Singidani (A Story From My Heart) - 17

ILIPOISHIA...
“Ndiyo maana nakuambia unataka kunichezea mchezo... mbona mimi nilikuja kutafutwa na maaskari wakisema nimetembea na mke wa mtu... tena mke wa mkuu wa kituo?”
SASA ENDELEA...
“Ndiyo maana nakuambia unataka kunichezea mchezo... mbona mimi nilikuja kutafutwa na maaskari wakisema nimetembea na mke wa mtu... tena mke wa mkuu wa kituo?”
SASA ENDELEA...
LAURA alihisi kizunguzungu kikali.
Yeye awe mke wa mtu? Tangu lini ameolewa? Alihisi kichwa chake kikigonga kwa
kasi sana. Ukweli alioujua yeye ni kwamba hakuwahi kuolewa achilia mbali
mchumba wa uhakika.
Hakuposwa!
Hakuposwa!
Hakuwa na pete ya uchumba. Hata
mwanaume wa uhakika pia hakuwa naye. Ni kweli hakuwa ameolewa. Ilikuwa ni yeye
na masomo na starehe tu. Mara chache kuna wakati alikuwa akitoka na wanaume
tofauti kwa ajili ya liwazo la moyo wake. Hivyo tu!
Laura alishtuka si mchezo!!!
Laura alishtuka si mchezo!!!
“Aaaaah! Sasa naanza kupata picha.
Hata mimi pia nilifuatwa nikaambiwa kwamba, wewe ni mume wa mtu na mkeo yupo
palepale Singida. Nilikwenda hadi kituoni kutafuta ukweli, lakini cha
kushangaza, wakasema hakuna kitu kama hicho na wala hakuna maaskari waliotumwa
kunitafuta mimi kwa madai ya kutembea na mume wa mtu!” akasema Laura kwa sauti
tulivu akionekana dhahiri kuwa na uhakika na alichokuwa akikizungumza...
Chris alibaki mdomo wazi. Hata
hivyo, bado hakumwamini Laura hata kidogo.
“Nitaaminije?” akauliza Chris akimkazia macho Laura.
“Subiri,” Laura akasema kwa sauti ya chini.
“Nitaaminije?” akauliza Chris akimkazia macho Laura.
“Subiri,” Laura akasema kwa sauti ya chini.
Alichokifanya ilikuwa ni kufungua
pochi yake, kisha akatoa kitambulisho chake cha chuo na kumkabidhi. Baada ya
hapo alitoa kitambulisho cha kupigia kura nacho akamkabidhi. Chris akaonekana
akivitazama vile vitambulisho kwa makini sana.
“Kwahiyo sasa hii inathibitisha nini?”
“Kwahiyo sasa hii inathibitisha nini?”
“Kwamba mimi ni mwanafunzi wa chuo.”
“Kwani mwanachuo hawezi kuolewa?”
“Anaweza, lakini uliambiwa mimi siyo mwanachuo ni mke wa mtu tu.”
Chris akatulia kwa muda.
“Kwani mwanachuo hawezi kuolewa?”
“Anaweza, lakini uliambiwa mimi siyo mwanachuo ni mke wa mtu tu.”
Chris akatulia kwa muda.
“Na hiki kitambulisho cha kura?”
“Angalia nimejiandikishia wapi? Nilishakuambia mimi kwetu siyo Singida, natokea Mwanza. Naona hata kitambulisho changu kimekuthibitishia hilo sasa.”
“Siyo kigezo sana Laura, lakini naomba nikuulize kitu.”
“Uliza tu.”

“Kwanini umekuja Dar?”
“Nimekuja kwa ajili yako Chris. Nakupenda sana, huwezi kuamini jambo hili hasa kutokana na mwanzo wetu ulivyokuwa, lakini nataka uamini kuwa umeingia moyoni mwangu kama cheche za umeme. Unaniumiza baba. Mapenzi yako yananitesa sana ndiyo maana nikaamua kuja hadi huku kwa ajili yako.

“Usinione tapeli au mwenye nia mbaya
na wewe, amini moyo wangu baba. Nakupenda sana. Nahitaji kutengeneza familia na
wewe. Najua ni kiasi gani una wasiwasi na mimi. Ni haki yako kuwa na mashaka
kutokana na mazingira yenyewe na hata mimi niliingiwa na wasiwasi kidogo baada
ya kufuatwa na maaskari eti natembea na mume wa mtu.
“Najua ni jambo gumu kidogo kupenya
kichwani mwako mpenzi lakini nakuomba sana utambue kuwa moyoni mwangu, mwanaume
pekee aliyejaa ni wewe. Niamini na unipe pumziko tafadhali,” Laura alizungumza
kwa dakika tatu peke yake bila kupumzika.
Kwa kiasi kikubwa, maneno ya Laura yalimwingia Chris taratibu ubongoni mwake. Alianza kumwamini taratibu kabisa...
Kwa kiasi kikubwa, maneno ya Laura yalimwingia Chris taratibu ubongoni mwake. Alianza kumwamini taratibu kabisa...
“Una uhakika na unayozungumza
Laura?”
“Zaidi ya uhakika.”
“Kweli?”
“Niamini.”
“Zaidi ya uhakika.”
“Kweli?”
“Niamini.”
Chris alitulia kwa muda tena.
Akamwangalia Laura sasa kwa macho ya kawaida yasiyo na hasira. Moyo wake
ulilipuka. Laura alikuwa mwanamke mrembo kuliko kawaida. Alihisi mpangilio wa
mapigo ya moyo wake ukibadilika kabisa.
Alijilamba midomo yake, akamwangalia
kwa makini Laura ambaye sasa macho yake yalishaanza kuchuruzisha machozi
mepesi. Chris akasimama na kumshika mikono Laura kisha akamwonyesha ishara
asimame. Laura akasimama. Chris kama aliyechanganyikiwa, alimvutia kwake, Laura
akaenda mzima-mzima.
Wakakumbatiana!
Wakakumbatiana!
“Nakupenda sana Laura, nakupenda
mama.”
“Nakupenda pia Chris.”
“Tafadhali usiniumize moyo wangu mama, usiniingize kwenye matatizo mama. Isije kuwa unatumiwa na watu ili uniharibie. Tafadhali sana mpenzi wangu, naomba unipende kwa moyo wako.”

“Sijui niseme nini ili uelewe hili
ninalosema lakini itoshe tu kukuambia kuwa, linatokea ndani ya moyo wangu!”
Waliangaliana kwa muda mrefu, macho ya wote yakapoteza uwezo wa kutazama vyema, wakakutanisha midomo yao kisha wakaanza kubadilishana mate.
Walidumu katika zoezi hilo kwa dakika mbili
nzima, kila mmoja akionyesha hisia kali kwa mwenzake.Waliangaliana kwa muda mrefu, macho ya wote yakapoteza uwezo wa kutazama vyema, wakakutanisha midomo yao kisha wakaanza kubadilishana mate.
“Pwaaaa! Pwaaaa! Pwaaaa! Pwaaaaaaa....” makofi yasikika yakipigwa!
Je, nini kitaendelea?
Post a Comment