ad

ad

HBABA: WANAUME WASIO NA MISIMAMO HUCHOSHA WANAWAKE

Msanii wa miondoko ya Bongo bolingo H Baba amefunguka na kusema kuwa wanaume wasiokuwa na misimamo na wasioridhika na upendo wa wapenzi wao ndiyo huwachosha wanawake.
Msanii H Baba
H Baba amesema kuwa mwanamke yoyote yule anaweza kuwa mzuri na kuendelea kupendeza ikiwa watakuwa wanapata wanaume wanaotulia na kuwapenda kwa dhati maana inawasaidia wanawake hao kutulia katika mahusiano hayo au ndoa hiyo na kulea familia.
"Mwanamke yoyote ni mzuri tu ila huchoshwa na wanaume wasiokuwa na misimamo, wasioridhika na umpendae hebu mpende umpendae uwone Kama utatangatanga,uroho usiokuwa na maana hausadii, ridhika na ulie nae, hebu Tazama mke wangu anavyowaka mimi namuita Miss World alishinda siku yandoa yetu. Upendo mzuri kwa umpendae unatakatisha Sura ni zaidi ya lotion mchanganyo"
H Baba ambaye ni baba wa mtoto mmoja na sasa anategemea kupata mtoto wa pili na Mkewe Flora Mvungi.
H baba anakiri kuwa wanaume ndio chanzo kikubwa cha baadhi ya wanawake kuchoka maana wanawatumia na kuwazalisha na kukataa kuwapa huduma huku wakiwa hawana njia ya kuwaingizia kipato hali inayopelekea kushindwa kujihudumia kama zamani au la wapo baadhi ya wanawake wanaoonekana kuwa na mahusiano mapya kila baada ya muda kutokana na kuachwa na watu ambao huingia nao katika mahusiano, hali ambayo nayo inapelekea mwanamke kuchoka.
Mbali na hilo Msanii H Baba wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari dogo lakini alifanikiwa kuchomoka katika gari hiyo bila kupatwa na jeraha lolote lile licha ya gari hiyo aliyokuwa akiitumia kuharibika vibaya sehemu ya mbele.

No comments

Powered by Blogger.