ad

ad

Yanga “tulihitaji sana pointi tatu” Tumezikosa Dhidi Ya Mwadui 0-0



Baada ya kutoka sare ya bila kufungana, kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amewapongeza Mwadui kwa kusema walitimiza vizuri majukumu yao na kupata walichokitaka.
Nsajigwa amesema timu yake ilihitaji sana pointi tatu lakini wameshindwa kufanya hivyo baada ya kubanwa kila kona na wapinzani wao ambao walizisoma mbinu zote walizojaribu kuzitumia kupata ushindi.

“Matokeo kwetu sio mazuri kwa sababu malengo yetu ni kutetea ubingwa, tulihitaji sana hizi pointi tatu za leo angalau tupunguze idadi ya pointi ambazo wenzetu wametutangulia, tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu lakini bahati mbaya tumeshindwa kupata pointi tatu ingawa tupo kwenye uwanja wa nyumbani.”
“Niwapongeze Mwadui kwakuwa wamefanya vizuri homework yao, mwanzo tulikuwa tunacheza kama wanavyocheza wao lakini baadaye tukabadilisha tukaanza kutumia mipira mirefu lakini njia zote waliziba.”
“Tukaamua kucheza kwa kutumia pembeni lakini bado hatukuwa na nguvu nzuri ya kwenda kumalizia magoli kwa hiyo niwapongeze Mwadui kwa walichokifanya, walicheza vizuri wamepata pointi moja.”

No comments

Powered by Blogger.