Ajali ya basi yaua 12 na kujeruhi 22 Iringa
Taswira kutoka eneo la ajali.
Takribani watu 12 wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine 22
wakijeruhiwa baada ya basi la New Force kupata ajali leo eneo la Mahenge
Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam na limepata ajali mchana huu.
Jitihada za kuondoa miili na kusafirisha majeruhi kuwapeleka hospitali zinaendelea.

Post a Comment