemba 21, 2001 inapata pigo kubwa zaidi baada ya ndege mbili kutekwa na kulipua Jengo la kituo cha Biashara cha Kimataifa jijini New York na katika Wizara ya Ulinzi (Pentagon), hatimaye ikaamua kumsaka Osama huko Afghanistan alikodaiwa kwamba alikuwa anafichwa na utawala wa Taleban wa Mulla Omar. Pamoja na kipigo hicho, Osama hakuonekana.
Mwaka mmoja baadaye linazuka tatizo jingine kubwa zaidi. Marekani ikadai kwamba Iraq inamiliki silaha za maangamizi ya halaiki, na kwa kutumia mamlaka yake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikataka kwenda kuipiga kivita. Umoja wa Mataifa ukamtuma Brian Walter kwenda kukagua kama kweli kulikuwa na silaha za maangamizi, lakini baada ya uchunguzi wa muda mrefu akarejesha ripoti iliyosema kwamba hakukuwepo na silaha hata moja. Marekani ikasema ni uongo, ikaingia vitani Mei 2003 na kuipiga nchi hiyo, kipigo kikubwa kuliko kile cha mwaka 1991, bado silaha hazikuonekana.
Ingawa Marekani ilianikiwa kumkamata kiongozi wa Iraq, Suleiman al-Mahmoud katika kile kilichoonekana kama kutaka kujisafisha na kshfa hiyo nzito, bado suala la kutoonekana kwa silaha hizo lilikuwa likiwachanganya wengi, hasa ilipoelezwa kwamba huenda hizo zilikuwa ni tetesi tu. Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza, nchi ambazo zilikuwa mstari wa mbele katika vita vya Iraq, walikuwa na wakati mgumu sana kwa wananchi wao kwa kupoteza gharama nyingi kwenye vita ambayo kisa chake kilikuwa ni cha kufikirika na kulikuwa na wasiwasi mkubwa kwamba wangeweza kushindwa katika chaguzi zao.
Hali hiyo ikawafanya wakuu wa upelelezi kutoka mashirika ya Mataifa ya Magharibi kukutana kwa siri katika kitengo cha ujasusi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuangalia upya hali hiyo na kutafiti kama kweli Iraq haikuwa inamiliki silaha za maangamizi. Je, wanaweza kuupata ukweli wowote? Ni kweli Rais Suleiman al-Mahmoud hakuwa gaidi kama Marekani ilivyodai? Hebu ungana na msimulizi wako katika hadithi hii mpya ya kufikirika lakini ya kusisimua na yenye mvuto wa aina yake....
Ukumbi mzima ulikuwa kimya kabisa. Mihemo ya wajumbe ndiyo iliyosikika tu huku ikionekana kama vile kila mmoja alikuwa akiogopa kuchangia hoja. Kilikuwa ni kikao cha siri mno cha Kitengo cha Ujasusi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambacho leo hii kilikuwa kinaingia katika siku yake ya tatu katika Jengo hili la Usalama jijini New York. Katika siku zote hizo hakuna suluhu yoyote iliyoweza kupatikana katika kufumbua kitendawili kilichokuwa mbele yao.
Nyuso za wajumbe wote ishirini zilionekana zilionekana kuwa na wahaka, fadhaha na tahayuri. Hali hii ilikuwa dhahiri pia hata kwa mwenyekiti wao, ambaye alionyesha wazi kwamba usingizi na mawazo vilikuwa vimeelemea. Ndiyo. Haikuwa kazi rahisi hata kidogo kutanzua jambo hilo gumu, lakini ulikuwa ni wajibu wao kutafuta ufumbuzi. Walikuwa na dhamana kutoka katika nchi zao kuhakikisha kwamba ufumbuzi unapatikana haraka iwezekanavyo kwa sababu hali haikuwa shwari hata kidogo kwa wananchi wengi.
Ulikuwa na kila dalili kwamba Waziri Mkuu wa Uingereza Bwana Dick Johnson angepoteza nafasi yake kufuatia mawaziri watano kujiuzulu kwa kupinga nchi hiyo kuingia vitani, na Rais wa Marekani Caesar Leon alikwishaziona dalili za kuangushwa katika kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliokuwa ukitarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka.
Hata hivyo, kubwa zaidi ambalo liliwaumiza vichwa kubwa wakuu hao wa ujasusi kutoka nchi ishirini za Ulaya Magharibi na Marekani ni hofu ya kutokea Vita Kuu ya Tatu ya Dunia. Nchi ambazo hazikuhudhuria ni Russia, Korea Kusini na Kaskazini, China na Japan. Ndiyo, kulikuwa na kila dalili kwamba nchi nyingi zilikuwa zimechoshwa na propanganda za Marekani za kuzusha mambo ya uongo kwa faida yake. Korea Kaskazini ilikuwa tayari kupigana na Marekani kutokana na madai kwamba nchi hiyo ilikuwa inatengeneza silaha za sumu, Syria nayo ikasema haiwezi kuingiliwa na Marekani katika mambo yake, na nchi nyingi za Kiarabu ziliendelea kupinga ubabe wa Marekani dhidi ya nchi zinazoendelea.
Marekani ilikuwa imesababisha kuvunjika kwa iliyokuwa Urusi ya zamani mwaka 1992, ikaendelea kusaidia kuwaondoa madarakani viongozi ambao kwa mtazamo wake iliwaona kama madikteta. Hata wale washirika wake walikuwa wanalitambua hili, lakini baadhi yao walikaa kimya kwa kuhofia kwamba wangeweza kunyimwa misaada. Ndiyo. Hali hii ingeweza kuendelea zaidi na zaidi mpaka kuwachosha watu wengi, wakiwemo hata wananchi kutoka nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kama wangeamua kuchukua silaha kuwang’oa madarakani viongozi wao hali ingekuwa mbaya zaidi. Hakuna mtu aliyekuwa tayari kuona hali hiyo inatokea katika kipindi hiki cha utandawazi baada ya watu kuchoshwa na vita. Hakuna aliyetaka kupigana kwa bunduki, kwani hata nchi zinazoendelea zilikuwa zinapigania maendeleo, si vinginevyo.
“Jamani, naona kila mmoja amekaa kimya muda mrefu wakati bado hatujapata suluhu na leo ni siku ya tatu. Ndugu zangu, hebu kumbukeni kwamba, kuna hatari ya kuzuka Vita Kuu ya Tatu ya Dunia kama suala hili halikuchunguzwa kwa undani na kupatiwa ufumbuzi. Tuna kila sababu ya kuzama kwa undani zaidi kuangalia kama kweli Iraq ilikuwa inamiliki silaha za maangamizi ya halaiki ama la, naomba mapendekezo yenu tufanye nini maana leo hii lazima tukifie muafaka kama tulivyokubaliana,” Mwenyekiti wa Kitengo cha Ujasusi cha Baraza hilo, Mmarekani Jenerali Frank Dux alisema akiwatazama wajumbe wake mmoja baada ya mwingine. Ukimya uliendelea kwa sekunde kadhaa, lakini baadaye mjumbe mmoja akanyoosha mkono. Bwana Frank Dux akafurahi kuona angalau wajumbe walikuwa wanapata mawazo.
“Ndiyo Inspekta Jenerali Alfonso Gonzalez Cardoso?” Jenerali Dux alisema na kumruhusu mjumbe huyo wa Hispania.
“Asante sana mwenyekiti,” alikohoa kidogo kulegeza koo lake na kuendelea. “Mimi wasiwasi wangu ni kwamba, tunaweza kuingia gharama kubwa bure halafu tukaambulia patupu. Hebu fikiria, Brian Walter aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kitengo hiki cha Ujasusi, ni jasusi mashuhuri sana duniani kutoka Austria. Kama ripoti yake inasema kwamba hakuna silaha za maangamizi, basi inabidi tuamini, kwa nini tuingie kwenye gharama zisizo na msingi? Nafikiri tufikirie kwa undani kabla hatujaamua!”
“Ndiyo. Mimi namuunga mkono mjumbe aliyepita. Jamani, tusifanye vitu kwa hisia na tetesi, utafika wkati tutakuwa tunakimbia vivuli vyetu, na hiyo itakuwa hatari zaidi. Imeelezwa na Tume ya Bwana Brian Walter kwamba hakuna silaha za maangamizi, leo hii sisi tuendelee kushikilia kwamba zipo, hivi hamuoni kwamba tutakuwa tunapoteza fedha nyingi ambazo ni kodi za wananchi wetu? Kama tunazo fedha, kwa nini basi tusisaidie nchi maskini, tunasikia Tanzania hivi sasa wananchi wake wanakula mboga za majani na mizizi kwa sababu ya njaa, kwa nini tusinunue ani za mahindi tukazisafirisha?” Inspekta Jenerali Franco Lamouche wa Ufaransa alisema.
“Jamani, nashukuru wa hoja zilizotolewa na wajumbe wenzangu, lakini kidogo mimi napingana nao. Brian Walter alichunguza kivyake, na ingawa aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kitengo hiki siyo kigezo cha kusema kwamba anafahamu kila kitu. Sisi tutaingia kuchunguza kwa njia zetu za siri, siyo za wazi kama yeye alivyofanya. Kama tukikosa kupata silaha hizo basi jamani tutakuwa tumekula hasara, lakini tutakuwa tumejiwekea mazngira mazuri yasiyo ya hofu ya kuwepo kwa silaha za maangamizi. Mimi nadhani tukubaliane tu hapa, kwamba tutafute vijana tuwatume huko Iraq wakajaribu kufuatilia kwa karibu, hata kama itachukua miaka kumi, lakini mpaka tuupate ukweli. Tufikirie mara mbili, kama hatukupeleleza, halafu baadaye yakazuka maangamizi, ni nani atakayeubeba msalaba huu na sisi ndio tuliopewa dhamana na wananchi wetu kuhakikisha kwamba wanaishi kwa amani? Tukubaline kitu cha msingi kuona kwamba tunaufanya huu kama mpango wa muda mrefu na wakati huo huo wa muda mfupi,” Carl-Heinz Bismarck Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Ujerumani DSB (Dutch Securitats Bund) alisema na kwa mshangao wa wengi ukumbi mzima ukalipuka kwa makofi.
Ni dhahiri kwamba hoja yake ilikuwa ya msingi. Wajumbe waliutumia muda uliosalia kujadili namna ya kuwapata vijana, hasa baada ya kukubaliana kwa kauli moja kwamba lazima wapeleke vijana ili kupeleleza. Swali lililojitokeza na kwamba, vijana gani waliokuwa wanafaa kupelekwa huko.
“Nafurahi kuona angalau tunapata mwanga kidogo,” Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ndiye aliyekuwa Mkurugenzi wa Kitengo hicho cha Ujasusi, Frank Dux, alisema na kuendelea; “Nafikiri sasa ni wakati kwa wajumbe wote kutoa mapendekezo yao ya kijana gani anayefaa kupewa jukumu hilo.”
“Mwenyekiti, nadhani siyo busara kuendelea kupoteza muda wakati majina ya vijana wengi unayo hapo kwenye kompyuta. Kwa nini usiyataje halafu tuyajadili na kutoa mapendekezo?” Benitto Candido, mjumbe wa Italia alisema.
“Hapana, hiyo siyo busara, nafahamu kwamba ninyi ndio wakuu wa usalama kutoka katika nchi zenu. Inawezekana kabisa kuna vijana wengine wapya lakini wenye uwezo mkubwa.”
Wajumbe walipendekeza majina ya vijana zaidi ya hamsini, lakini baada ya mjadala mrefu ikiwa ni pamoja na kuangalia rekodi zao za utendaji, waliona kwamba hakuna ambaye angeweza kufaa kwa kazi hiyo.
“Hawa ndiyo, wameshafanya kazi nyingi kwa ufanisi, lakini hofu yangu ni kwamba, wanaweza kushtukiwa mapema kwa sababu Shirika la Ujasusi la Russia (KGB) lina orodha ndefu ya majasusi duniani, hivyo hatuwezi kuwa na uhakika wa moja kwa moja kama wanaweza wakawa salama. Nadhani tufanye kila liwezekanalo kuangalia vijana chipukizi na wenye uwezo ili tuwatume. Hii itarahisisha utendaji wetu wa kazi kwa sababu hawatashtukiwa mapema,” Frank Fux alisema.
Hoja hii ilikubaliwa lakini kwa kadiri walivyotazama, wajumbe hawakuona kama walikuwa na vijana wengine wenye uwezo. Kwa kitambo kirefu walikaa kimya wakifikiria namna ya kufanya. Baada ya muda Carl-Heinz Bismarck alikohoa na kuwafanya wenzake wainue nyuso zao kumtazama. Mwenyekiti akamruhusu aendelee kama alikuwa na hoja.
“Mwenyekiti ni pendekezo moja, ingawa nadhani kuna ugumu kidogo wa utekelezaji wake,” alisema Bismarck.
“Toa pendekezo tafadhali, tunaweza kujadiliana namna ya kulitatua kama tutaona lina manufaa.”
“Kuna kijana mmoja alikuwa akichukua mafunzo ya ujasusi nchini kwangu, lakini baadaye akatoweka. Nilikuja kusikia baadaye ameibukia nchini kwake Tanzania ambako aliibuka siri kubwa ya wanawake watatu mashuhuri nchini humo waliokuwa wakishirikiana na tajiri mmoja kunyonya damu watoto na kuiuza katika nchi zilizokuwa na mapigano. Kadhia hiyo ya ‘Utatu wa hatari’ ilikwisha baada ya kazi ngumu ya kijana huyo...”
“Bismarck usituambie kwamba unamzungumzia Dennis Geoffrey Mikwambe!” Inspekta Jenerali Alfonso Gonzalez Cardoso wa Hispania alisema kwa furaha na wengine nao wakionyesha mshangao.
“Usiniambie kama unamfahamu kijana huyu?” Bismarck alisema kwa mshangao pia, hakutegemea kama kadhia ile ilifahamika na watu wengi.
“Hakuna mtu aliyepitwa na kadhia ile, mimi kwanza sikujua kama yule kijana alitokea Ujerumani, nilidhani pengine alikuwa ametoka Cuba ama Israel kupata mafunzo yale, kwanza nilishangaa inakuwaje nchi maskini kama Tanzania inakuwa na vijana wenye vipaji kama yule!” Inspekta Jenerali Franco Lamouche wa Ufaransa alisema.
“Huyo ndiye nilikuwa namsema, lakini tatizo lake ni kwamba, hatujui kwa sasa yuko wapi, maana baada ya hukumu ile akatoweka Tanzania na hajulikani aliko. Nilijitahidi sana kuwasiliana nao ili kijana yule amalizie masomo yake lakini wakaniambia kwamba hata wao hawajui aliko...”
“Bwana Bismarck, hapa hakuna mchezo na hatuwezi kujadili zaidi. Yule kijana anafaa zaidi na fanya kila liwezekanalo kuhakikish anapatikana,” Frank Dux aliamuru. Mjadala ukafungwa na wajumbe wakaruhusiwa kuondoka siku hiyo wakiahidi kwamba wangetoa msaada wa kutosha kwa kijana huyo huku kila mmoja akiapa kutunza siri.
**********
Dennis Geoffrey Mikwambe alikuwa amepumzika chumbani kwake katika moja ya vibanda vilivyoko kwenye Mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro Crater. Miezi mitatu ilikuwa imepita tangu alipoimaliza ile kadhia ya ‘Utatu wa hatari’ na aliona autumie muda wake kujipumzisha. Tayari alikwishalipa kisasi kwa wauaji wale waliojificha kwa mwavuli wa serikali na usamaria wema na hakuwa amefikiria jambo lolote la kufanya mpaka wakati huo.
Kwa bahati nzuri alikuwa amefanikiwa kuchukua kiasi kikubwa cha fedha nyumbani kwa Dk. Ritha Katunzi siku alipokwenda kuwakamata ambazo zilikuwa katika mkoba wa George Benson. Angeweza kufanya biashara yoyote ile, lakini aliona wakati wa kuanza kujishughulisha ulikuwa bado, akaamua kutembelea mbuga za wanyama na kuangalia utajiri wa asili wa Tanzania.
Kutokana na wingi wa mawazo, aliamua kugalagala tu kitandani wakati huo wa mchana, hasa kwa vile jua lilikuwa kali sana katika majira hayo ya kiangazi. Wakati akiendelea kufikiria hili na lile mara simu ikalia. Dennis alishtuka na kuikwapua haraka na kuipachika sikioni. Sauti nyororo ya kike ilisikika ikimweleza kwamba kulikuwa na simu yake na kwamba mpigaji hakutaka kujitambulisha kwamba anapiga kutoka wapi. Alishtushwa sana kwa sababu alivyojua hakuwa na ndugu yeyote Tanzania wala hakuwa anafahamiana na mtu yeyote. Lakini akaamua kuisikiliza.
“Hallow! Mheshimiwa Dennis Mikwambe?” sauti nzito ya mwanamume ilisema upande wa pili.
Je, ni nani huyo? Anataka kumweleza nini? Tafadhai fuatilia wiki ijayo upate uhondo wa hadithi hii ya kusisimua. Hakika utajuta endapo utaikosa hata sehemu moja ya simulizi hii....
Tatizo la ugaidi bado gumu kutatuliwa ulimwenguni, lakini tatizo la tishio la nchi ya Iraq kutengeneza na kumiliki silaha za maangamizi ya halaiki linakuwa kubwa zaidi na kuifanya Marekani ikaipige nchi hiyo pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupinga. Uchunguzi unaonyesha kwamba hakuna silaha za sumu wala dalili za kutengenezwa, lakini Marekani inadai kwamba Rais wa Iraq Suleiman al-Mahmoud amezificha. Anampiga na kumng’oa madarakani huku vikosi vingi vya kijeshi vikiwa vimetumwa huko. Kosa hili linamgharimu rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza kwamba wamefanya hivyo kwa ajili ya kujifurahisha na hakukuwa na sababu za msingi kuipiga Iraq kivita. Wakuu wa kitengo cha Ujasusi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanakutana ili kujaribu kuchunguza kama kweli silaha zile hazipo na ilikuwa ni propaganda za Marekani tu au zilihamishwa. Ndipo wanapokubaliana kumtuma jasusi chipukizi Dennis Geoffrey Mikwambe. Je, atakubali kwenda? Ni nani aliyempigia simu wakati akiwa mbugani Ngorongoro Crater? Endelea na simulizi hii...
Kwa sekunde kadhaa Den nis alibaki kimya akitafakari jinsi mzee huyo wa upande wa pili kwenye simu alivyolitamka jina lake bila taabu. Ilionyesha wazi kwamba mtu huyo alikuwa akimfahamu fika. Hata mwenyewe alikuwa akiifananisha sauti hiyo na ya mtu ambaye anamfahamu, japo siyo sana. Alifikiria ni wapi alikoisikia na kumuona mmiliki wa sauti hiyo lakini hakuweza kupata jibu katika kitambo kifupi hivyo. Alifikiria ni nani mbaye angempigia simu wakati huo kwa kuwa hakuwa na ndugu Tanzania wala jamaa.
“Dennis, unanisikia lakini?” sauti hiyo iliuliza tena.
“Yap! Endelea, ni nani mwenzangu?” Dennis alisema akiwa makini kuisikiliza sauti hiyo pamoja na kutafakari kile kilichomsukuma mzee huyo akampigia simu.
“Hujambo bwana? Unazungumza na Uisso Tarimo, hapa ni hekaluni Dar es Salaam. Nadhani umenikumbuka sasa! Mbona siku ile uliondoka bila kuaga? Nilitaka nikupe maagizo yako!”
Maelezo hayo yalimfanya Dennis azizime kwa muda. Kwa mtu wa kawaida asingeweza kuelewa, lakini kwa yeye ambaye alikuwa jasusi alielewa vizuri na alimtambua mtu aliyekuwa akizungumza naye. Mtu aliyekuwa akizungumza naye hakuwa Uisso Tarimo kama alivyojiita, bali alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Inspekta Haroun Mahundo. Dennis alifahamu fika kwamba mzee huyo alimtafuta kwa muda mrefu baada ya kumaliza kuitanzua ile siri ya Utatu wa Hatari, lakini alikuwa na hakika kwamba mzee huyo hakupiga simu ili kumuuliza sababu za kutoroka kwake. Alifahamu fika kwamba kulikuwa na jambo ambalo lilimfanya amtafute, tena mwenyewe bila kumtuma sekretari wake. Namna alivyofahamu mahali alikojificha ilikuwa ni siri yake na Dennis hakutaka kujishughulisha kufahamu, maana alijua kwamba majasusi siku zote wana kila njia ya kunusa nyayo za mtu, inawezekana hata hapo mbugani Ngorongoro kulikuwa na watu wa Usalama wa Taifa ambao waliweza kutoa taarifa hizo kwa mkubwa wao wa kazi.
“Unajua mzee, nilipata dharura, hivyo nikaona kwamba ninahitaji muda kidogo wa kupumzika hasa baada ya pilika pilika nzito.”
“Kweli kabisa, kazi uliyoifanya kila mmoja ameifurahia na ulimwengu mzima sasa unakutambua kama kijana jasiri mwenye uwezo wa hali ya juu kabisa. Kwa kweli Tanzania inajivuna kuwa na kijana kama wewe.”
“Ahsante Chifu! Hata hivyo, sidhani kama umepoteza muda wako wote kutafuta mahali nilipo ili unipe pongezi, najua kuna kitu kingine kilichokusukuma....”
“Kweli kabisa usemayo. Nimekutafuta kwa muda mrefu sana na nilikwishakata tamaa ya kukuona, nimeulizia hata kule shuleni kwako wakasema hawajakuona muda mrefu sana. Wewe kijana unaweza kabisa kuzificha nyayo zako. Hata hivyo, kilichonifanya nikutafute hivi ni kwamba, nimepokea simu kutoka New York tangu Ijumaa ikisema kwamba, mjomba wako amepata ajali mbaya sana ya ndege wakati akiwa njiani kwenda Afrika Kusini kwa kikao cha wafanyabiashara. Ajali yenyewe ilitokea muda mfupi kabla ndege hiyo haijatua kwenye Uwanja wa Jomo Kenyatta, Nairobi. Mjomba wako amenusurika kufa lakini ameumia sana na amelazwa Nairobi, unatakiwa uende haraka sana,” Inspekta Mahundo alisema kwa mara nyingine akitumia lugha ya kijasusi.
Dennis alicheka sana badala ya kusikitika. Alijua kwamba sasa watu walitaka kumtumia. Kauli ya Inspekta Mahundo kwamba mjomba wake alipata ajali ilikuwa ni ya mafumbo tu kwa sababu Dennis hakuwa na ndugu. Alichomaanisha hapo ni kwamba, kuna mgeni ametoka New York, Marekani ambaye amefikia Nairobi na alikuwa na ujumbe muhimu sana uliotakiwa kufanyiwa kazi haraka. Alijifikiria kwa nini waamue kumtafuta yeye ambaye pamoja na uwezo aliokuwa nao, lakini alikuwa bado hana uzoefu wa kutosha.
“Chifu, unajua unanichekesha sana!”
“Kwa nini?”
“Mimi ni mtoto mdogo tu na ndiyo kwanza nimemaliza shule, mbona wapo wengine ambao wanaweza kwenda kumhudumia, iweje waniite mimi?” Dennis alizungumza kwa mafumbo pia.
“Sikiliza Dennis, unajua kwa mtu mzima kama yule kuamua kukuagiza wewe uende wakati yeye ana matatizo ujue ni heshima kubwa mno, na huwezi kujua ni kitu gani ambacho atakwenda kukueleza. Hii ni heshima kubwa sana kwako na kwetu, tafadhali sana kijana wangu nenda. Ningependa nije huko tuzungumze kwa kirefu, lakini muda hauruhusu kabisa kutokana na hali aliyonayo mjomba wako. Hata hivyo, tutakutana Nairobi kwa sababu mimi pia naondoka leo kwa ndege ya Air Tanzania.”
“Una maana kwamba mimi natakiwa kuondoka leo?” alisema Inspekta Muhando.
“Haswa! Tafadhali fikiria heshima uliyopewa.”
Walizungumza kwa kitambo kirefu huku Dennis alionekana kusita kwenda. Angeweza kukataa, lakini nafsi yake ilimsuta hasa kutokana na kiapo alichokula. Alijua kwamba alikuwa na wajibu wa kuitumikia jamii. Hata hivyo, hakuweza kuelewa huyo mtu aliyekuwa anamhitaji aliitwa nani na alikuwa na kadhia gani ambayo iliwashinda wote na kuamua kumjia yeye.
“Sawa nitakwenda! Wito haukataliwi. Sasa nitaondokaje hapa, maana kwenda mpaka Arusha ni mbali sana....”
“Usijali, kuna ndege itakuja huko mbugani wakati wowote kuanzia sasa, wewe jiandae tu kwa safari. Vitu vyako vingine viache hapo tutavichukua na kuvihifadhi,” Inspekta Mahundo alisema kwa furaha baada ya kuona Dennis amekubali.
*********
Hali ya hewa ilikuwa mbaya sana angani kutokana na mawingu mazito ya mvua. Ndege aina ya Twin Alter iliyokuwa na abiria mmoja na rubani wawili ilikuwa ikiyumba na kupoteza mwelekeo. Ilikuwa imeruka umbali mrefu kiasi kutoka Mbuga ya Ngorongoro Crater wakati hali ya hewa ilipobadilika. Mvua ikaanza kunyesha na kuwafanya marubani waanze kuhangaika.
Wakati marubani hao wakihangaika, abiria wao hakuonekana kuwa na hofu yoyote na alikuwa akiwaangalia tu na kisha kutingisha kichwa. Aliwahurumia sana, kwa sababu aliwaona kama wanacheza na walikuwa wamepoteza mwelekeo wao wa kufikiri. Ghafla ndege hiyo ikanza kuyumba na kupoteza mawasiliano kabisa. Taratibu abiria huyo alifungua mkanda wake na kwenda walipo marubani ambao walikuwa wakiendelea kuhangaika kuirudisha ndege kwenye usawa wake.
“Samahani, naweza kuwasaidia?” abiria huyo kijana mwembamba, mrefu na mtanashati ambaye tangu alipoingia ndani ya ndege hakutaka kuzungumza na mtu, alisema na kuwaacha marubani hao watazamane.
“Kama sisi wenyewe tunashindwa, wewe utawezaje?” mmoja wa marubani hao alisema kwa dharau.
“Ni kweli, lakini inawezekana wewe unajua kuongoza ndege tu hujui ufundi, pengine mngenipisha mara moja maana angalieni tunaweza kufa na hewa imekuwa nzito sasa,” abiria huyo aliendelea kusema kwa sauti ya taratibu.
“Yanapotokea matatizo kama haya hatuna budi kutafuta kila namna kuokoa ajali. Maulid, hebu acha ubishi, tumpishe mwenzetu anaweza kutusaidia...” rubani mwingine alimweleza mwenzake.
“...Peter wewe huelewi, yakitokea matatizo makubwa zaidi mimi ndiye nitawajibika...” kabla hajamaliza mara injini moja ikazima. Akamtazama mwenzake ambaye alimuangalia kwa jicho la kumsuta. “...Eee bwana eee, njoo ujaribu na wewe!” rubani huyo alitambulika kwa jina la Maulid alisema na kumpisha yule abiria aketi mahali pake na yeye akasimama pembeni.
Abiria huyo alichokonoa nyaya fulani na baada ya dakika moja hivi injini iliyokuwa imezima ikawaka, akabonyeza vitu fulani huku akirekebisha nyaya, mara ndege hiyo iliyokuwa imekwenda juu zaidi ikaanza kuteremka kwa kasi, lakini wakati huo huo abiria huyo akajitahidi kuzigusa gusa nyaya mbalimbali na mara ndege hiyo ikaanza kwenda kwa mwendo wa kawaida ikachukua usawa wake na kusonga mbele. Hali ya hewa nayo tayari ilikwisharejea katika hali ya kawaida. Abiria huyo akatazama dira na kuigeuza ndege kuelekea kaskazini-mashariki kwani ilikwishaelekea magharibi. Baada ya mwendo mfupi hatimaye mwanga wa jua ukonekana kuonyesha kwamba sehemu hiyo haikuwa na mvua.
“Haya njoo uendelee na safari yako!” abiria huyo alisema na kumpisha rubani Maulid aiongoze ndege hiyo.
“Hongera sana ndugu yangu, tungeweza kufa,” Peter alisema na kuongeza. “Si vibaya kama tutafahamiana, mimi naitwa Peter!”
“Nashukuru kukufahamu, mimi naitwa Dennis Geoffrey Mikwambe!” alisema abiria huyo huku wakipeana mikono. Alikuwa na utaalamu kidogo wa masuala ya anga. Wakati huo Maulid alikuwa akiwasilina na uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kuwaambia kwamba walipoteza mawasiliano kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.
Walikuwa wamechelewa kwa zaidi ya saa moja, lakini baada ya mwendo mfupi hatimye waliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. Dennis alitoka nje akiwa kabeba mkoba wake. Suti nyeusi aliyoivaa ilimkaa vyema na kumfanya aonekane maridadi. Alivaa miwani yake maalumu ambayo ilikuwa kama kamera iliyokuwa inachunguza watu wote kama kulikuwa na mtu mwenye silaha. Ndani ya mkoba wake alikuwa ameficha bastola zake tatu pamoja na kamera zake maalumu ndogo na ingewachukua maofisa miaka kadhaa kugundua kama mkoba huo ulikuwa na silaha.
Alitoka nje ya uwanja na kuangaza huku na kule. Macho yake yakamuona kijana mmoja mweusi aliyekuwa anajishughulisha na kusoma gazeti lakini macho yake yakiwa yanatazama kwa chati kuangalia huku na kule. Dennis alimtambua kijana huyo kama ndiye mtu aliyetumwa, lakini akampita tu kwa mwendo wa kawaida huku akiitengeneza tai yake na kupapasa ukosi wa shati. Akasimama akiwa ameiweka briefcase yake chini na kutoa kalamu kwenye mfuko wa shati kisha akabadilisha mkono na kuiweka kwenye mfuko wa suruali, ile briefcase akibeba kwa mkono mwingine. Yule kijana aliyekuwa pembeni akazielewa ishara hizo, naye akafanya vivyo huku akilidondosha gazeti na kuliokota kwa kutumia mkono mwingine.
Dennis akaelekea mahali zilipoegeshwa teksi na kuchukua mojawapo aliyoiona nzuri. Halafu kwa sauti kubwa, pengine akitaka yule kijana aliyekuwa akija nyuma taratibu asikie, akamwambia dereva. “Nipeleke Hilton Hotel, tafadhali!” akaingia ndani ya gari na kuondoka. Walipotoka kwenye maegesho na kuchukua barabara ya kuelekea mjini aligeuka nyuma na kuiona gari aina Mercedes Benz ikija nyuma yao na baadaye ikawapita kwa kasi. Alimtazama dereva huyo na kumuona akiwa anazungumza kwa kutumia simu yake ya kiganjani.
Dakika ishirini baadaye wakawasili hotelini, Dennis akashuka baada ya kumlipa dereva ujira wake. Tayari ilikwishatimia saa 12.30 jioni. Alipoingia mapokezi hakushangaa kumkuta yule kijana mweusi akiwa kaketi pembeni kwenye makochi akisoma gazeti. Dennis alijua kwamba hiyo ilikuwa ni zuga yake tu, akaenda kwa mhudumu na kuomba apangishiwe chumba.
“Vyumba vimekwisha, kuna Executive Suite moja, kama hutajali nikupatie hiyo hiyo na gharama zetu ni rahisi sana,” alisema msichana huyo mrembo huku akitabasamu na kuyaacha mashavu yake yaache vishimo vidogo pembeni huku mwanya wake ukionekana. Kwa kweli alikuwa mrembo wa haja ambaye angeweza kumpagawisha mwanamume yeyote rijali.
“Ninachotaka mimi ni kufikia Hilton Hotel, haijalishi kama nitalala chumbani au kwenye Suite, nadhani ningeikosa hata hiyo suite usingeweza kukataa kunikaribisha kwako, au siyo,” Dennis naye alisema kwa masihara na kuzidi kumchanganya binti huyo Mkikuyu. “Mimi naitwa Dennis, sijui mwenzangu unaitwa nani?”
“Nani mimi?”
“Ndiyo, kwani nazungumza na nani?”
“Ooh! Naitwa Lucille Mungai!”
“Nashukuru kukufahamu!”
“Nami pia nashukuru kukufahamu. Haya jaza fomu hii kisha lipia,” alisema mhudumu huyo akimuelekeza Dennis mahali pa kujaza. Alipomaliza kulipia na kupewa risiti yake akauliza. “Kwa hiyo ni suite namba 7, siyo?” alisema kwa sauti ili kumfanya yule kijana aliyeketi pale asikie.
“Haswa, na kuna kila kitu, televisheni, magazeti, kompyuta, simu na kadhalika. Ukipenda huduma nyingine utapewa pia, kama hutajali,” alisema na kumkonyeza Dennis.
“Yaah! Kama sitajali, nadhani ninaweza nikapata,” Dennis alijibu na kurudisha tabasamu pana. Ndiyo kwanza msichana huyo akagundua kwamba Dennis pia alikuwa na mwanya, akazidi kuchanganyikiwa. Dennis alijifunza kwamba, kama unataka taarifa zozote za muhimu, hususan katika kazi hiyo, ni lazima kuwapumbaza sana wanawake na wanawaweza kuwa silaha za kuwaangamiza adui au hata mwenyewe.
Wakati akiendelea kuzungumza hapo mkoba wake ulikuwa umechukuliwa na mhudumu mmoja wa kiume na kwenda nao hadi kwenye lift akiwa anamsubiri Dennis, ambaye aliondoka haraka haraka kumfuata.
Saa moja baadaye akiwa amekwishakula baada ya kuoga, aliketi kwenye televisheni akitazama kituo cha Sky TV kilichokuwa kikirusha matangazo ya kampeni za urais wa Marekani na kuonyesha kwamba mpinzani wa Rais Caesar Leon alikuwa katika nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo huku akitumia ripoti za Vita ya Iraq na madai ya kuwepo kwa Silaha za Maangamizi ya Halaiki nchini humo kama kigezo cha kumdondosha rais huyo madarakani. Aliona kama taarifa hizo zinakanganya sana, lakini wakati akitaka kubadilisha stesheni ya televisheni hiyo mara akasikia mlango ukingongwa.
Je, ni nani huyo anayegonga mlango? Ni yule mhudumu Lucille Mungai au yule kijana aliyekuwa akimfuatilia? Vipi kuhusu mzee aliyetoka Marekani? Je, anahusiana vipi na yule kijana? Fuatilia wiki ijayo upate uhondo wa hadithi hii ya kusisimua. Hakika utajuta endapo utaikosa hata sehemu moja ya simulizi hii....
Dennis amepigiwa simu na Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Tanzania aende Nairobi, Kenya, ambako amefika na kupata chumba katika hoteli ya Hilton. Wakati akitazama televisheni mara mtu anagonga mlango. Je, ni nani huyo? Endelea na simulizi hii...
Dennis alielewa kwamba mtu aliyekuwa akigonga lazima atakuwa huyo mtarajiwa ambaye alikuwa akimsubiri na alijua wazi kwamba yule kijana aliyemuona kule alikuwa ametumwa tu kumuatilia ili ajue angefikia wapi. Alifahamu hivyo kwa sababu aliamini kama angekuwa mhudumu lazima angempigia simu, lakini kwa vile mtu huyo hakupenda afahamike na mtu yeyote kwamba anamfuata yeye Dennis, aliamua kutumia mbinu za kijasusi zaidi.
Kwa haraka haraka alichukua bastola yake .45 Automatic na kuikamata vizuri mkononi, kisha akaenda mpaka mlangoni, lakini kabla ya kufungua akasema; “Simba...!” akajibiwa kwa sauti nzito “...Anararua!” Akauliza tena; “Paka...!” mgongaji akaijibu “...anakula nyama na kunywa maziwa!” Baada ya kusikia hivyo akabaini kwamba huyo alikuwa mwenzake maana hizo zilikuwa ni ishara za kutambulishana majasusi wa kimataifa.
Alifungua mlango na kumpisha mgongaji aingie huku yeye akiufunga mlango nyuma yake. Alishangaa kumuona mzee wa makamo mwenye mvi nyingi kichwani kwake, lakini akiwa na mwili uliokakamaa kimazoezi hasa. Alimkaribisha kiti mgeni wake huyo ambaye kwa sekunde kadhaa alikuwa akiyastaajabia mazingira ya kwenye chumba hicho kilichokuwa na kila kitu.
“Kweli bado kijana mdogo, unahitaji kufurahia maisha, na kazi zetu hizi kama hukufurahia maisha unapopata nafasi, basi unaweza usiyaone tena,” alisema mzee huyo huku akimeza funda la whisky aliyowekewa na Dennis kwenye meza ndogo ya kahawa mbele ya kiti chake.
“Mazingira nayo yanalazimisha,” alisema Dennis akimtazama kwa makini mzee huyo. Alifahamu ujio wake ulikuwa ni wa siri mno na alihitaji hali iwe vivyo hivyo. Kisha akamwambia “Umekosea kumtuma yule kijana!”
“Nani, unasema Carl Ochieng?” mzee huyo aliuliza.
“Ndiye huyo!”
“Hofu yako ya bure, yule ni kijana shupavu kweli na anaweza kumfuatilia mtu bila mwenyewe kujua!”
“Yule? Ana uwezo gani? Heeeh, mbona unachekesha, yaani mtu tangu nimeshuka uwanja wa ndege nimemtambua, na mbaya zaidi ni kwamba, nilipomtambua tu nikamfanyia ishara, naye kwa ujinga wake akajibu, ndiyo hapo ninapomuona kwamba ni mtoto mdogo tu. Kwanza nilidhani amekuja kunipokea, lakini baadaye mwenyewe nikaamua kuchukua gari nyingine ya kukodi, nilipofika hapa nikamkuta ameketi kwenye makochi, angekuwa adui ningekuwa nimemmaliza kitambo,” Dennis alisema akiichezea bastola yake.
Mzee huyo alimtazama kwa makini na kumuona kijana huyo aliyejiamini hata kwa kauli zake kuwa ni wa ajabu sana na ilielekea kwamba angeweza kukifanya kile ambacho alikinena. Moyoni mwake akasema kwamba walikuwa na mtu ambaye angeweza kuifanya kazi iliyokuwa mbele yao kwa umakini sana.
“Siamini hayo unayosema kabisa, Ochieng tunamwamini mno na jinsi ambavyo anaweza kuifanya kazi yake kwa ufanisi, sidhani kama anaweza kufanya upuuzi kama huo,” mzee huyo alizidi kumchimba.
“Siyo kwangu, yule ni mwanafunzi tu ambaye haelewi chochote, hawezi kujaa kwenye kiganja changu kabisa.”
“Sasa naamini maneno niliyoambiwa...”
“Uliyoambiwa? Na nani? Kwanza nieleze mwenzangu unaitwa nani, mana hatujafahamiana ati!”
“Ni kweli, mimi naitwa Collin Daniel, kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kitengo cha Ujasusi,” alipiga funda mbili za whisky na kuendelea; “Nadhani kwa hapo tunaweza kuwa tumeelewana kidogo. Hata hivyo, kwa kuwa siku hizi kuta zina masikio, nisingependa kupoteza muda, maana hata ujio wangu ni wa siri mno, sitaki kabisa mtu abaini kama niko kwako.”
“Enhe! Bwana Collin, hebu nieleze hicho kitu kilichokufanya unitafute mimi kutoka huko Marekani mpaka huku, wakati mnao wazee wa kazi wengi tu na wenye uzoefu kuliko mimi!”
Mzee Collin aligundua kwamba alikuwa anaongea na mtu asiye wa kawaida na alitakiwa kuwa makini zaidi katika mazungumzo hayo. Alikohoa na kuanza mazungumzo rasmi.
“Sikiliza Dennis, kwanza tuna kila sababu ya kujisifu kuwa na vijana shupavu kama wewe, wenye mtazamo wa kimapinduzi hasa na ambaye una uwezo wa kutanzua mambo. Kwa kuwa ni mpenda maendeleo ninaamini kwamba unapinga vitendo vya kigaidi kwa nguvu zote,” alimtazama Dennis ambaye alikuwa anamsikiliza kwa makini huku kamkazia macho, kisha akaendele; “Ninaamini kwamba unaelewa nini kinachoendelea kuhusu Iraq...”
“Ndiyo naelewa, kwamba utawala wa Rais Suleiman al-Mahmoud uliangushwa Mei 2003 na kwamba Marekani imefanikiwa kumkamata rais huyo!” Dennis alisema.
“Sawa sawa, lakini kuna jambo lingine zaidi, kwamba Marekani ilikwenda kupigana bila idhini ya Umoja wa Mataifa na nchi nyingi, hasa zinazoendelea zilipinga vita hivyo wakiwemo wananchi wa Marekani na Uingereza, nchi ambazo zilishiriki katika vita hivyo. Hivi sasa, nafikiri kama ulivyoona kwenye televisheni, rais wa sasa wa Marekani Caesar Leon na Waziri Mkuu wa Uingereza Dick Johnson wako katika wakati mgumu kutokana na ukweli kwamba vita hivyo viligharimu fedha nyingi bila msingi wowote. Kibaya zaidi ni kwamba, ripoti ya mchunguzi wa Umoja wa Mataifa Jenerali Frank Dux, ilieleza wazi kwamba, katika uchunguzi wao wa tishio la kuwepo silaha za maangamizi ya halaiki nchini Iraq hawakuweza kuona dalili zozote. Ni kutokana na hali hiyo ya kutokuwepo kwa silaha hizo na hali mbaya ya kisiasa inayoweza kuzikumba nchi hizi ndiyo maana Kitengo cha Ujasusi katika Baraza la Usalama kikaamua kuketi na kutaka kufanya uchunguzi ili kuhakikisha kwamba silaha hizo hazipo kweli ama kulikuwa na hila zilizofanywa kuficha ukweli.
“Sasa katika kikao hicho ikapendekezwa kwamba, dhamana hiyo ya kuishughulikia kadhia hii upewe wewe!”
“Mimi?” Dennis alisema kwa mshtuko.
“Ndiyo! Tumeona kwamba ni vyema jukumu hili ukalibeba wewe kwa sababu tunaamini kwamba unaweza kuifanya kazi hii!”
“Bwana Collin, mimi nadhani mmekosea sana, au inawezekana wewe hukuwaelewa wenzako walipokuagiza. Mimi siye ninayestahili kufanya kazi hii, sistahili kabisa, unaonaje kama ukiwapigia simu wenzako ukawauliza tena ni nani aliyependekezwa?” Dennis alisema huku akimimina kinywaji chake kwenye glasi.
“Sikiliza Dennis, pamoja na umri wangu mkubwa, lakini sijapoteza kumbukumbu hata kidogo... mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye kikao hicho na tukafikia maamuzi ya pamoja na wakuu wa usalama kutoka karibu nchi ishirini na tano duniani. Zaidi ya yote, hata mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Tanzania alipewa taarifa hizi na ndiyo maana aliamua kukutafuta ili uje hapa. Tunaamini kwamba wewe pekee ndiye unayeweza kutanzua siri hii kwa kuchimbua mizizi yote ili kupata ukweli. Fikiria heshima ambayo umepewa na mataifa yote haya,” Collin Daniel alisema kwa masikitiko.
“Ni heshima au maafa? Hivi mnadhani mimi mjinga kiasi hicho? Mimi naelewa kwamba mnataka kunifanya mimi chambo ili nikasafishe njia kwa ajili ya watu wenu, hamn lolote zaidi ya hilo. Labda nisikupotezee muda wako, naomba kawaeleze wenzako wote kwamba, yule waliyempendekeza kuifanya kazi hiyo amesema hawezi, ingawa alikula kiapo, kwa sababu hawezi kufanywa chambo. Naamini mnao watu wengi wenye uzoefu, kwa nini msiwatumie hao halafu mnijie mimi mbye bado kinda kabisa? Siwezi!” Dennis alisema bila kuonyesha masihara.
Collin alijitahidi kumbembeleza na kumshawishi akubali lakini ilikuwa kazi bure kabisa, kwani Dennis alishikilia msimamo wake wa kutokwenda. Hatimaye mzee huyo alinyanyuka na kuondoka bila kuaga akiwa amefadhaika sana moyoni mwake. Uso wake ulisinyaa na kumfanya aonekane kama mzee wa miaka 70 wakati alikuwa na miaka 55 tu! Dennis alimuonea huruma, lakini katu hakutaka kukubali ombi lake.
*********
Walikuwa wameketi kwenye meza ya chakula, Dennis na Jenerali Haroun Mahundo, katika mgahawa mmoja katikati kabisa ya Jiji la Nairobi. Jenerali Mahundo alikuwa amewasili jana yake usiku, na kwa vile hakuelewa Dennis alikuwa amefikia wapi na kuhofia kuvuruga mazungumzo yao na Collin Daniel, aliamua kujipumzisha katika hoteli ya Safari Park.
Kesho yake asubuhi akamtafuta Bwana Collin na kumuuliza nini kilichondelea, lakini alisikitishwa sana baada ya kuambiwa kwamba kijana huyo alikataa katakata kwenda kuifanya kazi hiyo. Alifikiria aibu ambayo alikuwa ameipata na namna Dennis alivyoidhalilisha Tanzania. Hasira zilimkaba na kuamua kumpigia simu akimtaka wakutane wakati wa chakula cha mchana kwenye mgahawa huu kwa ajii ya mazungumzo. Kila mmoja alikuwa na fundo moyoni mwake akimtazama mwenzake wa hisia tofauti. Hasira za Inspekta Mahundo zilijionyesha bayana, lakini Dennis alikuwa amejiandaa kwa kila swali ambalo angeulizwa.
Hawakuzungumza chochote hata walipokuwa wameletewa chakula na kuanza kushindilia. Dennis alikula harakaharaka kwa sababu njaa ilikuwa inamuuma sana. Dakika 30 baadaye tayari walikuwa wamemaliza kula na kuanza kupata vinywaji taratibu. Inspekta Mahundo aliona huo ndio ulikuwa wakati muafaka wa kuanza kumhoji huyo mwanaizaya. Alivuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha taratibu.
“Dennis! Nimesikitishwa sana na kile ulichomtendea Bwana Collin, tena sana. Lakini kwa nini uliamua kufanya vile?”
“Kwa vipi mzee?”
“Usitake tufanye mdahalo usio na maana, unajua kwamba umepewa jukumu kubwa la kimataifa, na hii ilikuwa ni heshima kubwa kwako na kwa Tanzania, lakini wewe ukaamua kukataa, tena bila kutoa sababu zozote za msingi. Hebu nieleze, ni kitu gani hasa ambacho kimekufanya ukakataa kazi hiyo?” aliuliza kwa utulivu.
“Nadhani mzee mwenyewe umeshasema kwamba sikutoa sababu za msingi, kwa hiyo hata kama nitakueleza bado utaelewa kwamba sina sababu za msingi. Labda ninachoweza kusema ni kwamba, siko tayari kwa kazi hiyo, sitaki kutolewa kafara. Mzee, lazima uelewe kwamba mimi bado kijana mdogo tu, Marekani na Uingereza ndiyo mataifa makubwa duniani na yana watendaji wazoefu wenye ujuzi mwingi, kwa nini wasiwatumie hao na badala yake waniambie mimi? Kama siyo kutaka kunifanya chambo ni nini basi? Hainiingii akilini hata kidogo. Wao wenyewe Marekani na Uingereza wameyataka, kwa sababu waliambiwa wasipigane wao wakaamua kuingia vitani, wamelikoroga sasa inabidi walinywe!”
“Dennis, tafadhali usirudie kusema maneno hayo. Unajua kwamba heshima ya Taifa lako unaiondoa vivi hivi? Hebu fikiria kwamba wamewaacha wapelelezi wa nchi zote hizo na kuamua kukufuata wewe, huoni kwamba hiyo ni heshima kwako? Tafadhali badilisha uamuzi wako na uende ukaifanye hiyo kazi,” Inspekta Mahundo alisema.
“Mzee, nadhani nimekwishaimba vya kutosha na sasa naona wimbo huu hauna korasi, kama huna jambo jingine zaidi mimi nakwenda na nashukuru kwa kuninunuli chakula na kinywaji,” Dennis alisema huku akiinuka kitini.
Inspekta alijaribu kumshawishi aketi kwanza, lakini katu hakukubali, akaamua kuondoka zake kurejea hotilini Hilton Hotel. Alijua kabisa alichokuwa anakifanya na wala hakuujutia uamuzi wake.
*******
Badala ya kwenda moja kwa moja hotelini, Dennis aliamua kwenda kwenye Uwanja wa Moi Kasarani kutazama pambano la soka baina ya timu mbili kongwe za nchini Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards zilizokuwa zikimenyana siku hiyo. Baada ya kutoka huko yapata saa moja usiku, alipitia kwenye duka moja kununua nguo na baadaye akaenda hotelini.
Alipoingia mapokezi akamkuta yule mhudumu Lucille Mungai, ambaye alikuwa ameingia mchana huo. Alipomuona tu tabasamu pana lilichanua usoni kwake na kuanza kumchangamkia Dennis. Pamoja na kwamba hakuwahi kujihusisha na mwanamke katika maisha yake yote, lakini alishtukia ghafla akivutiwa mno na msichana huyo mbichi kabisa.
“Wewe Dennis, sasa ndiyo ukanifanyaje jana?” Lucille aliuliza.
“Sijui, kwani nilifanya nini?”
“Si uliniambia kwamba ungekuja huku tuongee, mimi nilitaka nije lakini nikasita.” Ndiyo kwanza akakumbuka kwamba alimuahidi binti huyo kwamba angemfuata au la angempigia simu.
“Oooh! Samahani sana, unajua nilikuwa nimechoka mno kiasi kwamba baada ya kuoga na kupata mlo nilijitupa kitandani kama gogo, nimezinduka usiku wakati mbu wakining’ata. Hata hivyo, hakijaharibika kitu, unaweza kuja baadaye, kwani unakuwa na nafasi muda gani?”
“Tuko watatu hapa, ninaweza kuwaacha wenzangu nikaja, kwa hiyo nitakuja saa tatu na nusu,” Lucille alisema na kuzidi kuachia tabasamu lililomfanya apendeze zaidi. Wakati akimpatia Dennis ufunguo wake ndipo akakumbuka kitu.
“Samahani Dennis, kuna jamaa yako moja alikuja kukuulizia.”
“Jamaa yangu? Jamaa gani huyo na yukoje?” aliuliza taratibu bila kuonyesha mshtuko usoni mwake, lakini moyoni tayari alikuwa ameshtuka. Alijua kwamba hakuwa na mtu yeyote aliyekuwa anamfahamu zaidi ya Bwana Collin Daniel, Inspekta Haroun Mahundo na labda yule kijana Carl Ochieng.
“Mrefu, ana umbo kubwa, halafu sikio lake la kushoto ametoga na kavaa hereni!”
Dennis alifikiria kwa muda na kujua kwamba huyo mtu hakumfahamu kabisa, lakini ili kutoonyesha mshangao akatabasamu na kusema; “Oooh! Yule jamaa, hivi alikutajia jina?”
“Ndiyo, kasema anaitwa Ricardo Gonzalez, anasema umtafute, namba yake hii hapa!” Lucille alisema na kumpatia namba ya simu ya mkononi ya mtu huyo.
“Asante, nitamtafuta!” alisema na kuondoka akiwa anaendelea kujiuliza kwamba mtu huyo ametokea wapi.
Alifungua mlango wa chumba chake, lakini katika hali ya mastajabu akamkuta mtu huyo akiwa ameketi kwenye kiti akiutazama mlango, bastola aina ya Revolver ikiwa imara mkononi mwake.
“Ingia ndani taratibu na ufunge mlango, kisha nyoosha mikono yako juu. Usifanye ujanja wowote ule. Tunahitaji kuongea kama watu wazima. Toa bastola yako iweke chini.”
Je, kwa nini amekataa kufanya kazi aliyopewa? Mtu anayemtafuta ambaye yuko chumbani kwake ni nani? Ni nani atakayekwenda kupeleleza silaha za mangamizi? Ungana na msimulizi wako wiki ijayo katika kisa hiki cha kusisimua...
Dennis amekataa kata kata kutumwa kwenda Iraq pamoja na kubembelezwa mno. Anaporudi hotelini kwake anapewa taarifa kwamba kuna mtu anamtafuta na anapoingia chumbani anakutana uso kwa uso namtu huyo aiwa kamshikia bastola. Je, nini kitaendelea? Ungana na msimulizi wako...
Badala ya kushtuka, Dennis aliachia tabasamu pana na kuonyesha kana kwamba hakuwa anajali kuwepo kwa mtu huyo wala madhara ya silaha aliyokuwa ameishika mkononi. Hakuonyesha kujali kwa sababu tayari alikuwa amepata taarifa zake mapokezi na alitabasamu kwa kuwa ilikuwa ni kawaida yake kuonyesha uso wa furaha kila alipokabiliana na hatari kama hizo.
Baada ya kumuona Ricardo Gonzalez, Dennis alianza kufikiria mara mbili mbili alipata kumuona wapi mtu huyo. Alikuwa na hakika kwamba alishawahi kumuona mahali, kwani sura yake haikuwa ngeni kabisa machoni mwake, lakini hakukumbuka ni mahali gani. Aliendelea kuvuta kumbukumbu zake kwa sekunde kadhaa na baada ya muda alitabasamu! Ndiyo! Lilikuwa kama tabasamu la ushindi, kwani tayari alikuwa amekumbuka mahali alipomuona.
ÒRicardo Suarez Ganzalez, jasusi wa zamani wa CIA aliyeasi baada ya kurubuniwa na KGB pamoja na mashiraka ya kijasusi ya Mashariki ya Kati, lakini akiwa anafahamu siri nyingi za CIA. Kwa muda mrefu ametafutwa kila mahali bila kuonekana na inasemekana alijificha katika mojawapo ya nchi zilizomongÕonyoka kutoka Urusi ya zamani. Hatimaye nakutana naye ana kwa ana! Karibu sana bwana Rocardo!Ó alikuwa kama mtu aliyekuwa akijisemea mwenyewe, lakini alipotamka kauli yake ya mwisho alinyoosha mkono na kutaka kumsalimia kwa lengo la kumkaribisha.
ÒWewe kunguni unazungumza nini? Enhe? Nani aliyekwambia mambo yote hayo? Halafu unadhani hiyo inaweza kukusaidia, elewa kwamba nina uwezo wa kufumua kichwa chako sasa hivi kwa sababu hakuna mtu anayefahamu kama mimi niko hapa zaidi ya yule malaya wa mapokezi, ambaye naye dawa yake ni ndogo sana,Ó Ricardo alikuwa amekasirika kusikia historia yake ikitamkwa na Dennis, ambaye katu hakumtegemea kama angekuwa anamfahamu.
Dennis alitabasamu, maana alitambua kwamba kwa kumweleza vile jamaa asingethubutu kufanya lolote kwani tayari alimuonyesha kwamba anamfahamu. Aliamini pia kwamba, kama angehadhibika na kuanzisha vurugu angeweza kumdhibiti kwa kuwa angekuwa anapigana kwa hasira na alivyoiangalia ile bastola haikuwa na kiwambo cha uzuia sauti, hivyo Ricardo asingeweza kuitumia. Hakuna jasusi ambaye ni mjinga kiasi cha kufanya tukio la kuwavuta watu kwa kufyatua risasi ovyo. Historia ya Ricardo na jasusi mwingine Gerd Voeller wa Ujerumani waliyeasi pamoja kwenye mashirika yao baada ya kubainika kwamba wanatumikia pia mashirika mengine ya kijasusi na kuuza siri za mashirika yao, aliipata wakati akisoma Ujerumani na hakuna hata taifa lililojua walipo.
ÒSikiliza Ricardo, waweza kuniona kama kijana mdogo, lakini naelewa mambo mengi kuliko unavyofikiria. Hata hivyo, tuachane na hayo, najua ujio wako kwangu utakuwa na maana kubwa, nina maana kwamba lazima kuna jambo ambalo limekufanya uje huku,Ó Dennis alisema taratibu.
ÒSikuja hapa kusikiliza historia, nimekuja kukuonya usijiingize kwenye mambo makubwa yasiyokuhusu, tena nimetumwa nikwambie kwamba wanazielewa nyayo zako kuliko ambavyo unaweza ukiona kivuli chako mwenyewe...Ó
ÒNgoja kwanza Ricardo, hebu punguza hasira, twende taratibu lakini kwa haraka. Hebu nieleze ni nani aliyekutuma kwangu na ni kitu gani ambacho umeelezwa kwamba mimi naweza kujiingiza kwacho?Ó
ÒDennis, usidhani hakuna anayejua kinachoendelea. Kwa taarifa yako, kama nilivyokuambia awali, wanakufahamu kuliko wewe unavyojifahamu. Wanazielewa nyendo zako zote,Ó Ricardo alisema kwa kauli nzito iliyoendelea kumtanza Dennis.
ÒSikiliza, hebu usiendelee kutumia mzunguko, nenda moja kwa moja unieleze kitu gani ambacho umekusudia kunieleza, mpaka hapa sijakuelewa unachosema.Ó
Ã’Unajifanya hujui, lakini ngoja nikueleze pengine unadhani hakuna anayejua kinachoendelea. Wiki mbili zilizopita Kitengo cha Ujasusi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilikutana mjini New York na kupendekeza wewe ukachunguze kuhusu suala la kuwepo kwa silaha za maangamizi nchini Iraq na kwa kukuthibitishia hilo Collin Daniel yupo hapa Nairobi na jana milikuwa naye hapa akikutaka ukubali kwenda. Mchana huu ulikuwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Tanzania, Haruoun Mahundo, ambaye amekushawishi ukubali uteuzi huo.
Ã’Nataka nikueleze kwamba, Rais Caesar Leon ni mpuuzi mkubwa na ndiyo maana nikaamua hata kulitosa Shirika la Ujasusi la CIA, ni mpuuzi kwa sababu hashauriki. Shambulizi la Septemba 11, 2001 alipelekewa taarifa mwezi mmoja kabla, lakini alipuuzia, matokeo yake ndiyo yale. Halafu aliambiwa kwamba Iraq haina silaha za sumu na ripoti ya mchunguzi wa Umoja wa Mataifa ilieleza hivyo, lakini bado aliendelea kukaidi na kupeleka jeshi kuipiga nchi hiyo. Kwa kiburi chake akisaidiana na Dick Johnson wakaenda kuvuruga amani ya Iraq. Ndiyo maana Ujerumani, pamoja na kuunga mkono vita hivyo, iliamua kutopeleka jeshi huko na kusema kwamba iko tayari kutoa tiba kwa majeruhi wa vita hiyo pamoja na kupeleka msaada wa chakula. Sasa mambo yamewatokea puani wanaanza kuhamanika, waache watoswe na kama ningekuwa mimi, haki ya nani vile ningewashtaki kwa sababu wamesababisha maisha ya watu kupotea bila sababu ya msingi.
ÒHapa nimekuja kwa amani kabisa, nakuonea huruma bado mtoto mdogo, usije ukapoteza maisha yako bure, hakuna silaha za maangamizi Iraq na kilichopo ni tabia ya Marekani kutaka kujaribu silaha zake vitani tu. Kwanza hata kama zikiwepo, wewe itakusaidia nini kama siyo kutumiwa tu ili uokoe unga wa Caesar Leona na Dick Johnson? Nakuonya kwa mara nyingine, achana na mambo yasiyokuhusu, mwache Leon apigane na kivuli chake,Ó Raicardo alisema na kuinuka kwenye kiti.
ÒLakini hujui kama ninakwenda huko ama siendi, bali ni hisia zako tu,Ó Dennis alisema.
ÒIwe unakwenda ama huendi hainihusu chochote, ninachokwambia mimi ni kwamba usijiingeze huko. Kwanza nikikuangalia hujai hata kiganjani mwangu, halafu wapigania haki za wanyonge ni wengi mno, hufiki popote na nataka nimuonyeshe Collin Daniel kwamba tunaweza kufanya mambo yetu mbele yake, na kesho tu utasikia,Ó alisema na kufungua mlango ambapo bila kutegemea alikutana uso kwa uso na Lucille ambaye ndiyo kwanza alikuwa akijiandaa kugonga mlango.
ÒOoh, mrembo, karibu sana. Nashukuru nimeonana na rafiki yangu, tumeshamaliza mazungumzo yetu samahani sana kwa kukuweka muda mrefu ukisubiri kuingia,Ó Ricardo alisema akimmezea mate Luccile ambaye alipendeza kweli kweli.
ÒAsanteh, hata hivyo ndiyo kwanza nimefika,Ó Lucille alisema.
Ricardo hakusubiri jambo jingine, alimpisha mrembo huo na yeye akatokomea gizani. Lucille alimtazama kisha akatikisa kichwa. Yote haya yalikuwa yakishuhudiwa na Dennis ambaye muda wote alikuwa akitabasamu. Lucille alifunga mlango na alipogeuka akatua kifuani mwa Dennis ambaye alimkaribisha na kumketisha kwenye sofa. Akammiminia kinywaji na yeye akaenda bafuni kuoga na baada ya muda akaingia chumbani kubadili nguo. Alipotoka nje alikuwa amevaa suluari ya dengrizi nyeusi, fulana nyeusi na raba nyeusi, bastola zake mbili alikuwa amezichomeka kiunoni.
ÒHee, mbona hivyo tena, unatoka nini?Ó Lucille alimuuliza kwa mshango.
ÒSiendi mbali, nitarudi sasa hivi lakini naomba unisubiri. Eeeh, halafu unajua nimesahau kitu kimoja,Ó Dennis alisema akichukua kikaratasi chenye namba ya simu ambayo alipewa na Lucille kwamba ni ya Ricardo.
ÒNini tena?Ó
ÒHii namba uliyonipa!Ó
ÒImefanyaje tena?Ó Lucille aliuliza akiwa amekodoa macho.
ÒSi ya huyu rafiki yangu? Nimezungumza naye, sasa kuna kitu kaniambia nikachukue hotelini kwake, ajabu ni kwamba nimesahau kumuuliza hoteli aliyofikia nadhani unaweza ukwa unaifahamu hoteli inayotumia namba hii ya simu,Ó Dennis alidanganya.
ÒHii ni namba ya Safari Park Hotel, kwani vipi?Ó
ÒHakuna tatizo lolote, ni mambo ya heri kabisa, sijaonana naye miaka mingi sasa kaniambia kwamba ana mzigo wangu nikauchukue, nitarudi muda si mrefu mpenzi, jisikie huru kabisa,Ó alisema huku akimbusu. Baadaye alimwachia na kurudi tena chumbani ambako alifunga vitu vyake vizuri kabisa na kuchukua mashine zake maalumu kikiwemo kifaa cha kutegea simu. Kisha akatoka na kumuaga Lucille.
ÒTafadhali usichelewe mpenzi,Ó Lucille alisema huku akiwa karembua macho yake.
ÒSichelewi, ilikuwa tuondoke wote, lakini nikamwambia kwamba kuna mtu namsubiri, ndiyo maana yeye katangulia,Ó alidaganya tena.
************
Giza lilikuwa limetanda nje kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inataka kunyesha. Dennis alishukuru kwa sababu aliamini hiyo ingemsaidia kufanya kazi yake aliyoikusudia. Kwa bahati nzuri wakati ametoka nje ya eneo la hoteli aliiona teksi iliyokuwa tupu na kuipungia, akamweleza dereva amkimbize Safari Park.
Baada ya kufika alimlipa dereva ujira wake na kujifanya anaingia ukumbini ambako bendi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa ikitumbuiza. Ndani ya ukumbini aliangaza macho yake huku na huko na kama bahati kwake akamuona Ricardo akiwa ameketi pembeni kabisa na mwanamke mmoja wakinywa pombe. Hakuwa na habari kabisa kama Dennis alikuwa amewasili hapo na kwa jinsi alivyovaa ilikuwa vigumu kwa mtu yeyote kumtambua, kwani alivaa pia na kofia aina ya pama.
Dennis alifanya hima na kuzunguka nje ya hoteli kwa kutumia mlango mwingine na akiwa huko aliangalia juu kuona wapi waya wa simu ulikoingilia. Manyunyu yalikuwa yanaanza kudondoka na radi na ngurumo vilisikika kila mahali. Kwa bahati nzuri aliiona sehemu hiyo na kuamua kukwea kwa kutumia bomba la maji machafu. Alipofika kwenye kidude cha kuunganishia nyaya alikifungua na kwa kutumia utundu wake akakipachika kifaa chake maalum ya kunasia mazungumzo ya kwenye simu, kisha akakirudisha kifuniko na kuteremka haraka huku mvua kubwa ikinyesha.
Aliingia ukumbini na kukuta kila mtu akiendelea na usakataji wa muziki, akazunguka mpaka sehemu aliyomuona Ricardo. Kwa bahati nzuri kwake Ricardo alikuwa anainuka kwenye kiti na kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa akimua mwanamke huyo kwamba angerejea bada ya muda, kisha akaonekana akizikwea ngazi haraka haraka. Dennis alikwenda kwenye kona tulivu na kukiwasha kimashine chake kilichokuwa kikidaka mawasiliano yaliyonaswa na kifaa alichokipachika. Dakika tano baadaye kikapata uhai.
ÒHaloo! Mapokezi siyo .... naomba nipigie namba 2176540 Mombasa tafadhali,Ó sauti ya Ricardo ilisikika vizuri na kuitikiwa na sauti ya msichana wa mapokezi ambaye alizungusha namba kadhaa kisha baada ya muda akamuunganisha Ricardo. ÒHaloo! Ismail! Tafadhali hakikisheni kila kitu kiko sawa, shambulizi hilo kama tulivyopanga lifanyike saa 4.00 na tunapaswa kuudhihirishia ulimwengu kwamba tunaweza kufanya lolote... hiki ni kama kiinimacho tu cha kuwaiga Waisraeli, lakini lengo kubwa ni kumdhihirishia Rais Caesar Leon wa Marekani kwamba tunaweza kupiga ngome yoyote ile. Nataka kesho saa 4.15 nisikie kwenye redio wakitangaza Paradise Hotel imelipulipwa, kwa kwa njia rahisi sana ya kutegesha bomu kwenye gari la maji, tumeelewana?Ó alipomaliza kutoa maelekezo alikata simu.
Dennis akili alimruka kwa sekunde kadhaa baada ya kusikia taarifa hizo. Japo mvua ilikuwa inanyesha sana, lakini aliamua kutoka nje na kutembea kwa miguu mwendo mrefu kabla ya kuibahatisha teksi aliyoisimamisha na kumuomba dereva amkimbize stendi kuu ya mabasi. Kwanza dereva alikuwa na mashaka kwamba huenda huyo ni jambazi, lakini Dennis akamtoa shaka kwamba anataka akabahatishe gari la kwenda Mombasa kwa sababu amepigiwa simu usiku huo kwamba mama yake mzazi amefariki.
ÒPole sana rafiki yangu, hata hivyo sidhani kama muda huu unaweza kupata gari,Ó dereva huyo alisema.
ÒTumuombe Mungu, hata hivyo, hivi unaelewa sehemu yoyote ambayo ninaweza kupata huduma ya simu muda huu?Ó
ÒPale pale stendi kuna sehemu wanapigisha simu usiku kucha.Ó
Kwa bahati nzuri aliipata namba ya simu ya Paradise Hotel baada ya kupekua kwenye kitabu cha orodha ya simu na huku akiwa ameziba pua yake aliomba kuzungumza na Meneja na kumwambia kwamba afanye kila awezalo kuhakikisha kwamba kabla ya saa tatu asubuhi wapangaji wote wawe wametka vyumbani mwao kwa kuwa kuna watu waliotaka kuishambulia hoteli yake. Baada ya kuona meneja anabisha aliamua kukata simu kwa hasira na kuondoka kurejea hotelini kwake Hilton, ambako alimkuta Lucille akiwa anakoroma.
********
Kutokana na uchovu mwingi aliokuwa nao hasa baada ya kupata shuruba nyingine kutoka kwa Lucille aliyemganda usiku huo kama luba, Dennis hakuamka mpaka saa tano asubuhi, tena kwa kushtuliwa na Lucille, ambaye alimnyangÕanya shuka huku yeye akiwa kama alivyozaliwa. Kabla hajatahamaki, Lucille alimvaa na kuanza kumhenyesha kwa mara nyingine tena na alipokuja kutanabahi tayari ilikwishafika saa 5.40. alikurupuka kutoka kitandani na kukimbilia bafuni, kisha akavaa haraka haraka na kelekea kwenye sebule ambako aliwasha televisheni.
Alichokiona hapo kilimfanya achanganyikiwe. Hoteli ya Paradise ilikuwa inaungua moto huku mtangazaji wa televisheni akiwa pembeni akielezea tukio hilo kwamba karibu watu 48, wakiwemo wanawake na watoto raia wa Israel, wamekufa katika shambulio hilo la kigaidi. Hasira zilimkaba Dennis na kuanza kumlaumu moyoni mwake yule meneja wa hoteli hiyo ambaye alikuwa mgumu kuelewa. Ama angalisikiliza maagizo yake, kwa vyovyote vile lazima angewanusuru watu hao.
Huku uso wake ukionyesha tabasamu angavu, alimuaga Lucille kwamba anatoka mara moja angerejea baadaye na binti huyo, ambaye siku hiyo alikuwa mapumzikoni, akanyongea kutokana na kuachwa peke yake. Dennis hakuwa na jinsi, alielewa kama angeendelea kusikiliza kilio cha mwanamke huyo asingekwenda kule alikokusudia. Aliondoka haraka na kutokomea mitaani, ambako alikodisha teksi iliyomkimbiza Safari Park. Alipofika mapokezi hakutaka kupoteza muda kumuulizia Ricardo Suarez Gonzalez.
ÒHuyo mbona kaondoka saa moja iliyopita, amekwenda Dubai! Vipi mnafahamiana?Ó dada wa mapokezi alimuuliza Dennis. Dennis alivuta pumzi ndefu na kuzishusha, kisha akamweleza kwamba ni rafiki yake mkubwa ambaye amepotezana naye muda mrefu.
ÒBasi una bahati mbaya sana, lakini ni mteja wetu wa muda mrefu sana, tena huwa anatupigia simu kabla hajaja tunamuwekea chumba, halafu anakipenda kweli chumba namba tisa. Hata hivyo, jaribu kuangalia kama unaweza uwahi Kenyatta International Airport, kwani ndege ya Emirates inaondoka saa 5.30, una akika kama 15 tu.Ó
ÒSawa, pamoja na hayo, nadhani unaweza kunisaidia kitu kimoja, maana huyu mtu ni muhimu sana kwangu. Nahitaji unipatia namba yake ya simu akiwa Dubai,Ó Dennis aliomba.
ÒSubiri kidogo,Ó dada huyo alisema na kuanza kupekuapekua na baada ya muda akamuandikia namba kama tatu hivi na kjumkabidhi. Dennis alishukuru na kuondoka haraka kuelekea uwanja wa ndege. Wakati wanakaribia uwanja huo waliiona ndege ya Emirates ikipaa angani.
Je, mambo yatakuwaje? Kazi aliyotumwa ataifanya? Ungana na msimulizi wako wiki ijayo katika kisa hiki cha kusisimua...
Dennis amekutana na Ricardo Gonzalez, jasusi wa zamani wa CIA aliyeasi, ambaye anamtisha kwamba asithubutu kujiingiza kwenye kazi anayotaka kutumwa. Anaamua kumfuatilia na kujua mipango yake kwamba anataka kulipua hoteli ya mjini Mombasa, tukio ambalo kweli linatokea. Ndipo anapoamua kumfuatilia mwanaharamu huyo. Je, atampata? Ungana na msimulizi wako wiki ijayo katika kisa hiki cha kusisimua...
Nguvu zilimwishia Dennis kwa kuona ameshindwa kumkamata adui ambaye amesababisha mauaji. Alifahamu fika kwamba, Ricardo Suarez Gonzalez ndiye mhusika mkuu na kwa vyovyote vile anafahamu mambo mengi, ikiwa ni pamoja na siri za utengenezaji wa silaha za sumu huko Mashariki ya Kati. Ndiyo, kama ameweza kuamuru shambulio dogo kama hilo ili kumkomoa Rais wa Marekani Caesar Leon kwa kile alichokiita kiburi cha uwezo wa kivita na pia kumdhihirishia Bwana Collin Daniel kutoka kitengo cha ujasusi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hakika ni mtu ambaye alikuwa akiyafahamu mambo mengi ya siri kutoka upande wa pili.
Hata hivyo, hakubabaika sana. Alichofanya ni kwenda mpaka uwanjani, kisha akaenda kwenye dirisha la wakala wa Shirika la Ndege la Emirates ambapo kwa utmia utundu wake wote alijitambulisha kwa jina la bandia.
“Tukusaidie tafadhali!” msichana wa Kiarabu aliyekuwa dirishani alimpokea kwa bashasha na kumkaribisha.
“Ooh! Samahani sana kwa usumbufu, ni kwamba ndege iliyoondoka hivi sasa ilikuwa iondoke na rafiki yangu mmoja ambaye alitegemea nimletee mizigo yake hapa, lakini nimechelewa. Sasa sielewi kama naye ameondoka au la, na kama atakuwa ameondoka basi niangalie uwezekano mwingine wa kumtumia mizigo hiyo...” Dennis alisema huku akionyesha uso wa huzuni kidogo.
“Pole sana kaka yangu! Unaweza kunitajia jina la huyo rafiki yako?” dada huyo alisema huku akichukua orodha ya abiria wote walioondoka na ndege hiyo.
“Ricardo! Ricardo Gonzalez!” Dennis alijibu haraka haraka huku macho yake yakiwa yanapepesa kwenye orodha hiyo kupitia dirishani.
Kitendo cha kutaja jina hilo kilimfanya dada huyo ashtuke. Akamtazama Dennis kwa makini kisha akaendelea kuangalia. Dennis alimuona, akahisi lazima hapo kuna jambo na kwa vyovyote atakuwa amekosea kutaja jina hilo.
“Kwa bahati mbaya katika orodha hii hakuna jina la mtu kama huyo. Kwa kukusadia tu, pengine unaweza kunieleza wajihi wake, maana karibu abiria wengi nimewaona.”
“Ni mrefu, kifua kipana, sikio lake la kushoto limekatika kwa chini, anapenda sana kuvaa kofia...” maelezo hayo yalizidi kumtia mashaka mwanadada huyo ambaye alimtazama kwa makini Dennis. Hata hivyo, kama aliyegutuliwa akasema;
“Aaah, unasema Ahmed Kassim Al-Balawy? Hilo ndilo jina lake, ameongozana na Ismail Saifudin, wameondoka. Hivi wewe ni rafiki yake?”
“Ndiyo, nilikuwa naye jana, najua tumepoteana miaka mingi sana, ndiyo kwanza tumekutana hapa Nairobi,” Dennis aliendelea kudanganya na angalau kwa maelezo yake ya mwisho hofu ya dada huyo ilipungua. Dennis alifahamu kwamba kulikuwa na kitu hapo katikati, ingawa hakukijua. Alipoona hivyo akauliza tena; “Ninaweza kujua anafikia wapi?”
Swali hili lilikuwa rahisi kujibiwa kwa sababu ni swali la kawaida kabisa, lakini kidogo lilikuwa gumu kwa mwanadada huyu. Alifikiria mara mbilimbili kama amwambie au la, hata hivyo baadaye akaamua kumweleza kwamba anafikia Dubai.
“Ahsante sana dada, basi nitamwagizia mizigo yake, kwani hata hivyo ilikuwa haijakamilika,” alisema Dennis.
“Haya, umesema unaitwa nani vile?”
“Naitwa Gerd Voeller, Mjerumani mwenye asili ya Afrika,” alizidi kudanganya. Hata hivyo hakuwa mbali na ukweli, kwani jasusi Gerd Voeller wa Ujerumani alikuwa mtu mweusi.
Dennis aliondoka hapo dirishani na kuelekea kwenye eneo la teksi, alikodisha mojawapo na kumwelekeza dereva ampelekea Safari Park Hotel. Mawazo yake yalikuwa mbali sana akiwa anafikiria sababu za Ricardo kutumia jina la Ahmed Kassim Al-Balawy. Alifikiria pia mtu ambaye wamengozana naye, Ismail Saifudin. Akakumbuka kwamba wakati anapiga simu jana kule Mombasa alizungumza na mtu mwenye jina hilo, kwa hiyo inawezekana kabisa wamendoka wote na afari yao ilikuwa moja. Kitendo cha kushtuka cha yule mwanamke uwanja wa ndege nacho kilizidi kumtia mashaka, akaelewa kwamba, lazima atakuwa anamfahamu fika mtu aliyemuulizia.
“Brother, gari haiwezi kuingia ndani, au unaendelea na safari?” dereva wa teksi alimuuliza kwa Kiwahili cha Kikenya na kumgutua.
“Oooh! Samahani ndugu yangu, unajua unaweza kuwa nani ya gari unasafiri na akili yako nayo inasafiri mbali,” alijitetea na kutoa noti tano za shilingi mia mia akamkabidhi. Aliishuhudia teksi hiyo inaondoka, kisha yeye akavuka upande wa pili na kuanza kukata mitaa. Lengo lake lilikuwa kupoteza nyayo zake. Alipokata mitaa mitatu akapungia teksi iliyokuwa inapita mbele yake na kumweleza dereva ampeleke Hilton Hotel.
Kwa bahati nzuri hoteli kubwa na za nyota tano kama Hilton huwa zinakuwa na wakala wa mashirika ya ndege humo humo. Alichofanya Dennis baada ya kuwasili hotelini ni kwenda moja kwa moja mpaka kwenye shirika la ndege la Oman na kukata tiketi ili aondoke kesho yake kwenda Mascut akitumia jina la Dawood bin Mohammed Al-Kindy, raia wa Uturuki.
“Unasafiri wewe au mtu mwingine?” mwanadada aliyehusika alimuuliza.
“Anasafiri rafiki yangu, kasema nije nimkatie tiketi tu,” alidanganya.
“Tunaweza kuiona pasipoti ya huyo mtu anayesafiri?”
“Yah! Hii hapa!” Dennis alitoa pasipoti yake ya bandia ambayo ilimuonyesha kijana mmoja wa Kiarabu mwenye miaka 30, mzaliwa wa Istanbul, Uturuki, akiwa mfanyakazi katika mojawapo ya mashirika ya kimataifa ya kujitolea muhanga katika majanga mbalimbali. Pasipoti hiyo ilimruhusu kuingia nchi yoyote duniani bila pingamizi lolote.
“Ndege inaondoka kesho saa 8.15 mchana, anatakiwa kufika uwanjani saa 7.15, tunamtakia safari njema,” dada huyo alisema huku akimkabidhi Dennis pasipoti pamoja na tiketi.
“Nitamwambia awahi!” alisema na kuondoka kuelekea chumbani kwake ambako aliamini Lucille alikuwa anamsubiri.
***********
Uwanja wa ndege wa Kenyatta ulikuwa na pilika pilika nyingi kwani siku hiyo ya Jumatatu kulikuwa na ndege nyingi kubwa za kimataifa zilizokuwa zinatua na kuondoka. Kila mtu alionekana kuwa na hamisini zake. Kijana mmoja wa Kiarabu alionekana akiwa na mkoba wake wa kawaida tu mkononi akiwa miongoni mwa watu hao. Alifika mapema sana, tangu saa 7.00 mchana na baaa ya kuuweka mkoba wake mahali fulani akasimama pembeni na kuivaa miwani yake maalum. Kwa jinsi alivyoonekana, kila mmoja alijua kwamba huyo alikuwa mtu aliyeridhika na maisha. Aliranda huku na huko akisubiri muda wa kuondoka uwadie. Huyu alikuwa Dennis Geoffrey Mikwambe, mpelelezi chipukizi na jasiri ambaye alikuwa amejibadili kwa makusudi kabisa.
Jinsi alivyoondoka hotelini kwake anajua mwenyewe, maana alimtoa haraka chumbani Lucille ambaye alikuwa anang’ang’ania anendelee kubikia hapo kwa siku nyingine tena. Mara baada ya kuondoka Lucille, asubuhi hiyo hiyo Bwana Collin Daniel na Inspekta Haroun Mahundo waliwasili chumbani kwake kwa mazungumzo ya mwisho. Aliwasikiliza kwa makini kuhusu hoja yao ya kutaka afanye ujasusi nchini Iraq lakini akawaeleza kwamba hakuwa tayari kwa jukumu hilo.
“Niacheni nipumzike, watumeni watu wengine, mimi siko tayari,” alisema na kuzidi kuwasikitisha wazee hao. Mara walipoondoka chumbani kwake akaanza kupanga vifaa vyake vyote muhimu kwenye mkoba wake. Kwa jinsi alivyopanga aliamini kabisa kwamba hata kama kutakuwa na wapekuzi wa aina gani, kamwe hawawezi kugundua silaha zake.
Alipomaliza maandalizi hayo akaoga na kisha kuvaa sura za bandia na kuifanya sura yake ifanane kabisa la kilana Dawood Mohammed al-Kindy wa kwenye pasipoti, kama kweli alikuwepo. Alipohakikisha amejiweka sawa akaondoka na kwenda kukabidhi ufunguo mapokezi. Pembeni kabisa kwenye eneo hilo la mapokezi aliwaona Collin Daniel na Ispekta Mahundo wakiwa na nyuso za masikitiko. Walikuwa wameketi kwenye meza moja ya pembeni wakijadiliana jambo. Aliwahurumia na kuondoka.
“Abiria wanaosafiri kwa Oman Air, mruko namba FX 0008732A kwenda Muscat wanaombwa waingie kwenye ndege tafadhali!” sauti nyonyoro ya mwanamke ilisikika kupitia vipaza sauti vya hapo uwanjani kwa lugha ya Kiingereza, Kiswahili na Kifaransa. Abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege hiyo wakaanza pilika pilika za kuingia uwanjani. Dennis akatumia nafasi hiyo kuwatazama mmoja baada ya mwingine, alipohakikisha kwamba kuna usalama, akabeba begi lake na kuingia ndani.
Waliwasili Muscat saa 10.30. Baada ya kumaliza tararibu zote, Dennis alitoka nje ya uwanja na kuangaza angaza kwenye maduka hayo. Ghafla akabadili mawazo, badala ya kwenda mjini, aliamua kuunganisha siku hiyo hiyo kwenda Dubai. Alikwenda kwenye ofisi za mawakala wa ndege kuulizia kama kulikuwa na ndege iliyokuwa inakwenda Dubai, kwa bahati nzuri kulikuwa na ndege ya Emorates iliyokuwa inawasili hapo saa 12.00 kutoka Dar es Salaam, Tanzania na kuelekea Dubai. Akaamua kukata tiketi ili kuunganisha safari.
Wakati akisubiri muda wa safari ufike, aliamua kununua vijitabu vya ramani na maelekezo ya miji mbalimbali, hususan ya nchi za Kiarabu. Akanunua pia kitabu kilichokuwa na orodha ya simu za hoteli mbalimbali. Akaingia kwenye mkahawa wa uwanjani hapo na kuanza kunywa whisky taratibu huku akizipitia ramani hizo. Miwani yake haikumbanduka, kwa sababu ilikuwa ni aina fulani ya kamera ambayo ilikuwa ikichunguza mambo mmbalimbali, na kama kuna jambo au mtu aliyemtilia mashaka, aliifanya kama anairekebisha, kumbe alikuwa akiipiga na kuihifadhi picha hiyo.
Hatimaye muda wa kuondoka ulifika, ndege ikaiacha ardhi ya Oman na kuelekea kaskazini mashariki, Muungano wa Falme za Kiarabu. Mawazo mengi yalikuwa yanapishana kichwani mwa Dennis. Hakujua wakubwa wa Ricardo ni aina nani, ingawa aliamini kwamba lazima watakuwa ni watu wenye mtandao mpana. Kuingia katika ukanda huo wa Mashariki ya Kati kulikuwa kunahatarisha maisha ya mtu yeyote aliyekuwa na itikadi za kibepari au mtazamo wa Ki-Magharibi na kuishabikia nchi kama Marekani. Kwa historia ilivyoonyesha, hakuna kachero wa CIA ambaye alikwenda kanda huo akatoka salama hata baada ya kugundulika, hili Dennis alilifahamu fika.
“Vyovyote iwavyo, lakini nitahakikisha napambana kiume,” Dennis alijisemea mwenye moyoni wakati ndege ikitua. Alikuwa ameazimia kuendesha operesheni hiyo kimya kimya, ingawa hakutaka kuwaeleza akina Collin Daniel na wenzake. Alichotaka kufanya ni kuupumbaza ulimwengu ili ujue kwamba amekataa kazi.
********
“Hakuna anayeweza kuamini! Unasema kweli Collin?” wajumbe wa Kitengo cha Ujasusi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiongozwa na Marekani waliuliza kwa mshangao.
“Inabidi muamini ndugu zangu, nimejitahidi kwei kumuomba afanye kazi hii, lakini amekataa, tena siku peke yangu, nilikuwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Tanzania, Inspekta Haroun Mhando...” alijitetea Collin Daniel mbele ya kikao hicho cha dharura kilichofanyika kwa siri.
“Collin usitufanye sisi wajinga, kauli yako ni sawa na kusema kwamba umemuwekea paka maziwa akakataa kuyanywa. Hivi kweli mtu anaweza kukataa kama anapewa jukumu nyeti kama hili, ambalo ni sifa kwake na kwa taifa atokako?” aliuliza mjumbe kutoka Uingereza.
“Hivi unawezaje kukubali kijana kama yule akakukatalia hivi hivi?” mjumbe mwingine kutoka Ujerumani akauliza na kuongeza. “Kwanza sisi ndio tuliompa mafunzo, kwa nini asikamatwe na kuwekwa ndani kwa muda ili apate fundisho? Unajua namna hii anaweza kutugeuka na kuegemea upande wa maadui zetu!”
“Unayosema ni kweli, lakini naomba muelewe kitu kimoja, kuna hatari kubwa mbele katika suala hili, linahitaji ujasiri, kwa sababu sote tunaelewa kwamba suala hili linakwenda sambamba na magaidi... hebu fikiria mlipuko uliotokea kule Mombasa, Kenya na kuwaua watalii wa Kiisraeli, tena naambiwa kwamba kuna mtu alimtahadharisha meneja wa hoteli kuhusu tishio hilo, lakini akakaidi...” alisema Collin.
“Hapo sasa ndipo ulitakiwa kumbana Dennis ili aifanye kazi hiyo. Sasa cha kufanya ni hivi, Dennis akamatwe na kuwekwa chini ya ulinzi, baada ya mateso kidogo atajifunza na nafikiri atakubali,” mwenyekiti wa kikao hicho alisema.
“Mtamkamatia wapi?” Collin aliwahoji katika hali iliyowashtua wenzake.
“Huko huko Nairobi...”
“Ameondoka na hajulikani aliko...namna alivyoondoka hakuna anayefahamu, maana mimi nilirejea chumbani kwake saa mbili baada ya kuachana naye nikakuta mlango umefungwa, nilipouliza nikaambiwa ametoka, lakini namna alivyotoka ndiyo bado sijapata jibu, maana mimi nilikuwa mapokezi na sikumuona.”
Maelezo hayo yaliwachanganya wenzake na kuzidi kukuna vichwa. Hawakujua wafanye nini. Mkutano uliahirishwa bila ya kufikia ufumbuzi.
*********
Dennis alikuwa kwenye kibanda cha simu akipiga namba ambazo alipewa na dada wa mapokezi katika hoteli ya Safari Park kule Nairobi kwamba ndizo namba za Ricardo Suarez Gonzalez au Ahmed Kassim Al-Alawy kama alivyokuwa akifahamika huko Uarabuni. Tayari alikuwa amepata chumba katika hoteli moja yenye hadhi ya kati na baada ya hapo akaingia mtaani kwa kufuata ramani aliyoinunua Muscat.
“Al-Muntazir Hotel! Nikusaidie tafadhali?” sauti ya mwanamke iliyozungumza kwa lugha ya Kiarabu fasaha ilisema upande wa pili. Dennis akarekebisha koo lake na kwa kuwa aliifahamu lugha hiyo akajibu;
“Yah! Naweza kuzungumza na Bwana Ahmed al-Alawy?”
“Ni nani na unapiga kutoka wapi?”
“Naitwa Hamad Ussi bin Aziz, napiga simu kutoka Baghdad,” alidanganya.
“Samahani, bwana Ahmed ametoka kidogo, jaribu kama saa tano hivi usiku,” alisema dada huyo na kukata simu. Kitendo hiki kilimpa mashaka kidogo Dennis kwa sababu kama mtu huyo hakuwepo, hakukuwa na haja ya kumuulizia jina lake kabla. Alifahamu kwamba lazima kutakuwa na namna fulani huko.
Hapo hapo akaamua kutazama ramani na kuiona hoteli hiyo mahali ilipokuwa. Haikuwa mbali sana na alipopigia simu, hivyo akaamua kutembelea tu kwa miguu, lakini akiwa anatumia tahadhari ya hali ya juu. Miwani yake maalumu haikubanduka machoni mwake. Alipoikaribia hoteli hiyo akazunguka kwa nyuma na kuangaza mahali zilipopitia nyaya za simu. Akazunguka pande wa mbele la kuangalia hali ya ulinzi ilikuwaje, aliporidhika akarudi tena upande wa nyuma na kuona kwamba alikuwa na uwezo wa kupanda mpaka zinapoingilia nyaya hizo. Alizunguka mjini mpaka saa saba usiku, kisha akarejea hapo na kwa kutumia utundu wake akaweza kuruka uzio wa hoteli na kukwea mpaka juu.
Je, mambo yatakuwaje? Atampata mtu anayemtafuta? Lakini nini hatma ya yote haya? Ungana na msimulizi wako wiki ijayo katika kisa hiki cha kusisimua...
Dennis amewakatalia wakubwa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwenda kuchunguza kama kuna slaha za maangamizi ya halaiki nchini Iraq. Anakutana na jasusi wa zamani wa CIA aliyeasi, Ricardo Suarez Gonzalez, ambaye anamtisha kwamba asithubutu kabisa kujihusisha na upelelezi wa suala hilo. Pamoja na tishio hilo anaamua kufuatilia na tayari yuko Dubai ambako amekwenda katika hoteli aliyofikia Gonzalez kwa lengo la kupandikiza vifaa vyake ili anase mazungumzo ya kwenye simu. Je, atafanikiwa? Endelea na simulizi hii ya kuvutia ambayo mtiririko wake umepindapinda, lakini ukiifuatilia mpaka mwisho takuwa umepata uhondo wa kutosha na kutegua kitendawili...
Dennis alikipachika kifaa chake maalumu cha kunasia mazungumzo ya kwenye simu. Alipohakikisha amekamilisha kazi hiyo akateremka haraka na kuondoka kurejea hotelini kwake kwa ajili ya hatua nyingine. Alikuwa na uhakika kwamba kuanzia hapo angeweza kupata muongozo wa nini cha kufanya. Aliamini sasa hakuwa akiigiza, bali alikwishaingia msambweni na hakuwa na budi kugangamala.
Kitu kimoja ambacho aliamini ni kwamba, watu aliokuwa akikabiliana nao waliijua kazi yao vizuri. Walikuwa wajanja kuliko ambavyo wengine waliwafikiria. Hii ilitokana na ukweli kwamba, watu hao, hasa Waarabu, walikuwa radhi kujitoa muhanga wakati wowote katika kile walichokielezea kwamba kufa wakitetea imani yao. Dennis alilielewa hili na akadhamiria kuficha nyayo zake kwa kadiri awezavyo ili kuhakikisha kwamba hagundiliki kirahisi.
Alipofika hotelini kwake kitu cha kwanza kufanya ni kuitegea mitambo yake ili aweze kunasa mazungumzo ya kwenye simu, kisha akaingia bafuni kuoga kabla ya kushuka mgahawani kupata mlo wa jioni.
*********
Ricardo Suarez Gonzalez au Ahmed Kassim Al-Alawy alikuwa chumbani kwake akipanga mambo yake mbalimbali ambayo alitakiwa kuyafanya kama alivyoagizwa na wakubwa wake. Hoteli ya Al-Muntazir ilimilikiwa na mmoja wa mabosi wa kikundi cha kigaidi kilichokuwa na ushirikiano mzuri na nchi zote za Kiarabu. Kikundi hiki kilichojulikana kama Khalifa al-Jihad kilichokuwa na makao yake makuu nchini Lebanon, ndicho kilichotumika kusambaratisha mipango yote mibovu na ya hatari iliyopangwa na mataifa mengine dhidi ya taifa lolote la Kiarabu. Mbali ya hivyo, pia kilikuwa kikundi maalum kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa mataifa maadui.
Wahusika wa kikundi hiki walijitahidi kupanua mtandao wao kila sehemu duniani kwa kuwaweka vijana wao, tena wa mataifa husika. Hii iliwarahisishia utendaji wao wa kazi na katika kupata siri nyingi kutoka kwa mataifa waliyoona tishio kwao, waliamua kuwarubuni baadhi ya makachero wao na kuwahifadhi, hasa wale waliokuwa wanazifahamu siri nyingi za mashirika ya kijasusi duniani. Hapo ndipo walipoweza kumnasa Ricardo Suarez Gonzalez wa Hispania, ambaye alikuwa mwakilishi wa CIA huko Ujerumani Mashariki kabla ya nchi hizo kuungana. Kwa kuutambua umuhimu wake, hasa kwa vile aliifahamu mipango mingi ya Marekani na washirika wake, kikundi hiki kikaamua kumkabidhi kuwa mkuu wa operesheni zote. Walichofanya wao ni kumpa maelekezo, halafu yeye alipanga utekelezaji wake.
Jioni hii alikuwa akipitia agizo lililotolewa na wakubwa wake likimtaka afanye shambulizi la kwenye treni mjini Madrid, Hispania katika kumshinikiza rais wa nchi hiyo Eduardo Heleguera aondoe majeshi yake nchini Iraq haraka iwezekanavyo. Taarifa hii ilimchanganya sana, kwa sababu aliamini watakaokufa ni pamoja na ndugu zake. Hata hivyo, aliitazama kazi yenyewe na kugundua kwamba ni ya muda mfupi sana na alipokumbuka mamilioni ya Dinari yaliyokuwa yakimiminika katika akaunti zake zilizokuwepo kila nchi ya Kiarabu, aliona anaweza kuifanya bila matatizo.
Wakati akiendelea kuipitia taarifa hiyo mara simu ya mezani ikapata uhai. Aliinyanyua haraka haraka na kusikiliza. Alikuwa ni yule dada wa mapokezi akimpa taarifa kwamba kuna mtu amepiga simu akimuulizia, lakini kwa kuwa alikuwa na mashaka akamweleza kwamba Ahmaed Kassim Al-Alawy ametoka.
“Umesema anaitwa Hamad Ussi bin Aziz?” Ricardo aliuliza kwa mshangao.
“Ndiyo, kasema anapiga simu kutoka Baghdad na alikuwa na shida na wewe.”
“Hapana, simjui mtu mwenye jina kama hilo, au umeshindwa kulikariri jina lake?”
“Wakati akizungumza nilikuwa naandika, kwa hiyo nina hakika na ninachokisema. Lakini kama unaijua namba yake unaweza kumpigia ili uhakikishe, pengine alikuwa na shida na wewe!” alipendekeza dada huyo.
“Sawa usijali Zahra, nitapiga sasa hivi,” Ricardo alisema na kukata simu. Bado aliendelea kuwaza mtu huyo aliyempigia simu kwamba ni nani. Alifikiria kwamba huenda alikuwa ni mmoja wa wakubwa wake aliyetaka kuuliza kama ameipata taarifa yao. “Lakini mbona wanaifahamu namba yangu ya moja kwa moja? Au waliitafuta bila mafanikio, maana wakati mwingine hali ya hewa husababisha mawasiliano kuwa mabovu.” Aliwaza na wakati huo huo akanyanyua mkonga wa simu nyingine na kubonyeza namba kadhaa kisha akaendelea kusikiliza.
“Haloo Ahmed? Vipi kuna tatizo lolote?” sauti nzito iliyozungumza Kiarabu iliuliza taratibu.
“Hapana! Ndiyo kwanza nilikuwa naipitia taarifa....” alisema.
“Aaah! Umeipata siyo? Sasa inatakiwa kazi hiyo ifanyike baada ya wiki mbili kuanzia sasa. Nadhani maelekezo yote umeshayapata humo? Hakikisha treni lenye abiria linalipuka mjini Madrid wiki mbili kuanzia sasa, hili litakuwa fundisho kubwa kwa watu hawa wenye kimbelembele. Tukimaliza huko tunaelekea Uingereza, huko tutakupa maelekezo mengine,” sauti hiyo nzito iliendelea kuzungumza.
“Yaa, nimeyapata, nitajua nini cha kufanya kuanzia sasa hivi. Hata hivyo, nilikuwa nauliza mtu anayeitwa Hamad Ussi bin Aziz!”
“Ndiye nani huyo tena?” sauti ya upande wa pili iliuliza kwa mshangao.
“Mbona nimeambia amepiga simu muda si mrefu kutoka huko? Alikuwa anahitaji kuzungumza na mimi.”
Kabla ya kujibu mzee wa upande wa pili alipumua kwa nguvu, akakaa kimya kwa muda akitafakari, kisha akashusha pumzi.
“Ahmed, angalia usianze kuharibu mambo. Unafahamu fika kwamba huku hakuna mtu mwenye jina kama hilo. Angalia isije kuwa umeshaziacha wazi nyayo zako, utahatarisha maisha ya watu wengi pamoja na kuvuruga mipango yetu mingi...”
Ricardo hakutaka kujibu chochote. Alichofanya ni kuurudisha taratibu mkonga na kuanza kutafakari. Akili yake ilikuwa imechanganyikiwa. Alielewa ni kwa kiasi gani alikuwa ameanza kuvuruga mambo. Kwa hasira akagonga meza kwa nguvu na kuinuka akaanza kuranda chumbani. Alijiuliza ni nani mwenye jina hilo aliyekuwa akimuulizia.
Kwa jinsi alivyofahamu, ni watu wachache sana waliokuwa wanaijua namba ya simu na ambao walifahamu kwamba alikuwa akiishi hotelini hapo. Kwa mantiki hiyo, alihisi kwamba yeyote aliyepiga simu alimfahamu fika. Alijaribu kufikiria kwa muda kama kuna mtu yeyote aliyemhisi kwamba anaweza kumpigia simu lakini hakukumbuka. Siku zote hakuwa na uhusiano na mtu yeyote maana alielewa madhara ya kufahamiana na watu wengi nje ya kazi.
Aliposhindwa kupata jibu akaamua kutoka nje na kwenda baa ambako alianza kuagiza vinywaji vikali katika lengo la kujisahaulisha kwa muda mambo yaliyomvuruga akili.
*******
Dennis, ambaye ndiyo kwanza alikuwa amerejea kutoka mgahawani na kuurudisha nyuma mkanda uliokuwa ukirekodi mazungumzo ya kwenye simu alishtushwa mno na taarifa hizo mpya na za kutisha. Kulipua treni ya abiria mjini Madrid kama shinikizo la serikali ya Hispania kuondoa majeshi yake Iraq kilikuwa ni kitendo cha kinyama kuliko kawaida. Hakika asingekubali kuona maisha ya watu wasio na hatia yanateketea.
Alifikiria namna ya kufanya ili kunusuru shambulio hilo lakini akashindwa kupata jibu la haraka haraka. Kwenda huko ingekuwa jambo la msingi, lakini aliona itakuwa ni kazi ngumu kwake kuondoka katika eneo jekundu, Mashariki ya Kati, na kuiacha kazi ambayo hasa ndiyo iliyomfanya aje huku, japo hakuna hata kiongozi wala mtu yeyote aliyefahamu aliko.
Baada ya tafakuri ya muda mrefu, hatimaye alifikia uamuzi wa kumpigia simu Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Hispania, Inspekta Jenerali Alfonso Gonzalez Cardoso. Aliamini kwamba, endapo atamweleza kuhusu mpango huo uliopangwa kufanyika wiki mbili kuanzia wakati huo, basi angekuwa na uwezo wa kulizuia shambulio hilo.
“Lazima nimtaarifu usiku huu huu,” Dennis alisema na kuteremka ngazi na kisha kutoka nje ya hoteli. Aliamini kwamba kutumia simu ya kibandani kungekuwa na usalama mkubwa sana kwake badala ya kutumia simu ya hotelini ambayo angeweza kupewa bila matatizo yoyote.
Aliondoka na kuelekea katika eneo la kaskazini kulikokuwa na klabu moja ya usiku ambayo iliruhusu watu matajiri tu kuingia kutokana na sheria kali za Kiislam za kutoruhusu klabu kama hizo sehemu mbalimbali. Aliamini kwamba huko angeweza kupata mahali pa kupiga simu. Aliteremka kwenye gari alilokodi na baaa ya kumlipa dereva ujira wake, akaingia ndani baada ya kulipa kiingilio.
Mtu mwingine angeweza kuzuiwa, lakini utanashati wa Dennis, ambaye alionekana kama Mwarabu kutokana alivyojibadili kwa sura ya bandia huku akiwa katinga miwani maalum iliyozuia kupigwa picha, uliwafanya hata wasichana wengi waliokuwemo ndani kumkodolea macho na wengine walifikia hatua ya kumuomba kampani. Aliwapuuza wote na kutafuta mahali akapumzika huku akipata kinyaji chake taratibu.
Wakati wote macho yake yalikuwa yakiangaza huku na huko kuona kama kulikuwa na mtu aliyemfahamu. Alipoona hakuna akaamua kujichanganya kwenda kucheza kamari kwenye slot-machines. Alitumia akika kumi hivi kuwazuga watu, alipoona kila mmoja ana hamsini zake, akamwita mhudumu mmoja wa kike na kuomba kuelekezwa mahali kama kulikuwa na huduma ya simu ya kibandani. Alipoelekezwa aliondoka haraka haraka huku akiwa amevaa miwani maalum ambayo ilikuwa na lensi zilizozuia kupigwa picha. Hii ilikuwa ni tahadhali kwake kwa sababu sehemu kama hizi kunakuwepo na watu wengi ambao wengine kazi yao wanaijua vizuri.
“Haloo! Naitwa Kareem Mohammed Jabar, niko katika moja ya nchi za Kiarabu. Nadhani nazungumza na Inspekta Jenerali Alfonso Gonzalez Cardoso?” Dennis alisema kwa kutumia sauti nzito yenye lafudhi ya Kiarabu baada ya kubonyeza namba alizozitaka.
“Ndiye mimi, nikusaidie?” Inspekta Cardoso alijibu huku akiwa na mshangao mkubwa kutokana na mpigaji wa simu hiyo kutumia namba yake ya siri, tena ya nyumbani. Akili yake ilimtuma aamini kwamba huenda kulikuwa na ujumbe wa neema kutoka huko uliomhusu yeye.
“Nimetumwa!.....” kabla Dennis hajamaliza kusema akakatwa kalima.
“Enhe? Umetumwa na nani? Hebu nieleze, akina Abdulkarim wamefanikiwa kumficha Profesa?” aliuliza pupa kwa furaha akijua kwamba lazima mtu huyo atakuwa ni mmoja wa mabosi wake waliokuwa wakimtumia. Bila kujua kwamba alikuwa akifanya kosa kubwa sana, akaendelea. “Halafu kuna habari njema sana, yule bwana mdogo Dennis amekataa kuja kufanya upuuzi kama walivyokuwa wamepanga huku. Amewakatalia. Sasa najaribu kufuatilia watamtuma nani, kisha nitawaeleza. Haloo? Unanisikia?”
“Nakusikia vizuri Inspekta, nafurahi kusikia hivyo na napenda nikuhakikishie kwamba mchango wako ni mkubwa sana kwetu na mwishoni mwa mwaka lazima tukuvishe nishani ya utumishi mtukuka,” Dennis aligundua kwamba mtu aliyekuwa akizungumza naye alikuwa popo, yaani alikuwa msaliti hasa, hivyo aliamua kutumia mbinu za kisanii ili kumchota akili.
“Aloo mtakuwa mmefanya jambo zuri sana, lakini hakikisheni fedha zangu mnaziingiza benki kila mwezi kwenye benki za huko....”
“Usijali, hivi nikumbushe, tulikubaliana kiasi gani kila mwezi?” Dennis aliendelea kumtegea.
“Aah Bwana, si tulikubaliana dola 60,000 kila mwezi? Au wewe hujui?” Inspekta Cardoso alisema kwa kuamini kwamba anazungumza na mhusika mwenyewe.
“Mambo mengi sana ndugu yangu, unajua hawa jamaa wanatutisha kuhusu tishio lao la kutaka kuja kuchunguza kama kuna silaha za maangamizi, tulijua tumeshaokoka katika uchunguzi wa kwanza, sasa wameibuka tena.”
“Nimeshawaambia ondoeni hofu kabisa. Mimi najua kila kitu kinachoendelea kwenye Baraza la Usalama na mipango yao yote, yule bwana mdogo Dennis amekataa katakata, na hizi ni taarifa za faraja, kwa sababu huyu ndiye king’ang’anizi. Jambo la msingi tu ni kuhakikisha mnamficha Profesa na kumwekea ulinzi wa kutosha, halafu yeye aendelee na kazi zake kama kawaida. Lolote litakalotokea huku ntawajulisha.”
Dennis alichanganyikiwa baada ya kusikia kwamba mtendaji mkuu katika idara nyeti kama hiyo, na ambaye alikuwa na uwezo wa kuingia kwenye Baraza la Usalama, ndiye aliyekuwa anawasaliti wenzake. Akatambua kwamba kumbe alifanya jambo la busara kukataa na wote wakaamini kwamba amekataa. Kama angalikubali kazi hiyo ingemuwia vigumu kuifanya hasa kwa kuzingatia kwamba kumbe hata watu wa ndani walikuwa wakishirikiana na maadui. Hasira ilimkaba sana na ili kuonyesha kwamba amekasirika akaapa kufanya kila njia kuhakikisha anaifanya kazi hiyo na kuikamilisha operesheni yote.
“Sasa sikiliza Inspekta, nimetumwa nikwambie kwamba, wiki mbili zijazo tunataka tufanye shambulio kwenye mojawapo ya treni za abiria kama shinikizo la kumtaka Rais Eduardo Heleguera ayaondoe majeshi yake Iraq. Kwa hiyo uwe na taarifa kwamba tukio hili litatokea,” Dennis alisema kwa kumtegea.
“Sawa, hilo tu, mbona halina tatizo lolote. Nadhani hiyo itasaidia sana maana hata wananchi huku wamekuwa wakisumbua kweli kweli lakini rais mwenyewe mpuuzi sana, hataki kusikiliza maoni ya watu, na sisi tumemwachia. Nyie njooni tu... Haloo? Haloo?” Dennis alikuwa amekata simu na kuurudisha mkonga baada ya hasira kumkaba. Alikuwa amekasirika kusikia kwamba mtendaji wa usalama ndiye aliyekuwa kinara wa kuruhusu mambo kama hayo yatokee.
Alichofanya baada ya hapo ni kunyanyua tena mkonga na kupiga namba nyingine. Alisubiri kwa muda na baada ya hapo upande wa pili ukaitikia.
“Haloo, Berlin?” sauti nzito ya upande wa pili ilisema.
“Shambulio la kushtukiza litafanyika wiki mbili kuanzia sasa mjini Madrid, treni ya abiria italipuliwa, fanyeni muwezavyo kuhakikisha kwamba mnazuia shambulio hilo,” Dennis alisema kwa sauti yenye kithembe na kukata simu kabla ya upande wa pili kuuliza swali. Ujumbe ulikuwa umefika na aliamini hawa wasingefanya makosa. Alikuwa amewapigia kikosi maalum mjini Berlin, ambao walishirikiana sana na CIA.
Wakati anaweka mkonga wa simu, mara alishtukia kitu cha baridi kikigusa kisogo chake. Hakuwa na shaka yoyote kwamba huo ulikuwa ni mtutu wa bastola na tayari alikuwa ameingia kwenye mikono ya maadui.
“Karibu rafiki yetu, tulia kama ulivyo na hakikisha hufanyi ujanja wowote, vinginevyo ubongo wako utasambaratika sasa hivi,” sauti kali ilitoka nyuma yake ikimwamuru.
Je, ni nani huyo na anataka nini? Dennis ataokoka kweli? Ungana na msimulizi wako Jumatatu ijayo...
Dennis Geoffrey Mikwambe yuko Dubai akimfuatilia jasusi aliyeasi, Ricardo Suarez Gonzalez, au Ahmed Kaseem Al-Alawy, ambaye anawatumikia watu wengine huko Mashariki ya Kati. Akiwa huko anafuatilia nyendo zao na kunasa mazungumzo ya siri na anapompigia mkuu wa kitengo cha ujasusi cha Hispania anagundua kwamba kumbe naye ni ndumilakuwili, hivyo anampigia mtu mwingine huko Ujerumani. Anapomaliza kukata simu anashtukia akiwekwa chini ya ulinzi. Je, atanusurika? Endelea na simulizi hii....
Kijasho chembamba kilimtoka Dennis bila mwenyewe kujua. Katu hakutegemea kama kama hao wanaharamu wangeweza kumdaka kama kindege namna hiyo. Hata hivyo, hakuwa tayari kuona anakufa kikondoo, ingawa hakutaka kutumia nguvu. Alitamani sana kutumia hila za kijasusi ili aweze kuwakwepa. Taratibu aligeuka umtazama mtu alitemuwekea mtutu wa bastola kisogoni huku akinyenyekea.
“Ndugu yangu, hapa nilipo sina fedha yoyote zaidi ya dola hamsini tu, kama unataka chukua hizo niachie roho yangu,” alisema taratibu akijifanya kuwafananisha hao watu na maharamia ingawa alijua kwamba walikuwa ni watu wa kazi.
“Unafikiri unaongea na mtoto mdogo siyo? Nimekwambia nyoosha mikono juu haraka, hakuna mtu mwenye haja na visenti vyako!” mtu mwingine wa pili alisema kwa sauti nzito.
“Lakini jamani, ni kosa gani ambalo nimelifanya?” Dennis aliendelea kujifanya mjinga akiuliza maswali ili kuvuta muda na pia kubuni mbinu za kuweza kujinasua.
“Hazeem, hapa siyo mahali pa kuzungumzia, na kadiri tunavyozidi kukaa hapa tunachelewesha muda,” mtu huyo wa pili mwenye sauti nzito, ambaye kama mwenzake wote walikuwa Waarabu, alisema.
“Kweli kabisa. Haloo, hebu geuka haraka!” alisema kumwamuru Dennis. Sura yake, ambayo ilionyesha kwamba yeye ni Mwarabu, iliwafanya wachanganyikiwe. Hata hivyo, waliamini kwamba kwa vyovyote anaweza kuwa mtoa habari wa Mataifa ya Magharibi. Hazeem akamwamuru mwenzake amkague Dennis haraka kuangalia kama alikuwa na bastola. Pamoja na utaalamu wao wote walimpekua lakini hawakuweza kuona mahali ilipokuwa bastola. Dennis alikuwa jasusi aliyefuzu mbinu nyingi na hivyo hata uwekaji wake wa silaha ulikuwa wa siri mno kiasi kwamba ilikuwa vigumu kwa mtu asiyekuwa mtaalamu hasa kuweza kugundua mahali alipoificha.
“Aisee hana silaha yoyote!”
“Unasema kweli Haroub?” Hazeem aliuliza kwa mshangao. “Mbona bosi kasema kwa jinsi alivyokuwa akizungumza inaonyesha ni mtu hatari anayejua siri zetu?”
“Ndio ukweli wenyewe, hana silaha...”
“Hiyo siyo sababu, twende naye maskani!” alisema na kumvuta Dennis na umsukuma kupitia mlango wa nyuma. “Nyoosha mikono yako juu. Wewe Haroub wewe wasiliana na bosi mwambie tumemnasa mtu huyo na tunampeleka maskani. Mimi utanikuta nje kwenye gari nakusubiri. Huyu hanishindi!” alisema na kumpiga Dennis teke la kiuno lililompeleka chini.
“Jamani mnaniumiza bure, hivi nimefanya kosa gani?” alisema kwa maumivu makali aliyoyapata baada ya kudondoka chini.
Kabla ya kujibu, Hazeem akamnyanyua kwa kumshika suruali na kumsukuma mbele. “Utajua huko huko, hivi wewe unafikiri ulichokifanya hatukijui?”
***********
Muda mfupi baada ya kupokea simu ya mtu aliyejiita Kareem Mohammed Jabar, Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Hispania, Inspekta Jenerali Alfonso Gonzalez Cardoso alipokea simu nyingine ambayo ilimfanya achanganyikiwe. Hii ilikuwa inatoka mjini Baghdad, ambayo ilikuwa inampa taarifa kwamba wanataka kuteka treni ya abiria.
“Jamani, mbona mnanipa taarifa mara mbili mbili?” aliuliza kwa mshangao.
“Kwani vipi? Mbona ndiyo kwanza taarifa hizi zinakuja kwako?” iliuliza sauti ya upande wa pili.
“Nyie si mmemtuma Kareem Mohammed Jabar, ambaye nimeongea naye hivi punde?”
“Inspekta, unaota au ndyo kwanza unaamka?”
“Hayo ni matusi sasa! Mimi nakwambia nimezungumza na mtu amenipa taarifa hizo, na nikamwambia asiwe na hofu, tena kaniambia kwamba Profesa yuko katika ulinzi mkali....”
“Unajua Inspekta, inaonekana sasa unashindwa kufanya kazi. Tangu lini ukalisiki jina la Kareem Mohammed Jabar kutoka huku? Halafu umeanza lini kupokea taarifa kutoka kwa kila mtu? Sasa kwa taarifa yako ni kwamba, uliyezungumza naye anaweza kuwa kivuli chako, na taarifa ninayokupa ndiyo sahihi. Kuhusu huyo mtu, hakikisha hilo unalifanyia kazi mwenyewe na lisivuruge kabisa operesheni zetu,” sauti ya upande wa pili ilisema na kukata simu.
Inspekta Cardoso aligundua kwamba tayari amechemka. Alibaini kwamba mtu aliyezungumza naye siyo mwenzao. “Lakini mbona mipango yote aliyoniambia ni sawasawa?” alijiuliza bila kupata jibu.
Muda huo huo akanyanyuka na kwenda kwenye telephone monitor kuangalia nambari iliyoingia. Alikuwa ameitega hivyo simu kwa kujua kwamba ndicho kitu ambacho kingemsaidia katika masuala ya kijasusi na karibu majasusi wengi walikuwa na vifaa vya aina hii. Hakupata taabu kujua kwamba simu hiyo ilipigwa kutoka mjini Dubai, na hapo ndipo alipogundua kwamba alikuwa amehujumiwa. Hasira zilimkaba na kuamua kupiga simu kwa mtu wake akimpa namba hiyo ya simu. Mtu huyu hakuwa mwingine bali Ricardo Suarez Gonzalez, au Ahmed Kassim Al-Alawy kama alivyojiita.
Bila kuchelewa alijua namba hiyo ni ya klabu ya usiku iliyokuwa upande wa kaskazini wa mji huo. Akawatuma vijana wake waliokuwa ndani ya ukumbi huo kwenda kumnasa, ambapo haikuwachukua muda wakamkuta akiwa anaendelea kuzungumza na simu.
********
Dennis alikaa kimya huku akiendelea mbele kwa mwendo wa kasi. Alijua kwamba baada ya kufika nje lazima angekuwa peke yake na mtu huyo, kwa sababu, kwa mujibu wa mazungumzo yao, mwenzake alikuwa amerudi ndani kupiga simu.
“Wewe pusi, pinda kushoto kwenye huo mlango,” Hazeem aliamuru. Walipita kwenye chumba kimoja ambacho kwa mbele kilikuwa na mlango mwingine. Kulikuwa kuna ukimya wa aina yake.
Dennis akili ilifanya kazi haraka haraka na kuvua kopia yake ambayo ilidondoka kwa nyuma, yaani katikati yake na yule adui. Akataka kuinama ili aiokote, lakini adui huyo akamuwahi na kumwambia kwamba angeikota mwenyewe.
“Songa mbele, nakuokotea!” Hazeem alisema na kuinama. Hilo lilikuwa kosa kubwa kwake, kwani kitendo bila kuchelewa Dennis alipiga teke aina ya Mai Geli lililompaisha adui yake na kabla hajatua akaruka juu kwa juu na kumpiga na Yoko Geli, teke ambalo lilitua sawia kwenye mbavu na kumsukuma hadi ukutani ambako alijigonga vibaya kabla ya kuanguka chini puuu! Kama furushi la pamba. Hakuwa na uwezo hata wa kufyatua risasi hata moja. Dennis alimkaba kooni kwa mua mpaka alipohakikisha hawezi kuhema tena, akamwachia.
Kwa haraka alimbeba begani huku akichukua bastola ya adui yake na kofia yake iliyokuwa chini, akaufungua mlango huo ambao kwa bahati nzuri ulitokea nyuma ambako hakukuwa na ulinzi wa aina yoyote.
Alipoangaza, akaona geti nalo lilikuwa wazi, akatoka naye na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye gari lililokuwa limeegeshwa huko, ambalo lilikuwa tupu. Alifkiria ampakie kwenye gari, lakini akaona kwamba hiyo itamletea usumbufu. Akaamua kumtupa kwenye bustani moja ya maua iliyokuwa jirani na hapo, kisha yeye akaenda kwenye gari na kwa kutumia funguo malaya, akaingia.
Muda mfupi baada ya kuingia na kulipasha moto gari, Haroub alikuta mbiombio na bila hata simile akafungua mlango akiwa na furaha akidhani kwamba Hazeem ndiye aliyekuwa kwenye usukani. Badala yake akashangaa baada ya kukutana na mtutu wa bastola ukimwelekea kwenye paji la uso. Alitamani ashuke akimbie, lakini nafasi hiyo hakuwa nayo kwa sababu Dennis alikuwa ameifunga milango.
“Haroub, ninapenda uendelee kuishi, lakini utaweza kuishi endapo tu utanipa ushirikiano wa kutosha,” Dennis alisema huku kamkazia macho.
“Kwani imekuwa... Hazeem yuko wapi?” Haroub aliuliza kwa taharuki.
“Haikuhusu, huko aliko unaweza umfuata kama hukunipa ushirikiano,” alisema huku akiikoki bastola. Haroub akajua mtu huyo hakuwa akitania. Alipiga hesabu ya akika tano tu alizowaacha na yeye tayari alikuwa amemuua mwenzake, na hapo ndipo alipogundua kwamba huyo hakuwa mtu wa kawaida.
“Tafadhali ndugu yangu usiniue, mimi sielewi lolote...”
“Unaelewa, niambie ulikuwa unampigia nani simu?”
“Wapi? Kule? Nilikuwa nampigia jamaa yetu, tafadhali, sitaki uniue,” aliomba msamaha. Dennis alishangaa kuona mtu huyu mwenye mwili mkubwa alivyokuwa muoga wa kufa. Akajiuliza watu kama hawa walikuwa wanaingia vipi kwenye kazi ngumu kama hizo. Hata hivyo alijifariji kwamba, kazi yenyewe ilikuwa na fedha nyingi sana, hasa unapokuwa umeifanikisha.
“Sema basi ulikuwa unampigia nani ambaye mnamwita bosi?”
“Hazeem ndiye anamyejua, mimi kanipa namba ya simu nimweleze tayari tumekupata,” Haroub alitumia hila kuficha ukweli.
“Wewe unanitania,” Dennis alisema na kuweka kidole chake kwenye trigger, Haroub alipoachama mdomo kwa woga, yeye akauingia mtutu wa bastola mdomoni na kumwambia; “Umenichelewesha sana, sasa nakuba nafasi ya mwisho vinginevyo nafumua kichwa chako.”
“Ngoja, nitakwambia!” alisema kwa shida huku machozi yakimtoka. Siyo siri, wapo watu wengine ambao wanafurahia sana kuua, lakini inapofika zamu yao huwa ni kitimtim. “Ahmed, tumetumwa na Ahmed tukukamate.”
“Yeye yuko wapi?”
“Yuko Baghdad.”
“Kaenda kumficha Profesa, siyo? Hebu niambie Profesa anaitwa nani?”
“Kwa kweli mimi sijui,” alijitetea Haroub.
“Unaleta ujanja siyo? Haya sasa nakumalizia kama hukunieleza.”
“Kweli sijui, lakini nasikia anaitwa Profesa Hu....” kabla hajamalizia risasi mbili zilipenya na kutua kifuani mwa Haroub. Dennis aliwahi kukwepa na kwa kutumia uzoefu wake akavunja kioo cha mbele na kuserereka hadi chini huku akifyatua risasi kwenda gizani. Kwa mbali alisikia kishindo na sauti ya unyende kwamba tayari alikuwa amemtungua mtu. Hakutaka kupoteza wakati, akaamua kukimbia eneo hilo ambapo mbele kidogo alipata teksi iliyomkimbiza mpaka hotelini kwake.
Lengo lake halikuwa kuendelea kubaki hapo, alikwenda chumbani na kuchukua mkoba wake na kutoka mbio mbio. Aliamini kwamba majira hayo ya saa 7.30 usiku angeweza kubahatisha ndege yoyote kwenda ama Kuwait au hata Iran, kama siyo Iraq kabisa. Hasira zilimkaba baada ya kugundua kwamba baadhi ya wakubwa wa idara nyeti za usalama, ambao ndio wanaopaswa kulinda usalama, wanashirikiana na maadui kufanya maasi.
Hasira zake zilizidi baada ya kufika uwanja wa ndege na kukosa usafiri wakati huo. Aliamini kwamba mji huo haukuwa na usalama kwake, na kadiri alivyokuwa akichelewa kuondoka ndivyo alivyokuwa akichlewesha operesheni yake.
“Samahani dada, hivi hapa hakuna ndege za kukodi?” Dennis alizungumza Kiarabu cha ndani kabisa na msichana mmoja aliyekuwa kwenye ofisi za Emirates.
“Zipo, pesa yako tu.”
“Unaweza kunielekeza, tafadhali?”
“Nenda dirisha la tatu kutoka hapa, lakini ...”
“Lakini nini? Pesa siyo tatizo.”
“Lazima uwe na sababu za msingi.”
“Hilo halina tatizo, nina vielelezo vyote, mimi nataka kwenda Iran,” Dennis alisema na kuelekea kwenye dirisha la tatu. Baada ya kuulizia dirishani, akaambiwa kwamba alikuwa na bahati kwani kuna ndege ambayo ilikuwa iondoke nusu saa baadaye. Alilipa haraka haraka na kupewa risiti.
“Mtakuwa kama sita hivi, lakini inakwenda Baghdad, nadhani unaweza kuunganisha ukiwa huko.”
“Hamna shida, almradi itakuwa imenisogeza,” Dennis alisema na kuelekezwa ilikokuwa ndege hiyo. Akiwa amevaa suti maridadi pamoja na beji ya shirika la hiyari la kushughulika na waathirika wa maafa ya vita, Dennis alipia mlango wa pembeni ambao ulimfanya asikaguliwe, na kila askari aliyemtazama alijikuta akitamani kuzungumza naye. Hii yote ilitokana na beji aliyoivaa pamoja na kuonekana kama Mwarabu mwenzao.
Alipoingia ndani ya ndege akaamua kukaa siti ya nyuma kabisa. Ndani ya ndege kulikuwa na abiria wengine watano, kwa maana hiyo yeye alikamilisha idadi ya abiria waliotakiwa kusafiri. Aliangaza miongoni mwa abiria na mara moyo wake ukaruka paaa! Alikuwa amemuona abiria mwingine ambaye hakutegemea kumuona mahali hapo. Ndiye, alikuwa amemuona Ricardo Suarez Gonzalez, au Ahmed Kaseem Al-Alawy, adui yake namba moja. Gonzalez ndiye aliyeanza kugeuka, kwani alikuwa ameketi viti vya mbele kabisa, na kilichomgeuza ni beji aliyoivaa Dennis. Akatabasamu na kumpungia Dennis mkono, ambapo naye alifanya vivyo hivyo. Ilikuwa ni kawaida kupungiwa mkono kila alikopita, kwani aliheshimika kutokana na beji yake iliyomtambulisha kwamba alikuwa akitoa misaada.
Dennis alikabwa na hasira moyoni mwake, akiamini kwamba Gonzalez ndiye aliyekuwa kikwazo kikubwa. Hata hivyo, aliamini kwamba huyu ndiye angemwezesha kusonga mbele mpaka kukamilisha operesheni yake.
Je, atafanikiwa kweli kuongozwa na Gonzalez? Je, hawezi kushtukiwa? Vipi kuhusu tukio la kuiteka treni? Ungana na msimulizi wako Jumatatu ijayo...
Denis ananasa maongezi ya siri kwa njia ya simu kati ya gaidi Ricardo Gonzalez akipewa agizo la kulipua treni katika jiji la Madrid huko Hispania, ili kuzuia tukio hili Denis anaamua kumpigia simu Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi nchini Hispania Inspekta Jenerali Alfonso Cardoso kumpa taarifa ili afanye chochote kinachowezekana kuzuia.
Katika mshangao wake anagundua, kiongozi huyo muhimu kabisa katika usalama wa dunia ni msaliti yupo upande wa magaidi hivyo anatoa taarifa hiyo Berlin ili chochote kifanyike kuzuia maangamizi! Wakati anaweka mkono wa simu chini anashtukia kitu cha baridi kinamgusa shingoni nyuma yake, ni mdomo wa bastola na anatekwa.
Kwa uwezo wake wa kupambana kijeshi anafanikiwa kujiokoa na kugundua kuwa waliomteka walikuwa wametumwa na mtu aitwaye Ahmed ambaye yupo Baghdad ambako amekwenda kumficha Profesa, Denis hamtambui profesa huyo lakini ni mtu muhimu na ni lazima amfahamu, hivyo anambana mtu aliyemteka ili amtaje lakini kabla hajafanya hivyo, alishambuliwa kwa risasi na kufa! Denis akafanikiwa kuondoka eneo hilo akiwa salama na sasa yupo ndani ya ndege ya kukodi akielekea Baghdad! Cha kushangaza ndani ya ndege hiyo anakutana na mtu hatari aliyekuwa akimsaka tangu Nairobi, Ricardo. Hajui ni kwanini wamekutana na haelewi kama wamekutana kwa bahati mbaya au ni mpango wa mauaji yake.
Je, nini kitatokea? Sasa endelea..............
Denis alikaa kiti cha nyuma mwili wake wote ukitetemeka, halikuwa tegemeo lake kabisa angekutana na mtu hatari, msaliti na gaidi la kimataifa Ricardo Gonzalez ndani ya ndege hiyo ya kukodi, bado alijiuliza maswali mengi kichwani mwake bila kupata majibu, kukutana pale ilikuwa ni ajali au mpango maalum ulioondaliwa! Hakuamini kama ulikuwa mpango kwani hakuna mtu aliyefahamu kwamba alikuwa anaondoka kwenda Baghdad muda huo na kama alikuwa amegundulika basi watu aliokuwa akipambana nao hawakuwa wa mchezo hata kidogo!Macho yake yote mawili yalikuwa yameangalia mbele, mara chache kupitia kwenye kona ya jicho lake la kushoto alikuwa akimwangalia Ricardo aliyejifanya hana habari naye.
“Nina uhakika ni yeye na kama ni yeye simwachii, tukishuka tu Baghdad lazima nimbane ikiwezekana nimteke na kumpeleka mahali fulani ambako atanieleza kila kitu juu ya mtandao wake, huyu ni mtu hatari sana, kama anaweza kuwasiliana na Inspeckta Alfonso Cardoso mtu ambaye aliheshimika katika Umoja wa Mataifa? Ndio maana amani ya dunia ni ngumu sana kupatikana na mimi nitaushangaza ulimwengu pale nitakapothibitisha kuwa Inspekta Cardoso ni mmoja wa magaidi hatari duniani!” Aliwaza Denis huku akimwangalia adui yake.
Nusu saa wakiwa angani alimwona Ricardo Gonzalez akinyanyuka kwenye kitu chake na kuanza kutembea kurudi nyuma, alifikiri labda alikuwa akielekea msalani lakini alishangaa kuona anapunguza mwendo alipokifikia kiti chake na kukata kona, akaketi pembeni mwa Denis! Uso wa gaidi huyo ulijaa tabasamu lililomfanya Denis pia akenue meno yake kuonyesha tabasamu pia!
“Bwana Denis, haukutaka kabisa kunielewa nilipokuonya Nairobi sio?”
“Nilikuelewa!”
“Sasa mbona unanifuatilia?”
“Hapana sio hivyo! Nipo katika shughuli zangu binafsi!”
“Wewe si ndiye ulipiga simu hotelini na kujitambulisha kwa jina la Bw.Ussi?”:
“Sio kweli!” Denis alikanusha.
“Sasa utanieleza ukweli, maana mara ya kwanza nilikufuata kirafiki lakini ukaniona sina akili!”
“Sio hivyo, nimekwishakueleza kwamba niko katika shughuli zangu binafsi lakini hutaki kuelewa! Ina maana baada ya wewe kunipa onyo, sitakiwi kusafiri sehemu yoyote duniani?”
“Usibishane na mimi wala usijibu kwa ukali, Denis nina uhakika kabisa hauelewi vizuri mtandao wangu! Sasa kiburi chako kimekuponza, nilikuonya kama mtu ninayemheshimu lakini hukunielewa sasa shauri yako!......” Aliongea Ricardo kisha kunyanyuka kitini na kurudi mahali alipokuwa amekaa awali akimwacha Denis akidundwa na moyo kwa nguvu bila kuelewa siri zake zilivuja vipi, kwa jinsi alivyoachwa hakuwa na shaka kuwa abiria wote walikuwa ndani ya ndege hiyo kila mmoja alikuwa na safari yake, aliyafuta mawazo aliyokuwa nayo kichwani kwamba huenda watu wote ndani ya ndege hiyo walikuwa magaidi.
Ndege iliendelea na safari yake, masaa mawili baadaye taratibu ilianza kushuka na hatimaye ikatua katika uwanja wa ndege wa Nabeer, ndege iliposimama kabisa Denis alinyanyuka kitini mwake akasimama wima na kuchukua begi lake lililokuwa juu sehemu ya kutunzia mizigo kisha kuketi tena kitini mwake! Hakutaka kushuka mapema ili Ricardo Gonzalez atangulie na yeye amfuatilie nyuma ili gari atakaloingia alifuatilie mpaka aelewe mahali alipokuwa anafikia katika katika Jiji la Baghdad ili iwe rahisi kwake baadaye kumteka na kumpeleka mahali atakapokuwa amechagua, baada ya kulisoma vizuri jiji hilo na kumtesa ili atoboe siri ya mtandao wake hatari ulioisumbua dunia.
Hicho ndicho kitu alichokihitaji Denis lakini alielewa wazi kuwa kushughulika na mtu kama Ricardo, gaidi mzoefu haikuwa kazi rahisi! Hakuwa na uhakika kama zoezi lake lingeisha kwa usalama, hakuogopa wala hakusita pamoja na kuwa na hofu kidogo moyoni ilikuwa ni lazima apambane kwa faida ya dunia nzima.
Akiwa bado amekaa kitini alishangaa kuwaona abiria wote ndani ya ndege hiyo isipokuwa Ricardo wakitoa bastola kwenye makoti yao na kumlenga yeye!Mwili wa Denis ulitetemeka, mipango yote aliyokuwa nayo kichwani mwake ilifutika akagundua tayari alikuwa katika hatari kubwa, akiwa mbali na nyumbani kwao! Nchi ya Waarabu ambako hakutegemea kupata msaada wowote kunusuru maisha yake ukizingatia hata viongozi wake wa kazi hawakuelewa mahali alipokuwa.
“Uko chini ya ulinzi, tulia kama ulivyo na tunaomba utukabidhi silaha yoyote uliyonayo!”
Denis hakuwa mbishi, alielewa wazi mahali alipokuwa hapakuwa pa kuchezea wala kuleta mzaha! Aliingiza mkono wake wa kuume kwenye koti na kuuzungusha mgongoni na kutoa bastola yake ndogo aina ya SD120, Striker iliyotengenezwa Uingereza maalum kwa ajili ya Wapelelezi wa Kimataifa ili waweze kupita katika viwanja vya ndege bila kugundulika.
“Una nyingine?”
“Hapana!”
“Lete begi!”
Denis alikabidhi begi lake pia na likaanza kupekuliwa, hakuna silaha iliyogundulika ndani yake! Hapohapo mmoja wa majambazi hao alimsogelea na kumfunga mikono na miguu pamoja, kisha kitambaa cheusi kikafungwa kichwani mwake!
“Sasa sikiliza, hutakiwi kupiga kelele wala kusema chochote kuanzia muda huu! Na unatakiwa kutii kila amri tutakayokupa, unasikia?” Alisema Ricardo.
“Nasikia!”
“Waambie waiingize hiyo gari ndani!” Ricardo alimweleza mmoja wa watu aliokuwa nao, muda mfupi baadaye mtu huyo akawa anaongea kwa simu akijaribu kumwelekeza mtu mwingine aliyekuwa nje ya uwanja mahali ndege ilipokuwa! Denis alikuwa amekata tamaa kabisa na kuamini kifo chake kilikuwa kimefika, hakuwa na njia yoyote ya kujiokoa. Kwa mara ya kwanza tangu aanze kazi ya Upelelezi aligundua alikuwa amefanya makosa kuingia kazini bila kuwataarifu Wakuu wake wa kazi.
“Wangekuwa na habari lazima kungekuwa na watu wanaofuatilia na lazima ningeokolewa, lakini hivi sasa...!” Aliwaza Denis kabla hajamaliza sentensi yake kichwani aliamriwa kusimama, gari lilikuwa chini.
Alibebwa juujuu na kuteremshwa hadi mahali gari lilipokuwa, akatupiwa ndani yake kama mzigo na sekunde chache baadaye gari liliondoka kwa kasi likipiga kingora kama ambavyo magari ya wagonjwa hufanya! Sauti ya Ricardo ilisikika kiti cha mbele kabisa akihimiza dereva aendeshe gari kwa mwendo wa kasi zaidi.
Hakuelewa alipokuwa anapelekwa, hakuwa na uhakika alikuwa akielekea Kaskazini, Kusini, Mashariki ama Magharibi! Kilikuwa ni kitendawili ambacho kwa hakika kuteguliwa kwake siku hiyo ilikuwa ni kifo chake. Ni kiarabu tu kilichotawala ndani ya gari, kuanzia kwa dereva mpaka kwa Ricardo ambaye kiasili hakuwa Muarabu, Denis hakuambua kitu katika maongezi yao.
Dakika chache baadaye gari lilipunguza mwendo na kukata kona kulia, halikusonga zaidi likasimama kabisa mahali ambako kwa masikio na hisia zake Denis aliposikia vyuma vikilia mbele alielewa ni lango lilikuwa likifunguliwa, gari lilisonga mbele tena kidogo na kusimama kisha kuzimwa kabisa.
Milango ya nyuma ya gari ilifunguliwa na Denis akabebwa juujuu na kutolewa hadi nje na akaendelea kubebwa hivyo hivyo kwa dakika nyingine mbili zaidi! Ingawa alikuwa haoni sababu ya kufungwa na kitambaa cheusi usoni alielewa alikuwa akiingizwa ndani ya nyumba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
“Mkalisheni hapo chini!”Sauti iliamuru na Denis aliielewa sauti hiyo ilikuwa ya Ricardo.
Hakukalishwa kama ilivyoamriwa bali alitupwa chini na kuanguka sakafuni, kwa sababu ya mazoezi makali aliyopitia hakulia wala kupiga kelele yoyote! Denis alikuwa kimya kabisa, tangu waondoke uwanja wa ndege alikuwa hajaongea chochote.
“Mfungueni kamba kisha mvueni nguo zote, halafu mfungeni kwenye hicho kiti cha kuzunguka! Nataka kuongea naye ili anieleze vizuri kwanini ananifuatafuata wakati nilishamwonya aachane na sisi!” Aliendelea kuamuru Ricardo na kweli Denis katika muda wa sekunde ishirini akawa amevulishwa nguo zote na kubaki kama alivyozaliwa. Hakuweza kufanya lolote kujizuia kwa sababu hakuwa na uwezo wa kupambana nao, alishanyoosha mikono na kuwa na uhakika kabisa kifo kilikuwa mali yake siku hiyo.
Kiti alichokalishwa juu yake kilikuwa cha chuma na mikono na miguu yake pamoja na tumbo vilifungwa tena kwenye kiti hicho, Ricardo akaamuru afunguliwe kitambaa usoni ili waangaliane macho kwa macho! Denis aliogopa alipowaona watu waliosimama mbele yake, wote walikuwa na bunduki midomo ya bunduki hizo yote imemwelekea yeye.
“Rafiki yangu utakufa vibaya sana, sikutanii mimi ni mtu mbaya kuliko unavyoniona! Kwa niliyoyafanya Nairobi ulikuwa ni uungwana tu lakini kwa sababu hukutaka kunielewa sasa ninakumaliza ili uache sisi tuendelee na kazi yetu ya kuiporomosha Marekani, kisifa, kiuchumi na kisiasa! Na hilo litawezekana tu, mpaka Rais Caesar Leon pamoja na waziri Mkuu wa Uingereza Dick Johnson waondoke, Rais wa Irak Suleiman al-Mahamoud aachiwe huru, majeshi ya nchi za Magharibi yaondoke Irak! Hayo ndiyo malengo yetu ndio maana tuko kazini, hatufanyi kazi hivihivi bali tunashirikiana na watu ndani ya Umoja wa Mataifa! Sasa nakuomba usali sala yako ya mwisho kabla sijaamuru vijana wausambaratishe mwili wako kwa risasi!” Aliongea Ricardo kwa ukali.
“Nitasali vipi wakati mmenifunga mikono?”
“Wewe sali bwana acha kututania na kama hutaki basi shauri lako....... vijana kaeni tayari nikisema fyatua, basi fanyeni hivyo ili tuendelee na kazi nyingine!”
“Sawa bosi!” Vijana hao waliitikia kwa pamoja na kurudi kinyumenyume kama hatua mbili, wakamlenga Denis kwa bastola zao! Kwa woga alifumba macho na kuutayarisha mwili wake kwa risasi akisubiri kusikia neno fyatua! Hakuwa na namna ya kujiokoa, alikuwa kwenye mlango wa kuingia Kuzimu! Aliikumbuka Tanzania na viongozi wake wa kazi.
“Laiti ningejua ningewashirikisha, hakuna mtu atakayejua nimefia huku na wala maiti yangu haitaonekana!” Aliwaza Denis chumba kikiwa kimya, vijana wa Ricardo walikuwa wakisubiri agizo tu ili watekeleze kazi ya kumsambaratisha Denis.
“Fya...!” Ilikuwa ni sauti ya Ricardo akiamuru risasi zianze kumiminwa, hakuweza kuikamilisha sentensi yake, alishuhudia vijana wake wote wakianguka chini na milio ya risasi ikisikika chumba kizima! Alishindwa kuelewa ni nini kilikuwa kimetokea.
Ricardo alielewa ni hatari na wakati akijaribu kuingiza mkono kwenye koti lake kutoa bastola, alishangaa kusikia maumivu kwenye bega! Risasi mbili tayari zilishapenya, alikuwa na uhakika mtu aliyekuwa akitumia bunduki hiyo ni mzoefu na mwenye shabaha kupita kiasi.
Denis alibaki mdomo wazi, hakuelewa kabisa ni kitu gani kilichotokea, alibaki akijiuliza ni nani aliyekuwa akimimina risasi kiasi hicho! Kwani hakumfahamu mtu katika nchi ya Irak ambaye angeweza kumwokoa kutoka mdomoni mwa kifo.
Aliangaza macho yake huku na kule bila kumwona mtu, bila kutegemea alimwona msichana mrembo akiruka kupitia dirishani! Denis hakuamini, ilikuwa ni kama ndoto kwake.
“Lucille!” Aliita kwa mshangao, alikuwa msichana aliyemwacha hotelini Nairobi! Hakutaka kukubali kuwa msichana aliyefanya naye ngono hotelini naye alikuwa mpelelezi, alishuhudia akimmiminia Ricardo risasi kadhaa kisha kumsogelea akampekua na kumnyang’anya bastola yake.
“Ni wewe? Umefikaje Baghdad na umejiingizaje katika suala hili?” Aliuliza Denis huku akishuhudia Lucille akimfungua kamba zilizomfunga mwilini.
“Tutaongea baadaye kwa sasa tufanye kazi kwanza!” Alijibu msichana huyo.
Alipokuwa Denis kabla hata ya kuvaa nguo zake aliruka na kuchukua bastola mbili kati ya zilizokuwa zimedoshwa na vijana wa Ricardo, kwa hasira akawamiminia risasi wote kuhakikisha wamekufa kabisa.
“Ahsante Lucille!”
“Ahsante kushukuru! Kinafuata nini?” Lucille alijibu.
“Huyu tuondoke naye kwenda mahali pengine, tumtese mpaka atueleze watu anaoshirikiana nao na mahali zilipofichwa silaha za maangamizi! Nakushukuru sana umeifanya kazi kuwa rahisi! Nilishakata tamaa kabisa, nilijua nakufa na bila wewe sasa hivi ningekuwa marehemu! Sijui nikulipe nini?”
“Usijali!”
Kwa kamba alizogunguliwa Denis walimfunga Ricardo aliyekuwa hoi bin taabani kwa maumivu na Denis kumbeba juujuu akikimbia huku Lucille akilinda kwa nyuma na bunduki mbili mkononi hadi nje ambako walimpakia katika gari alilokuja nalo Lucille, Denis alipoisoma ubavuni iliandikwa UNHCR! Alibaki mdomo wazi.
Waliondoka kwa kasi kurudi mjini.
Je, nini kitatokea? Ricardo atakubali kutoboa siri zote? Fuatilia wiki ijayo.
Akiwa katika shughuli nzito ya kufuatilia silaha za maangamizi bila kuwataarifu wakuu wake wa kazi, Denis anatekwa na magaidi wanaoongozwa na Ricardo Gonzalez na kupelekwa katika jengo moja nje kidogo ya jiji la Baghdad, hana matumaini ya kuokolewa kwani anaamini hakuna mtu mwenye taarifa juu ya kuwepo kwake katika nchi hiyo.
Magaidi walipomfikisha katika jengo hilo walimtangazia moja kwa moja nia yao ya kumuua na Ricardo anawaamuru vijana wake wamsambaze Denis kwa risasi lakini kabla hawajafanya hivyo, majambazi ndio wanaanguka chini baada ya kupigwa risasi, Ricardo pia anashambuliwa alipojaribu kuchomoa bastola yake! Denis haelewi ni nani amefanya kitendo hicho lakini alipoangalia vizuri akamwona msichana, Lucille aliyekuwa naye Nairobi.
Je, nini kinaendelea?Fuatilia........
Lucille alikuwa miongoni mwa wanawake wapelelezi hatari duniani, aliyetegemewa kwa kiasi kikubwa na shirika la ujasusi la Marekani CIA. Alikuwa raia wa Kenya aliyesoma na kufanya kazi Marekani kwa kipindi kirefu ni huko ndiko alikopewa kazi hii! Alitumika katika upelelezi hatari peke yake hasa uliohusisha kugundua siri kutoka kwa watu hatari.
Alikuwa mwanamke mrembo mwenye kila aina ya sifa, hakuna mwanaume angekutana na Lucille na kumpita bila kugeuza shingo! Alikuwa na weusi wa metaliki, umbile la namba nane, usafiri wa uhakika, tabasamu la kuvutia na vishimo kwenye mashavu kila alipocheka! Zaidi ya sifa hizo zote alikuwa na mwanya, alizaliwa miaka thelathini na mbili iliyopita nchini Kenya akiitwa Lightness Mungai lakini alibadili jina hilo alipojiunga na mambo ya kijasusi.
Alishafanya kazi nchini Urusi wakati ule wa shirikisho la Urusi, Bosinia Herzgovina na Panama ni yeye aliyetumwa kwenda kuchunguza kujishirikisha kwa Rais wa nchi hiyo, Noriega na dawa za kulevya!Baada ya shughuli hizo zote alikwenda Afrika Kusini akiwa na cheti cha Mambo ya Utawala wa hoteli na kuajiriwa katika hoteli ya Hilton ili aweze kupeleleza mambo ya watu hatari walifikia katika hoteli hiyo.
Alifanya kazi hiyo kwa uaminifu na kupata mafanikio makubwa, alipigiwa simu na kutakiwa kuripoti katika hoteli ya Hilton Nairobi siku moja kabla Denis hajatakiwa kufika Nairobi, Lucille hakupelekwa nchini Kenya kuendelea na kazi ya hoteli bali alitakiwa kuungana na Denis kwenda Irak kuchunguza silaha za maangamizi kama zilikuwepo au la! Lakini alifikia katika hoteli hiyo kama mfanyakazi mpya.
Denis alipofika siku iliyofuata ni Lucille aliyempokea hotelini hapo akijifanya ni mtu wa mapokezi, baadaye alitaarifiwa na wakuu wake wa kazi kwamba Denis alikuwa amekataa kazi aliyokuwa amepewa na kutakiwa kumchunguza kama alikuwa ameisaliti kazi yake ya upelelezi na kununuliwa na upande wa maadui.
Ilibidi Lucille ajifanye kuwa katika mapenzi mazito na Denis, kwa uzuri aliokuwa nao mwanaume huyo hakuweza kustahilimi na kujikuta anaingia katika mtego na kulala naye usiku mzima chumbani kwake, ni kati usiku huo ndipo Lucille alifanikiwa kutega vifaa vyake vya mawasiliano na kunasa mahali popote mtu alipokuwa kama vile simu za mkononi zionyeshavo.
Aligundua baadaye kuwa Denis alikuwa na mpango wa kusafiri kwenda Muscat kumfuatilia mtu aliyeitwa Ricardo Gonzalez, alitoa taarifa hiyo kwa wakuu wake wa kazi na kutakiwa kumfuatilia akiwa chini ya kivuli cha shirika la kushughulikia wakimbizi, UNHCR.
Kwa ndege ya shirika hilo Lucille aliondoka Nairobi na kuwasili Muscat ambako aliendelea kumfuatilia Denis taratibu kila alikokwenda, akifanya kila kitu kwa uangalifu bila kugundulika hata Denis alipovamiwa akiwa chumbani kwake na baadaye kujiokoa, Lucille alikuwa na taarifa lakini kabla hajafanya lolote Denis aliondoka kwa ndege ya kukodi kuelekea Baghdad
Alimfuatilia kwa ndege aliyoondoka nayo Nairobi na kutua uwanja wa ndege wa Nabeer nusu saa kabla ndege aliyopanda Denis haijatua, hakushuka ndani ya ndege bali alitoa taarifa kwa wakuu wake wa kazi na kupewa watu wa kumsaidia waliofika uwanjani hapo na gari lao wakijifanya watu wa shirika la kusaidia wakimbizi na kumtaarifu Lucille kuwa walikuwepo nje ya uwanja wakimsubiri.
Ndege iliyombeba ilitua uwanjani katika muda uliopangwa, Lucille alishuhudia Denis akishushwa ndani ya ndege akiwa chini ya ulinzi mkali, alielewa tayari alikuwa ameingia mikononi mwa maadui na lilikuwa jukumu lake kumuokoa! Hakutaka kufanya ajizi mara moja alishuka kwenye ndege haraka na kuanza kukimbia kwenda nje ambako alijitambulisha kwa watu waliokuwa wakimsumbiri na kuwaeleza kazi iliyokuwa mbele yao.
“Tupo tayari!” Walimjibu.
“Kuna mlango mwingine wa magari kutoka uwanjani?”
“Hapana ni mmoja tu!”
“Uko wapi?”
“Ule pale!”
“Basi kuna gari moja aina ya Rangerover nyeusi litatoka uwanjani sasa hivi, jiandaeni tulifuate humo ndimo mtu ninayemfuata amebebwa tena akiwa chini ya mtutu wa bunduki!”
“Akinanani wamemteka?”
“Sijaelewa bado ila tutafahamu baada ya muda mfupi!”
“Naitwa Abdul! Huyu hapa ni Rasheed, Ramadhan na Rahman!” Mmoja wa vijana wa Kiarabu wenye misuli aliokutana nao nje ya uwanja wa ndege alijitambulisha kisha kuwatambulisha aliokuwa nao ndani ya gari.
“Naitwa Lucille!”
“Tunafurahi kukufahamu!”
“Ondoa gari!Ifuate ile Rangerover nyeusi, wote tayarisheni silaha zenu! Tumekwishaingia kazini, muwe wanaume wa shoka hawa watu tunaoshughulika nao si wa mchezo!”
“Usiwe na wasiwasi mkuu tunajiamini!”
Gari lao liliondoka likifuata Rangerover waliyoonyeshwa hadi nje kidogo ya jiji la Baghdad ambako walishuhudia gari hilo likikata kulia na baadaye kuingia kwenye ngome kubwa ambayo mbele yake iliandikwa WFP,ilikuwa ni ngome ya shirika la mpango wa chakula duniani. Lucille alishauri gari liegeshwe nje ya ngome hiyo na watafute namna ya kuingia ndani na kufanya mashambulizi.
“Hapana!” Kijana mmoja alikataa na waliendelea kujadiliana kwa karibu dakika kumi na tano nzima, Lucille akiwa amekataa kabisa kuingia na gari akidai lilikuwa jambo hatari.
“Sasa tufanyaje?”
“Hili ni gari la Shirika la Msaada kwa wakimbizi, nafikiri tunaweza kuingia ndani ya ngome hii bila wasiwasi wowote! Tena huwa tunakuja hapa mara kwa mara”
“Oh, yes! Nilikuwa nimesahau, endesha gari mpaka getini!”Alisema Lucille aliyekuwa amesahau kabisa kama gari alilopanda ni la UNCHR.
Walikubaliana na gari likaendeshwa hadi langoni ambako kabla ya kupiga honi Lucille aliwashauri vijana wote waliokuwa ndani ya gari washuke yeye aendeshe gari mpaka ndani ili kama kungetokea hali yoyote ya kuzidiwa na maadui wavamie kwenda kumsaidia, hapo wote walikubaliana na kushuka! Lucille akapiga honi na lango likafunguliwa na walinzi wenye bunduki mkononi.
Hakutaka kuruhusu maswali aliendesha gari kwenda mbele na kuegesha, akashuka haraka na kuanza kutembea bila kuelewa ni jengo gani kati ya mawili yaliyokuwemo ndani yake alitakiwa kuingia na kujaribu kumwokoa Denis.
“Psiiii!” Ilibidi amwite mmoja kati ya walinzi waliokuwepo langoni, alishangaa ni kwanini hawakumtilia mashaka lakini alihisi ni sababu ya aina ya gari aliloingia nalo
“Naweza kufanya lolote?” mlinzi aliuliza
“Ndiyo! Unaweza kunionyesha mahali walipoingia?”
“Kwenye lile jengo dogo!”
“Ahsante!” Alishukuru Lucille na kuanza kutembea kuelekea kwenye jengo dogo lililojengwa kwa mbao,alifanikiwa kugundua dirisha moja lilikuwa wazi na kusogea hadi mahali hapo, akatupa macho yake ndani na kushuhudia Denis akiwa amefungwa kwenye kiti na watu watano wakiwa wamenyoosha bunduki zao tayari kumlipua! Hakuona sababu ya kupoteza muda, alijikunja vizuri na kuanza kufyatua risasi kabla wao hawajafanya kitendo hicho! Wote wakaanguka chini na mmoja tu akabaki wima, alikuwa Ricardo Gonzalez kabla hajachomoa bastola yake Lucille alimuwahi na kumtandika risasi begani akatulia.
Kwa kupitia dirishani aliingia hadi ndani, Denis hakuamini macho yake kugundua mwanamke aliyefanya naye ngono jijini Nairobi ndiye aliyemwokoa. Alifunguliwa kamba zilizomfunga na zikatumika kumfunga Ricardo, kabla ya kutoka Lucille alichungulia kupitia dirishani kwa mbali aliwalenga walinzi wawili waliokuwepo langoni, wakaanguka chini na kufa!
Walichofanya baada ya hapo ni Denis kuvaa nguo zake kisha kumbeba Ricardo na kutembea naye hadi kwenye gari, wakampakia na kuondoka zao! Nje Denis alishuhudia vijana wengine wakipanda garini, alichomoa bastola yake tayari kupambana akiamini walikuwa ni magaidi.
“Acha!Acha!Acha Denis!”
“Hawa ni akina nani?”
“Ni wenzetu!”
Lucille alimpisha dereva kwenye usukani na gari likaondoka kwa kasi hadi makao makuu ya shirika la kuhudumia wakimbizi jijini Baghdad ambako gari liliingizwa ndani na Ricardo kushushwa haraka kupelekwa katika moja ya ofisi ambako mahojiano yalianza, hakuwa tayari kutoboa siri pamoja na mateso yote aliyopewa! Kubanwa sehemu za siri hata kuchomwa moto mwilini mwake, kila mtu aliamini Ricardo alikuwa gaidi!
“Ipo njia anaweza kusema!” Denis alishauri.
“Njia gani?”
“Nusu kaputi!”
“Kweli eh?”
“Tukishamlewesha kwa dawa hiyo halafu tukaanza kumhoji atasema kila kitu! Vinginevyo tutakesha!”
“Nyie vijana tutapata wapi nusu kaputi?”
“Labda tukanunue hospitalini!”
“Fanyeni hivyo haraka hatuna muda wa kupoteza, tunataka tuikamilishe kazi hii leo!” Lucille aliamuru na vijana hao walitii ingawa ilikuwa ni mara ya kwanza kufanya kazi na Lucille pamoja na Denis, waliagizwa kutoa kila aina ya ushirikiano uliohitajika.
“Sawa mkuu!” Walijibu na kuondoka, waliporejea dakika ishirini na tano baadaye waliongozana na daktari akiwa na dawa ya nusu kaputi iliyoitwa Ethyl Chloride na kumvutisha Ricardo puani, haikuchukua muda mrefu tayari akawa amelewa ndipo msururu wa maswali ukaanza.
“Bwana Ricardo!”
“Na..am!” Aliitika bila ubishi.
“Wewe ni nani?”
“Kwanini una..taka ku..jua?”
“Ni vizuri tukakufahamu? Una uhusiano gani na Alfonso Cardoso?”
“Ni rafiki yangu!”
“Anafanya kazi wapi?”
“Ni Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi nchini Hispania!”
“Dunia inazitafuta silaha za maangamizi, je unafahamu zilipo?”
“Silaha.....silaha.....silaha, zilihamishwa muda mfupi kabla Majeshi ya Marekani hayajaingia Baghdad!”
“Ziko wapi?”
“Zilikuwa njiani kupelekwa Syria lakini mpaka ukafungwa, baada ya nchi hiyo kutishwa na Marekani, hivyo zikachimbiwa hapohapo mpakani!”
“Nani anazitengeneza?”
“Profesa Ludovic Cheznob!”
“Huyu ni nani?”
“Ni mtaalamu wa silaha za maangamizi aliyesoma Marekani lakini ni raia wa Urusi!”
“Hivi sasa yuko wapi?”
“Amefichwa kwenye handaki sehemu iitwayo Nasbir huko huko mpakani akiendelea kutengeneza silaha nyingine zaidi!”
“Kwa hiyo sio kweli kuwa silaha za maangamizi hazikuwepo Irak?”
“Dunia ilidanganywa!”
“Mnashirikiana na nani ndani ya Umoja wa Mataifa?”
“Ni Alfonso Cardoso peke yake!”
“Analipwa na nani?”
“Al-qaeda!”
“Ahsante kwa ushirikiano ulioutoa!” Denis alisema huku akicheka na kuwageukia vijana wa Kiarabu waliopewa kuwasaidia, aliwauliza kama walifahamu eneo lililotajwa!
“Ndio tunapafahamu lakini hali ni mbaya sana huko, eneo hilo linalindwa na watu wanaomtii Rais aliyekamatwa na Marekani! Sina uhakika kama tutafanikiwa kurudi salama!”
“Unaogopa?”
“Sio hivyo nilikuwa natoa tahadhari!”
“Tuelekeze sisi tutakwenda!” Lucille aliongea na vijana hao walianza kuwachorea ramani kuonyesha mahali eneo lililodaiwa kuwa na handaki lenye silaha za maangamizi lilipokuwa.
“Twende zetu Lucille!” Alisema Denis.
“Poa!”
Je, watafanikiwa? Fuatilia sehemu ya mwisho wiki ijayo.
Baada ya ramani kuchorwa ilikabidhiwa kwa Denis na Lucille wote wakaiweka mezani na kuanza kuiangalia, walitakiwa kusafiri umbali wa kilometa mia nane na hamsini mpaka kufikia mahali kijiji cha Nasbir ambalo silaha zilichimbiwa na huko ndiko Profesa Ludovic Cheznob alikokuwa amejificha akiendelea kutengeneza silaha zaidi za maangamizi, alikuwa ni mtu hatari pamoja na silaha alizozitengeneza ambazo zingeweza kuiteketeza kabisa dunia hivyo ilikuwa ni lazima akamatwe na wote waliojihusisha na mpango huo wafikishwe mbele ya sheria akiwemo Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi la Hispania, Inspekta Alfonso Cardoso, mtu aliyeaminiwa sana na Umoja wa Mataifa lakini kumbe alikuwa ni nyoka mwenye sumu kali.
“Lazima twende! Kazi iliyobaki ni ndogo sana inahitaji ujasiri tu!Alisema Dennis huku gaidi Ricardo Gonzalez akiwa amelala usingizini mbele yao.
“Kweli kabisa!” Lucille aliitikia.
“Na huyu tumfanye nini sasa?”Aliuliza Dennis.
“Unaonaje kama tungemkabidhi mikononi mwa majeshi ya Marekani!”
“Hapana!”
“Kwanini?”
“Sitaki kabisa mtu aelewe kuwa niko kwenye operesheni hii kwani niliikataa tangu mwanzo, nataka kuweka historia kuwa ninaweza kupeleleza jambo mwenyewe bila msaada wa Marekani au Umoja wa Mataifa na nikalifikisha mwisho tena kwa mafanikio makubwa!Alisema Dennis.
“Nakuelewa lakini kwa hapa tulipofikia haiwezekani tena kufanya peke yetu, tutauawa kabla hatujamaliza kazi yenyewe! Nakushauri Denis, kubali tuujulishe Umoja wa Mataifa ili tupatiwe msaada zaidi, isitoshe mimi nilitumwa na wao kwa hiyo sioni sababu ya kwanini tusiwataarifu!”
Denis alinyamaza kwa muda wa kama dakika tano akijaribu kutafakari juu ya ushauri aliopewa na Lucille, upande mmoja wa akili yake ulikubali lakini mwingine uligoma kabisa! Hakutaka kushirikisha umoja wa Mataifa wala Marekani akiamini lazima kungekuwa na watu wa kusaliti na hivyo kuyaweka maisha yake katika hatari zaidi kabla hajaikamlisha kazi! Alimweleza tena Lucille msimamo wake, lakini bado waliendelea kutofautiana hatimaye kukasirishana kabisa.
“Nimekwishasema sitaki Umoja wa Mataifa wala Marekani washirikishwe, kama hutaki kunielewa basi kila mtu achukue njia yake mwenyewe, wewe si ni mpelelezi vilevile kila mtu aende kivyake ili mradi tumekwishapaelewa Nasbir!”Aliongea Denis, picha ilikuwa wazi kabisa kwamba watu hao walishahitilafiana vya kutosha na hapakuwa na namna wangeweza kufanya kazi pamoja tena.
“Sawa ila najau lazima utauawa Denis!”
“Hilo sio tatizo kwangu, nilichagua kifo nilipochagua kazi hii, kifo huwa hakinitishi na hakimtishi mpelelezi mwingine yeyote wa ngazi yangu! Kwaheri! Alimaliza Denis na kuanza kuondoka akirudi kinyumenyume kuingia kwenye gari la UNHCR walilokuwa wakitumia, akiwa ndani ya gari alimwita mmoja wa vijana wa Kiarabu waliopewa kuwasaidia na kumwomba waende pamoja kwenye ofisi za UNCHR mjini Baghdadi ambako alijaza mafuta tenki nzina kuondoka peke yake ndani ya gari, akiwa amebaba silaha zote muhimu kwa kazi iliyokuwa mbele yake.
Hakuna mtu aliyeamini kuwa Denis angefanikiwa kufika alikokuwa anakwenda kwani huko ndiko kulikokuwa na mapigano makali zaidi, kijana wa kiarabu waliyeondoka naye kwenda kujaza mafuta alijaribu kumshauri kadri uwezo wake asiende lakini hakukubali! Denis alikuwa amedhamiria kuikamilisha hiyo yenye mwenyewe bila msaada wa mtu.
Baada ya Denis kuondoka Lucille aliwasiliana na ofisi za Umoja wa Mataifa moja kwa moja nchini Marekani kwani zile za Baghdad zilishalipuliwa na mabomu, aliwataarifu kial kitu juu ya kazi yake na namna alivyokutana na Denis na kumwokoa akiwa katika hatari ya kufa lakini aliwasikitisha zaidi alipowaeleza yeye na Denis walikuwa wamehitilafiana ikiwa ni namna ya kufanya kazi.
“Kwa hiyo Denis yuko wapi?”
“Ameondoka!”
“Kwenda wapi?”
“Nasbir!”
“Kaondoka na nani?”
“Peke yake!”
“Wewe una mpango gani?”
“nataka kwenda hukohuko Nasbir lakini si kwa njia ya nchi kavu, nahitaji helkopta!”
“Uko wapi hivi sasa?”
“Niko Baghdad, ninaye gaidi Ricardo Gonzalez, bado yupo usingizini!”
“Tunatuma helkopta ya Kijeshi utamkabidhi Ricardo kwa wanajeshi wa Kimarekani watakaokuja na watakuchukua wewe hadi Nasbir!”
“Ninahitaji kuongezewa nguvu! Kwa ninavyosikia hali yuko ni mbaya sana!”
“”Tumekwishawasiliana na serikali ya Marekani na Uingereza juu ya hilo, utapewa makomandoo kumi ambao utakwenda nao huko Nasbir hakikisheni silaha zinapatikana ili tuuthibitishie ulimwengu kuwa sababu ya kuvamia Irak haikuwa ya makosa tunakutegemea sana Lucille!” Alisema mwenyekiti wa kitengo cha Ujasusi cha baraza hilo Jenerali Frank Dux.
Lucille alibaki hapo akisubiri helkopta ifike, tofauti na alivyofikiria kuwa ingewasili mapema ilifika baada ya saa tatu! Alitambulishwa kwa makomandoo ambao angeongozana nao kwenda kazini huko Nasbir naye akamkabidhi gaidi Ricardo Gonzalez mikononi mwa wanajeshi, akapakiwa ndani ya helkopta iliyoondoka Baghdad kuelekea Nasbir kabla haijarejea tena Basra, waliwachukua vijana wawili wa kiarabu ili kuwaongoza hadi eneo zilipokuwa silaha za maangamizi kwa kutumia ramani iliyochorwa kwa kutumia maelezo ya gaidi Ricardo Gonzalez, kulikuwa na kila aina ya silaha ndani ya helkopta hiyo na zote Lucille alijua jinsi ya kuzitumia, alikuwa na mafunzo makali ya kijeshi aliyoyapata katika nchi mbalimbali yaliyomwezesha kupambana katika hali yoyote.
“Jamani nafikiri mnaelewa tunakwenda kufanya kazi ngumu kiasi gani?” Lucille aliwauliza makomandoo waliokuwemo ndani ya helkopta, miili yao ilitisha, walikuwa ni wanaume wea miraba mine lakini wote walitakiwa kuwa chini yake! Lucille alitisha kwa uwezo wake wa kupambana kijeshi.
“Ndio tunafahamu!”
“Hatutashuka ndani ya helkopta wote kwa pamoja ila tukikaribia eneo kulikochimbiwa silaha tutaanza kudondoka na Parachuti mmoja baada ya mwingine mpaka wote tuwe chini ndipo tutakutana na kupanga namna ya kuvamia!”Alisema Lucille na wote wakaitikia.
Hilo ndilo lililofanyika, Lucille alikuwa mtu wa kwanza kushuka kwa parachute walipofika kijijini Nasbir, akifuaitwa na vijana wa kiarabu kasha makomandoo wanane, kabla wote ahawajamalizika Lucille alishangaa kuona helkopta inawaka moto! Tayari ilikuwa imelipuliwa, alilia machozi na uchungu wake kuongezeka mara mbili hasa alipofikiria ni kwa kiasi gani alikuwa amekwepa kifo kupitia tundu la sindano.
Kama mpiganaji, hakutaka kuumia sana kwani yaliyotokea yalikuwa ni sehemu ya mchezo wenyewe! Alianza kuwakusanya wenzake ili watekeleze kilichowaleta eneo hilo lakini kabla hawajafanya lolote tayari walishazungukwa na kuwekwa chini ya ulinzi na watu wenye silaha kali kuliko walizokuwa nazo.Lucille na makomandoo wengione walichanganyikiwa na kushindwa kuelewa nini cha kufanya ni kweli walikuwa wamefanikiwa kufika eneo ambako profesa Cheznob na silaha za maangamizi alizozitengeneza zilikuwa zimechimbiwa, lakini hawakuwa na la kufanya zaidi ya kutulia.
Waliamriwa na kutupa silaha zao zote chini, wakaonekana kusita kidogo! Risasi zikafyatuka kutoka katika bunduki za maadui na kuwafumua vichwa makomandoo wawili kati ya wane waliokuwepo, kuonyesha kuwa jambo lililokuwa likisemwa halikuwa utani! Bila ubishi waliweka silaha zao chini na wote wakafungwa kamba mikononi na miguuni pamoja na vitambaa vyeusi usoni, tayari walikuwa ni mateka.
Lucille alianza kumkumbuka Denis ingawa hakuwa na uhakika kama naye alikuwa hai katika kipindi hicho, zoezi zima la kuzitafuta silaha za maangamizi kwa upande wa Lucille lilionekana kufika mwisho! Kilichokuwa mbele yake wakati huo haikuwa kingine bali kifo, tena cha kikatili kutoka kwa Wairak wasio na huruma.
Walipakiwa ndani ya gari aina ya Landrover na safari ya kwenda kusikojulikana ikaanza, Lucille alikuwa akilia machozi na kukumbuka nyumbani kwao Kenya, hakuwa na matumaini hata kidogo ya kuokolewa.
Nembo ya UNHCR, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi iliyokuwa kwenye gari aliloliendesha Denis ilimsaidia kuvuka vizuizi vingi njiani bila kuuliza maswali, ujanja alioufanya ni kupakia akinamama na watoto waliokuwa wakikimbia kutoka Baghdad kwenye vijijini kulikokuwa na usalama! Kila aliposimamishwa alisema alikuwa akiwasafirisha wakimbizi hao kwenda sehemu salama, alifanikiwa kuvuka vizuizi vyote hatimaye kufika Nasbir saa kumi baadaye! Lengo lake likiwa ni moja tu kuzitafuta silaha za maangamizi!Hakuwa na habari kama Lucille alishafika eneo hilo na kutekwa.
Je, nini kitaendelea? Fuatilia wiki ijayo! Imeshikana kuisha leo, lakini kumbuka mwisho wa hii kuna nyingine kali iitwayo Memories of Hell(kumbukumbu za kuzimu) nafikiri sijawahi kuandika hadithi kali na tamu kama hii.
Tayari Denis alikuwa ameingia na Nasbir, mahali zilipofichwa silaha za maangamizi, kazi yake ilikuwa moja tu ni kutafuta mahali zilipokuwa zimefichwa, kumkamata profesa Cheznob na kuutangazia ulimwengu kwamba tayari alikuwa ameikamilisha kazi kubwa aliyokuwa amepewa. Alimfikiria Lucille na kushindwa kuelewa mahali alikokuwa, lakini moyoni mwake alijipa matumaini kuwa tayari alishaingia na alikuwa akiendelea na kazi hivyo lazima angekutana naye akiwa katika utekelezaji wa kazi ngumu ya kufichua silaha za maangamizi, hakuwaza wala kufikiria msichana huyo angekuwa ametekwa na wapiganaji wa Kiirak.
Milipuko ya mabomu ilisikika kila mahali, hali katika mji wa Nasbir ilitisha,watu walikuwa wakikimbia huku na kule kuokoa maisha yao! Majeshi ya Marekani na washirika wake yalikuwa katika mji huo yakipambana vikali na wapiganaji waliomtii Rais Suleiman Al-Mahmoud ambaye tayari Marekani ilishamtia mkononi, kwa hali ilivyokuwa Denis aliamini asingeweza kufanya kazi peke yake bila kuutaarifu Umoja wa Mataifa ili umuunganishe na majeshi ya Marekani afanye kazi pamoja, kabla ya kufanya hivyo aliichukua ramani kutoka ndani ya gari lake na kuitandaza mbele ya macho yake akiwa amesimama nje na kuanza kuisoma, aliitambua barabara kubwa iliyochorwa katika ramani hiyo na kuelewa mahali handaki lilipokuwa.
“Ni mbele! Itabidi nisonge zaidi!” Aliwaza kisha kuikunja ramani yake na kuirudisha mfukoni akaanza kutembea kurudi nyuma ya gari ambako aliwaeleza wanawake aliowabeba kuwa hapo ndipo ulikuwa mwisho wa safari yake, alisikitika sana moyoni mwake lakini pia alielewa mbele kulikuwa na hatari kubwa zaidi, asingeweza kwenda nao! Walijaribu kumkatalia ikabidi awaeleze kila kitu waziwazi kuwa yeye hakuwa mfanyakazi wa shirika la kuhudumia wakimbizi kama walivyomtambua bali mpelelezi aliyekuwa akifuatilia silaha za maangamizi, hawakumwamini mpaka alipotoa kitambulisho chake na kuwaonyesha, akawauliza kama kuna mtu aliyeufahamu vizuri mji wa Nasbir. .
“Mimi!” Mmoja wa watu hao alisema.
“Unaweza kuongozana na mimi?”
“Kwenda wapi sasa?”
“Njoo usome hii ramani!” Denis alisema huku akiingiza mkono wake mfukoni.
Aliyejitolea kumsaidia alikuwa msichana mdogo tu mwenye umri usiozidi miaka ishirini na mbili, msichana mrembo na mwenye kuvutia! Aliisoma ramani hiyo kwa dakika moja kisha akamgeukia Denis na kumweleza wazi kuwa alilifahamu eneo hilo! Denis alifurahi na kumwomba msichana huyo apande ndani ya gari tayari kwa kusonga mbele, alikuwa na matumaini makubwa ya kukamilisha kazi yake siku hiyo hiyo na aliamini msichana aliyembeba ndani ya gari angeweza kumsaidia.
Aliwashusha wanawake wengine na watoto aliosafiri nao kutoka Baghdad na kuwaficha kwenye moja ya magofu yaliyokuwa jirani na mahali walipokuwa akiwaomba wabaki eneo hilo mpaka atakaporudi kama angefanikiwa kurejea salama.Baada ya hapo hapakuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya kupiga simu Umoja wa Mataifa kutoa taarifa juu ya kuwepo kwake nchini Irak, hakutaka iwe siri tena na alihitaji msaada mkubwa sana wa Marekani na Umoja wa Mataifa.
“Uko wapi?” Ilikuwa ni sauti ya Mwenyekiti wa Kitengo cha Ujasusi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Bw.Frank Dux, sauti yake ilikuwa ikitetemeka! Hakuamini kama kweli alikuwa akiongea na Denis ambaye awali alikataa kuchukua jukumu la kwenda Irak kupambana ili kujua kama kweli silaha za maangamizi zilikwepo.
“Niko Irak!”
“Kweli?”
“Nafikiri Lucille aliwaeleza kila kitu!”
“Ndio lakini hatukuamini!”
“Nipo Irak na kazi inakwenda vizuri, nimekwishagundua mahali silaha za maangamizi zilipo na pia mtaalamu wa kuzitengeneza, hivi sasa ninavyoongea na wewe nipo njiani kuelekea eneo hilo lakini nahitaji msaada mmoja, siwezi kupambana peke yangu! Ningefurahi kama ungeyataarifu majeshi ya Marekani yaliyoko hapa Nasbir ili tusaidiane katika kazi hii ngumu!”
“Una habari juu ya yaliyompata Lucille?”
“Hapana mimi na yeye tulishindwa kuelewana juu ya jambo fulani, tukatengana, nikaondoka Baghdad kwa gari nikamwacha yeye na vijana wengine wa kiarabu wakifanya mpango wa kusafiri kwa Helkopta kuja hapa Nasbir! Kwani kimetokea nini?”
“Habari nilizozipata kupitia televisheni ya Al-jazeera, inayoonyesha kila kitu ambacho majeshi ya Irak yanawafanyia Wamarekani ni kwamba Helkopta waliyopanda imelipuliwa na Lucille pamoja na watu wote waliokuwepo ndani ya Helkopta hiyo wameteketea pamoja nayo!”
“Unanitania!” Alisema Denis akiwa amejishika mikono yake yote miwili kichwani, haikuwa rahisi kwake kuamini kuwa msichana mrembo Lucille aliyeokoa maisha yake alikuwa marehemu, alimwaga machozi na kulia kwa uchungu! Hasira yake iliongezeka mara mbili, hakutaka kupoteza muda alichomweleza Jenerali Frank Dux kabla hajakata simu ni kumuomba awasiliane na mkuu wa majeshi ya Marekani na washirika wake nchini Irak ili atume majeshi haraka iwezekanavyo kwenda kitongoji kilichoitwa, Albakir, kilichokuwa umbali wa kama kilometa ishirini kutoka katikati ya mji mdogo wa Nasbir! Huko ndiko silaha zilikokuwa.
Aliendesha gari kwa kasi huku akitokwa na machozi, kifo cha Lucille kilimuumiza sana moyoni! Alikuwa ameyaamini maneno yote aliyoambiwa na jenerali Frank Dux, wazo kwamba Lucille alikuwa ametekwa halikuwemo kabisa kichwani mwake, hakukutana na kizuizi chochote njiani lakini walipobakiza kilometa kama tatu kufika eneo lilipokuwa handaki, msichana aliyekuwa ndani ya gari alimwamuru Denis asimamishe gari naye akafanya hivyo.
“Kuna ulinzi mkali sana!”
“Kwa hiyo?”
“Ni bora tuliache gari hapa kisha tutembee kwa miguu!”
“Hapana, gari hili tulilonalo ni la Umoja wa Mataifa, hakuna mtu anayeweza kulitilia mashaka! Unaweza kuendesha gari?” Denis alimuuliza msichana huyo.
“Ndio”
“Kutumia silaha je?”
“Hakuna kijana katika nchi yangu mwenye umri kama nilionao mimi asiyejua kutumia silaha!”
“Sasa naomba uelewe kuwa tunakokwenda si mchezo, kutakuwa na mapambano makali kuliko unavyotegemea, si umeamua kunisaidia?”
“Ndio”
“Lazima uwe tayari kufa!”
“Niko tayari, nimechoshwa na utawala wa Rais Suleiman Al-Mahmoud”
“Haya njoo ukae kwenye usukani uendeshe mimi niwe tayari na silaha zangu mkononi!”
“Sawa”Aliitikia msichana huyo, akanyanyuka na kuzunguka upande wa pili na kukaa kwenye usukani, akawasha gari kisha kuingiza gia namba moja na safari ikaanza! Jinsi alivyoliondoa gari tu kulimfanya Denis aamini kuwa msichana huyo alikuwa dereva pengine kumshinda yeye, mbele kidogo Denis alichukua kiona mbali chake na kuanza kuangalia mahali walikokuwa wakielekea, jengo kubwa lilionekana ambalo mbele yake kulikuwa na askari wengi wenye silaha! Alikiri moyoni mwake kwamba eneo hilo lilitisha, hata hivyo hakusita ilikuwa ni lazima asonge mbele.
“Endesha kwa kasi sana mpaka kwenye lango ambapo utasimama, najua watakuja wakitaka kukagua, usistuke hapo ndipo mimi nitafanya mambo! Nikianza tu kurusha risasi, utaingiza gia namba moja na kuligonga lango la kuingilia ili tuingie ndani, sawa?”
Msichana huyo aliitikia na kuliwasha gari, kasi aliyoondoka nayo hata Denis ilimshtua! Alikwenda moja kwa moja hadi kwenye lango kubwa lililokuwa mbele ya jengo ambamo silaha za maangamizi zilihifadhiwa, alikanyaga breki wanajeshi wasiopungua watano walilisogelea gari na kuanza kumhoji dereva maswali, kabla hawajaendelea sana Denis alianza kurusha risasi juu kuwapa mshtuko ni kweli wote waliruka na kulala chini! Wakiwa chini Fatma aliliendesha gari kwa kasi kama alivyokuwa ameelekezwa na kuligonga lango kwa nguvu likafunguka na gari lao kuingia, almanusura wachomoke kupitia kioo cha mbele lakini mikanda waliyofunga iliwasaidia.
Wakiwa ndani Denis aliendelea kurusha risasi huku macho yake yakiangalia huku na kule, upande wa kulia aliona kibao kilichoandikwa Intrance, alielewa mara moja kuwa ndio hapo palikuwa mahali pa kuingilia! Akaruka kutoka garini huku akipiga kelele na kumuomba Fatma aache gari, achukue moja ya bunduki iliyokuwemo ndani ya gari na kumfuata. Msichana huyo alitekeleza maagizo aliyopewa na kukimbia akimfuata Denis ambaye tayari alishaanza kuingia ndani ya handaki baada ya kufunua bati lililofunika sehemu ya kuingilia, kabla msichana huyo hajaingia alipigwa risasi zisizopungua tano na kuanguka pale pale, Denis alishangaa ni bahati kubwa kiasi gani aliyokuwa nayo mpaka yeye kutopigwa risasi hizo, aliamini ulikuwa mkono wa Mungu!
Kulikuwa na ngazi za kushuka chini kuliko kuwa na giza lakini mwanga wa taa ulisaidia, Denis alizidi kukimbia kwenda mbele zaidi akizama ardhini, kwenda mahali alikoamini ndiko silaha zilikokuwa, kila mtu aliyekuja mbele yake alimuangusha kwa risasi na kusonga mbele! Njia zote ndani ya handaki hilo zilieleweka hapakuwa na haja ya kuuliza! Mpaka anafika kwenye chumba kilichoandikwa Scientist room, watu zaidi ya ishirini walishaanguka chini kwa risasi zilizotoka katika bunduki yake, mtu wa mwisho kumuua ndiye aliyechukua kilemba chake na kujifunga kichwani na pia kumvua kanzu na kuivaa mwilini mwake. Chumba kilichokuwa mbele yake kilitengezwa kwa vioo, ndani yake alikaa mzee mwenye mvi nyingi aliyevaa miwani mikubwa usoni mwake, akili yake ilionekana kuzama kwenye kazi aliyokuwa akiifanya! Denis alikuwa na hakika mzee huyo ni Profesa Cheznob! Mrusi aliyekuwa akitengeneza silaha za kuiangamiza dunia.
Aliupiga mlango teke na kuingia ndani, mzee aliyekuwa mbele yake alidondosha chupa mbili alizokuwa nazo mkononi na maji yaliyokuwemo ndani yake kumwagika sakafuni! Alionyesha mshtuko wa ajabu, jambo lililokuwa likitokea hakulitegemea. Bunduki ya Denis ilikuwa mbele yake ikiwa imemlenga katikati ya paji la uso wake.
“You are under arrest Mr Cheznob! For your safety please show me the weapons!” (Uko chini ya ulinzi bwana Cheznob, kwa usalama wako tafadhali nionyeshe silaha za maangamizi) aliongea Denis kwa ukali, macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira aliyokuwa nayo na ili kuonyesha kwamba alichokisema ilikuwa si utani risasi moja ilichomoka na kuzama kwenye mkono wa kulia wa mzee huyo, akaanguka chini kwa maumivu ni hapo ndipo Denis aligundua kuwa mzee huyo hakuwa na miguu yote miwili.
“Dont kill me!” (Usiniue!)
“Then show me the weapons!” (Nionyeshe silaha zilipo)
“I will! I will!” (Nitakuonyesha! Nitakuonyesha!)
“I want to see the weapons now!” (Nataka kuziona sasa hivi!)
“Help me to sit on my wheel chair!” (Nisaidie kukaa kwenye kiti changu cha matairi!) Profesa Cheznob aliongea akizidi kulia kwa maumivu makali aliyokuwa nayo, Denis kwa mkono mmoja alimbeba na kumkalisha kitini kisha kuendelea kumuamuru aonyeshe mahali silaha zilipokuwa, profesa hakuwa mbishi alimuomba amsukume akiwa kwenye kiti chake ili ampeleke mahali silaha zilipokuwa! Walitembea kama kilometa nzima chini ya ardhi na kukifikia chumba kilichoandikwa Explosives, do not enter without permission, maneno hayo yalimaanisha vitu vilivyokuwa katika chumba hicho vilikuwa vya kulipuka hivyo hapakuwa na ruhusu kwa mtu kuingia bila ruhusa.
“This is the room where all the weapons are kept!” (Hiki ndio chumba ambamo silaha za maangamizi zinatunzwa!”
“Open the door!” (Fungua huo mlango)
“It is fatar!” (Hicho ni kitendo cha kufisha!) Aliongea profesa Cheznob kwa huzuni.
Kwa Denis mpaka kufikia hapo alikuwa ametosha kabisa, alikuwa amefanikiwa kuziona silaha za maagamizi ambazo wakaguzi wa kimataifa walishindwa kuzipata na kuwafanya Maraisi wa Uingereza na Marekani kuwa katika wakati mgumu baada ya dunia nzima kulalamika kwamba hapakuwa na sababu ya kuivamia Irak kama silaha zilizokuwa zikitafutwa hazikuwepo. Ilikuwa ni heshima kubwa kwa Denis na hakuelewa dunia ingemchukuliaje baada ya siku hiyo, alitamani Lucille angekuwepo kushuhudia heshima ambayo wote wawili wangepewa lakini mpaka wakati huo aliamini msichana huyo alikuwa marehemu.
Akijisikia mshindi moyoni mwake alimnyanyua profesa Cheznob na kuanza kutembea naye na kwenda nje ya handaki, hakujua kilichokuwa juu lakini alikuwa tayari kupambana na yeyote ambaye angejitokeza! Bunduki yake ilikuwa mkono wa kulia mkanda wa risasi ukiwa umemzunguka kiunoni, kanzu aliyoivaa ilitapakaa damu! Alipandisha ngazi bila woga na kutokeza nje akiwa na profesa Chezob begani, alipoangaza macho yake huku na kule alifurahi kuwaona maaskari wa Kimarekani, Kiingereza na Mataifa mengine yaliyokuwa vitani nchini Irak wakiwa wamelizunguka eneo hilo.
Wote walimsogelea na kumzunguka, kamera za televisheni mbalimbali zilikuwa zimemzunguka akipigwa picha zisizo na idadi kwa ajili ya habari hiyo kutangazwa duniani kote, mmoja wa wanajeshi waliokuwepo alimsogelea Denis na kumshika mkono akimpongeza, Denis alishindwa kujizuia na kulia kwa uchungu. Hakuamini kama ni yeye aliyefanya kazi kubwa kiasi hicho na kuiletea sifa kubwa nchi yake ya Tanzania
“I am general John Collins, the Chief Commander of America and allies Army in Iraq, Conglaturations you are the man!” (Naitwa jenerali John Collins, mkuu wa majeshi ya Marekani na washirika wake hapa Irak, Hongera Dennis wewe ni mwanaume!)Aliongea mzee huyo.
“Thanks, the glory be to the Lord !” (Ahsante, utukufu uende kwa bwana!) Aliongea Dennis akimkabidhi profesa Cheznob mikononi mwa wanajeshi waliosogea ili kumpokea, kisha akaanza kuwapa ripoti juu ya hali ilivyo chini ya ardhi na mahali silaha zilipokuwa, wakati anakamilisha zoezi hilo jenerali Collins alinyoosha mkono wake na kumkabidhi Dennis simu ya mkononi aliyokuwa nayo ili aongee na mtu ambaye hakumfahamu.
“Who is he?” (Nani )Aliuliza Dennis akitaka kufahamu ni nani aliyetaka kuongea naye!
“The President of the United States of America!” (Rais wa Marekani!)
“Sure?” (Hakika?) Aliuliza Dennis kwa mshangao, hata siku moja hakuwahi kutegemea angeongea na Rais wa Taifa kubwa kama hilo duniani.
Nini kitatokea? Hakikisha unafuatilia toleo lijalo.
Wajumbe wa baraza la salama la umoja wa mataifa walibaki midomo wazi huku bila kuamini kilichokuwa kimetokea, kwa jinsi jina la Alfonso Gonzalez Cardoso alikuwa na uhusiano wa Al-qaeda na ni yeye alittoa siri za umoja huo akijifanya mtu mwenye sauti na aliyeaminika miongoni mwa wenzake
ÒNo! It cant be!Ó (hapana haiwezekani huo kuwa ukweli)
ÒWe can justify ItÓ (Tunaweza kuthibitisha) Mkuu wa CIA aliueleza uliotumwa na baraza
ÒWe need your justificationÓ (Tunahitaji uthibitisho wenu)
Hakuna aliyekuwa tayari kuamini taarifa hiyo hawakuondoka makao makuu mpaka kikao kilipokaa na kuelezwa jinsi Alfonso alivyowasiliana na gaidi Ricardo Gonzalez majina yao yalikuwa yanafanana lakini hawakuwa na undugu, kila kitu kiliwekwa wazi na hata malipo aliyoyapata kutokana na kazi hiyo, ilikuwa ni habair ya kusikitisha kwani ndio walijua ni kwanini siri zao zilivuja, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuiacha CIA ifanye kazi yake, waliondoka wakiwa wamenyongÕonyea kurudi makao makuu ya umoja wamataifa ambako kikao cha dharura kiliitisha kujadili suala la Inspekta Alfonso Gonzalez Cardoso walishindwa kuelewa ni kitu gani kingefanyika baada ya, baada ya kujadiliana kwa muda wote wakaamua wakakubaliana kwamba kama ingethibitika kuwa kweli Inspekta Jenerali huyo ana uhusiano na mtandao hatari wa Al-qaeda sbasi ilikuwa ni lazima afikishwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake
CIA hawakuw ana mchezo na Inspekta Cardoso, maelezo waliyoyapata yalitosha kabisa kuwahakikishia kwamba ana uhusiano na Al-qaeda, hata hivyo ilibidi ahamishwe na kupelekwa katika jumba la mahojiano ambako kulikuwa na mateso ya kila aina ili aweze kueleza ukweli juu ya mambo yote yaliyoelezwa juu yake, jumba hilo lilikuwa umbali wa kilometa mia moja nje kidogo ya jiji la Washington, aliingizwa ndani ya jumba na mahojiano kuanza, hakuna mtu aliyeingizwa ndani ya jumba hilo akatoka nbila kueleza ukweli lakini Alfonso alikana kila kitu alichoambiwa lakini baadae mateso yalipokamilika hakuwa na chaguo jingine zaidi ya kukubali na kueleza jinsi alivyowasiliana na Al-qaeda na kuusalciti umoja wa mataifa
ÒTunataka utueleze jambi mojaÓ
ÒJambo gani?Ó
ÒKuna watu wametekwa bila shaka utakuwa unafahamu waliko!Ó
ÒNdioÓ
ÒWako wapi?Ó
ÒWako Irbil kwenye kambi ya mauajiÓ
ÒAsanteÓ alimaliza mpelelezi wa CIA aliyekuwa akimhoji Inspekta Cardoso, Ilikuwa ni habari ya kusikitisha ambayo ilitegemewa kutawala vyombo vyote vya habari
Baada ya mawasiliano hayo yaliyochukua saa mbili, CIA iliwasilisha ripoti yake makao makuu ya jeshi, Pentagon na kuwaeleza juu ya mahali walipofichwa mateka wa kivita waliokamatwa na askari wa Iraq, habazi hizo zilitumwa moja kwa moja hadi Basra huko Iraq ambako kiliundwa kikosi maalum kwa ajili ya kwenda kuwakomboa mateka waliyo chini ya askari wa Iraq kikiwa chini ya Dennis Geofrey Mwikwambe, kijana wa Kitanzania aliyefanya kazi kubwa ya kuzifichua silaha za maangamizi, aliheshimiwa na kila mtu na wote waliamini opereshseni hiyo ikiwa chini yake ingefanikiwa
ÒNina uhakika hata Lucille yuko hukoÓ
ÒInawezekanaÓ
ÒNi lazma tuondoke sasa hivi kwenda kukabiliana na lolote litakalokuwepo lakini mateka ni lazima waokoleweÓ Aliongea Dennis wote wakimsikiliza
Ramani ya Iraq iliwekwa mezani na kusomwa mpaka eneo la Irbil likaonekana, mpango kamambe wa kuvamia eneo hilo uliandaliwa kwa kutumia majeshi ya nchi kavu hawakutaka kutumia Helkopta wala ndege kwa kuhofia mateka kuuawa kama watekaji wangeshtuka juu ya kilichokuwa kikiendelea, operesheni hiyo ilibandikwa jina la Soul Saving Operation yaani operesheni ya kunusuru roho za watu!, Dennis alikuwa tayari kupoteza roho yake lakini aokoe roho za watu waliokuwa chini ya mateso ya askari wa Iraq
Magari ishirini yaliyojaza askari yaliondoka Basra kwa mwendo wa kasi na kuwasilia Irbil masaa ishirini na nne baadae lakini kabla hawajafika kwenye kambi ya mateso magari yaliegeshwa na wanajeshi wote wakashuka na kuzunguka kambi yote ili wote waivamie kwa pamoja, amri zote zilitoka kwa dennis na hivyo ndivyo ilivyofanyika kambi ikavamiwa watekaji walipogundua hatari iliyokuwa imejitokeza wakaanza kuwaua mateka mmoja baada ya wengine lakini kabla hawajafikisha watu kumi tayari majeshi ya Marekani yalikuwa yameshaingi na kwa kuogopa kuingia mikononi mwa Wamarekani wakaanza kujilipua wao wenyewe na kufa kabla majeshi ya Wamarekani hayajawafanya chochote
Mateka wote walinyanyuka na kushangilia kukombolewa kwao, wakawazunguka wanajeshi wa Marekani na kuwapa shukrani halikuwa jambo rahisi kuamini kwamba walikuwa wamewekwa huru, Dennis alikuwa na furaha kupita kisai lakini fraha yhake ilikuwa haijakamilika mpaka amuone Luucille na hakukuwa na mateka wa kike wote walikuwa ni wanaume alishindwa kuelewa na ni wapi alikokuwa na kulazimika kuuliza
ÒTafadhali nisikilizeniÓ Ali0ongea kwa sauti Dennis na mateka wote wakawa kimya
ÒNdiyo tunakusikilizaÓ
ÒNafurahi mmekuwa huru tuliyatoa maisha yetu kwa ajili yenu, hii ndiyo kazi ya jeshi lakini kuna kitu kimoja nataka kuwauliza, Je hapa kwenu paliwahi kuwepo mateka wa kike?Ó
ÒndioÓ
ÒWako wapi?Ó
ÒWalichukuliwa siku moja usiku na hawakurudi tena, tuna wasi wasi waliuawawaÓ alisema mmoja wa mateka hao
ÒMnaweza kuwa mnawafahamu majina yao?Ó
Ã’Mmoja aliitwa Anne na Mwingine hatukuwahi kumfahamu jina lake kwani ndio kwanza alikuwa amefika!?
Òalipokuja alikuwa peke yake?Ó
ÒHapana aliletwa na wenzie wakiwa nane lakini hao walipigwa risasi siku hiyo hiyo na kufa, baadae tulisikia walikuwa ni makomandoo wa Kimarekani waliotekwa huko NasbirÓ
Maneno hayo peke yake yalitosha kabisa kumuonyesha Dennis kwamba watu waliokuwa wakongelewa na mateka hao walikuwa ni Lucille na makomandoo wengine aliotekwa nao, aliinamisha uso wake kwa uchungu na kulia, hapo hapo alianza kiuzivamia nyumba zilizokuwepo pembeni na kuzichunguza, hakukuta mtu 0hata mmoja askari wa Kiirak wengi walishatoroka alishindwa kuelewa kama walitoroka pamoja nao au waliwaua kabla Dennis na wanajeshi wengine wa Kimarekani hawajafika, kichwani mwake alikuwa na kitendawili katu hakutaka kukubali kwamba Lucille alikuwa amekufa
ÒKwanini una haraka, kwanini utumie nguvu na wew ni mwanaume mzuri kiasi hicho?Ó Ndiyo maneno aliyoyasema Lucille kwa Mohamed au Mo kama walivyomuita wanajeshi wengine wa Iraq kabla hajamuingilia kimwili
ÒKwa hiyo?Ó
ÒKwa nini uswaondoe hawa watu wote kisha ukafaidi mwenyewe, mimi nakupenda na nafurahi hukuniua hakuna ninachoweza kukuzawadia zaidi ya huu mwili wangu, nataka nikupe penzi zuri ambalo hujawahi kukutana naloÓ Aliongea Lucille kwa sauti ya kulegeza mbinu aliyoitumia haikuwa ya kubuni bali alijifunza nchini Marekani namna ya kujiokoa unapokutana na adui mwenye lengo la kukuingilia kimwili.
ÒKweli eeehÓ
ÒHakika nakueleza!Ó
Maneno ya Lucille akiwa maelegeza sauti yalimwingia Mo moja kwa moja moyoni mwake yakawa kama uchawi mara moja akabadili mawazo na kuwaamuru wenzake wote watoke nje na wamwache yeye na Lucille ambaye alionekana kumuamini kupita kiasi bila kuelewa alikuwa ni mtu hatari kuliko yeye, hakuna kitu alichokifikiria zaidi ya kutoroka na hakujua angekwenda wapi na kama huko kungekuwa na usalama ama la! Alichotaka yeye ni kuondoka na hakutaka kuondoka peke yake alitaka kuondoka na Anne msichana pekee aliyetokea kulewana nae katika muda mfupi aliokaa kwenye kambi yha mauaji.
Kweli Lucille na Anne waliachiwa na maaskari wengine wa Kiarabu wakaanza kutembea kuelekea nje kama walivyoamriwa na Mo aliyeonekana kuwa ndiye mkuu wakambi hiyo.
ÒHutaki kufurahi na wanawake wawili?Ó
ÒSijawahi ila juwa naona kwenye luningaÓ
ÒBasi leo utafaidiÓ
ÒKweli?Mnaweza?Ó
ÒKwanini tusiweze na tutakufanyia hivyo kila sikuÓ
ÒHakikaÓ
ÒHakuna sababu ya kukudanganya hebu lala kifudi fudi tuanze kukuonyesha mamboÓ Aliongea Lucille huku akimkonyeza Anne na bila ubishi Mo akaweka bunduki yake pembeni na kulala kifudi fudi hilo ndilokosa pekee alilofanya kwa ushirikiano Anne na Lucille walianza kumchua mzee huyo mgongo hatimaye akajikuta amelala usingizi bila kufanya kitu chochote, hawakukoma waliendelea kumchua mpaka akaanza kukoroma!
Tayari ilikuwa ni saa saba usiku fikra za mauaji zilimwijia Lucille na alimwambia Anne juu ya mpango wake wa kumuua Mohamed na kutoroka
ÒTutakwenda wapi? Ambako hatutakutana na wanajeshi wa Kiirak?Ó
ÒSikiliza Anne hata ukikaa hapa mwisho wake ni kifo! Sasa kwa nini tusijaribu kujiokoa na kama ni kufa basi tufe mbele ya safari?Ó
Ã’Sawa lakini hapa ni porini
ÒSasa sikiliza mimi namuua Mo kama unataka kunifuata utanifuata na kama unataka kubaki utabaki, lakini kumbuka kitu kimoja watakapokukuta hapa Mo akiwa amekufa hawatakuacha haiÓ Alipomaliza kusema maneno hayo Lucille alinyanyua bunduki ya Mo kwa lengo la kumpiga nayo kichwani lakini alighairi baada ya kuona njia hiyo haikuwa sahihi, ni lazima angepiga kelele ambazo kwa hakika zingewaamsha wanajeshi wengine na mpango wake ungekwama
ÒNimfunike na mtoÓ Aliwaza Lucille na kuliona ni sahihi na kumuomba anne amsaidie kumgandamiza Mohamed kitandaji wakati yeye akiwa amemfunika na mto puani na mdomoni ili asipumue, wote walikubaliana na Lucille alipohesabu moja mpaka tatu aliushusha mto na kumfunika Mohamed Pua na mdomo, huku Anne akimgandamiza kitandani ilikuwa heka heka lakini dakika kumi baadae Mohame alitulia akiwa kimya hiyo ilikuwa ni ishara kwamba tayari alishafariki na kweli walipomgusa kifuani moyo wake ulikuwa umetulia tuli, walifurahia kifo cha binadamu mwenzao kilichokuwa kimebakia mbele yao kilikuwa ni kutoroka lakini walishindwa kuondoka wakati huo wakasuburi usiku uwe mkubwa zaidi
Walitulia chumbani humo wakiwa na maiti ya Mo mpaka saa tisa za usiku ndipo wakafungua mlango na kunyata taratibu hadi nyuma ambako alianza kutambaa hadi kwenye ngome ya wavu iliyozunguka kambi kwa nguvu zao walianza kungÕoa wavu mpaka wakapata tundu lililowaruhusu kutoka nje ambako walianza kukimbia kuelekea kusikojuliakanawakipita kati kati ya pori ambalo hawakuelewa kama kulikuwa na wanyama wakali ama la! Walichotaka wao ni kusonga mbali basi na kama ni kufa wafe wakijarbu kuokoa maisha yao
Walitembea porini usiku mzima na kulipokucha walijificha kwenye vichaka kusubiri usiku mwingine ili wasonge mbele ambako hawakujua ni wapi hawakutaka kutembea mchana kwa kuwa hawakutaka kuingia tena mikononi mwa sakari wa Kiirak wakati tayari walishawakimbia hawakuwa na habari kabisa juuu ya mpango uliokuwa ukifanywa na umoja wa mataifa ukishirikiana na CIA juu ya kuwaokoa mateka, siku tatu baadae ndipo Dennis pamoja na makomandoo wengine wa Kimarekani walipovamia kambi ya Irbil na kuwakomboa mateka wengine, kwa mujibu wa maelezo waliyopewa waliamini Lucille alikuwa amekufa
Hapakuwa na jambo jingine zaidi ya kuwachukua mateka waliowaoka na kuwarudisha Basra ambako walipakizwa ndani ya ndege maalum na kuopelekwa moja kwa moja Saudia Arabia ambako walichkuliwa katka ndege maalum na kurudishwa katika nchi zao, dunia nzima ilitaarifiwa juu ya hilo kupitia vyomb vya habari, kila mtu alisikitika kusikia Lucille na mtangazaji wa televisheni ya CTV Anne Christopher aliuawa hakuna aliyefahamu kwamba wanawake hao wlaikuwa hai wakikimbia porini wakijaribu kuokoa maisha yao hata Dennis baadaye alikubaliana na maneno hayo akawa amekata tamaa alilia kwa uchungu, alimpenda Lucille kwa sababu aliokoa maisha yake.
ÒPopote ulipo Lucille iwe Jehanam au peponi nataka ujue kuwa nakupenda kwa sababu uliokoa maisha yangu na nilichokuwa nimepanga hata kama sikukueleza ni kukuoa mara baada ya kumaliza kazi hii, lakini bahati mbaya umekwenda na umeniacha peke yangu, nitakupenda siku zote za maisha yangu mpaka siku nitakapokutana na weweÓ Aliongea Dennis huku amepiga magoti mikono yake ikiwa imeinuliwa juu akimuomba Mungu ailaze roho ya Lucille mahali pema peponi.
Dennis hakuwa na kazi tena nchini Irak kama ni silaha za maangamizi alikuwa aalishazipata kilichofuata ni yeye kwenda umoja wa mataifa ambako alikuwa anahitajika na wajumbe wa baraza hilo il kupewa zawadi maalum, hakuwa na ubishi tena kwani kitu kilichomfanya aendelee kuwa Irak ni kumtafuta Lucille lakini wakati huo aliamini mwanamke huyo jasiri alikuwa marehemu hivyo ilikuwa ni lazima aondoke kwenda Marekani, ndege maalumu iliandaliwa na kasafirishwa mpaka Washington, ni kweli alikuwa ameshafanya kazi kubwa lakini furaha yake ilikuwa haijatimia kwa sababu hakuweza kumuokoa Lucille
Mapokezi aliyopewa nchini Marekani hayakuwa ya kawaida gari la wazi liliandaliwa na watu walijipanga barabarani kumpokea akiwa shujaa aliyezigndua silaha za maangamizi ambazo wakaguzi walishindwa kuzipata, alikuwa mtanzania lakini Marekani walijivuna kupita kiasi kuwa nae katika nchi yao na walitaka abadilishe uraia, jambo ambalo Dennis alimkatalia hata Rais wao.
Usiku ulipoingia wakiwa na uhakika hali ilikuwa salama, Anne na Lucille waliamua kusonga mbele kuendelea na safari yao wakijaribu kuokoa maisha, waliojiona ni wenye bahati kubwa kufanikiwa kutoroka kutoka kwenye kambi ya mauaji walikoacha idadi kubwa ya mateka wa Kimarekani na nchi nyingine nyingi wakisubiri kifo, waliamini kabisa mara baada ya maaskari wengine wa Kiiraki kugundua kuwa mkuu wao Mohamed alikuwa ameuawa na wao kutoroka msako ungekuwa mkali kupita kiasi na pengine wangeingiwa na hasira na kuamua kuwaua mateka wote, fikra hizo zilimfanya Lucille aingiwe na huzuni sana moyoni mwake akiwahurumia watu wote waliobaki nyuma, hata hivyo hakuwa na la kufanya kuwaokoa, kwa wakati huo alitaka kwanza ajiokoe yeye mwenyewe pamoja na Anne na kama wangefanikiwa kufika mahali kwenye usalama na kukutana na maaskari wa Kimarekani, ndipo wangetoa taarifa juu ya mahali walipokuwa wamefichwa mateka wengi wa Kimarekani hivyo mipango ya ukombozi kuandaliwa.
Hakuelewa kabisa kuwa wakati akifikiria hivyo tayari Denis na wanajeshi wengine wa Kimarekani walishaivamia kambi ya mateka na kuwakomboa wote, safari ilikuwa ndefu na ngumu hasa kwa Anne ambaye hakuwa na uzoefu kabisa wa kutembea kwa miguu, kwa Lucille aliyekulia nchini Kenya tena sehemu za Kiricho ambako alisafiri umbali mrefu kwa miguu kwenda shule, safari hiyo haikuwa na matatizo sana ukizingatia alikuwa na mazoezi makali ya kijeshi! Usiku mzima walipita katikati ya pori bila kuelewa walipokuwa wakielekea ni Kaskazini, Kusini, Mashariki au Magharibi, hawakuwa na dira ya kuwawezesha kufahamu hilo lakini kwa msaada wa nyota waliweza kuhisi walikuwa wakielekea Mashariki.
“Lazima tutafika tu mahali pa usalama!”
“Lakini ni lazima tuangalie sana tusije tukaingia tena mikononi mwa Wairak, watatuua!” Aliongea Anne kwa sauti ya chini chini, alikuwa amechoka kupita kiasi, mwili wake ulijaa vipele vingi sababu ya kuumwa na wadudu pamoja na Mbung’o! Katika maisha yake hakuwahi kuingia katika taabu kama aliyokuwa akiipata katika safari hiyo, wote wawili hawakuwa na nguo mwilini mwao, walijifunga majani ya miti kuficha sehemu zao za siri.
Kwa siku nne nzima waliendelea kutembea kwa mtindo huo huo wa kuendelea na safari usiku na kulipokucha kujificha katika vichaka wakisubiri usiku mwingine lakini bila kufika mahali popote pa msaada, chakula chao kikubwa katika siku zote hizo kilikuwa matunda ya mwituni hasa mapera yaliyostawi sana katika Misitu ya Irak na walikunywa maji ya mito na mabwawa bila kufikiria usalama wa afya zao, siku ya tano wakisonga mbele usiku Anne alishindwa kabisa kuendelea, miguu yake ilikuwa imevimba! Lucille alijaribu kumtia nguvu ili waendelee lakini haikuwezekana ikabidi walale msituni siku hiyo wakipumzika na kulipokucha walishinda ndani ya kichaka wakisubiri usiku mwingine, mapumziko ya siku moja yalimfanya Anne apate nguvu kidogo.
“Nafikiri usiku wa leo tunaweza tukaendelea na safari yetu au?”
“Nitajitahidi najisikia nafuu kidogo!”
Kweli usiku ulipoingia walianza kusonga mbele, Lucille akiongoza msafara wao na Anne akimfuata kwa nyuma, bado hawakuwa na uwezo wa kutembea kwa kasi kubwa kama aliyokwenda nayo Lucille jambo lililomfanya hata yeye apunguze kasi ili asiweze kumwacha mwenzake, kulikuwa na umbali wa kama hatua tano kati yao, ni Lucille aliyeonyesha njia ambayo Anne aliifuata! Akiwa katika fikra nyingi juu ya kama wangefanikiwa kufika mahali pa usalama, Lucille alisikia kelele nyuma yake! Alishtuka na kugeuka na kumkuta Anne akipiga kelele na kukimbia kuelekea upande mwingine na mbele kidogo alianguka chini.
“Vipi?” Lucille aliuliza alipomfikia.
“Wadudu wananiuma!”
“Wadudu gani?” Alizidi kuuliza Lucille huku akishuhudia mwenzake akitupa mikono huku na kule! Kabla hajafanya lolote naye alishtukia ameanza kuumwa na wadudu ambao hakuwaelewa, alimpiga mmoja aliyekuwa akimng’ata kwenye mkono na kisha kumgandamiza na kumkamata kwa vidole vyake kisha kumwangalia vizuri, alimtambua! Walikuwa ni nyuki wengi kupita kiasi, ilivyoonekana wakati Anne anapita katika moja ya vichaka lazima aligusa makao yao na kuwatibua, tayari walishamfunika mwili wake wote kuanzia kichwani hadi miguuni! Anne alikuwa haonekani na wote walikuwa wakimshambulia yeye, aliendelea kupiga kelele akimwomba Lucille amsaidie.
Pamoja na kuwa hata yeye Lucille alikuwa aking’atwa vibaya na nyuki aligundua ilikuwa ni lazima afanye kitu kumwokoa mwenzake aliyekuwa amefunikwa na nyuki, kwa harakaharaka alikata majani ya miti na kuanza kumpigapiga Anne mwilini ili kuwaondoa nyuki, alifanya kazi hiyo kwa karibu dakika kumi na tano nzima ndipo mwili wa Anne ukabaki wazi, nyuki wote wakawa wameondoka na kurudi kwenye mziga wao! Wote walikuwa wameumwa lakini Anne alikuwa ameharibiwa zaidi, hakuweza hata kunyanyuka mahali alipolala.
“Anne!Anne!Anne!” Lucille alimwita lakini Anne hakuitika aliendelea kulia kutokana na maumivu makali aliyokuwa nayo..
Hawakuweza tena kuendelea na safari yao, hali ya Anne ilikuwa mbaya wakalazimika kulala tena sehemu hiyo mpaka asubuhi, mwili wa Anne ulimshangaza Lucille kulipokucha, ulikuwa umevimba kupita kiasi na wote ulikuwa mwekundu! Hata macho yake hayakuweza kufunguka, kila sehemu ilikuwa imevimba,Lucille alishindwa kuelewa ni nini angekifanya kumsaidia rafiki yake mpendwa, mpaka jioni ya siku hiyo hali ya Anne ilikuwa bado mbaya na mwili wake ulizidi kuvimba.
“Nipeleke hospitali!”
“Wapi sasa rafiki yangu? Hata mimi natamani kufanya hivyo lakini tuko porini mahali ambako hapana tiba yoyote!”
“Nitakufa!”
“Haiwezekani! Mungu atakusaidia, baada ya siku mbili mwili wako utapungua tena, sumu itakuwa imekwisha katika nyama zako!”
“Kweli?”
“Hakika!”
“Kuna mtoto wa shangazi yangu aliwahi kuumwa na nyuki hivi hivi lakini alipona!”
“Lakini mimi sidhani kama nitapona! Huu ndio mwisho wangu, nafikiri Mungu alipanga maisha yangu yakatikie porini huku Irak!”
“Sio hivyo Anne, usiyape nafasi mawazo ya kifo!”
Walibaki eneo hilo kwa karibu siku mbili, wakila matunda lakini hali ya Anne ilizidi kuwa mbaya, wazo la kumpeleka hospitali lilianza kutawala akili ya Lucille kwani kuendelea kukaa eneo hilo kusingesaidia chochote, alitaka kujaribu pengine alikuwa amekaribia kufika karibu na barabara mahali ambako angeweza kutafuta msaada wa gari! Mawazo hayo yalimfanya Lucille afikie uamuzi wa kumnyanyua Anne aliyekuwa bado amevimba mwili mzima na kumbeba mgongoni akaanza kutembea naye taratibu bila kujali ulikuwa ni mchana, hakuogopa tena kukamatwa kwa sababu alitaka kuokoa maisha ya msichana aliyeteseka naye ambaye tayari alimhesabu kama ndugu kwa sababu wote walikuwa katika tatizo moja.
Alitembea naye kutwa nzima bila kufika barabarani, akipumzika kila baada ya kilometa moja ama moja na nusu, alikuwa amechoka kupita kiasi lakini ilikuwa ni lazima asonge mbele, hata yeye mwili wake ulikuwa umevimba lakini si kama ilivyokuwa kwa Anne! Usiku hakuweza kuendelea ilibidi alale katika kichaka alichochagua mpaka asubuhi ambayo Anne hakuweza hata kuongea, alikuwa amezidiwa zaidi ya siku iliyopita!Lucille alijipa moyo na kumbeba tena kisha kuendelea na safari, hakutembea hata kilometa moja akashtukia Anne akimwachia na kuanguka chini akimwacha Lucille ameshikilia miguu, macho yake yalikuwa yamegeukia juu na alikuwa akitupa shingo yake huku na kule, picha hiyo ilimwonyesha Lucille kila kitu kilichotaka kutokea, alielewa Anne alikuwa anakata roho! Alilia kwa uchungu lakini hakuweza kuubadilisha ukweli, msichana huyo akawa amekata roho mikononi mwake.
“Sitakuacha! Nitasonga mbele na wewe mpaka nitakapokuta bendera ya Marekani, siwezi kukuacha uharibikie porini ni lazima uzikwe kwa heshima Anne! Ulilipigania sana Taifa lako!” Aliongea Lucille akilia na hapohapo mwili wake ukawa umejazwa nguvu za ajabu ambazo hakuelewa zilikotokea, aliunyanyua mwili wa Anne ambao tayari haukuwa na uhai na kuubeba begani, safari ikaendelea huku akiendelea kulia na kushangaa ni kwanini alikuwa hafiki barabarani, hakuogopa tena kuingia mikononi mwa askari wa Kiirak, moyo wake ulijaa ujasiri.
Alitembea na maiti ya Anne begani kwa siku tatu, ikawa imezidi kuvimba na kuharibika kabisa, hapo hakuwa na jambo jingine la kufanya zaidi kwani tayari maiti ya Anne ilikuwa ikitoa harufu. Aliamua kuiweka chini na kufikia uamuzi wa kuizika kwa heshima ingawa alikuwa peke yake porini, kwa kutumia miti alifanikiwa kuchimba shimo la kama futi tatu ardhini na kuuweka mwili wa Anne ndani yake kisha kufukia na mchanga, hakusahau kuweka alama ya msalaba juu ya kaburi, ingawa hakuwahi kumuuliza Anne juu ya dhehebu lake aliamini alikuwa ni Mkristo kufuatana na jina lake lilivyokuwa.
Alifanya kazi hiyo akilia kwa uchungu! Moyo wake ulikuwa umeumizwa sana na tukio hilo, hasa kuona amebaki peke yake, pamoja na hayo yote alielewa ilikuwa ni lazima safari iendelee, alichofanya ni kupiga magoti mbele ya kaburi la Anne na kusali kwa mara ya mwisho kisha akaanza kutembea, mbele kama hatua ishirini aligeuka na kuliangalia eneo hilo ili asije kulisahau maana alijua ni lazima siku moja, kama angefanikiwa kufika katika kambi ya majeshi ya Marekani, angerudi kuja kuyachukua mabaki ya rafiki yake na kwenda kuyazika kwa heshima nchini mwake.
“Mungu atanisaidia ili nifike ninakokwenda nikiwa salama!” Aliwaza Lucille akisonga mbele.
Hakujali usiku wala mchana, alizidi kutembea na hakufika mahali popote palipoonyesha dalili za kuishi binadamu, kila sehemu ilikuwa ni pori na cha kushangaza zaidi hakukutana na mnyama hata mmoja wa porini! Alimshukuru Mungu kwa hilo, alitembea siku mbili zaidi na siku ya tatu kama saa mbili ya usiku, mbele yake aliona moto ukiwaka! Furaha ikamjaa moyoni, matumaini ya kuokoka yakamwingia, hakutaka wala kujiuliza moto huo ulikuwa wa wanajeshi wa Marekani na washirika wake au wananchi wa kawaida wa Irak, kilichomfurahisha yeye ni kuona dalili kwamba alikuwa karibu na makazi ya watu.
Hakuogopa kuuawa wala kusita kusonga mbele alichofanya ni kutembea kuufuata moto huo akitaka kufahamu ni watu gani walioishi hapo, akiwa amebakiza kama hatua mia tatu aufikie moto huo, alishangaa kuona ngome kubwa na mbele yake kulikuwa na maaskari wengi, aliponyanyua macho yake juu aliona sehemu iliyojengwa kwa ajili ya walinzi wa kuangalia usalama, ilikuwa ni kambi ambayo hakujua ni ya jeshi gani.
“Hapa inabidi niwe makini sana, vinginevyo naweza kuuawa!” Aliwaza Lucille na kwa mara ya kwanza katika muda mrefu alishangaa kujikuta akimkumbuka Denis, alishindwa kuelewa kama alikuwa hai au marehemu maana kwa hali ilivyokuwa nchini Irak wakati huo hapakuwa na uwezekano wa yeye kusafiri hadi Nasbir bila kuingia mikononi mwa wauaji wa Irak waliokuwa na chuki na kila raia wa nje ya nchi hiyo.
Alitambaa kwa tumbo akisonga mbele zaidi na kuikaribia kabisa ngome hiyo, alifanya kila kitu kwa uangalifu ili aendelee kuwa salama, kati yake na ukuta wa kambi hiyo kulikuwa na kama mita hamsini tu, akiwa hapo alinyanyua tena macho yake juu na kuangalia, alishangaa kuona kitu ambacho hakukitegemea kabisa alama ya bendera ya Marekani ilikuwa imebandikwa kwenye kibanda cha mlinzi kilichokuwa juu, furaha nyingi ilimjaa moyoni na hakuwa na wasiwasi tena kama kambi hiyo ilikuwa ni ya Wamarekani au Wairak! Akanyanyuka na kusimama wima huku akishangilia na kuanza kukimbia kwenda mbele akipiga kelele na kusema “Viva Amerika! Ahsante Mungu kwa kuokoa maisha yangu”
Askari aliyekuwa juu alisikia sauti hiyo na kuangalia chini, kwa msaada wa taa alimwona mwanamke akiwa nusu uchi akikimbia kuelekea kwenye ngome yao, hapohapo alipiga kipenga na sauti ya king’ora ikasikika! Watu wengi wenye silaha mkononi walijitokeza na kumweka Lucille chini ya ulinzi, huku bunduki zao zikiwa zimemlenga yeye! Tofauti na alivyofikiri kwamba alikuwa ameingia katika mikono ya Wamarekani alishangazwa na sura za watu waliokuwa wamemzunguka, hazikuwa sura za Kimarekani! Walikuwa ni watu wenye ndevu nyingi na waliovaa kanzu pamoja na vilemba vichwani mwao, kila mmoja alikuwa na bunduki aina ya LMG na wakiwa wamejizungushia mikanda ya risasi.
“Dont kill me, because I’m your fellow American!”(Msiniue mimi ni Mmarekani mwenzenu!) Aliongea Lucille akiamini kwa kusema hivyo kungewafanya watu hao wasiitoe roho yake!
“Ha!Ha!Ha!Ha! Who told you we are Americans?”(Nani amekuambia sisi ni Wamarekani?) Mmoja wa watu hao aliuliza.
Je, nini kitampata Lucille? Ni akina nani hao waliomtia mikononi? Fuatilia wiki ijayo.
Lucille na mtangazaji wa televisheni ya CTV, Anne Christopher wanafanikiwa kutoroka katika kambi ya mateso huko Irbil na kuingia porini ambako wanatembea kwa siku nyingi bila kufika mahali popote pa usalama, lakini matumaini makubwa ya kunusurika na kifo.
Anne amechoka kupita kiasi kwa sababu ya kutokuwa na uzoefu wa kutembea kwa miguu umbali mrefu! Hatimaye anashindwa kabisa na kulazimika safari yao iwe ya taratibu wakati mwingine wakishinda mahali siku nzima Anne akipumzika.
Pengine hilo lisingekuwa tatizo kubwa sana kama Anne asingedumbukiza mkono wake kwenye tundu la mti ambako nyuki wengi walipafanya makao na wote kumvamia na kumshambulia, hili ndilo lilisababisha mwili wake wote uvimbe na hatimaye kufa porini na Lucille kumzika kisha kusonga mbele na safari yake.
Baada ya safari ya siku mbili Lucille alifika mahali ambako aliona moto ulioashiria maisha ya binadamu na kuamua kutembea hadi eneo hilo, kwa macho yake aliona alama ya bendera ya Marekani na kupata matumaini kwamba alikuwa amekutana na watu wa kumwokoa! Bila woga wala hofu alijitokeza tena akishangilia lakini cha kushangaza ni pale alipogundua kuwa kumbe watu aliokuwa anawakimbilia hawakuwa Wamarekani, waliibandika alama hiyo juu ili kuwanasa mateka na wanajeshi wa Kimarekani.
Je, nini kinaendelea? Akina nani hao waliomteka Lucille? Je, watamwacha hai? Fuatilia...........
“
I’m asking you! Who told you we are Americans?”(Nakuuliza nani amekuambia sisi ni Wamarekani?) Mmoja wa watu hao alimuuliza tena.
“I saw the American flag sign over there!”(Nimeiona ile alama pale juu!)
“It was put there to make it easy for you Americans to get into our hands!”(Iliweka pale kufanya iwe rahisi Wamarekani kuingia mikononi mwetu)
“So you are not Americans?”(Kwa hiyo nyie sio Wamarekani?)
“That is the answer!”(Hilo ndilo jibu!)
Lucille alimwaga machozi tena, alijilaumu kwa kujikuta ameingia katika mikono ya wauaji kirahisi kiasi hicho, alifungwa kitambaa usoni na kuanza kuvutwa kupelekwa ndani ambako alifungiwa katika moja ya vyumba na kuanza kuteswa, askari wa Kiirak walikuwa wamemkamata Mmarekani na kila walipofanya hivyo ilikuwa ni lazima wawataarifu waandishi wa habari wa televisheni ya Al-Jazeera waje kupiga picha na kutangaza katika televisheni yao na hivyo ndivyo ilivyokuwa, saa nzima baadaye walikuwa hapo na Lucille alipigwa picha nyingi, maaskari wa Kiirak wakiwa wamemwekea visu shingoni na walivyohojiwa na waandishi walisema kama Marekani isingeondoa majeshi yake nchini Irak Mateka huyo angechinjwa.
Jioni ya siku hiyo hiyo picha ya Lucille ilionyeshwa na televisheni ya Kiarabu ya Al-Jazeera, jamii yote ya Waarabu iliiona! Mwanamke mrembo akiwa nusu uchi na amefungwa na kitambaa cheusi usoni huku watu wenye visu wakiwa wamemwekea shingoni wakitamka wazi kuwa kama Marekani na washirika wake wasingeondoa majeshi yao nchini Irak katika muda wa siku tano basi msichana huyo angechinjwa na kuondolewa kichwa na picha yake ingeonyeshwa katika televisheni ya Al-Jazeera na baadaye kusambazwa katika mtandao.
Ilikuwa ni habari ya kusikitisha kwa Wamarekani wote na hata majeshi ya Ushirika, lilikuwa ni sharti gumu sana kwao, isingewezekana kuondoa majeshi lakini pia isingewezekana kumwacha msichana huyo auawe! Hivyo ilikuwa ni lazima chochote kifanyike kuokoa maisha yake, makomandoo wote walikusanyika na kupanga mkakati mzito wa kufanya ukombozi, kwanza upelelezi ulifanyika ili kujua msichana huyo alikuwa amefichwa katika kambi gani nchini humo, lakini upelelezi huo ulitakiwa kukamilika katika muda wa siku mbili kwani watekaji walikuwa wametoa siku tano tu kabla hawajamchinja! Haikuwa kazi ngumu kwao hasa kwa kuwatumia baadhi ya wakazi wa mji wa Basra ambao ulielewa moja kwa moja ni wapi alikokuwa msichana huyo.
“Hiyo ni kambi ya Nashiif! Ipo karibu na mji wa Najaf!”
“Kilometa gani kutoka hapa?”
“Labda mia tatu na hamsini hivi kuelekea Kaskazini!”
“Ni sehemu ya wazi?”
“Hapana ni porini!”
“Unaweza kuongozana na sisi kwenda huko?”
“Hakuna matatizo!” Kijana huyo aliyeitwa Said alikuwa miongoni mwa watu waliofurahishwa na kuwepo kwa majeshi ya Marekani na Washirika wake nchini Irak.
Mipango iliandaliwa ili siku hiyo hiyo, Majeshi yaondoke kwenda Nashiif kufanya kila linalowezekana kumkomboa msichana huyo aliyeaminika kuwa mateka peke yake wa Kimarekani au washirika wake nchini Irak.
******
Habari kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Hispania, Alfonso Gonzalez Cardoso alikuwa na uhusiano na Al-qaeda na kwamba ndiye aliyetoa siri za umoja huo kwa maadui zilimsikitisha kila mtu, maandamano yalifanyika kila sehemu ya Marekani yakiomba sheria kali sana ichukuliwe dhidi yake! Hapakuwa na namna ya kumlinda kwani hata vyombo vya habari vilikuwa vikipiga kelele juu ya jambo hilo, ilikuwa ni aibu kubwa kwani mtu huyo alikuwa miongoni mwa watu walioheshimika sana katika baraza hilo, alikamatwa na baada ya kuhojiwa na CIA na kukiri kila kitu alipakiwa katika ndege na kupelekwa katika gereza maalum lililokuwepo huko Sanfransisco, ni huko ndiko alikokutana na Profesa Cheznob mtaalam wa kutengeneza silaha za maangamizi, hawakuwahi kukutana hata siku moja, lakini walifahamiana kutokana na maongezi kwa njia ya simu.
“There is no way we can get out of this!”(Hakuna namna yoyote tunayoweza kujiepusha na matatizo haya!) Alfonso Gonzalez alimwambia Profesa Cheznob baada ya maongezi ya muda mrefu gerezani, alijilaumu sana moyoni mwake kwa yote aliyoyafanya, tamaa ilikuwa imemponza! Alitamani kufa, hakuwa tayari kuuangalia ulimwengu tena na alijua wazi kila mtu alimchukia.
“For sure! To me this is my end!”(Hakika! Kwangu mimi huu nauona ndio mwisho wangu!) Profesa Cheznob mzee mwenye umri wa miaka isiyopungua sabini alisema, kwake yeye hapakuwa na maisha marefu sana mbele! Kifo kilikuwa kimekaribia, kwa hali hiyo alijikuta akiwa tayari kwa lolote.
Umoja wa Mataifa ulikuwa umepata pigo kubwa na skandali ya aina yake, kwa mtu mkubwa kama Alfonso Cardoso kuingia katika kashfa lilikuwa ni jambo la kusikitisha lililolazimisha utaratibu wa kujisafisha na kuchunguzana uanze mara moja, Marekani iliyoonekana kama ndio Umoja wa Mataifa ilikasirishwa sana na tukio hilo la usaliti na kuahidi kutumia kila uwezo iliokuwa nao kuwasaka watu wabaya ndani ya Umoja wa Mataifa.
“We will make sure United Nations is purified!”(Tutahakikisha Umoja wa Mataifa unasafishwa!) Rais wa Marekani alisema katika mkutano wa dharura ulioitishwa.
******
Denis Mwikwambe alikuwa amejipumzisha katika hoteli ya Hilton baada ya kufanya mazoezi ya asubuhi na kuoga, mhudumu wa hoteli alipogonga na kuingia! Aliweka kifungua kinywa mezani kisha kumkabidhi Denis magazeti ya asubuhi hiyo, lililokuwa juu kabisa lilikuwa ni gazeti la Washington Post, picha iliyokuwa ukurasa wa mbele ilimshtua! Msichana akiwa amefungwa kitambaa cheusi usoni na nusu ya mwili wake ukiwa wazi alionekana, watu watatu waliofunika nyuso zao na kuacha macho peke yake walikuwa wamemwekea visu shingoni. She will be slaughtered if American and his allies a not out of Iraq! Hicho ndicho kilikuwa kichwa cha habari cha gazeti hilo kikimaanisha msichana huyo angechinjwa kama Marekani na Washirika wake wasingeondoa majeshi yao nchini Irak.
Habari hiyo ilitawala si gazeti la Washington Post peke yake bali hata The Sun, NewYork Times, News of the World na mengineyo mengi, habari ya kutekwa haikumshtua sana Denis kwani katika vita hayo yalikuwa ni mambo ya kawaida, kilichomshtua sana ni sura ya msichana ambaye picha yake ilikuwa mbele ya magazeti yote! Pamoja na macho yake kufungwa kwa kitambaa, bado Denis aliweza kumtambua, alikuwa Lucille! Moyo wake ulikuwa ukipiga kwa nguvu sana, alifurahi kugundua msichana huyo alikuwa bado hai ingawa hakuelewa nini kilichotokea mpaka akawa hai wakati kambini walikokuwa mateka wengine hakumkuta na alielezwa kwamba huenda aliuawa.
Alinyanyuka kitandani haraka, hakutaka tena kusoma magazeti, alichofanya ni kuvaa nguo zake haraka iwezekanavyo kisha kutoka nje ya chumba chake na kufunga, ilikuwa ni safari kuelekea makao makuu ya CIA, wala hakutaka kupiga simu, alichotaka ni kufika mwenyewe na kuongea na Mkurugenzi juu ya jambo alilolisoma kwenye vyombo vya habari, tayari moyo wake ulishatamani kuingia vitani tena, kumbe kazi ilikuwa bado haijamalizika!
“Nimekuja!” Alimwambia Mkurugenzi baada ya salamu
“Nilijua utakuja na nilikuwa nakusubiri kwa hamu kubwa, nimekwishawasiliana na wakuu wa majeshi walioko Irak juu ya jambo hili na wanajiandaa kwenda mahali aliko msichana huyu! Ni lazima akombolewe na ninafikiri ni vyema na wewe ukaenda ili kuongeza nguvu!”
“Mkurugenzi hivi unaelewa huyu msichana ni nani?”
“Hapana!”
“Nitakuambia!”
“Ni nani?”
“Lucille!”
“Denis unanitania! Lucille si ulisema alikufa?”
“Hata mimi nashindwa kuelewa ni kitu gani kimetokea mpaka akawa hai tena!”
“Haiwezekani! Nina uhakika kabisa umemfanananisha!”
“Nakuambia kweli Mkurugenzi!”
Mkurugenzi mpya wa CIA Bw. John Tent, aliyeshika madaraka baada ya aliyemtangulia kujiuzuru, alibonyeza kitu fulani ukutani na kumwambia sekretari wake amletee magazeti ya siku hiyo na alifanya hivyo haraka, wote wawili wakakaa na kuanza kuiangalia picha iliyokuwa juu ya magazeti kwa makini, Mkurugenzi mpya hakumfahamu vizuri Lucille, ingawa tayari alishasikia habari zake, hakutaka kubisha zaidi alimwomba Denis amweleze nini ilikuwa mipango yake.
“Nitafutie ndege niondoke leo hii hii kwenda Baghdad! Lazima nimkomboe Lucille, nipo tayari kufia vitani!”
“Watafurahi kusikia unakwenda!”
Ndege iliandaliwa na siku hiyo hiyo jioni Denis aliondoka Washington kuelekea Baghdad tena kabla hata ya kukabidhiwa zawadi ambayo Marekani walitaka kumpa kwa jinsi alivyofanikiwa kuzigundua silaha za maangamizi.
Je, nini kitaendelea? Fuatilia wiki ijayo.
Lucille anaonekana kwenye luninga akiwa ametekwa na wapiganaji wa Kiirak, wanaotishia kumchinja kama Marekani na washirika wake hawataondoa majeshi yao nchini humo! Dennis ambaye siku zote alikuwa akiamini msichana huyo anayempenda alikuwa marehemu, anashtuka kuiona picha hiyo na ni hapo ndipo anaamua kurejea tena vitani kumkomboa msichana huyo! Ndege inatafutwa kwa ajili ya kumpeleka Irak. Je, atafanikiwa kumkomboa msichana huyo? Endelea.......
Kila Dennis alipoiona picha ya mateka Lucille kwenye luninga akiwa ndani ya ndege hasira yake iliongezekana maradufu, alitamani kufika Basra muda huo huo kuungana na makomandoo wengine kwenda kuendesha zoezi la ukombozi, ingawa ndege ilikwenda kwa kasi kubwa aliona mwendo wake ulikuwa hautoshi!
Mara kwa mara alimhimiza Rubani aipeleke kwa kasi zaidi, naye alitii ndege ikaanza kutembea kwenye mshale mwekundu, kasi ambayo rubani alitakiwa kuitumia katika wakati wa hatari. masaa manne baadaye tayari walikuwa wakitua katika uwanja wa ndege wa Basra na kupokelewa na magari ya makomandoo yaliyoandaliwa tayari, taarifa za ujio wake zilishamtangulia!
Kila alikopita wanajeshi wa Marekani walipiga saluti, aliheshimwa na kila mtu na wengine walisikika wakishangilia kwa sauti kuonyesha furaha ya ujio na Dennis! Halikuwa jambo rahisi kuamini kuwa kijana huyo alikuwa Mtanzania lakini mwenye uwezo mkubwa kupambana kijeshi na kufanya upelelezi, kuja kwake tena Irak baada ya kuwa amezigundua silaha za maangamizi ziliwapa matumaini maaskari wote kuwa hata mateka aliyekuwa mikononi mwa wapiganaji wa Irak pia angekombolewa! Hakuna mtu hata mmoja aliyeutilia shaka uwezo wa Dennis aliyekuwa kimya muda wote akielekezwa gari la kupanda.
Kutoka uwanja wa ndege walikwenda moja kwa moja hadi ilipokuwa kambi ya wanajeshi wa Marekani katika mji wa Basra, huko kiliitishwa kikao cha dharura na Dennis akauliza juu ya mipango iliyokuwepo kumkomboa mateka, mkuu wa majeshi ya Marekani na washirika wake nchini Irak ndiye aliyeeleza kila kitu kwamba walikuwa wakijiandaa kwenda kuivamia kambi ambako mateka alikuwa! Dennis aliwasikiliza kwa makini akitingisha kichwa kuonyesha ni kiasi gani alikuwa hakubaliana na mpango huo.
“Kamanda!” Dennis alimwita.
“Naam!”
“Nasikitika kukueleza wazi kuwa mpango wako hautafanikiwa, kabla hatujamkomboa atakuwa ameshauawa!”
“Sasa tufanye nini?”
“Sikilizeni!” Aliongea Dennis na makamanda wote chumbani wakakaa kimya na kisha aliomba ramani ya Irak na kuiweka mezani wakaanza kwa pamoja kuchambua maeneo ilipokuwa kambi ya Nashiif, waligundua ilikuwa katikati ya pori pembeni mwa mji wa Najaf! Walijaribu kuangalia njia za kupita mpaka kuiweka kambi hiyo katikati kabla ya kuivamia na kumkomboa Lucille.
“Tutaingiaje hapo?” Mmoja wa Makomandoo aliuliza.
“Halitakiwi jeshi kama mlivyokwishapanga, bali tunahitaji kikundi kidogo tu cha watu wanaojiamini, wanaweza kuwa kumi na tano au ishirini lakini wenye uwezo wa kupambana bila woga! Tutaongozana nao hadi kambini na kumkomboa Lucille, najua itakuwa kazi ngumu na kuna uwezekano kabisa baadhi yetu tukapoteza maisha lakini Lucille akakombolewa, hilo ni lazima mlifahamu!”
“Kwanini tusitumie jeshi?”
“Kufanya hivyo itakuwa na kuhatarisha maisha ya mateka! Tunachotakiwa kufanya ni kitu kimoja, kuwaita CNN na BBC ambao watapiga picha wanajeshi wetu pamoja na vifaa vya kivita vikiondolewa Irak, hiyo itawafanya maadui waamini Marekani na washirika wake wamenyoosha mikono, wakati hayo yakiendelea mimi nitakuwa nawaongoza makomandoo wote kwenda kuivamia Kambi ya Nashiif na nina uhakika kabisa Lucille atakombolewa, sitaki afe! Alinisaidia sana na sasa ni wajibu wangu kumkomboa!” Aliongea Dennis kwa jazba mishipa ya shingo ikiwa imemvimba, alionyesha waziwazi hasira yake huku misuli ya mikono ikiwa imetuna.
Alikuwa na umbile la kikomandoo, alifanana kabisa na na mcheza sinema pia mtunisha misuli Anold Schwazineger, vazi la kijeshi alilovaa ambalo lilikatwa mikono kuanzia begani liliionyesha vizuri misuli yake ya mikononi na pia upana wa kifua chake! Kila aliyemwona alikiri alikuwa mwanaume wa shoka, alikuwa simba aliyejeruhiwa aliyekuwa na hamu ya kuua na kumkomboa Lucille, wote walimsikiliza yeye na hatimaye walikubaliana na kile alichokisema, uzoefu wake wa upelelezi na vita uliwafanya wote wamtii ingawa hakuwa na cheo kikubwa sana jeshini.
Mara moja waliteuliwa vijana ishirini wenye nguvu kuungana na Dennis katika operesheni ya kumkomboa Lucille, walikabidhiwa silaha walizozihitaji na walipewa uhuru wa kuchagua silaha nyingine yoyote waliyoihitaji, kila mmoja alijifunga sawasawa na kuridhika kwamba silaha walizokuwa nazo zilifaa kupambana na adui wa aina yoyote!
“Kuna kitu kimoja cha muhimu sana tunakihitaji?”
“Nini?”
“Ethyl Chloride!”
“Unafikiri itasaidia?” Mkuu wa majeshi aliuliza, alikuwa tayari kuwapa vijana wake kitu chochote walichokihitaji ili mradi tu Lucille akombolewe, hakuwa tayari kuona msichana huyo mrembo aliyetoa maisha yake kwa ajili ya Marekani wakati yeye alikuwa ni Mkenya akichinjwa..
“Itasaidia?”
“Ndio!”
“Tulikuwa nayo kidogo stoo! Hebu mtu mmoja akaangalie!” Mkuu wa Majeshi aliamuru na mmoja wa makomandoo akaondoka mbio kuelekea stoo ambako yeye na mtunza stoo ambaye pia alikuwa mwanajeshi walisaidiana kutafuta na kupata boksi moja lililokuwa na makopo kumi na mbili ya dawa hiyo ambayo kwa kuyaangalia mtu angeweza kufikiri ni dawa ya mbu ya Doom kwani pia yalikuwa ni ya kubonyeza na kupuliza kama watu wafanyavyo katika kuua wadudu ndani, lakini mtu yeyote ambaye hunusa harufu yake hulala usingizi mara moja. Ni dawa hiyo ndiyo Marekani ilitumia hata katika kuwakamata maadui wake waliojificha katika mashimo
Dennis alikuwa kiongozi wa kikosi kuelekea Nashiif, wote walitakiwa kumtii na kusikiliza alichosema! Walikubaliana mara tu baada ya kuondoka, mkuu wa majeshi ya Marekani na washirika wake nchini Irak angewaita waandishi wa habari na kuongea nao kwamba nchi hizo zilikuwa zinajiondoa nchini Irak na kuwaachia Wairak matatizo yao wenyewe, taarifa ilipelekwa Washington na ruhusa ikatolewa ili kuudanganya ulimwengu kwa muda wakati zoezi la kumkomboa Lucille likiendelea.
Saa moja baada ya Dennis na kikosi chake kuondoka kuelekea Nashiif waandishi wa habari waliitwa kambini na mkuu wa majeshi aliongea nao juu ya uamuzi wa Marekani na Washirika wake kuondoka nchini humo, hakudiriki kufungua mdomo wake na kuwaeleza siri iliyokuwepo nyuma ya maneno hayo! Waandishi wa habari hawakuamini, haikuwa Marekani waliyoifahamu ambayo ingeweza kunyoosha mikono yake kwa watu iliyowaita magaidi na kuionyesha dunia kwamba ilikuwa imeshindwa vita! Lakini kwa sababu aliyekuwa akiongea ni kiongozi wa juu wote walilazimika kukubali, wakapiga picha za wanajeshi wakijiandaa kuondoka na siku hiyo hiyo habari hizo zilianza kutangazwa katika televisheni dunia nzima! Dunia ikawa imedanganywa, wapiganaji wa Irak walishangilia ushindi bila kuelewa kuwa Dennis alikuwa akiongoza makomandoo wenye hasira kwenda kumkomboa Lucille.
Iliwachukua Dennis na wenzake masaa manne kusafiri kutoka Basra hadi Najaf, mji ambao pia kulikuwa na kambi ya Wamarekani walitoa taarifa kambini na kuendelea na safari yao kuelekea Nashiif, kilometa mia tatu na hamsini kuelekea Kaskazini mwa Irak! Ulikuwa umbali mkubwa lakini katika muda wa masaa mawili tayari walishaingia, kijana waliyemchukua Basra aliwaelekeza kila kitu, alielewa njia zote sababu aliwahi kuwa mwanajeshi katika utawala wa Kidikteta wa Rais Suleiman Al-Mahamoud kabla hajakamatwa.
“Kata kulia hapo!”
“Una uhakika lakini?”
“Kabisa!”
“Usije ukatupoteza?”
“Haiwezekani!” Alijibu kijana huyo na dereva aliyeendesha gari kubwa walilopanda makomandoo wote walikata kulia na kuingia porini, safari ilizidi kusonga mbele kwenda katikati ambako hapakuwa na dalili ya kuishi watu! Dennis alikuwa kimya akitafakari namna ya kufanya,alielewa ugumu wa kazi iliyokuwa mbele yake na hakufahamu kama angetoka huko akiwa salama, hakuogopa kufa kama tu ilikuwa ni kwa sababu ya Lucille! Bado alikumbuka namna alivyookolewa na msichana huyo mjini Baghdad, alipokuwa ametekwa na gaidi Ricardo Gonzalez, bila yeye asingekuwa hai ndio maana alikuwa tayari kupoteza uhai wake kwa ajili ya msichana aliyempenda ukizingatia wakati huo alijisikia kuwa katika mapenzi mazito zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.
Kichwani mwake alikuwa akimfikiria sana kijana aliyewasaidia,hakuamini kama msaada wote alioutoa ulikuwa ni bure! Isingewezekana hata siku moja raia wa Irak atoe msaada mkubwa namna hiyo kwa Marekani, lazima kulikuwa na kitu na pengine usaliti! Hicho ndicho kitu kilichoendelea kichwani mwake, hakuamini kama kijana huyo alikuwa mwema na alikuwa akijaribu kutafakari ni kwa namna gani angeweza kuwa na uhakika kuwa kijana huyo hakuwa hatari.
“Said!” Alimwita makomandoo wengine wakisikiliza gari likiendelea na safari..
“Kuna umbali gani kutoka hapa tulipo hadi Nashiif?”
“Tumebakiza kama kilometa hamsini!”
“DEREVA SIMAMAAAAA!” Dennis alipiga kelele akimwamuru dereva asimamishe gari, wote ndani ya gari walishtuka na kushindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kimetokea! Dereva hakuwa na la kufanya zaidi yakukanyaga breki na kuegesha gari kandokando ya barabara akisubiri amri nyingine.
“Wote teremkeni! Tumekaribia sana kufika, hili ni jambo la hatari, hatuwezi kwenda kama Ng’ombe wote tutauawa!” Aliongea kwa sauti ya juu Dennis na maaskari wote walishuka garini silaha zao zikiwa tayari kwa lolote.
“Ingiza hilo gari porini halafu urudi hapa!” Aliamuru Dennis na dereva alitii kwa mara nyingine na kulipitisha gari katikati ya miti hadi mbele ambako halikuonekana kabisa, akaliacha na kurudi hadi mahali alipowaacha wenzake, alimkuta Dennis amemkalisha kijana wa kiarabu chini akimhoji maswali mbalimbali aliyoyajibu huku akitetemeka, wasiwasi wake haukuwa bure kwani alipompekua alimkuta ana chombo kidogo cha mawasiliano kiitwacho WaveCatcher kinachomwezesha mtu kuwasiliana na mtu yeyote duniani kwa kutumia mawimbi yaendayo kwa kasi, kila mtu alibaki mdomo wazi na kuhisi kijana huyo alikuwa gaidi aliyetaka kuwaingiza katika mtego wa mauaji.
“Sema wewe ni nani?”
“Mimi ni Said!”
“Na hiki chombo umekipata wapi?”
“Ni changu!”
“Utasema tu......!” Aliongea Dennis akikimbia kuelekea mahali lilipofichwa gari, lengo lake likiwa ni kwenda kuchukua bisibisi ili aje kumtesa vizuri kijana huyo na aeleze ukweli juu ya maisha yake, hawakuwa na wasiwasi wowote juu ya kambi ya Nashiif ni kweli alikokuwa akiwapeleka ndiko ilikokuwa lakini walishindwa kuelewa ni kwanini alikuwa na kifaa hicho kama hakuwa mpelelezi wa wapiganaji wa Irak.
“Mamaaa!Bomu! Ana bo...!” Dennis alisikia sauti hiyo akiingia ndani ya gari na muda huo huo alisikia mlipuko usio wa kawaida, akaruka hadi chini na kulala chini ya gari, hali ilipotulia alinyanyuka na kurudi hadi mahali alikowaacha wenzake! Wote walikuwa wamelala chini wakiwa wamekufa, kumbe kijana waliyembeba hakuwa mwema bali muuaji wa kujitoa mhanga aliyetaka kuwateketeza wote, Dennis hakuamini kama kwa mara nyingine alikuwa ameokoka na kifo! Ilikuwa ni kama hadithi ya Alfu Lela Ulela, hakuna mtu angeamini kama jambo hilo liliwahi kutokea na yeye akanusurika, huku akilia alipiga magoti chini na kumshukuru Mungu, mwili wa Said ulikuwa umesambaratishwa kabisa na bomu, alipita kwa maaskari wenzake akiwatingisha kuona kama kulikuwa na hata mmoja aliyekuwa hai lakini alithibitisha kabisa wote walikuwa wamekufa. Hiyo ilimwongezea hasira maradufu.
*****
Tayari alikuwa amebaki peke yake lakini kazi ilikuwa lazima iendelee, ingawa kwa uangalifu mkubwa mpaka Lucille akombolewe! Alikaa chini kwa muda akitafakari ni nini cha kufanya kabla ya kusonga mbele, akili yake ilizunguka kwa kasi akawa amepata wazo aliloamini kabisa lingemfanya afanikiwe katika kazi ya ukombozi na yeye mwenyewe kurudi akiwa salama! Kama mwehu aliondoka na kuanza kukimbia kuelekea porini, alipoibuka kutoka huko baada ya nusu saa alikuwa amebeba gogo zito begani kwake, alikwenda nalo hadi barabarani na kulilaza akiziba kabisa njia.
“Watakuja tu! Haiwezekani wasipite hapa usiku mzima mpaka kesho asubuhi, ikitokea hivyo basi kutakuwa hakuna kambi ya jeshi huko tulikokuwa tunaelekea!”Alijisemea moyoni mwake.
Baada ya hapo alianza kuibeba miili ya makomandoo wenzake mmoja baada ya mwingine na kuipeleka kwenye gari, alipokuwa anamaliza mtu wa mwisho alisikia muungurumo wa gari na kujua alichotaka kufanya kimefika wakati wake! Alirudi harakaharaka hadi pembeni mwa barabara na kulala kwa tumbo bunduki yake ikiwa mkononi, kila kitu kilikuwa tayari kwa vita! Alikuwa tayari kuua kufidia damu ya makomandoo wenzake waliouawa na baada ya hapo ndipo safari yake ingeendelea, lakini kama tu gari lililokuwa linakuja lilikuwa ni la jeshi la Irak! Dakika tano baadaye gari kubwa aina ya Isuzu lilisimama nyuma ya gogo kubwa lililowekwa katikati ya barabara na wanaume wawili wakashuka wakishangaa namna hali ilivyokuwa katika eneo hilo.
“Kuna bomu limetupwa hapa?” Mmoja wao alisema akijaribu kulinyanyua gogo, hapohapo ndipo Dennis alianza kuitumia vizuri bunduki yake, risasi zilianza kumiminika kama mvua na kusambaza vichwa vya wanaume wote wawili walioshuka ndani ya gari, alikuwa na uhakika kabisa walikuwa wanajeshi wa Irak kwa jinsi gari lao lilivyokuwa! Lilikuwa na namba za jeshi na hicho ndicho kitu alichokihitaji, pamoja na kuwaua hao wawili bado hakuwa na uhakika kama kulikuwa na usalama, aliendelea kumimina risasi hadi nyuma ya bodi lakini hakusikia kelele, hapo ndipo alipojitokeza! Kwa ukaguzi wake alikuwa na uhakika kabisa kuwa gari hilo lilikuwa na watu wawili tu.
Alipekua kila mahali na aliporidhika alimvua mmoja wa watu aliowaua kanzu na kilemba chake na kuvaa juu ya nguo alizokuwa nazo mwilini kisha akafunga kilemba kichwani na mara moja akarukia garini na kuendelea na safari kwenda mahali ambako hata siku moja hakuwa kufika lakini aliamini ndiko kambi ya Nashiif ilikokuwa na ndiko Lucille alikamatwa mateka, njiani hakupisha hata na gari moja jambo lililomshangaza.
Akiwa amesafiri umbali wa kilometa arobaini kutoka eneo ambako bomu lililipukia na kuwaua wenzake, aliona moto mbele yake! Akawa na uhakika hiyo ndiyo kambi aliyokuwa akiitafuta, moyo wake ulidunda mara moja na baadaye kurudi katika hali yake ya kawaida, hivyo ndivyo ilivyomtokea kila mara alipokaribia kuingia katika hatari! Hakuwa na hofu za ajabuajabu, moyo wake ulikuwa jasiri! Hakusita wala kukanyaga breki, alichokifanya ni kuongeza kasi hadi kwenye lango la kuingilia katika kambi hiyo, mkono mmoja ukiwa kwenye usukani na mwingine ukiwa umeshika bunduki yake aina ya LMG, mkanda wa risasi ukiwa umemzunguka mabegani na kiunoni.
Alishangaa kuona lango likifunguliwa bila hata kupekuliwa na akaliingiza gari lake moja kwa moja hadi ndani, ulikuwa ni usiku wa manane, watu wote walionekana kuwa usingizini, kama vile mwenyeji alilizungusha na kwenda kuligesha mahali yalipokuwa yameegeshwa magari mengine! Hali ilikuwa kimya na hapakuwa na ulinzi wowote ndani! Baada ya kuliegesha aliruka na kutua chini, akafunga mlango na kuanza kutafakari nini cha kufanya, alikuwa na uhakika Lucille alikuwa katika moja ya vibanda vilivyokuwemo ndani ya ngome hiyo lakini hakuelewa ni kibanda gani na asingeweza kuvamia chochote na kuanza kupekua, hiyo ingemaanisha hatari kubwa kwake! Ilikuwa ni lazima atumie akili nyingi.
Akiwa katika mawazo hayo mara ghafla alishtukia mtu mmoja akija kwa nyuma yake na kumsemesha kwa lugha ya kiarabu, aliielewa lugha hiyo kidogo sana si kiasi cha kuongea na mtu yeyote! Alihisi kama angefungua mdomo wake kuongea lazima angeingia matatani, alikaa kimya na kusubiri mtu huyo amsogelee zaidi.
“Uko chini ya ulinzi! Hutakiwi kupiga kelele au kufanya lolote, kwa usalama wako naomba unieleza mahali alipo Lucille!” Dennis aliuliza kwa lugha ya kiingereza.
“Wewe nani?”
“Hutakiwi kuniuliza jina langu tafadhali toa jibu haraka!”
“Siwezi!”
Ni hapo ndipo Dennis alilikumbuka kopo la Ethly Chroride lililokuwa kiunoni mwake, akalichomoa haraka na kumpuliza mtu huyo puani, dakika mbili baadaye alilegea na kuanza kuingia usingizini! Huo ndio ulikuwa wakati muafaka kwa Dennis kuuliza maswali yake na kujibiwa, alianza kuuliza moja baada ya jingine na mtu huyo mwenye ndevu nyingi aliyajibu bila ubishi akiwa nusu usingizini, ndio maana dawa hiyo iliitwa na watu wengi Nusu Kaputi!
“Yuko kule nyu...ma kwenye kibanda am....bacho kipo karibu na tan....ki!” Aliongea mwanaume huyo bila kujitambua
Dennis alinyanyua kichwa chake na kuangalia mbele, kweli alikiona kibanda kilichotajwa na bila kupoteza muda alimwongezea mtu huyo dawa kisha yeye kuanza kutembea taratibu kuelekea kwenye kibanda hicho, alipokifikia alizunguka nyuma hadi dirishani na kuchungulia! Msichana alionekana akiwa amekaa kwenye kiti na kufungwa kamba kila sehemu usoni akiwa amefungwa na kitambaa cheusi. Bila kutegemea alisikia watu wakiongea mbele ya kibanda hicho tena wakitembea kuelekea nyuma alikokuwa, mwili wake ulitetemeka akiamini mapambano mengine yalikuwa yamewadia.
Je, nini kitaendelea? Atafanikiwa kuondoka na Lucille akiwa salama? au ndio mwisho wake? Fuatilia wiki ijayo.
Dennis ni kijana mpelelezi wa Kitanzania alifikiri amemaliza kazi kumbe nyingine kubwa zaidi ilikuwa mbele yake, akiwa nchini Marekani alikokwenda kupumzika baada ya kugundua mahali zilipoficha silaha za maangamizi na kuzikabidhi mikononi mwa Wamarekani na majeshi mengi ya Ushirika yaliyokuwa nchi Irak na akiamini msichana aliyempenda Lucille ni marehemu, ghafla anagundua msichana huyo bado yuko hai na ametekwa na majeshi ya Irak na zimetolewa siku tano kabla msichana huyo hajachinjwa kama walivyochinjwa mateka wengine wa majeshi ya kigeni yaliyoko nchi Irak!
Dennis analia machozi baada ya kugundua ukweli huo, ni lazima afanye kila kinachowezekana kumwokoa Lucille. Bila kuchelewa anaripoti makao makuu ya ya CIA na kukutana na Mkurugenzi, anamweleza nia yake ya kurudi Irak tena na kukubaliwa, ndege iliyomsafirisha Dennis peke yake inaondoka Marekani na kufika Basra masaa machache baadaye.
Huko Dennis anaunda kikosi cha makomandoo kwa ajili ya ukombozi wa Lucille na wote wanaondoka kuelekea kambi ya Nashiif huko ndiko Lucille amefichwa akipata mateso huku akisubiri siku yake ya kuchinjwa, anayewaelekeza njia za kuelekea katika kambi hiyo ni kijana wa Kiirak, Said! Hakuna mtu hata mmoja kati yao anayejua kuwa kijana huyo ni kibaraka, wakati wanagundua walikuwa wamechelewa kwani bomu alilolibeba kijana huyo lililipuka likamuua yeye na makomandoo wengine wote isipokuwa Dennis ambaye ananusurika kwa sababu hakuwepo eneo la tukio.
Hii haimkatishi tamaa, baadaye Dennis anasonga mbele kwa kutumia gari la wanajeshi wa Irak aliloliteka na kwenda moja kwa moja hadi ndani ya kambi ya Nashiif bila kugundulika, humo anamteka mwanajeshi mmoja na kumwamuru aonyeshe mahali Lucille alipofichwa! Anakataa, hapohapo Dennis anatumia dawa ya Ethyl Chloride kumlewesha mwanajeshi huyo, akiwa katika hali ya kulewa anamtajia kibanda alimofichwa Lucille. Dennis anamwachia na kusonga mbele hadi kwenye kibanda hicho na kuzunguka nyuma yake, alipochungulia ndani alimwona Lucille akiwa amefungwa kwenye kiti, wanajeshi wote waliokuwemo ndani ya kibanda hicho wakiwa usingizini.
Kwa Dennis hii ni nafasi muafaka ya kumkomboa mwanamke aliyempenda na aliyefikiria awe mke wake baada ya mapambano hayo lakini kabla hajafanya lolote anasikia sauti za wanajeshi wa Kiirak wakiongea huku wakitembea kuelekea mahali alikojificha. Je, nini kitatokea? Endelea..............
*************************
"Wacha waje, leo ndio watatambua kuwa mimi ni mtoto wa Kitanzania tena niliyekulia Mwananyamala!î Aliwaza Dennis akiwa amenyooka sambamba na ukuta wa kibanda alimokuwa Lucille, kwa kanzu na kilemba alichovaa alikuwa na uhakika isingekuwa rahisi kwa watu hao kumgundua, mkononi kushoto alishikilia kopo la Ethyl chloride na mkono wa kulia alishikilia bunduki yake aina ya LMG iliyojazwa risasi tayari kwa kazi, hakuwa na hofu yoyote moyoni mwake, tayari alishajihesabu mshindi kama tu alifanikiwa kuingia ndani ya kambi hiyo bila mtu kugundua, watu hao walizidi kutembea hadi hatua mbili kutoka mahali aliposimama.
ìAsalam Aleikum!î Waliongea wote kwa pamoja.
ìHawa nikiwajibu noma!î Aliwaza Dennis.
ìAsalam Aleikum!î Walizidi kumsalimia, Dennis aliona wazi watu hao walikuwa wakimzingua alichofanya kwa haraka na kwa kasi ya radi alinyoosha mkono wake wa kushoto kuwaelekezea watu hao, walionekana kuduwaa na hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya Dennis kufanya kazi yake.
ìPsiiiiiiiiii!Psiiiiiiiiiii!Psiiiiiiiiiii!î Ulikuwa ni mlio wa hewa ikitoka katika kopo la Ethyl Chloride alilolishika Dennis katika mkono wake wa kushoto, hewa hiyo ilitembea sawa sawa kwenye pua za waarabu hao na akashuhudia wote wawili wakienda chini taratibu na kulegea, kilichomsaidia yeye ni vidonge vya kuzuia kuathirika na dawa ya Ethyl Chloride alivyomeza, hakushikwa na usingizi, kulewa wala kulegea mwili.
ìNilisema mimi mtoto wa Mwananyamala bwana! Bila uzoefu wa mtaani hapa huwezi kuondoka salama!îAlisema Dennis akiwaruka watu walioanguka mbele yake na kusonga mbele, kwa mara ya kwanza katika muda wa masaa sabini na mbili alitabasamu akiwa peke yake, alitamani awepo mtu mwingine wa kushangilia naye ushindi huo au kuonyesha alama ya dole lakini kwa sababu alikuwa peke yake na alitaka kufanya hivyo kuifurahisha nafsi yake, aliiweka bunduki kwapani mkono wa kushoto kisha kunyanyua dole lake la mkono wa kulia na kujionyesha mwenyewe usoni kama alama ya ushindi.
ìNifanye nini sasa wakati niko peke yangu? Si mbaya nikijifagilia mwenyewe, waa- waaa!î Alisema kwa sauti ya chini Dennis huku akitabasamu, kilikuwa kitendo cha kitoto na cha kuchekesha lakini alikifanya kama njia ya kujipongeza na kufurahia ushindi alioupata, haikuwa kazi rahisi kuingia ndani ya kambi ya Nashiif na kufanya vitendo alivyokuwa akivifanya bila kugundulika. Alikata kona haraka haraka kama afanyavyo Celestine Babayaro wa Nigeria akiwa katika harakati za kuelekea kwenye goli la timu pinzani na zikiwa zimebaki dakika mbili mpira uishe Nigeria ikiwa nyuma kwa goli moja.
Kilikuwa ni kitendo cha kasi ya sauti, tayari Dennis akawa amezunguka mbele ya kibanda bila kugundulika, alishangaa kukuta mlango uko wazi na kuusukuma kisha kuingia hadi ndani ambako alikuta watu wote wapo usingizini, ili kuwalaza zaidi alipulizia tena Ethyl Chloride na kutembea harakaharaka hadi mahali alipokuwa amefungwa Lucille, shingo yake ilianguka kifuani akiwa usingizini! Dennis hakutaka kupoteza muda, alichokifanya ni kuchomoa kisu kilichokuwa kimechomekwa kwenye mkanda pembeni mwa suruali yake na kuanza kuzikata kamba zote zilizomfunga, Lucille akawa huru!
Bila kuamini kama kazi ya kumfikia na kumkomboa ilikuwa imekwisha kwa urahisi kiasi hicho, Dennis alimnyanyua na kumbeba kwenye bega lake la kushoto na kumshikilia vizuri, mkono wake wa kulia ukiwa na bunduki yake iliyokuwa tayari kufanya lolote kulinda uhai wake na wa Lucille! Alitoka hadi nje na kuangaza huku na kule lakini hakumwona mtu, akakatiza taratibu hadi lilipokuwa gari lake, hakuwa na uhakika wa kufika eneo hilo salama lakini alitaka kujaribu, alipolifikia gari na kumpakia Lucille ndani yake ndipo akaamini kazi ilikuwa imemalizika.
ìSasa ni safari kuelekea Basra, bila shaka hawa wajinga langoni hawatakuwa na kizuizi!î Aliwaza Dennis akikaa kwenye usukani na kuliwasha gari kisha kuondoka kuelekea langoni ambako kwa mshangao kuona kama ilivyotokea wakati anaingia, maaskari wakimfungulia bila kuuliza hata swali moja tena wakipiga saluti kuonyesha heshima! Hakuyaamini macho yake, kirahisi kabisa akawa ameondoka na Lucille ambaye bado alikuwa hoi bin taaban kwa usingizini uliosababishwa na dawa aina ya Ethly Chloride.
Aliendesha gari kwa kasi ya ajabu na mbele kidogo eneo bomu lilipolipuka na makomandoo wenzake wote kuuawa hapo aliliegesha gari pembeni mwa barabara na kumshusha Lucille kisha kukimbia naye hadi kwenye gari alilosafiri nalo kutoka Basra lililokuwa limefichwa porini na kumpakia Lucille ndani yake kisha kuanza kulirudisha kinyumenyume hadi barabarani. na kuondoka tena kwa kasi ya ajabu akielekea Basra alikofika masaa manne baadaye akiwa amechoka hoi bin taaban, hakuna mtu aliyekuwa tayari kuamini kuwa kweli Dennis alikuwa amefanikiwa kumkomboa Lucille akiwa hai ingawa kwa gharama ya makomandoo ishirini waliokufa kwa kulipukiwa na bomu la kijana wa kujitoa mhanga.
Alisimulia kila kitu kilichotokea na makomandoo wote walishangilia na kumpigia makofi na walikiri hapakuwahi kuwa na Mwanajeshi wa aina hiyo katika historia ya nchi ya Marekani ndani ya vita vyote ambavyo nchi hiyo ilipigana ikiwemo ya Vietnam ambayo Marekani kamwe haitaisahau! Dennis hakutaka kubaki tena nchini Irak kwani kazi mpya iliyokuwa imejitokeza alikuwa ameimaliza! Alichofanya asubuhi hiyo ni kuondoka kwa ndege aliyokuja nayo kurejea Marekani akiwa na Lucille.
Ulikuwa ushindi mkubwa sana kwake kwa kukamilisha kazi mbili ngumu, kwanza ile kugundua mahali silaha za maangamizi ambazo wakaguzi wa Umoja wa Mataifa walishindwa kufahamu zilipofichwa. Pili, ya kumkomboa Lucille, kwa hakika sifa zake zilikuwa zimeongezeka hasa alipojumuisha na ile ya utatu wa hatari aliyoikamilisha miezi michache kabla. Moyo wake ulijaa furaha na ndege ilikwenda kwa kasi isiyo ya kawaida angani kwa masaa karibu mawili ya safari hiyo macho ya Dennis yalikuwa usoni kwa Lucille akiangalia kama angezinduka na kumwangalia lakini hiyo haikutokea na kwa sababu ya uchovu mkubwa aliokuwa nao naye alijikuta akipitiwa na usingizi na kuzinduka wakati ndege ikitua katika uwanja wa ndege, tayari alikuwa nchini Marekani!
Kabla hata ya kushuka alichungulia dirishani kuona watu wengi wakipeperusha bendera za Marekani, Umoja wa Mataifa na Tanzania ilikuwa ni siku ya furaha kupita kiasi nchini Marekani sababu ya ushindi ambao Dennis aliiletea nchi hiyo. Alipoangalia vizuri katikati ya watu hao aliweza kumwona Rais wa Marekani, Bw Caesar Leon na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Dick Johnson na wakuu wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vinyweleo vya mwili wa Dennis vilisimama wima na mwili kumsisimka sababu ya furaha kubwa aliyokuwa nayo moyoni mwake, machozi yakamtoka. Ghafla alishtuka alipoguswa begani mwake, hakusita kugeuza shingo yake.
ìDennis!î Ilikuwa ni sauti ya Lucille
ìLucille!î Dennis aliita
ìNi wewe au naota?î Lucille akauliza.
ìNi mimi!î
ìHapa tuko wapi?î
ìNdio kwanza tumetua Washington!î
ìWashington?î
ìNdio!î
ìNani ameniokoa kutoka Nashiif?î
ìNi habari ndefu nitakusimulia baadaye, kwanza tushuke Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza wanatusubiri chini! Unaweza kutembea peke yako?î Aliongea Dennis na kisha kuuliza swali, Lucille hakuweza kujibu swali hilo kilichotokea ni kububujikwa na machozi akiwa amemkumbatia Dennis.
ìDennis niambie nani ameniokoa?î
Je, nini kitaendelea? Fuatilia wiki ijayo.
Dennis amefanikiwa kuonyesha mahali silaha za maangamizi zilipofichwa na bado amefanikiwa tena kurudi Irak na kumkomboa Lucille! Huu ni ushindi mkubwa, hivi sasa yeye na Lucille wanashuka uwanja wa ndege huko Washington DC ambako Rais wa Marekani pamoja na waziri mkuu wa UIngereza wako tayari kuwapokea mashujaa hawa lakini Lucille mpaka sasa haelewi ameokolewa na nani, anajaribu kumuuliza Dennis lakini hayuko tayari kumweleza.
Je, nini kinafuata katika sehemu hii ya mwisho? Endelea.....
L
ucille alikuwa haamini ma cho yake kama kweli alikuwa ndani ya ndege pamoja na Dennis, halikuwa jambo rahisi kukuba kwani kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu zake na kuziweka sawa, alijikuta yupo katika chumba akiwa amefungwa kwenye kiti na watu wengi wakiwa wamemzunguka tena akiwa amekata tamaa kabisa akihesabu masaa kabla hajachinjwa kama ilivyotokea kwa mateka wengine waliotekwa nchini Irak! Alishindwa kuelewa nini kilitokea mpaka akawa hapo na kilichomchanganya zaidi ni kauli ya Dennis kwamba tayari walikuwa Washington, hakuamini lakini alipotupa macho yake kupitia dirishani aliutambua uwanja wa ndege.
“Kweli tupo Marekani!”
“Ndio na Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza wapo chini wanatusubiri!”
“Dennis tafadhali niambie ni kitu gani kimetokea? Ni wewe umeniokoa?”
“Nitakueleza baadaye kwa sasa tumshukuru Mungu kwamba tumefika salama!”
Dennis alimnyanyua Lucille kutoka kitini na kuanza kumsaidia kutembea wakizifuata ngazi na baadaye kuanza kushuka chini, idadi kubwa ya watu iliyokuwepo uwanja wa ndege iliwashangaza wote wawili! Watu walikuwa wakishangilia na kuwaita mashujaa, walishindwa kuvumilia na kujikuta wakimwaga machozi ya furaha. Zulia jekundu lilikuwa limetandikwa chini na hapo ndipo walipokanyaga na kupokelewa na Rais wa Marekani Bw.Caesar Leone ambaye aliwatambulisha kwa Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Dick Johnson pamoja na viongozi wengine waliokuwepo.
“Welcome to America Dennis and Lucille, my country is very proud of you guys, you have done a great job!”(Karibuni Marekani Dennis na Lucille, Taifa langu linajivunia sana ninyi kwani mmefanya kazi kubwa!)
“Thanks! Making the World a better place for living is every mankind’s responsibility, when it comes to world peace there is no America, Tanzania, Kenya, Nigeria or Argentina! We have to come together!”(Ahsante! Kuifanya dunia mahali pazuri pa kuishi ni wajibu wa kila mwanadamu aishie, linapokuja suala la amani ya dunia, hakuna Marekani, Tanzania, Kenya, Nigeria au Argentina ni lazima tuwe pamoja!) Aliongea Dennis akiwasalimia viongozi mbalimbali wa Marekani waliokuwepo uwanja wa ndege na baadaye walivishwa mashada ya maua na kuondoka hadi katika chumba kilichoandaliwa rasmi ambako walisaini vitabu vya wageni.
Kutoka uwanja wa ndege walikwenda moja kwa moja hadi Ikulu ya Marekani ambako madaktari waliitwa kupima afya ya Lucille na kugundua hapakuwa na tatizo kubwa zaidi ya majeraha waliyoyashughulikia mara moja, ilikuwa ni furaha kubwa kwa kila mtu lakini moyoni mwa Lucille bado hakuridhika, alitaka sana kuelewa nini kilitokea mpaka akakombolewa kutoka mikononi mwa wauaji wa Kiirak mara kwa mara alimuuliza Dennis lakini hakuwa tayari kumweleza, alizidi kumwomba avumilie akidai yalikuwa maongezi marefu.
Wakiwa Ikulu walipewa nafasi ya kupiga simu nyumbani na kuwataarifu wazazi wao kwamba walikuwa hai, Lucille aliongea na wazazi wake pamoja na rafiki zake nchini Kenya na kuwathibitishia kwamba alikuwa akipumua hewa ya Mungu! Pamoja na kuongea na waandishi wa habari uwanja wa ndege bado kila walikokwenda walifuatwa na waandishi wa habari na kila tukio lilionekana moja kwa moja kwenye televisheni dunia nzima, watekaji wa Irak kule Nashiif hawakuamini walichokiona kwenye luninga, hawakuelewa ni saa ngapi Dennis aliingia na kumkomboa Lucille! Lakini maiti zilizoonekana barabarani pamoja na watu waliolala usingizi mzito baada ya kupuliziwa dawa, walipozinduka walieleza kila kitu kilichotokea, wakakiri Dennis hakuwa mtu wa kawaida.
“Sasa itabidi mkapumzike kidogo, baadaye jioni tutakuwa na dhifa maalum iliyoandaliwa na Rais wa Marekani kwa ajili yenu! Itafanyika hapahapa Ikulu, kwa hiyo tunawachukua kuwapeleka kwenye nyumba ya wageni hapa Ikulu mpaka saa moja ya usiku tutakapokuja kuwachukua
Walipewa nyumba maalum ya kuishi Ikulu wakisubiri muda huo, kila mtu na chumba chake lakini Lucille hakutaka kukaa peke yake chumbani na kuamua kuhamia kwenye chumba cha Dennis ambako kiu yake ya kutaka kufahamu kilichotokea iliendelea kumsumbua, hakutaka kumpa Dennis nafasi zaidi alisisitiza aelezwe ukweli.
“Dennis tafadhali niambie nani aliniokoa?”
“Ni mimi Lucille!”
“Kweli?”
“Ndio!”
“Ulijuaje nilikuwa kule wakati ndege tuliyosafiri nayo wakati ule ililipuliwa? Mimi nilijua utakuwa unaamini nilikufa katika ajali ya ndege!”
“Ni kweli kabisa! Hicho ndicho kitu nilichoamini, nilisikitika sana na niliahidi kupigana hadi mwisho mpaka silaha zipatikane kwa ajili yako, kazi hiyo ilipokwisha nilikuja hapa Marekani kupumzika, ndipo siku moja nikisoma gazeti nikaona sura yako ukiwa umetekwa na magaidi, sikuwa na la kufanya zaidi ya kurudi tena Irak kukukomboa!”
“Ulifanyaje?”
“Mbinu za kijeshi zilitumika, nikaingia hadi kambini Nashiif na kukukomboa bila wanajeshi wa Irak kunigundua, ila makomandoo wote niliokuwa nao walikufa kwa kulipukiwa na bomu, kijana tuliyembeba ili atuonyeshe njia ya kutufikisha Nashiif kumbe alikuwa muuaji wa kujitoa mhanga, ilikuwa ni bahati yangu vinginevyo na mimi mwenyewe ningekufa bila kukuona!” Aliongea Dennis na baadaye kumsimulia Lucille aliyekuwa akilia mfululizo kwa furaha kila kitu kilichotokea na tayari walikuwa wamekumbatiana.
“Dennis una mpango gani na mimi?”
“Kuhusu nini Lucille?”
“Kwanini tusioane?”
“Ni kweli niliwahi kulifikiria jambo hilo lakini nimebadili mawazo, haiwezekani tena, tunahitaji muda wa kufahamiana zaidi!”
“Dennis! Binadamu huwa wanakutana kwa sababu maalum, mimi naamini tuko hai ili hatimaye tuishi pamoja na kuzaa watoto!”
“Hilo siyo rahisi kuliongelea sasa hivi!”
Tayari Lucille alikuwa katika mapenzi mazito, alichotaka wakati huo ni ndoa tu na si kitu kingine chochote lakini Dennis hakuwa tayari, alimbembeleza kwa muda mrefu lakini bado alikataa na kusisitiza wawe marafiki wa kawaida kwani kila mmoja aliokoa maisha ya mwenzake!Hawakuweza hata kupumzika, walichofanya ni kujiandaa kwa ajili ya Dhifa ya Kitaifa, nguo kutoka duka maarufu la wabunifu wa mitindo la Styles zilikuwa zimeletwa kwa saizi mbalimbali ili wachague ambazo wangeweza kuzivaa jioni hiyo, kila mtu alichagua na walishauriana mpaka wakawa na uhakika kwamba wamependeza ndipo wakakaa kusubiri, tayari ilikuwa saa kumi na mbili na nusu na ilipogonga saa moja jioni mlango wa chumba cha Dennis uligongwa, alinyanyuka na kufungua! Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa nje akiwataarifu kuwa muda wa kwenda kwenye dhifa ya Kitaifa ulikuwa umefika.
“Are you ready for the party!”(Mpo tayari kwa sherehe) Aliongea Waziri akitabasamu.
“We are, not only ready but anxious!”(Tupo tayari, si tayari tu bali tunatamani sana kwenda!)
“Lets go then!”(Twendeni basi!)
Walitoka nje na mlango ukafungwa kisha wakaondoka hadi nje ambako waliingia katika gari maalum lililoandaliwa na msafara ukaanza kuelekea kwenye ukumbi ulioitwa White Pigeon, maalum kufanyia sherehe za Kitaifa! Tayari Dennis na Lucille walikuwa watu maarufu duniani, walipoingia ukumbini watu wote walinyanyuka na kuanza kupiga makofi! Dennis na Lucille walibubujikwa machozi ya furaha, hawakuamini kilichokuwa kikitokea, karibu kila mtu maarufu nchini Marekani alikuwepo ndani ya ukumbi huo, Dennis aliwaona watu kama Mohamed Ali, Magic Johnson, Mchungaji Jesse Jackson, Tiger Wood, Michael Jackson na wote walitamani kumshika mkono na kumpongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya.
Hapakuwa na shughuli nyingine ya kufanya katika ukumbi huo zaidi ya kula, kunywa na kufurahi, Dennis na Lucille waliweka sahihi katika vitabu vya watu mbalimbali waliokuwepo, baadaye walipewa nafasi ya kuhutubia, hawakuwa na mambo mengi ya kuongea zaidi ya kuwashukuru Wamarekani kwa wema waliouonyesha kwao na kuketi vitini.
“Dennis you can choose anything you want as a prize for what you have done for America! Anything! Anything! I’m repeating again and again, ANYTHING YOU WANT, EVEN MY DAUGHTER TRACY BUT NOT MY WIFE!”(Dennis unaweza kuchagua chochote kama zawadi kwa mambo uliyoifanyia Marekani! Chochote!Chochote narudia tena na tena! Chochote unachohitaji, hata kama ni binti yangu Tracy lakini usiseme mke wangu!) Rais wa Marekanialiongea akicheka na ukumbi mzima ukapiga makofi na kushangilia, Dennis aliangaza macho yake huku na kule kumwangalia huyo mtoto wa Rais alikuwa yupi lakini hakugundua.
“Is the Presindent’s daughter here?”(Mtoto wa Rais yuko hapa?)
“She is the one sitting on the front row, second from right!”(Ni yule aliyekaa kwenye mstari wa kwanza, wa pili kutoka kulia!)
“My God! She is the most beautiful thing my eyes have ever come across!Look at God’s creation! You can not believe she is a human being!”(Mungu wangu! Huyu ndiye mwanamke mzuri kuliko wote ambao macho yangu yamewahi kuwaona! Hebu angalia uumbaji wa Mungu! Huwezi kuamini kwamba ni binadamu!) Dennis alijikuta akitamka maneno hayo na alipogeuka kumwangalia Lucille alikuwa akilia, kitu kama mwiba ulimchoma moyoni akakumbuka wema ambao msichana huyo alimfanyia, hakuwa mbaya wa sura na hapohapo alijikuta akibadili msimamo wake.
“I made up my mind, will marry you Lucille because I love you!”(Nimebadili msimamo wangu, nitakuoa Lucille kwa sababu ninakupenda!)
“I love you too Dennis! I promise to be faithful to you”(Nakupenda pia Dennis na ninaahidi kuwa mwaminifu kwako!)
Dennis alipopewa nafasi ya kuongea tena hakuwa na la kuchagua kama zawadi, aliachia Serikali ya Marekani iamue cha kufanya, Rais akasimama na kutangaza kuwa Dennis na Lucille walikuwa wamepewa uraia wa Hisani wa jiji la Washington pamoja na dola milioni ishirini kwa Dennis na kumi kwa Lucille, kila mtu alishangilia na wiki moja baadaye waliondoka kurejea Tanzania ambako pia walipokelewa kama mashujaa, hapakuwa na kitu kingine cha kufanya zaidi ya kufunga ndoa, Dennis akastaafu kazi ya upelelezi na kuanzisha biashara zake binafsi akijihusisha na uuzaji wa Madini nchi za nje, yeye na mke wake ndio walikuwa Wakurugenzi wa kampuni hiyo.
“Dennis umesikia?”
“Nini?”
“Profesa Cheznob, Rais wa zamani wa Irak Seleiman Al-Mahmoud na Alfonso Gonzalez Cardoso wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa ukatili walioufanya!”
“Nani amekueleza?”
“Niliona leo kwenye taarifa ya habari ya CTV!”
“Achana nao! Watu hao ni hatari kwa amani ya dunia!”
Mwisho.
Post a Comment