HII KALI, ETI SIMBA WALICHEZA NA TOTO NDANI YA BWAWA
Mvua
kubwa iliyonyesha juzi Jumamosi jijini Mwanza, ilitibua mipango ya Simba
ya kuondoka na pointi tatu ilipopambana na Toto Africans kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba.
Katika
mchezo huo, Simba ilikuwa mgeni wa Toto na matokeo ya mwisho yalikuwa
sare ya bao 1-1, bao la Simba lilifungwa na Danny Lyanga dakika ya 22
huku Toto ikisawazisha kupitia kwa Evarist Benard katika dakika za
nyongeza baada ya zile tisini kumalizika.
Baada
ya mchezo huo, Kocha wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema mchezo
huo haukupaswa kuchezwa siku hiyo kutokana na uwanja kujaa maji, lakini
anashangaa mwamuzi aliamuru uchezwe.
“Kabla
ya kuanza kwa mchezo, mwamuzi alisema ataukagua uwanja kwa kudundisha
mpira kama unadunda mechi ichezwe na kama haudundi basi iahirishwe kama
sheria za soka zinavyosema.
“Lakini
tunashangaa hakufanya hivyo na badala yake akaruhusu mechi ichezwe, hii
haipo sawa kabisa na huku ni kuvunja sheria za soka kwani sheria hizo
zipo wazi na kila mmoja anazifahamu.
“Ni
wazi mashabiki walikosa ladha ya mchezo kabisa. Kutokana na masuala ya
soka yanavyoendeshwa hapa nchini naamini soka la hapa halitiliwi maanani
hata kidogo, haiwezekani mnacheza mpira huku viatu vimefunikwa na maji,
sasa hapo mtachezaje kama siyo kuchoshana tu?
Post a Comment