ad

ad

HADITHI: RAHA YENYE MAUMIVU - 01


MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
Hali ya hewa katika mji wa Arusha ilikuwa ya ubaridi kila mmoja alikuwa na nguo nzito za kukabiliana na hali ya hewa. Ila kwa wenyeji wa mkoa huu walikuwa na nguo za kawaida kwao ile hali ya ubaridi kwao ilikuwa ya kawaida hata nguo walizovaa zilikuwa nyepesi tofauti na mgeni wa mkoa huo.
Katika hotel ya New Arusha kila mmoja alikuwa bize na unywaji wa pombe na utafunaji wa nyama choma. Mmoja ya waliokuwa wakipata moja moto moja baridi alikuwepo mama mmoja ambaye umri wake ulikuwa umekwenda kidogo lakini kutokana na uwezo wake wa kipesa alionekana bado.
Yule mama mmoja ya wafanya biashara wakubwa pia alikuwa wanawake wenye pesa nyingi. Pale Arusha alikuwepo kibiashara akiwa safarini nchi za Ulaya. Ni mkazi wa jiji la kila aina ya maraha jiji la Mheshimiwa Rukuvi hapo mwanzo lilijulikana kama jij la Muheshimiwa Kandolo.
Katika maisha yake alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 19 ambaye alikuwa yupo kidato cha tano moja ya shule za gharama nchini.
Kwa muda huo hakuwa na mume baada ya kuachana na mume wake, kwa jeuri ya pesa ilimpelekea kuachana na mumewe kwa kuona maisha ya ndoa ni utumwa ambao yalikuwa yakimwekea mipaka ya kazi zake.
Toka aachane na mumewe hakuwa na haja ya kuolewa tena na mwanaume zaidi ya akili yake kuielekeza kwenye biashara ambayo ilimfanya awe na uwezo mkubwa kipesa na kuwa na uwezo wa kufanya lolote atakalo.
Biashara zake zilivuka mipaka mpaka nje ya nchi alijikuta muda mwingi aliutumia kusafiri kwa ajili ya biashara zake hata jina lake lilikuwa moja na watu wenye uwezo wa kifedha jijini. Kitu kilichomfanya asiwe na wazo la kuolewa tena na kuchukulia mwanaume ni kitu cha starehe kwake.
Kutokana kuwa na pesa nyingi alipokuwa akishikwa na haja za kimapenzi alimhonga mwanaume yoyote amtakaye na amalizapo kumstarehesha huupa ujira ambao alijua lazima utamfurahisha hakuwa na bwana maalumu kwa kuogopa kuoneana wivu. Kitu kilichomfanya kuwa na uhuru wa kufanya mambo yake bila kuingiliwa na mtu.
Mam’ kubwa kama jina lake maarufu jijini Dar, akiwa jijini Arusha ambako alipita kufuatilia madeni yake akiwa njiani kwenda Uingereza baada ya kukusanya madeni yake alipanga kwenye Hotel ya new Arusha. Majira ya saa moja usiku alijumuika sehemu ya vinywaji kupata moja moto moja baridi.
Akiwa ametafuta meza ya pembeni aliagiza bia yake ya castle ya kopo na kunywa taratibu huku akifikiria safari yake ya asubuhi katika uwanja wa ndege wa KIA alikuwa amepanga kuondoka na ndege ya saa kumi na mbili asubuhi ya shirika la Gurf Air.
Pombe zilivyo kuwa zikimzidi kumpanda alijikuta akipata hamu ya kuwa na mwanaume kama kawaida yake alivutiwa na kijana mmoja aliyekuwa mhudumu upande wa uchomaji wa nyama. Kijana ambaye alikuwa akimletea nyama, wakati akiendelea kukata maji taratibu kama mamba mzee kwenye bwawa.
Wakati yule kijana akimletea maji ya kunawa alijikuta anamuuliza kwa sauti ya kilevi kidogo.
"Samahani kijana sijui unatoka kazini saa ngapi?"
"Muda si mrefu kuanzia sasa wanaokuja kutupokea wameisha ingia hapa najiandaa kwenda kuoga."
"Mmmmh sawa," alijibu huku akichukua kopo la bia na kupeleka kinywani.
"Kwani vipi?"
"Hapa Arusha una kaa wapi?" Alimuuliza baada ya kumeza funda ya pombe.
"Unga limited."
"Umeoa?"
"Maisha ya kuoa yapo wapi ma’ mkubwa, hela ninayo pata hailingani na hali halisi ya maisha. Mwenyewe tu maisha yananipeleka mchakamchaka huyo mwanamke nitamlisha hewa."
"Mmmh pole sana...Sasa ni hivi naomba kabla ya kuondoka tuonane shika na hii hela njoo na vinywaji nipo chumba namba 033 ...sawa."
"Sawa mama," yule kijana aliondoka kwenda kujiandaa kukabidhi kazi kwa wenzake, wakati huo mam’ kubwa alimsindikiza kwa macho alijua kijana kaisha nasa kwenye mtego wake.
Mam’ kubwa alibeba kinywaji chake kilichobakia na kwenda nacho chumbani kwake kusubiri mtego wake kama utanasa japo alikuwa na imani kwa asilimia 99%. Alipofika chumbani kwake alikwenda bafuni kuoga harakaharaka na kuvaa nguo nyepesi ya kulalia na nguo moja ya ndani.
Alipulizia mafuta yenye harufu nzuri na kukaa mkao wa mamba majini wa kumvizia mwanadamu. Akiwa anamalizia kinywaji chake alisikia mlango ukigongwa moyo ulimpasuka alimkaribisha.
"Pita mlango upo wazi," mlango ulifunguliwa na kuingia mkusudiwa alipomuona aliachia tabasamu pana.
"Oooh karibu sana."
"Asante," alikuwa ameshikia vinywaji alivyo agizwa.
"Karibu jisikie uhuru wa lolote utakalo nina imani usiku wa leo utakuwa pamoja nami," Mam’ Kubwa alisema huku akiachia tabasamu la jisikie huru.
"Hamna tabu mama."
"Usiniite mama niite Sweet."
"Hamna tabu Sweet."
"Ukinifurahisha na wewe nitakufurahisha, hutanisahau kama vile utavyonifanya nisilisahau penzi lako."
Kijana hakuwa nyuma waliendelea kupata vinjwaji huku wakipapasana hapa na pale kila mmoja akijitahidi kumfurahisha mwenzake. Muda ulipotimu kijana alitumia ujuzi wake wote kuhakiki anamkata jimama kiu.
Mtinange ulikuwa mzito uliomfanya kijana wa watu awe hoi kama dume la bata na kujikuta akipitiwa usingizi mzito. Penzi alilopewa jimama lilimrusha akili kama isingekuwa safari angeongeza siku za kuwepo Arusha ili kuendelea kukatwa kiu na kijana. Penzi ambalo anakumbuka alilipata wakati anavujwa ungo.
Jimama aliamka alfajiri ili kuwahi safari yake wakati huo kijana alikuwa bado amelala hajitambui. Hakutaka kumsumbua aliamua kumuachia pesa ambayo alijua itamsaidia maishani mwake na kumuachia ujumbe mfupi uliosema:
Mpenzi..Tino nina imani jana ilikuwa siku yangu ambayo itakuwa ya kuikumbuka maishani mwangu. Penzi ulilonipa sijui kama nitalipata tena.
Kama nilivyokuahidi nami sina budi kukupa zawadi ambayo itakusaidia kusogezea siku. Bakia salama Mungu akijalia tutaonana ni mimi mama Teddy.
Alikiweka kile kikalatasi na shilingi laki saba kwenye mfuko wa suruali wa kijana Augustino Tamilway kisha alimpiga busu kwenye shavu na kuondoka kuwahi usafiri wa ndege uwanja wa ndege wa kimatafa wa Kilimanjaro (KIA)
Aliwasiri kiwanjani nusu saa kabla ndege haijaondoka na kufuata taratibu zote zilizomwezesha kukamilisha taratibu za usafiri na saa kumi na mbili juu ya alama Mam’ kubwa au mama Teddy aliiaga anga ya Tanzania.

Nini kitaendelea? Endelea kufuatilia Mkasa huu.

Powered by Blogger.