MNIGER WA YANGA MAMBO SAFI, TAYARI APEWA MAKAZI JIJINI DAR
Wakati
Simba ikiwa kwenye mvutano na kiungo wake raia wa Zimbabwe, Justice
Madjavi, kuhusiana na suala la kutompa nyumba ya kuishi, upande mwingine
Yanga inaonekana haina shida na suala linaloitwa nyumba kwa wachezaji
wake, kwani imempatia nyumba nzuri ya kuishi kiungo mpya Mniger, Issofou
Boubacar Garba, iliyopo maeneo ya Shekilango jijini Dar.
Yanga
ilimsajili Boubacar katika usajili wa dirisha dogo kwa lengo la kuziba
nafasi ya kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho waliyemfungashia virago vyake
hivi karibuni.
Katibu wa timu hiyo, Dk Jonas Tiboroha, amesema kuwa, wamempatia nyumba mchezaji huyo maeneo ya Shekilango ikiwa inajitegemea.
“Kwa
kawaida yetu Yanga huwa tunawapatia nyumba wachezaji wetu wote wa
kimataifa tunaowasajili na hakuna hata mmoja anayekaa hotelini, ili
kuweza kuepuka usumbufu wa hapa na pale.
“Kila
mtu anapatiwa nyumba yake na kama itatokea watakaa nyumba moja, basi
‘apartment’ tofauti, hakuna anayekaa sehemu moja na mwenziye, tumempatia
Mniger nyumba maeneo ya Shekilango ila hatuwezi kusema tumempangia kwa
kiasi gani, hiyo ni siri yetu,” alisema Dk Tiboroha.
Post a Comment