RIWAYA: SIKU YA GRADUATION....SEHEMU YA 2
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI
EMAIL; 0768 22 33 44
SEHEMU YA PILI
Nilizidi kuingiwa na hofu kubwa kufuatia tahadhari alizoniachia Ntahondi, chumba nilikiona kidogo utadhani nimo ndani ya yai, kila nilipojaribu kujikaza na kuutafuta usingizi ilishindikana, niliendelea kujilaza tu pale kitandani na hatimae nilikuja kushtuka ilikua ni saa kumi na mbili asubuhi, kilichonishtua ni mlio wa simu yangu, nikaamka na kuiangalia simu yangu ili nijue nani anaenipigia simu asubuhi yote ile, Alikua ni Jarufu, kaka yangu aishie mkoani Tabora
“Hallow”
"Ehh za asubuhi"
“Salama tu bro za huko?”
“Ahh nzuri kiasi, pole kwanza na matatizo yako”
“Ahsante nashukuru, mbona umesema nzuri kiasi kuna nini?”
“Mama yuko hoi huku, Presha imepanda hapa tuko Hospitalini Kitete”
“Hee jamani, imekuaje?”
“We si umempigia na kumueleza hayo mambo ya huko kwako”
“Ndio nilimpigia lakini…..”
“Sasa kwanini ulimpigia na unamjua jinsi alivyo na hamaki!?”
“Lakini mimi sikumpigia kwa nia mbaya, ilikua ni kumfahamisha tu hali ilivyo huku..”
“Sasa mwenzio ulivyompigia tu akapandwa na jazba zake akajiandaa na hapo hapo akaenda Rufita kwa mama Ramla”
“Jamani enhee ikawaje?”
“Nasikia alivyofika tu wakaanza kutukanana sana almanusura washikane, nasikia wasamaria wema ndo wakawaamua. Kilichomzidisha hasira zaidi mama Nasikia huyo mama Ramla alikua akitoa maneno machafu sana kuhusu wewe, anasema tunamuonea wivu mwanae kwa kuolewa na Tajiri pia anasema kama mwanamke hakutaki tena ya nini kumng’ang’ania!!”
Yaani maneno ya Jarufu yalizidi kuniumiza, kila nikikumbuka jinsi huyu Mama alivyokua akiniheshimu na kunijali kipindi chote nilichokua nikimsomesha na kumuhudumia mwanae, Kumbe ilikua ni geresha tu sasa anamjali tena tajiri ambae hamjui hata kwa sura!! nikiwa bado nimeshikilia simu yangu yangu sikioni, kaka alizidi kunivuruga kichwa
"Baada ya mama kurudi nyumbani ghafla akaanza kuishiwa nguvu, mara akapoteza fahamu nadhani itakua ni Presha, ndo hapa tupo Hospital" Baada ya kumaliza kuniambia maneno hayo alikata simu nikabaki nimeduwaa kama Chizi, Siku hiyo kwangu ilikua mbaya iliyojaa hofu na simanzi, Hofu itokanayo na maelezo niliyopewa na Ntahondi kuhusu usalama wangu, nilikua na Simanzi iliyochagizwa na
hasira dhidi ya Ramla na mama yake Mzazi ambao wote wamekula fadhila
zangu za pesa na misaada kadhaa Lakini leo wananiona si chochote si
lolote na kuamua kushirikiana kunisaiti kinyama, Pia nilikua namuwazia mama yangu mzazi alieko Tabora akiwa hoi kitandani kwa ajili yangu. Basi nikajiandaa haraka haraka na kwenda kazini, nilipofika kazini nilianza kutekeleza majukumu yangu kama kawaida japo nilishangazwa na hali niliyomkuta nayo
Boss wangu Mr Jimmy a. hakua katika hali ya furaha wala uchangamfu niliozoea kumuona nao siku zote, nilianza kuhisi kua hali haikua shwari kabisa kwa maana huyu bwana mkubwa inasemekana ndie anaetumiwa na PABLO Mwaki kumuunganishia kwa Ramla. hivyo inawezekana amegundua kua nimeshajua hila zake zote zinazoendelea. Lakini mimi sikujali nikaendelea na shughuli zangu kama kawaida
Nikiwa naendelea kuchapa kazi kwenye Computer yangu pale ofini nilipokea
ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa Ntahondi akinilaumu "Nilikuomba uwe na Subra pia uwe Msiri lakini sasa Umeshindwa” nikamjibu haraka haraka “Kwani kuna nini tena Ntahondi?”
“kwanini umemueleza mama yako mambo haya?, Mama yako kaenda
nyumbani kwa Mama yake na Ramla wametukanana sana na sasa Imeshajulikana
kua wewe umegundua mpango wao, kwa sasa Mwaki anamtafuta anaeyevujisha siri hizi sasa UNATAKA NIUAWE?" Sikushtuka sana kwa kua tayari nilikua nimeshajua kua Mama alienda kwa Mama Ramla na
walilumbana sana ila sasa hofu yangu ikawa kwa usalama wa Ntahondi endapo atagundulika kua ndie anaenipa siri zao nyeti, nikiwa bado nawaza jambo hili nikaanza kupata picha ya kwanini Mr Jimmy hakunichangamkia wakati naingia ofisini, kitu ambacho si kawaida yake
Niliendelea na kazi katika hali hofu kwa takribani wiki tatu mfululizo bila ya kua na Mahusiano mazuri ya kimazungumzo na Boss wangu Mr Jimmy, haikunipa tabu kwa kua nilikua nimeshamjua Vema kua ni miongoni mwa watu hatari katika maisha yangu kwa sasa, Lakini pia katika kipindi hiki chote sikuwasiliana na Ramla kitu ambacho si kawaida yetu japo hali hii ilizidi kunithbitishia kua sasa taa ya hatari ilikua imeshamulika. Ila nachoshukuru Mungu ni kua nimeendelea kupokea taarifa za kuimarika kwa hali ya Mama kule nyumbani, pia nami nimekua nikipokea massage za kunifariji na kunipa kuniliwaza kutoka kwa ndugu zangu kutokana na matatizo haya, Pia niliendelea kupata taarifa za kiusalama kutoka kwa Ntohondi . japo kwa sasa haikua taarifa Nzito pengine hakua akipata taarifa kutokana umakini mpya kufuatia kuvuja kwa siri zao, au pengine alizipata ila hakuniambia kwakua haniamini sana katika utunzaji wa siri hizo..
Siku moja majira ya saa mbili kasoro(usiku) nilikua nimeenda nyumbani kwa Mwl Honde katika maongezi yetu akijaribu kunishauri nini cha kufanya japo mwanzo alipokua akinidokeza kuhusu
kinachoendelea kati ya Ramla na Pablo Mwaki nilikua nikimuona kama Mchonganishi na Fatani wa Penzi letu lakini kwa sasa amekua ndo kimbilio langu, Tukiwa katikati ya mazungumzo Ghafla nilipokea ujumbe mfupi wa Maandishi kutoka kwa Ntahondi akinitaka tuonane haraka sana maeneo ya Leaders Club, Ikanibidi sasa haraka haraka nisimame na kumuaga Honde ili nimuwahi Ntahond nikijua tu kuna taarifa za muhimu sana nikazipate, nikaondoka moja kwa moja mpaka Leaders japo kulikua na foleni ndefu ila kwa umahiri wa dereva boda boda niliekua nae ndani ya dk 20 tukawa tumewasili,
nilipofika nikaenda mpaka Kiwanjani pembeni ya Bendi ya Muziki iliyokua ikitumbuiza pale Leaders nikachukua kiti na kuagiza kinywaji, kisha nikatoa simu yangu na kumpigia Ntahondi ili nimtaarifu kua nimeshafika, Nilipompigia akapokea na kusema "Nimeshakuona ulipo nakuja hapo hapo" kisha akakata simu
Baada ya muda kidogo akaja mpaka pale nilipo kisha akaketi na kunisalimu, nae akaagiza kinywaji chake kisha akaniambia kua tungeenda upande wa pili kule wanapouza Nyama choma ili tuwe salama zaidi..
Tukaenda ule upande wa pili na kisha tukaanza mazungumzo japo mie nikiwa na mchecheto zaidi wa kutaka kujua kinachoendelea, nae Ntahondi bila ajizi akaanza kufunguka
“Mambo vipi”
“Poa tu za tangu jana?”
“Nzuri hivyo hivyo, kwanza pole na Mchoko”
“Ahsante”
“Sasa nimekuja kukuongezea mchoko mwingine,” Maneno haya yalipenya sawia katika masikio yangu nikawa namsikiliza kwa makini, kisha akaendelea
"Ni hivi Mwaki sasa yuko serious anataka kumvisha pete ya uchumba Ramla, na Tendo hilo wamepanga kulifanya hadharani, itakua ni siku ya Graduation yetu, Wakati wa zawadi Mwaki amepanga kumpa Ramla zawadi ya Gari ya kifahari na kisha baada ya hapo atamvisha na Pete ya uchumba” Akashusha tena pumzi kabla ya kuendelea kufunguka
“Na tayari sasa ameshaanza mchakato wa kukusaka ili usije ukaleta usumbufu siku hiyo, na kama atakutia mikononi pengine ndo itakua mwisho wa maisha yako, hivyo kua makini ikiwezekana hata kazini kwa sasa usiende maana Boss wako Mr Jimmy nae ni mwanamtandao, pia ikiwezekana hata pale kwako uhame haraka na ukipata muda ukatoe taarifa Polisi kwa usalama wako” baada ya maelezo hayo mdada akasimama kisha akaniaga na kunisisitiza niwe makini sana, Wakati tunaondoka akanikumbusha tena jambo jingine
“Pia inabidi ubadili namba yako ya simu maana hawa jamaa wana mtandao mkubwa wasije wakatufuatilia wakagundua mambo yetu” tukaagana kisha Ntahondi akaondoka zake, nilibaki namshangaa sana sikuamini kama motto wa kike kama Yule angekua na ujasiri na uelewa wa mambo kwa kiwango kile,
Nami nikasimama na kuondoka mpaka kituo cha polisi cha Msimbazi ili kutoa taarifa ya kila kinachoendelea japo nilikumbana na vikwazo vya hapa na pale kutoka kwa ma askari wapenda rushwa ambao wanaijua nguvu ya PABLO MWAKI Lakini hatime nilifanikiwa kufungua kesi kisha nikarudi mpaka kwangu nilipofika chumbani nikajilaza kidogo juu ya kochi ili nitafakari pa kwenda kulala tofauti pale Nyumbani kama alivyonielekeza Ntahondi lakini hapo hapo usingizi ukanipitia..
*****
Nikaamka na kwenda kuoga haraka kisha nikarui ndani kuvaa ili niende kwa Mwl Stephen Honde nikamueleze hali ilipofikia, Pia nikiwa na lengo la kwenda kukata tiketi ya Buss nirudi kwanza nyumbani Tabora nikatulize akili ili nijipange kupambana na huyu fedhuli, nilipotoka kwangu nikatembea mpaka barabarani, ikanibidi nikachukue Tax kiusalama maana sasa sikupaswa kuonekana kwakua tayari nilikua kwenye mtego wa Mwaki, nikamchukua Tax driver ambae hua ananibeba mara kwa mara na kumuelekeza anipeleke Stand ya Ubungo ili nikakate tiketi na kisha anipeleke IFM Kwa Mwl Stephen Honde tukiwa njiani dereva aliniomba tupitie Shelly tukaweke mafuta, nikakubali, ila cha ajabu huyu dereva alikua akiendesha huku akiwa bussy na simu yake aki chart kitu ambacho nilishindwa kuvumulia ikabidi nimlalamikie nae akaniomba radhi, akaendelea kuendesha mpaka Shelly ya mafuta..
Baada ya kujaza mafuta akatoa pesa na kumlipa muhudumu pale shelly, ila kabla hatujaanza kuondoka wakatokea jamaa wawili, watanashati, wakamwambia dereva kua awapeleke Ubungo, dereva akawajibu kua tayari ana abiria mwingine japo nae anaenda huko huko ngoja tumuombe kama atakubali, aliponiomba nikaona acha tu nimsaidie kijana huyu aingize riziki,nikawakubalia wakaingi ndani ya gari vijana wale kisha wakakaa seat za nyuma na tukaendelea na safari yetu tukiwa ndani ya gari ghafla huyu kijana aliekaa nyuma yangu nikasikia kanishika begani, nilipogeuka tu nikasikia nimepigwa na kitu kizito kichwani kabla sijakaa sawa huyu mwingine aliekua nyuma ya dereva nae akanipiga ngumi nzito, basi ikawa ni kichapo juu kichapo mpaka nikawa nasikia kizunguzungu, mara mmoja akaniwahi mikono kisha huyu mwingine akanifunga kitambaa cheusi usoni, Wakati haya yakiendelea huyu Dereva alikua katulia kimya akiendelea kuendesha gari taratibu hapo ndo nikajua kua alikua anajua kila kitu,
Nikiwa nimefungwa kitambaa usoni nilimsikia Yule kijana aliekua nyuma ya dereva akimuuliza dereva kua anaielewa vema njia waliyomuelekeza? Dereva nae akajibu kua anaijua vizuri hapo sasa nikajua tayari nimeingi mikononi mwa PABLO MWAKI, Gari ilikua ikitembea kwa kasi huku nikiwa sijui tunaelekea wapi, Nikawa katika majuto ya hali ya juu sana, Lengo langu kwenda Tabora sasa limekufa na hata Mwl Honde ndo simuoni tena, Nilijua sasa Kifo kipo mlangoni, Gari ikiwa inaendelea kuchuka kasi ghafla meseji ikaingia kwenye simu yangu sikujua ni nani lakin, yule kijana aliekua nyuma yangu akaingiza mkono kwenye mfuko wa wa suruali yangu na kuitoa simu yangu, Nikasikia akishangaa na kuniuliza
"We mbwa, huyu Ntahondi ndo nani?" nikajua tu itakua ni Ntahondi ndie amenitumia ujumbe, na kabla sijajibu chochote akaendelea kuongea
"Kumbe huyu ndie anaetoa siri zetu eeh?, tutamshughulikia" Nilizidi kuchanganyikiwa na sikujua Ntahondi alikua ameniandikia ujumbe gani, japo mimi tayari nimeshakamatwa ila niliamini kua wa kuniokoa ni Ntahondi tu kwakua alikua akijua kila kinachoendelea hivyo kama atawasiliana na watu wa kwetu akawapa maelekezo yote huenda wakamtia nguvuni huyo Pablo na hatimae nikapatikana, lakini sasa nae kaishagunduliwa
INAENDELEA HAPA SEHEMU YA ===>www.2jiachie.com/2014/04/riwaya-siku-ya-graduationsehemu-ya-3.html
LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment