ad

ad

ROSE NDAUKA NA RICHIE:PAMOJA TENA!


Ikiwa ni siku chache tu zimebakia tuuage mwaka 2014 na tuukaribishe mwaka wa 2015 Mungu akipenda. Waigizaji  Rose Ndauka na Single Mtambalike ‘Richie ‘ waneonekana wakiwa "Location"wakitengeneza filamu mpya ambayo kwa mujibu wa Rose ndauka kazi hiyo inafanyika chini ya kampuni ya Bulls Entertainment na kuongozwa na Richie ambae ni mkurugenzi wa kampuni hiyo.
Rose ndauka akionekana mwenye furaha akiwa na Richie alitupia picha mtandaoni na kuandika  kwa kifupi zaidi kuwa watu wakae mkao wa kula  kusubiri kazi yao hiyo mpya. “Tunawaandalia Movie mpya kutoka Bullz entertainment#kaa mkao wa kula”
Wapenzi  na mashabiki wengi walionyesha kufurahi  na kuisubiri kwa hamu kubwa kwani wawili hawa huwa wanaendana na hutoa kazi nzuri sana. Wengi walishusha comment nyingi sana  za maswali kama jina la filamu, inatoka lini ambayo hata hivyo Rose hakuyajibu.
Ikumbukwe kuwa Bulls Entertainment ambayo ni kampuni ya Richie ndio iliyomkuza  na kumfanya  Rose Ndauka leo hii kuwa ni moja kati ya waigizaji wakike bora zaidi hapa Tanzania. Na badaye Rose aliondoka Bulls na kuanza kufanya kazi zake mwenyewe,.Kitendo cha kufanya kazi tena na Bulls wengi wamekitafsiri kuwa ni sawa na motto kurudi  nyumbani.
Wawili hawa (Rose na Richie)  waliwahi kutikisa  anga la filamu hapa bongo wa filamu  kwa kazi nyingi ila filamu ya ‘Skendo’, iliyowajumuisha  waigizaji kama  marehemu Adam Kuambiana, Dk. Cheni, Mobby Mpambala, Faiza Ally na Barafu chini ya bulls intertainment ilikuwa ni moja kati ya kazi zao bora zaidi .

No comments

Powered by Blogger.