Zari kumuunganishia Harmonize kwa Huddah Monroe
Mpenzi
wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ anadaiwa
kumkuwadia dogo anayeishi na kufanya kazi ya muziki na Diamond, Rajabu
Abdulkhali ‘Harmonize’ kwa mrembo maarufu Afrika anayeishi Kenya, Huddah
Monroe.
Chanzo
chetu kilicho karibu na mastaa hao kilitutonya kuwa, Zari na Huddah
walikuwa nchini Kenya ambapo Diamond akiwa na Harmonize walitua huko kwa
mambo yao ya kisanii.
“Harmonize na Diamond walipotua airport, Zari na Huddah ndiyo waliowapokea. Wakawachukua mpaka hotelini.
“Walipofika,
baba na mama Tiffah wakawa bize na yao, hapo ndipo Zari alipomchombeza
Huddah ajiweke kwa Harmonize. Si unajua tena Huddah naye hajatulia,
hakukataa na ndipo dogo akajichukulia mzigo na kwenda nao chumba
kingine,” kilidai chanzo hicho.
Kikazidi kudai kuwa, walichokifanya huko wanakijua wenyewe ila walipigana picha na kurekodiana video zikiwaonesha kimahaba.
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, Ijumaa
lilifanikiwa kunasa baadhi ya picha zikimuonesha Huddah na Harmonize
wakiwa ‘romantic’ ikiwa ni pamoja na clipu ikiwaonesha wakishikana na
kuchezeana kimalovee.
Harmonize atafutwa
Jitihada
za kumpata Harmonize zilifanyika kupitia simu yake ya mkononi na
alipopatikana alisema ni kweli alipokuwa Kenya alifanikiwa kukutana na
Huddah, akakiri kuwa aliyewaunganisha ni Zari.
“Unajua
mimi sikuwa nikimjua Huddah, nilikuwa nikimuona kwenye TV na magazeti
tu. Sasa tukiwa kule Zari aliponiona niko mpwekempweke, ndiyo akaniweka
pale, mambo mengine ni siri yetu bwana,” alisema dogo huyo anayefanya
vizuri kwenye muziki.
Huddah ni nani?
Ni modo anayefanya shughuli zake nchini Kenya lakini amekuwa akishaini Afrika kutokana na skendo zake za kupiga picha za utupu.
Mrembo
huyo aliwahi kuingia kwenye bifu zito na Mtangazaji wa Clouds, Loveness
Malinzi ‘Diva’ chanzo kikiwa ni Mwanamuziki Jackson Makini ‘Prezzo’
aliyekuwa mpenzi wa Huddah lakini akachepukia kwa Diva.
Mbali na habari hii, soma makala inayowahusu Harmonize na Huddah ukurasa wa 11.
CREDIT: GPL
Post a Comment