AZIZA WA FACEBOOK - 8

Maisha yalikuwa yakiendelea kama kawaida, kuhusu Aziza, wala sikuwa na wasiwasi kwa kuamini kwamba piga ua huyu mtoto ni lazima ningemchukua bila tatizo lolote lile.
Sasa endelea...
Kila siku nilikuwa nikiwasiliana nae, alikuwa akionekana kunikubali sana, chatting zangu zilizokuwa zikitabasamu zikaonekana kuuteka moyo wake. Nilikuwa na marafiki wengi facebook lakini nikikaa bila kuchati na Aziza sikuwa nikijisikia furaha kabisa.
Japokuwa Eduado alikuwa amenipa ishu ya kumfuatilia Aziza kama mchezo fulani lakini kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo nami nikazidi kufall inlove. Nilikuwa nikipenda sana Aziza, kila nilipokuwa nikiingia facebook na kumkosa, sikuwa nikijisikia raha kabisa.
Kuna nyakati za shida zikaingia, nyakati ambazo sikuweza kumuona Aziza hewani. Katika nyakati hizo maisha yalikuwa ya tabu sana, nilikuwa nikikosa furaha hata katika maisha ya kawaida. Nilimzoea sana Aziza, nilimpenda sana Aziza kwa hiyo kutokuuona uwepo wake machoni mwangu kilikuwa ni kitu ambacho kiliniumiza sana.
MIMI: Eduado vipi?
EDUADO: Poa. Inakuwaje?
MIMI: Kama kawa. Mbona Aziza simuoni siku hizi?
EDUADO: Tupo kwenye mitihani kaka.
MIMI: Sasa mkiwa kwenye mitihani ndio haruhusiwi kuwa hewani? Mbona wewe upo?
EDUADO: Mimi si unajua mbishi kaka.
MIMI: Dah! Nimemmisi sana Aziza. Nimemmisi ile mbaya kaka.
EDUADO: Usijali kaka. Mitihani ikiisha atakurudi hewani tu.
MIMI: Poa. Ila mnamaliza lini?
EDUADO: Wiki ijayo.
MIMI: Duh!
EDUADO: Nini tena kaka?
MIMI: Nahisi kama nitakufa kwa mawazo. Nahisi nitaweza kufa kaka.
EDUADO: Usijali kaka. Wewe vumilia tu utakula mbivu.
MIMI: Poa kaka.
Katika kipindi hicho ndicho nikajua kwamba moyo wangu ulikuwa ukimpenda sana Aziza.
Huyu Aziza ndiye ambaye alinifanya niwaone wasichana wote kuwa wa kawaida sana, yeye ndiye aliyenifanya nimuone kuwa msichana mzuri kuliko wasichana wote duniani. Uwepo wake katika mtandao wa facebook bado nilikuwa nauhitaji sana, nilikuwa nikijisikia mpweke kupita kawaida.
Aziza...Aziza...Aziza...upo wapi wewe msichana uje kuupoza moyo wangu ulio kwenye maumivu makali?
Siku zikaendelea kukatika na hatimaye siku ambayo ilionekana kunifurahisha ikawadia. Siku hiyo nikawa kama nimepigwa na mshtuko mkubwa moyoni, sikuamini kile ambacho kilikuwa kikionekana machoni mwangu, Aziza alikuwa hewani. Sikutaka kupoteza muda, sikutaka kuleta pozi, kwa haraka sana nikamtumia meseji.
MIMI: Mungu wangu!
AZIZA: Nini tena.
MIMI: Umekuja at last.
AZIZA: Yeah! Nilipotea kwa kipindi fulani hivi, si unajua mitihani wangu.
MIMI: Pole sana. Mmekwishamaliza?
AZIZA: Yeah! Tumekwishamaliza. Ila nami nilikumisi sana.
MIMI: Nashukuru kwa kunimis, ila ulimiss nini kutoka kwangu?
AZIZA: Chatting zako, meseji zako zimekaa kitofauti sana na watu wengine.
MIMI: Kivipi?
AZIZA: Zipo kitofauti sana. Katika maisha yangu nimewahi kuchati na watu wengi sana, ila zako...dah!
MIMI: Bado haujaniambia kivipi.
AZIZA: Kwanza hauandiki kimkato kama neno ‘sijui kuliandika cjui’, yaani maneno ya mikato huwa hauitumii kabisa.
MIMI: Kwani hiyo nayo ni sababu?
AZIZA: Ngoja nikwambie kitu Ibra. Hii ni siri ambayo wanaume wengi wamekuwa hawaielewi na ndipo wanapofanya makosa kila siku.
MIMI: Siri gani?
AZIZA: Unajua unapochati na msichana yeyote ambaye haujawahi kuonana nae, unatakiwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, hiyo ndio sifa moja kubwa ya kumteka msichana kwa sababu hisia zetu hazitekwi na mambo makubwaaa, hapana, hivi vitu vidogo vidogo ambavyo wavulana wanavipuuzia ndio vinatuteka.
MIMI: Kama vitu gani.
AZIZA: Cha kwanza salamu Ibra. Hivi unajua kwa sababu gani meseji yako ya kwanza kabisa uliyowahi kunitumia sijakujibu?
MIMI: Hapana. Sijajua kwa nini.
AZIZA: Salamu. Wanawake wengi wanalichukulia tofauti neno ‘mambo’. Unapomsalimia msichana kwa mara ya kwanza kwa kumwambia ‘Mambo’, wanaojibu ni wachache sana.
MIMI: Kwa nini sasa?
AZIZA: Kwa sababu mwanamke anapenda kufuatwa kinidhamu.
MIMI: Sasa nilitakiwa kukusalimia vipi ili ujibu?
AZIZA: Unapomfuata msichana yeyote duniani, anza kwa kumsalimia ‘Habari yako’ au salamu yoyote iliyokaa kinidhamu. Kidogo ukisalimia hivyo, kuna asilimia kubwa sana ya msichana kukujibu.
MIMI: Duh! Kumbeee!
AZIZA: Yeah! Hiyo ni siri ya kwanza Ibra, wavulana wengi huwa wanafeli hapo tu kitu ambacho kinawafanya kila siku kulalamika kwamba wasichana tuna mapozi kujibu salamu zao, hapana, hatuna mapozi bali wanakosea kusalimia, wanakosa nidhamu katika kusalimia.
MIMI: Nimekuelewa. Naomba siri nyingine.
AZIZA: Chatting. Unajua usipende kuchati na msichana kifupi kama nilivyokueleza toka mwanzo. Andika neno lote kwa ujumla, unajua unapoandika kifupi, unaupa kazi ubongo wa mtu kulifikiria neno na matokeo yake akili yake inachoka na kukatisha chatting na wewe.
MIMI: Ila mimi sijawahi kuchati namna hiyo Aziza.
AZIZA: Najua. Ila ninakumegea siri juu ya vitu ambavyo msichana anavipenda na vile asivyovipenda.
Itaendelea Siku ya kesho ijayo.
Post a Comment