ad

ad

ROSE NDAUKA ATOA ZAWADI KWA WATOTO WALEMAVU

            
Rose Ndauka akihojiana na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari kabla ya kuonana na watoto hao.
 
Mkurugenzi wa shule hiyo,  Wilson  Chacha, akizungumza na waandishi kuhusu matatizo yanayowakabili kituoni hapo hasa watoto wanaoondoka shuleni na kushindwa kurejea kutokana na ukosefu wa  nauli za kurudi shuleni hapo.
 
Rose Naduka akiwa amebeba baadhi ya vitu walivyopeleka shuleni hapo.
 
Akiongozana na familia yake kuonana na watoto hao.
 
Picha ya pamoja.
 
Dk. Rusigwa, akizungumza na waandishi wa habari  kwenye hafla hiyo.
 
Mkuu wa shule na msaidizi wake wakipozi mbele ya kamera.
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka, jana aliungana na familia yake ya ‘Rozzie Magazine’ na na Mkurugenzi wa Sure Herbal Clinic,  Simon Rusigwa, wametembelea  shule ya watoto walemavu ya Salvation Army, iliyopo Kurasini jijini Dar, na kutoa zawadi mbalimbali kuwasaidia watoto hao ambao wana ulemavu mbalimbali wa viungo na ngozi.
Akizungumza na mtandao huu, Rose alisema yeye na mfadhili wake Dk.  Rusigwa, waliona ni jambo jema kuwasaidia na kukaa na watoto hao ili kuwajenga kiakili wajione sawa na watoto wengine.

No comments

Powered by Blogger.