Mjengo mpya ya Wema Sepetu Utata!..Upo ufukeni jijini Dar
UTATA umegubika kuhusu umiliki wa mjengo aliohamia staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ambapo maswali yanayowasumbua wengi ni je, ameingia kwa kupanga au ameununua? Amani linakwenda sambamba na msomaji.
TUANZIE HAPA
Hivi karibuni, Wema aliyekuwa akiishi kwenye nyumba ya kupanga iliyopo Kijitonyama ya Makumbusho jijini Dar, alidaiwa kutimuliwa na mwenye nyumba baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco) kumtumbua jipu la madai ya kuchakachua huduma hizo.
ATII AMRI, AHAMA
Wema aliihama nyumba hiyo usiku wa Ijumaa iliyopita lakini haikujulikana mara moja anakokwenda kuishi licha ya lori lililomhamisha, aina ya Toyota Canter kuandikwa nyuma, ‘Mtu Kwao’.
HABARI ZA JUMANNE SASA
Juzi Jumanne, chanzo kimoja kililipasha Amani kwamba Wema amehamia kwenye mjengo mkubwa na mzuri uliopo Ununio, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. “Jamani nilisoma habari kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda (ndugu na hili) la Jumatatu jana, zikisema kwamba Wema ametimuliwa kwenye ile nyumba ya Makumbusho lakini hamkusema amehamia wapi. “Sasa mimi nawapa ubuyu. Wema amehamia hapa Ununio. Amepata nyumba nzima, kubwa. Lakini nisiwe msemaji wake mkuu, sijajua ni yake
au amepanga,” kilisema chanzo hicho.
PAPARAZI WETU NYUMBANI KWA WEMA
Baada ya chanzo kuanika madai hayo, paparazi wetu alikanyaga mafuta akifuata maelezo ya chanzo mpaka kufanikiwa kufika kwenye nyumba hiyo.
SIFA ZA NYUMBA
Ni nyumba kubwa kuliko aliyokuwa akiishi Makumbusho. Ina eneo kubwa linalokaribiakaribia ukubwa wa uwanja wa mpira. Magari makubwa matano na madogo kumi yanaweza kuegeshwa eneo la wazi la ndani. Pia Wema anaweza kufanyia ndani kwenye uwazi huo zile sherehe zake. Na kuna madai kwamba anaandaa sherehe kubwa kwa ajili ya kuumaliza mwaka 2015 akiwa mzima wa afya njema.
PAPARAZI AZUIWA KUINGIA NDANI
Hata hivyo, paparazi wetu alipotaka kufanya utalii wa ndani, alipigwa stop na msichana mmoja aliyejitambulisha kuwa ni ndugu wa Wema pia akimhoji paparazi wetu alifikaje ndani ya ukuta wa nyumba hiyo na kusema Wema hakuwepo. Lakini kwa macho ya haraka, paparazi wetu alibaini kuwa nyumba hiyo ina vyumba vya kulala vinne, stoo, jiko, bafu na choo kwa ajili ya jumuiya, sehemu ya kulia chakula na sebule kubwa.
AMANI LAFANYIA KAZI UTATA Licha ya msichana huyo kumkataza paparazi wetu kuzama ndani na kujionea kwa macho yake yaliyomo, alimuuliza kama anajua Wema ni mpangaji au mmliki. “Wema amejenga hii nyumba. We huoni kuwa ni mpya! Watu
wanadhani Wema hawezi kujenga nyumba siyo! Loo! Wataisoma namba mwaka huu,” alisema msichana huyo.
PETIT MAN
Katika kuchochea utata huo, paparazi wetu alibahatika kukutana uso kwa uso na mpambe mkubwa wa Wema, Petit Man ambaye jina lake halisi ni Ahmed Hasheem na kuzungumza naye kuhusu kutolewa Makumbusho na kuhamia huko kwa sasa. Alisema: “Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beach.” (Ununio huhesabika kuwa ipo Mbezi Beach).
NANI MKWELI? Madai ya msichana aliyekutwa nyumbani, anasema Wema amejenga nyumba hiyo. Ina maana alipata kiwanja, akatafuta mafundi, wakaanza ujenzi. Madai ya Petit Man ni kwamba Wema ameinunua! Kwamba, nyumba hiyo ilijengwa na mtu mwingine, akaamua kuiuza, akanunua Wema.
WEMA HAYUPO HEWANI Juzi, paparazi wetu alimsaka Wema kwa simu ya mkononi ili kumsikia anasemaje lakini hakuwa akipatikana hewani.
MENEJA WA WEMA Paparazi wetu alimpigia simu meneja wa Wema, Martin Kadinda na kumuuliza kuhusu umiliki au upangaji wa nyota huyo kwenye nyumba hiyo ya Ununio. “Kusema kweli nilisafiri, ndiyo nimerudi usiku wa jana. Muda huu najiandaa kwenda kukutana naye. Nitakuwa na majibu baadaye,” alisema Kadinda
Post a Comment