RIYAMA: NIKITONGOZWA SINA HIYANA
STAA wa filamu Bongo, Riyama Ally amesema katika maisha yake hajawahi kumtukana mwanaume pindi anaponitokea hata kama hamuhitaji, anamjibu kwa busara.
Staa wa filamu Bongo, Riyama Ally
Akipiga stori , Riyama alisema yeye yupo tofauti na
wasichana wengine ambao wamekuwa na tabia ya kuwatukana wanaume pindi
wanapowasilisha hisia zao za kimapenzi kwa sababu tu hawavutiwi kuwa
nao.“Hata kama mtu akinitongoza na nikawa simuhitaji kamwe siwezi kumtukana wala kumuonyesha dharau , kimaadili sisi sote ni binadamu na kila mtu ana hisia zake na maamuzi yake, namjibu tu kistaarabu kwamba mimi nina mtu wangu, kumjibu mwanaume vibaya Mungu hapendi,” alisema Riyama.

Post a Comment