Wema Hamjui Mwenye Mimba, Ampa Idris 50% na Mbunge 50%
Wema Sepetu ‘Madam’
Na Mwandishi Wetu, Risasi
DAR
ES SALAAM: Habari zinazosambaa kwa kasi ya ajabu kama moto wa kifuu
zinaeleza kuwa, mtoto mzuri ndani ya Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’
mbali na taarifa za kuwa mjamzito, hadi sasa bado yupo kwenye wakati
mgumu kuweza kutegua kitendawili cha nani mmiliki halali wa kiumbe
kilichopo tumboni mwake, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.
Hivi
karibuni, magazeti tofauti ya Global Publishers ndiyo yalikuwa ya
kwanza kuripoti kuhusu uwepo wa mimba ya mlimbwende huyo asiyechuja
Bongo, ambapo awali, vyanzo mbalimbali vilieleza kuwa mhusika ni mbunge
mmoja machachari ambaye ndiye anayemuweka Wema mjini kwa sasa.
Kitumbo cha Wema Sepetu
MAJIBU YA WEMA ALIPOBANWA
Kwenye
habari ya awali iliyoripotiwa na gazeti la Ijumaa, Wema alipotafutwa
kusomewa mashitaka yake kuwa ana ujauzito wa mbunge huyo, kupitia simu
ya shosti wake, Aunt Ezekiel, staa huyo hakutaka kufunguka sana kuhusu
mbunge huyo zaidi ya kusema; “ndiyo nina mimba, tena ya miezi sita.”
UBUYU MPYA SASA
Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini, Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006
amejiridhisha kuwa ni mjamzito baada ya kupima kwenye hospitali moja
maarufu (jina tunalo) na kuondoka na furaha ya ajabu lakini kitendawili
alichoondoka nacho ni kuwa hamjui mhusika wa kiumbe hicho.
WOTE AWAPA ASILIMIA 50
“Madam
alifurahi kweli maana suala lililokuwa linamnyima usingizi siku zote ni
kutopata mimba. Baada ya furaha hiyo, ishu ikawa ni kumtambua mhusika
kwani kwa nyakati tofauti ameshabanjuka kimalavidavi na mshindi wa Big
Brother Hot Shot 2014, Idris Sultan na mbunge yule anayempa jeuri ya
pesa kwa sasa, wote amewapa asilimia hamsini hajajua nani hasa ndiyo
mhusika,” kilisema chanzo hicho.
WOTE WAWILI KAWAMILIKISHA
Chanzo
hicho kilizidi kutiririka kuwa, baada ya kuona ameshachanganya madawa,
Madam aliamua kila mmoja kumwambia kuwa ‘mzigo’ huo ni wake hivyo wote
kwa pamoja na nyakati tofauti wanahudumia na kumjali staa huyo, tena kwa
nguvu zote.
“Yaani
kila mmoja kamwambia mimba yake. Wote wawili wamezipokea taarifa za
ujauzito kwa bashasha huku kila mmoja akijiamini kuwa ni mhusika pasipo
kujua Madam hajui nani hasa ndiye halisi.
MBUNGE, IDRISS ‘FULL’ KUHUDUMIA
“Yani
ni full kuhudumia. Mbunge kwa wakati wake amekuwa akimwaga chapaa kama
hana akili nzuri. Amelipia nyumba ile ya Ununio jijini Dar na kama hiyo
haitoshi, amekuwa akisimamia shopping za maana tu mjini na hata ile
ndiga aliyojizawadia Wema katika sherehe yake ya kuzaliwa, mbunge huyo
alihusika katika malipo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Idris naye si haba. Anajitutumua kwa upande wake, anaamini kwamba mzigo ni wake bila kujua mimba hiyo ina figisufigisu.”
IDRIS ASAKWA, AFUNGUKA
Gazeti hili lilimtafuta Idris kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopokea, alitiririka hivi:
Risasi: Mzee tumepata habari kwamba wewe ndiyo mhusika wa mimba ya Madam, vipi unazungumziaje taarifa hizo?
Idris: Kwenye hilo kwa sasa siwezi kuliongelea, labda unipe mwezi mmoja. Kichwa changu hakijatulia.
Risasi: Lakini inasemekana unagharamia kila kitu kwa sasa, ukiamini mzigo ni wako?
Idris: Aaa! Acha kuniingizia hayo mambo bwana. Wewe subiri huo mwezi mmoja ukipita nitakueleza kila kitu.
SHOGA ZAKE WAMSHANGAA!
Mashosti
wake waliozungumza na Gazeti hili ambao hawakutaka kutajwa majina yao,
walisema ni jambo la kushangaza kwa mwanamke kushindwa kumjua mwanaume
aliyempa ujauzito.
WEMA ANASEMAJE?
Gazeti
hili lilifanya jitihada za kutosha kumsaka Wema kwa kumpigia simu na
kumtumia ujumbe mfupi lakini hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
KUTOKA KWA MHARIRI
Mimba
ni jambo la kheri hivyo kwa kuwa Wema ameziona simu za wanahabari wetu
zikimuuliza juu ya mhusika wa kiumbe hicho, ni vyema akawapigia na
kuanika kila kitu kuhusu habari hii.
CHANZO: Global Publishers (GPL)

Post a Comment