Singidani (A Story From My Heart) - 16

ILIPOISHIA...
“Mimi ni daktari kitaaluma. Tena nimesoma nje ya nchi, mimi siyo bwege!” alisema Dk. Chris kwa hasira.
SASA ENDELEA...
CHRIS alikuwa anatetemeka kwa hasira. Kichwani mwake aliamini kwamba, Laura alikuwa akimchezea mchezo. Aliamini alikuwa kwenye mtego ili atapeliwe. Hakuwa tayari kwa jambo hilo hata kidogo. Chris alikuwa amefura kwa hasira.

Kitu ambacho hakukijua ni namna
msichana yule alivyokuwa akimpenda. Alikuwa akimpenda kwa moyo wake wote, ndiyo
maana alifunga safari kutokea Singida kumfuata yeye. Kilichompeleka Dar
kilikuwa ni mapenzi tu!
Dk. Chris!
Hilo tu!
Dk. Chris!
Hilo tu!
Hakutaka kulipa nafasi jambo hilo
kichwani mwake. Alidhamiria kukaa naye mbali kabisa. Hisia za mapenzi
zilishahama. Hakutaka kumuendekeza. Ramsey rafiki yake kipenzi, akamwangalia
yule msichana kwa makini.
Alishawishika sana na urembo wake.
Kwa stori za Chris kuhusu mwanamke aliyetaka kumwingiza kwenye matatizo mjini
Singida, alianza kuamini kuwa ndiye aliyekuwa mbele yao. Alichokifanya ilikuwa
ni kumtuliza rafiki yake kwanza...
“Kaka tulia tafadhali... lakini ni
nani huyu msichana?” Ramsey akauliza kwa sauti ndogo.
“Ni yule mwanamke wa Singida niliyekuambia. Anataka kuniharibia maisha yangu huyu. Sikia wewe... umekosea njia, ondoka kwenye maisha yangu,” akasema Dk. Chris kwa hasira na sauti ya juu.

Laura alikuwa analia machozi. Hakuwa
anaigiza, alikuwa analia machozi ya kweli kabisa...
Kama angekuwa mbele ya kamera akirekodi filamu, angekuwa amefanikiwa kuvaa uhusika katika kiwango cha mwisho kabisa. Laura aliweza kuonesha kilichotakiwa kufanyika. Lakini haikuwa hivyo... ilikuwa halisi.

Laura alikuwa analilia mapenzi!
“Chris nina kosa gani mimi? Wewe ndiye umekuja kwenye maisha yangu, ukasema unanipenda, nakiri kweli mwanzoni sikuwa na hisia hizo, lakini sasa nimegundua upendo wangu kwako, ndiyo maana nimetoroka chuoni na kuja huku kwa ajili yako.

“Nakupenda Chris. Nakupenda sana
baba. Usinifikirie vibaya baba. Ni mapenzi tu. Nakupenda mpenzi wangu. Naomba
unipe nafasi, nipe pumziko la moyo ndani yako...” maneno haya yalisikika huku
machozi yakiendelea kutiririka machoni mwake.
“Acha uongo wewe... unajifanya mwanafunzi, wewe ni mwanafunzi au mke wa mtu? Nimesema sitaki mawasiliano yoyote na wewe.”

Laura akazidi kulia.
Chika, Katibu Mkuu wa Bongo Film Club, aliingilia kati. Alimshika mkono Laura, akamsihi anyamaze, akatulia kidogo. Chika akaanza kuzungumza: “Maneno ya huyu binti si ya kupuuzwa, anahitaji kusikilizwa. Tafadhali Chris, Ramsey na Jaybee naomba tuzungumze pembeni. Naamini tutapata ufumbuzi.”

“Sitaki!” Dk. Chris akajibu kwa
hasira.
“Utataka!” Jaybee, mwenyekiti wa nidhamu wa klabu hiyo alisema.
Dk. Chris akanywea!

Isingekuwa rahisi hata kidogo
kumpinga Jaybee, msanii mwenye jina kubwa na sauti Bongo Film Club. Heshima
yake ndiyo hasa iliyosababisha akabidhiwe kofia ya kusimamia nidhamu klabuni
hapo. Ramsey alijua alichotakiwa kufanya.
Alitoka na kusogea pembeni, Chika
akafuta, Jaybee ndiye aliyekuwa wa kwanza akitangulizana na Laura. Dk. Chris
akawa wa mwisho. Walitembea mpaka pembeni kidogo na kaunta iliyokuwa ndani.
Wakaketi jirani na runinga.
“Wakati mwingine huwa inanilazimu
kutumia ukali kidogo ili mambo yaende sawa. Sikuwa na lengo la kukudhalilisha
ila nilipenda haya mambo yajadiliwe kwa staha na siri. Chris lazima tuzungumzie
huku pembeni,” alisema Jaybee, safari hii kwa sauti tulivu.
“Nimekuelewa...” akasema Chris.
“Huyu msichana unamfahamu?”
“Nimekuelewa...” akasema Chris.
“Huyu msichana unamfahamu?”
“Ndiyo... lakini hafai huyu.
Unajua...” akaanza kuzungumza kwa hasira lakini Jaybee akamkatiza.
“Tulia, swali nililokuuliza ni moja tu; unamfahamu?”
“Ndiyo.”

“Utapenda haya mambo tuzungumze pamoja
au mtayajadili wenyewe?” akauliza tena Jaybee.
Dk. Chris alitulia kwa muda, alionekana akitafakari jambo kwa kina kidogo. Kichwa chake kilifanya kazi kama umeme. Pamoja na yote hayo, bado hakutaka mazungumzo yale yasikike na kila mtu. Haraka akajibu:

“Nataka tuzungumze mimi na yeye tu!”
“Si unaona mambo hayo?” Chika akasema na wote kwa pamoja wakasimama na kuwaacha Dk. Chris na Laura peke yao.
***
“Nataka uniambie ukweli, umeolewa au hujaolewa?”

Chris akamwuliza Laura.
“Mbona maajabu tena mpenzi wangu? Niolewe na nani sasa?”
“Jibu swali, wewe ni mke wa mtu au sivyo?”

“Sivyo. Sijaolewa mimi.”
“Ndiyo maana nakuambia unataka kunichezea mchezo... mbona mimi nilikuja kutafutwa na maaskari wakisema nimetembea na mke wa mtu... tena mke wa mkuu wa kituo?”
Itaendelea

Post a Comment