NYOTA YA LOWASSA YAZIDI KUNG'ARA AWAPIKU WENZAKE KWA ASILIMIA 20 NI KATIKA KUWANIA URAIS WA TANZANIA
| Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Samunge Social Research Centre, George Nyaronga kutoka Chuo Kikuu Huria (OUT). |
NYOTA ya Waziri Mkuu
mstaafu Edward Lowassa yazidi kung'aa baada utafiti uliofanywa na
Samunge Social Research Center na kugundua wananchi wengi kumpenda na
kumuhitaji agombea urais wa mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mtafiti Mkuu wa Tafiti hiyo
George Nyaronga alisema baada ya Waziri huyo kudai kuwa atagombania
wananchi wengi wameonyesha kumuhitaji kwa kiasi kikubwa.
Alisema katika utafiti huo walioufanya waligundua kuwa Waziri huyo
mstaafu anaongoza kwa asilimia nyingi kuliko wenzake anaowafata.
Akitaja asilimia hizo alisema Edward Lowassa anaongoza kwa asilimia
20.7 akifuatiwa na Wilbroad Slaa asilimia 11.7, Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia (Chadema)Freeman Mbowe asilimia 3.4, Mwenyekiti wa Chama cha
Wanachi CUF Ibrahim Lipumba asilimia 4.2.
Wengine ni pamoja na Waziri wa Ujenzi John Magufuli 7.6, Naibu
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba asilimia 4,Waziri Mkuu Mizengo Pinda
asilimia 2.4,Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Bernard Membe7.0 na
Mwenyekiti wa chama cha Nccr Mageuzi James Mbatia 1.2.
Alisema kwa kutokana na nchi kuelekea katika uchaguzi wananchi
wamekuwa na muamko wa hali ya juu katika kuhakikisha kila mmoja
atapigapiga kura kwa mwaka huu.
"Tumefanya tafiti hizi na kuona kwamba watanzania wengi wameamua
kuingia kwenye masuala ya siasa na kuleta mabadiliko katika nchi yao na
si kupigiwa kura,"alisema.
Alisema kutokana na utafiti wao wamegundua kuwa wananchi wanahitaji
rais ambaye ni muadilifu, msema ukweli, mwenye afya asiwe na udini wala
ukabila na mzalendo wa nchi yake
Alisema kutokana na majina hayo ya urais pia katika tafiti zao
imeonekana kuwa vyama vinavyoongoza katika kupendwa na wananchi ni
pamoja na Chama cha Mapinduzi kuonekana kupendwa sana kuliko vyama
vyote.
Alivitaja vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM)
53.5,Chama cha Demokrasia (Chadema) 34.2 ,Chama cha Wazalendo (ACT)1.2
na Umoja wa Katiba Mpya (Ukawa) 6 na Chama cha wanachi CUF 6.
Stori na Habarijamii
Post a Comment