Love Stori: Muhanga wa mapenzi - 02

Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 02
Mtunzi: Ally Mbetu
ILIPOISHIA:
Baada ya yule kijana kupita alimwacha Rachel katika lindi la mawazo juu ya kijana yule na kujiuliza sijui kama atamtia tena machoni . Rachal baadaya kubadili nguo na kuvaa nguo za kupendeza alisimama mbele ya kioo na kujisifia jinsi alivyo mzuri na jinsi alivyopendeza . Alijikumbatia mwenyewe huku akisema:
“ Jinsi alivyopendeza halafu nipate kijana mzuri kama niliyemwona muda ule mbona dunia nitaisanifu.“
Rachal alizivua zile nguo na kubakia na nguo ya ndani na kujitupa katika kitanda cha sita kwa sita na kujipindua kitanda kizima huku akimuwaza yule kijana ambaye ameuteka moyo wake kwa ghafla.
SASA ENDELEA...
Rachel alijikuta kwenye wakati mgumu wa kuugua homa ya mapenzi huku akimuogopa kumweleza muhusika kutokana na dharau alizomfanyia alijuuuta kumdharau asiyemjua. Hali ile ilimfanya awe mwingi wa mawazo muda wote kila alipokuwa akimuona yule kijana akipita moyo wake ulimlipuka na kujikuta kwenye wakati mgumu.
Muda mwingi alikuwa mtu wa mawazo kipindi kitu kilichopelekea kumshtua kila mmoja kuanzia wazazi wake , walimu hata rafiki yake mkubwa Joyce .
“Rachel vipi mbona siku hizi mbili unaonekana una mawazo mengi,“ Joyce alimuuliza.
“Joyce ni kweli kuna kitu kimenisibu lakini si leo, ila ipo siku nitakuelezea ili unisaidie, “ alimjibu rafiki yake kwa sauti ya unyonge.
“Hapana Rachel wewe ni rafiki yangu na siri zetu hatufichani naomba uniambie huenda nikakusaidia hata kimawazo.”
Rachel ilibidi amueleze ukweli Joy jinsi anavyompenda mtu asiyejua mapenzi yake kwake.
“ Kwanini uutese moyo wako wakati mtu mwenyewe hayupo mbali mueleze ukweli ujue moja siku zote kwenye maumivu ya moyo unatakiwa kujitoa muhanga kwa kujiweka wazi mbele ya yule umpendaye.”
Rachel aliahidi kuyafanyia kazi yale aliyoelezwa na shogae Joyce .
***
Kutokana na gari linalomfuata kumchukua shule kuchelewa Rachel aliomba lift kwenye gari la kina Joyce ambalo lilimshushia karibia na kwao. Baada ya kuteremka katika gari aliagana na Joyce wakati anageuka ili aondoke nusra aanguke kwa mshtuko pale alipokutana uso kwa uso na mtu ambaye alimuona hana hadhi ya kuzungumza naye lakini akatokea kuwa ugonjwa wa mahaba yake.
Kutokana na tabia yake ya nyodo hata kumueleza alishindwa alibakia kumsindikiza kwa macho tu na kuingia ndani mwao huku moyo wake ukizidi kutaabika juu ya mapenzi.
Siku iliyofuata baada ya kutoka shule na kuingia chumbani kwake alielekea dirishani ili afungue pazia atazame nje wapita njia. Hakuamini macho yake pale alipomwona tena yule kijana akipita. Safari hii alifurahi zaidi kwani alikuwa amesimama akizungumza na mtu na alipomwangalia vizuri alimtambua kuwa ni yule kijana aliyemzodoa siku moja akiwa katika mavazi ya kawaida.
“ Dah! Kumbe bonge la hand some boy, ni kijana mzuri sana tena sana …. Mmh, maskini sijui kama atanielewa nikimweleza nampenda wakati niliisha mtoa nishai,” Rachel aliwaza peke yake bila kupata jibu kitu kilicho mnyima raha.
****
Athuman akiwa anatoka katika shughuli zake, alijirudisha nyumbani kwa mwendo wa taratibu mara alishtushwa na sauti ya mtoto mdogo wa kiume ikimwita kwa nyuma.
“Kaka ……kaka.”
Athuman aligeuka na kumtazama yule mtoto na kumuuliza.
“Unasemaje?”
“Kuna barua yako, “ alisema yule mtoto huku akinyoosha mkono kumpa barua.
“Inatoka kwa nani?” aliuliza huku akiipokea.
“Yule.”
Alimuonesha binti Rachel aliye juu katika jumba la kifahari ambalo anakaa tajiri mmoja John Mulisa. Alimuangalia yule binti ambaye alikuwa amesimama mbele ya kibaraza. Alipomwangalia vizuri ili amtambue alijificha kwa aibu, lakini Athuman alimkumbuka ndiye aliyenitoa nishai siku moja.
Aliifungua ile barua na kuisoma palepale maneno niliyoyakuta yalimshtua kidogo nakumchanganya. Eti anamtesa moyo wake, yeye ndiye mwokozi wake na anasubiri jibu kama wokovu barua yenye maneno machache ilimalizia kwa manane: deep love Rachel.
Athuman alicheka kidogo kisha alinyanyua tena macho na kumwangalia kama mwanzo alijificha tena . Alijiuliza ni yeye au kuna mtu mwingine aliyempelekea ile barua mwenye hadhi ya kuzungumza naye . Athuman aliamini ile barua si yake mtumwaji atakuwa amekosea.
Aliachana na ile barua na kutupa vipande vyake vilivyo peperushwa na upepo kisha alipiga hatua kuondoka eneo lile. Rachel alimfaidi Athuman kwa kumuona vizuri tena kwa ukaribu zaidi.
Wakati Athuman anasoma ile barua Rachel alikuwa amefumba macho huku amejikumbatia kwa mikono yake miwili. Lakini moyo ulipasuka baada ya kushuhudia barua yake ikichanwa na kalatasi kutupwa barabarani. Kitendo cha Athuman kuichana barua yake kilikuwa kama kuuchana moyo wake.
Alijikuta akilia kwa uchungu huku akikimbilia kitandani na kuukumbatia mto huku akiendelea kulia na kulitaja jina la yule mvulana baada ya kulitambua jina lake kutokana na kusikia akikitwa na mtu.
“Athuman mpenzi kwa nini umeuchana moyo wangu, kwa nini huna huruma na mateso yangu ya moyo? Athuman nisamehe sikujua nitendalo lilikuwa sawa na kuupasua moyo wangu kwa kisu kisicho na makali bila ganzi. Hebu fikiria ni maumivu gani moyoni mwangu?”
Rachel alijizungumza huku akilia kwa sauti ya chini, mama Rachel alikuwa akiingia chumbani kwa mwanaye ili kumwita kwa ajili ya chakula cha mchana. Sauti ya kilio cha kulalamika kilimshtua na kuingia ndani taratibu ili ajue kuna nini. Alishangaa kumkuta akiwa amekumbatia mtu kitandani peke yake huku akizungumza kama anazungumza na mtu. Alipomwita aligundua mwanaye yupo usingizini.
Alitoka huku akijiuliza Athuman ni nani anayemsumbua mwanaye na kumuingiza kwenye dunia mbaya ya mateso ya nafsi ya mapenzi. Moyoni aliapa kumsikisha adabu huyu kijana anayeitwa Athuman.
Nini kitaendelea? Tutukutane toleo lijalo siku ya kesho.
Post a Comment