ad

ad

SANDRA: WEMA ACHA KUJIPAISHA


MUIGIZAJI wa fi lamu Salama Salmini anayefahamika zaidi kama Sandra, amemtaka Wema Sepetu kuacha kujipaisha kwa maneno ya uongo, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwachafua wasanii wote. 

Akipiga stori na paparazi wetu, Sandra alisema ni vizuri Wema angejitambua kuwa yeye ni mtu mzima na kioo cha jamii, hivyo aache tabia ya uongo yenye lengo la kujipaisha kwani kabla ya kudanganya kuwa Range Rover aliinunua mwenyewe, alishawahi kudanganya kuwa nyumba anayoishi ni mali yake.

 “Namshangaa sana Wema, yaani simpatii jibu nikitafakari, anatufanya wasanii wote tunaonekana ni waongo tunafanya maisha ya maigizo wakati si kweli, kwa nini asikubali uhalisia wa maisha yake, alidanganya ile nyumba yake kumbe kapanga, hilo gari kajitapa nalo yanaibuka mapya mara akasema kaolewa kumbe si kweli, haifai anapaswa kubadilika hata Mungu hapendi.”
Powered by Blogger.