ad

ad

RIWAYA: SIKU YA GRADUATION...SEHEMU YA 3

MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI
SEHEMU YA TATU
Msafara uliendelea huku nikiwa nimefungwa kitambaa cheusi usoni, Majadiliano yaliyokua yakiendelea ndani ya Tax kati ya hawa maharamia na huyu dereva wa Tax yaliashiria kua dereva huyu alikua amelipwa kwa ajili yakufanikisha mpango wa kuniteka, iliniuma sana kwa jinsi nilivyomuamini kijana huyu leo kwa tamaa yake ya pesa tena pesa yenyewe itakua ni kidogo t undo ameamua kushiriki kitendo cha kunitoa uhai wangu. Siku na lakufanya kabisa, Safari ikazidi kuchukua kasi Ilituchukua muda mrefu takribani saa moja na nusu hivi tukiwa njiani tu, mpaka hatimae tukafika Eneo lililokusudiwa

Gari yetu ilisimama kwa muda kama wa dk mbili kisha nikasikia Geti likifunguliwa na kisha gari ikaingia ndani baada ya gari kusimama walishuka vijana wale wawili na mmoja akafungua mlango wa mbele upande niliokua nimekaa mimi akanivuta kama kiroba nikajikuta nimeshuka kama mzigo mpa chini kisha akanifungua kitambaa usoni. nilijaribu kuangaza huku na kule lakini sikuelewa tuko wapi! ilikua ni ndani ya Fance kubwa iliyozunguka Jengo kubwa sana chakavu mfano wa magodaun ya Tumbaku. mule ndani kulikua na vijana wengine watatu, woteni warefu, wamejazi misuli yao vilivyo, wawili wametinga miwani myeusi, na mmoja akiwa hana miwani na kavaa Suti nyeusi. walinichukua na kuniingiza ndani kabisa ya jengo hilo..

Mazingira ya ndani ya Jengo hilo yaliku ni ya kutisha sana maana kulikua na ukimya wa hali ya juu, pia hata hawa jamaa sura zao zilivyokaa kikatili ukiwaangalia tu utahisi harufu ya kifo, nilipo fikishwa mule ndani nikafungwa kamba mikono kisha wakanining'iniza juu mithili ya mbuzi anaesubiri kuchunwa ngozi kisha jamaa hawa wasio na huruma hata chembe walianza kunichapa mijeredi ya nguvu, nililia nakupiga kelele mpaka nikawa naioshiwa nguvu,lakini kele zangu hazikuwazuia hawa jamaa kuendelea kuniadhibu. mwili wote ulikua umevimba vimba kwa alama za Fimbo.. baada ya Muda akaja kijana mmoja akiwa ameshika Msumari uwa moto nadhani ndo ulikua umetoka jikoni, Naam ulikua umewiva kisawasawa akaja mpaka pale niliopokua nimetundikwa akaanza kufanya kama vile anachora maandishi kifuani kwangu, kwenye mapaja, na mgongoni nilisikia maumivu makali sana nililia kwa sauti mpaka nikajihisi sasa kupoteza fahamu..

Ndani ya dakika kama kumi na tano nilizofikishwa mule ndani nilikua nimeshaharibika mwili mzima kwa adhabu na mateso makali niliyokumbana nayo mule. wakati nikiendelea kupewa adhabu za kila aina ghafla akaja yule kijana aliekua amevaa suti, alikua kama amechanganyikiwa na jambo fulani;
"Jamani kuna hali ya hatari kidogo"
wale viajana wote wakamgeukia na kumsikiliza, kisha akaendelea
"Wakati akina Zungu wanamteka huyu Dogo, nasikia walianza kumpiga mule mule ndani ya Tax sasa kuna watu walishuhudia hilo tukio hivyo wamechukua namba ya Tax na wameenda kutoa taarifa Polisi"
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa jamaa huyu ambae alionekana kama ndie msimamizi wa kitngo kile cha mateso akadakia kijana mwingine aliekua akiniunguza na Msumali wa moto
"Hili sasa ni tatizo lakini kwa kua huyu Tax Driver hajaondoka me nadhani tumzuie mpaka Soo likitulia huko town ndo tumuache aende..." kabla hajamaliza yule mwenye suti akadakia
"Hapana, hatupaswi kumuachia, akibanwa huyu atasema tu, muingizeni ndani mummalize kimya kimya" Nilishtuka sana niliposikia kua kijana Yule anatakiwa auwawe, hapo ndipo nikajua kua sasa hata mimi siponi tena, baada ya maelekezo yale vijana wa kazi wote wakatoka nje wakaniacha mie nikiwa pale juu naning’inia

Ndani ya muda mfupi walirudi ndani wakiwa na kijana yule dereva tax japo hawakuingia nae katika chumba nilichokuwepo mie wakaenda nae mpaka chumba cha mbele kisha nikaanza kusikia kelele kali za kilio alichokua akilia kijana huyu, alilia kwa sauti ya hali ya juu kisha akatulia kimya, sikumsikia tena wala sikujua wamemfanya nini, baada ya muda wakaja wale vijana waliokua wakinitesa mimi walipofika pale usawa wangu wakaikata kamba niliyokua nimefungwa nayo pale juu nikaanguka kama kiroba cha taka mpaka chini kisha wakanimwagia maji mengi halafu wakaondoka

Ilipofika jioni nikiwa nimelala pale chini kama mzoga waliingia tena wale vijana na kuniinua kisha wakaniambia niwafuate, nilianza kuwafuat huku nikichechemea kwa taabu kutokana na maumivu niliyoyapata siku nzima, tukafika mpaka kwenye Chumba kilichoandikwa PEPO HURU, sikuelewa maana ya neno hilo nikahisi ndani mule kuna raha japo kidogo ila hali ilikua tofauti nilipoingia nilikuta maiti ikiwa imelala juu ya dimbwi la damu, utumbu ukiwa nje ya tumbo. Niliogopa sana hali ile nikajikaza na kusogea eneo lile Kuangalia vizuri 'Tobaa", alikua ni yule kijana dereva wa Tax.. wameamua kumuua ili asiende kutoa siri. na hapo sasa nikazidi kupoteza Bima ya Matumaini kama nitatoka salama mule ndani. Vijana wale wakaniamuru nimnyanyua maiti yule kisha nimpeleke nje halafu nirudi kusafisha damu na uchafu wa maiti yule..

Nilimuonea huruma sana kijana huyu dereva wa Tax kwa kifo cha kinyama kama kile japo niliamini Mungu ameamua kunilipia kwa ushenzi alionifanyia mimi wa kunikamatisha kwa maharamia hawa kwa Tamaa ya pesa kidogo, Nikafika mpaka alipolala kijana huyu ili nimnyanyue, Cha ajabu wakati nikiwa nimeinama naanza kuibeba maiti ile maharamia hawa wakawa wananipiga picha, niliogopa kuhoji kuhusu picha hizo nilizokua nikipigwa nikijua nitapewa kiminyo kikali kuliko kile cha awali, nikaibeba maiti ile mpaka nje kabisa nikaicha kisha nikarudi ndani kusafisha lile eneo alilouliwa.. na baada ya hapo nilirudishwa ndani kuendelea na Adhabu,

Ilipita wiki moja nikiendelea kupata mateso makali sana ikiwemo kupigwa na shoti za Umeme, Hali ilikua ngumu sana kwangu, kila siku nilikua nikapata adhabu kali na za kila aina huku nikipewa chakula kidogo sana na maji. siku moja nikiwa nimefunguliwa kamba niko nimekaa kwenye sakafu napata chakula nakumbuka ilikua ni ugali na dagaa Ghafla nlisikia mlango ukifungulia kisha akaangizwa Msichana mmoja akiwa kalainika sana bila shaka ni kwa kichapo alichopewa na mafedhuli hawa, Sikumjua kwa haraka ila nilipotuliza macho kumuangalia vizuri alikua ni Ntahondi, Shemeji yangu kwa Ramla, ilikua ni vigumu kumtambua kwa urembo wake aliokua nao maana kwa sasa alikua amesawajika, amevuja damu mpaka zimeganda mwili mwake, inaonekana alipigwa sana. nilijisikia majonzi mpaka hamu ya kula iliniisha..

Nilipomsogelea niligundua kua alikua amepoteza fahamu, Roho iliniuma sana nikiamini kua ni mimi ndie nimemponza mpaka kufikishwa pale, nikiwa nimesimama nisijue cha kufanya likaniijia wazo nikaenda pembeni mwa chumba kile nyuma ya Mashine ya umeme waliyokua wakiitumia kunitesea nikachukua Dumu la maji nikaja nalo mpaka pale alipolala nikammwagia maji mengi kichwani na mwilini, baada ya muda sio mrefu alizinduka!! Aliponiangalia alianza kulia kwa uchungu sana, nilijaribu kumbembeleza lakini hakunyamaza.. mpaka baadae kabisa alitulia na kuanza kunisimulia yaliyomkuta japo alikua akiongea kwa taabu sana kutokana na maumivu anayoyapata
"Siku ulipotea ghafla tulijitahidi sana kukutafuta bila ya Mafanikio, kesho yake kaka yako wa Tabora alikuja Dar tukaendelea kukutafuta kila kona bila ya Mafanikio, Ramla aligoma kushiriki kabisa kukutafuta yeye alikua busy na Mipango yao ya Kuvishana pete, na Mwaki ameamua kugharamia Sherehe yote ya wahitimu Hakuna mwanachuo yeyote kulipa gharama za Sherehe" alikaa kimya kwa muda kasha akaendelea
"Kilichotushangaza zaidi baada kama ya siku tatu mbele uliokotwa Mwili wa huyo dereva Tax akiwa ametumbuliwa tumbo, katobolewa macho nk walipojaribu kuupekua vizuri mwili wake wakakuta picha mbili zikikuonesha wewe ndo uko nae, na Mpaka sasa vyombo vyote vya habari vimesha riport kua wewe inasemekana ndo umemuua" Maneno ya Ntahondi yalizidi kunifanya niwe kama kichaa, nilizidi kuchanganyikiwa, yaani sasa mjini mimi Ndo natafutwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ambayo sikushiriki, nilishindwa kujizuia nilianza kulia nikijua sasa vyovyote iwavyo Mwisho wangu umefika,

Ntahondi aliendelea kunipa habari kua kule mjini Mama yangu amekua akipoteza fahamu kila saa kufuati kutoweka kwangu na taarifa za habari kua natafutwa kwa Tuhuma za Mauaji ya Dereva Tax, Pia akaniambia Mpango uliopo ni kwamba tunatakiwa kuuawa siku hiyo ya Graduation ili Ramla na hawara yake Mwaki waweze kuishi kwa Amani..

Pia Ntahond alinieleza kua anaenishughulika zaidi kule mjini ni Jarufu, pamoja na Mwl Honde. nilifarijika kidogo kusikia kua swahiba wangu Mwalimu Honde ananishughulika, nilipata matumaini kwa kua najua fika kua Honde amemuoa mdogo wake na Waziri Mkuu wa Nchi yetu hivyo niliamini kua inaweza ikawa ahueni kama Honde ataamua kulifikisha suala hili kwa Mhe Waziri..

Nikiwa naendelea kububujikwa na machozi kutokana na maneno yaliyouchuma na kuuunguza moyo wangu kutoka kwa Ntahondi, nae aliendelea kunipa Story za kila kinachoendelea kule mjini na mpaka yeye kukamatwa na kufikishwa kule Msituni.
"Nilipopata taarifa kua unatakiwa kukamatwa siku hiyo nikawahi kukutumia ujumbe mfupi kwenye simu yako ili uzidi kujihami kumbe tayari ulikua umeshakamatwa, na baadae nikapokea msg kutoka kwako kua tuonane Maeneo ya Coco Beach, kumbe walioijibu msg ile walikua ni hawa Majambazi wa Mwaki na hatimae wakanitia nguvuni, wakanipiga sana na kunitesa kinyama, nimeumizwa sana mbaya zaidi nimedhalilishwa kwa kuvuliwa nguo zote kisha nikaanza kuchapwa bakoro mwilini mpaka nikapoteza fahamu, nazinduka ndo najikuta humu" Alimaliza kuongea Ntahondi kisha akanitaka na mimi nimuelezee hali ikoje kwangu na mule ndani kwa ujumla, na vipi tungejikomboa kutoka katika makucha ya Ibilisi huyu

Nami nilimueleza mateso niliyopewa mule ndani ila ikabidi baadhi ya mateso nimfiche nikihofia kumzidisha hofu na kumkatisha tamaa ya kuishi, lakini Mwisho kabisa nikamwambia sisi ni vijana makini Lazima tupiganie Maisha yetu na yuhakikishe tunatoka humu, wakati nikiongea kwa uchungu maneno haya ya kijasiri ambayo naimani bila shaka kichwani mwa Ntahondi ilikua ni Ndoto ya mchana, ni kama kujifunika Tishu kwenye mvua ya Elninino

ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA

 LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

No comments

Powered by Blogger.