Mwili wa Dotto Mzava wa JF wasafirishwa kwenda Same kwa mazishi
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa
Mwandishi wa Habari wa Jamii Forum, Dotto Mzava likishushwa kwenye gari
maalum mara baada ya kuwasili katika Kanisa la Wasabato Manzese Uzuri
jijini Dar kwa ajili ya sala ya kabla ya kusafirishwa kuelekea Wilaya ya
Same Mkoani Kilimanjaro leo.
Mchungaji wa Kanisa la Adventist
Wasabato akiendelea na ibada wakati wa ibada ya kumuombea marehemu kabla
ya kusafirishwa kuelekea Same, Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Jamii Media, Maxence Mello akitoa historia fupi ya marehemu Dotto Mzava
ambae pia alikua mmoja wa watumishi katika kampuni hiyo.
Heshima za mwisho zikiendelea kutolewa.
Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John
Mnyika akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava
kabla ya kusafirishwa kuelekea Same, Kilimanjaro kwa mazishi
yanayotarjiwa kufanyika kesho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media
akitoa heshima za mwisho kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa
kuelekea Same mkoani Kilimanjaro mapema leo.
Picha na Richard Mwaikenda Blog

Post a Comment