Washindi
wa tatu bora wakiwapungia mkono mashabiki, katikati ni Junes Ndalima
aliyefanikiwa kutwaa taji hilo, kushoto ni Georgia Gordian ambaye ni
mshindi wa pili na kulia Nasra Moffat ambaye amekamata nafasi ya tatu.
Ma-MC wa kinyang’anyiro hicho Hamis Dakota na Neema Nyangasa wakifanya mambo.
Walimbwende wakiwa kwenye kivazi cha jioni.
Majaji
wakifanya yao, katikati ni Salma Dacota kulia ni Mike Lucas na kushoto
ni Michael Maurus wakihakikisha wanatenda haki kumpata mrembo mwenye
vigezo.
Washindi wa mwaka jana wakiwa wameketi.
Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akitumbuiza.
Bendi ya Mashujaa ikifanya yake.
Mwanadada Junes Ndalima amefanikiwa kutwaa taji la Miss Chuo cha
Ustawi wa Jamii mwaka 2013/2014 huku nafasi ya pili ikikamatwa na
Georgia Gordian na nafasi ya tatu inashikiliwa na mwanadada Nasra Moffat
katika kinyang’anyiro hicho.
Mshindi wa kwanza alikabidhiwa shilingi 7,000,000 huku wa pili
akijinyakulia shilingi 500,000 na wa tatu shilingi 300,000 huku mshindi
wa nne na wa tano wakipewa shilingi 100,000 kila mmoja na washiriki
waliobakia walipewa shilingi 70,000 kila mmoja.
Post a Comment