ad

ad

ARSENAL VS MAN CITY FUNGA KAZI USIKU WA LEO

 Hii ndiyo mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England kabla ya sikukuu ya Krismasi.

Arsenal wanakuwa wenyeji wa Manchester City kwenye Uwanja wa Emirates jijini London.

Mechi inasubiriwa kwa hamu kubwa, wengi wanaonekana kuipa nafasi Arsenal ingawa soka halina mwenyewe.

Mechi tano zilizopita kwa kila timu, inaonekana Arsenal imeshinda mara nne na sare moja. Upande wa City, nao wameshinda mechi nne, wamepoteza moja.


Si mechi ya mzaha wala hakuna anayeweza kuwa na uhakika kwa kuwa uwezo kwa timu hizo unaonekana kulingana kabisa na ndiyo zimekuwa zikibadilishana kiti cha kileleni pamoja na Leicester City. Acha tuone wakati nyasi za Emirates zikiwaka moto.
Powered by Blogger.