ad

ad

MKE WA JAJA NDIYO TATIZO KWA JAJA!

 
Mshambuliaji Geilson Santana ‘Jaja’.
Hans Mloli na Sweetbert Lukonge
SIRI imefichuka, ni ya kile kilichosababisha mshambuliaji Geilson Santana ‘Jaja’ kuamua kuondoka Yanga ikiwa ni baada ya kuichezea timu hiyo mechi saba tu za Ligi Kuu Bara.Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, uongozi utakutana na kujadili iwapo uchukue hatua kwa kulifikisha suala hilo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na baadaye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), hasa kama halitapatiwa ufumbuzi.

Lengo hasa la Yanga kutaka kulifikisha suala hilo TFF na baadaye Fifa ni kutaka Jaja alipe fedha za kuvunja mkataba, lakini kikao kinachotarajiwa kufanyika ndani ya siku tatu ndiyo kitatoa uamuzi.
 

Taarifa zinaeleza kwamba, Jaja ameamua kuondoka nchini si kwa kuwa ameshindwa soka, badala yake uamuzi wa mkewe kusisitiza kwamba hawezi kuishi Tanzania na hakuna shule za Kireno kwa ajili ya mwanaye.
Katika barua ya kuiacha Yanga, Jaja amesisitiza kwamba familia yake ndiyo namba moja. Hivyo angependa kuiacha Yanga ili aendelee na familia na hasa akizingatia zaidi suala la mwanaye na shule.
 

“Kweli amesema asingeweza kuendelea wakati familia yake ikiwa mbali, hivyo ameamua kubaki Brazil ili aendelee na maisha yake akiwa na familia yake na mwanaye akisoma shule sahihi,” kilieleza chanzo.
Awali ilielezwa, Yanga ilikubali kumkatia tiketi mkewe ya kwenda na kurudi kila mwaka mara moja, lakini baadaye Jaja akageuza uamuzi haraka na kuwashitua Yanga kwa kuwa wakati anaondoka nchini, hakusema lolote zaidi ya wao baadaye kuisikia kwenye bomba tu.
Kitendo cha Jaja kuamua kubaki Brazil, kimewashitua wengi licha ya kwamba Yanga inatarajia kupata mrithi wake ambaye anatarajia kuwasili nchini kesho Jumanne mchana akitokea kwao Brazil.
Emerson ni kiungo na ana uwezo wa kucheza kama mlinzi na huenda sasa Yanga italazimika kuongeza wafungaji au kuwapa nafasi zaidi Jerry Tegete, Hussein Javu na Said Bahanuzi.
Jaja alifunga bao moja katika mechi saba za ligi, lakini alifunga mabao mawili murua katika mechi yake ya kwanza inayotambulika na TFF baada ya kuiongoza Yanga kushinda mabao 3-0 dhidi ya Azam FC na kubeba Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
CHANZO: CHAMPIONI JUMATATU

No comments

Powered by Blogger.