ad

ad

AWADHI JUMA ATOA BAO LAKE ZAWADI KWA MKEWE, WATOTO WAKE



Kiungo nyota wa Simba, Awadhi Juma ambaye amefunga bao pekee katika mchezo wa leo na kuiwezesha Simba kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Prisons, amelitoa zawadi.

Juma amelitoa bao hilo zawadi kwa mkewe na watoto wake kutokana na kumuunga mkono huku akiwashukuru mashabiki na viongozi wa Simba.

“Mke na watoto wangu ambao wamekuwa wakiniunga mkono muda wote, hii ni zawadi yao,” alisema Juma.


Kiungo huyo aliingia katika dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Justuce Majabvi aliifungia Simba bao safi katika dakika ya 87 akipiga shuti kali nje ya 18 na kuipa Simba ushindi safi.

No comments

Powered by Blogger.