ad

ad

YANGA KANYAGA TWENDE ...PICHA ZIPO HAPA

 PICHA ZOTE NA 2JIACHIE,DAR
Dar es Salaam. Mshambuliaji Mrisho Ngassa wa Yanga leo atakuwa chini ya ulinzi mkali kwa ngome ya Al-Ahly wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ngassa ameweka rekodi ya kufunga mabao matatu mara mbili wakati mabingwa hao wa Tanzania walipoweka rekodi ya kufunga jumla ya mabao 12 katika mchezo wa hatua ya awali.
Baada ya kufunga mabao sita dhidi ya timu dhaifu ya Komorozine ya Comoro, Ngassa atajikuta kwenye ulinzi mkali mbele ya safu ya ulinzi wa Al Ahly utakaoongozwa na beki mzoefu Wael Gomaa.

Mbali ya Ngassa, Ahly pia wanatakiwa kuwa makini na Mrundi Didier Kavumbagu na Mganda Hamis Kiiza, ambao kila mmoja alifunga mabao mawili dhidi ya Wacomoro.
Pia kwa mara ya kwanza mpachika mabao mahiri wa Uganda, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuwamo kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya Yanga baada ya kukosa mechi zilizopita kutokana na utata wa usajili wake.

Washambuliaji hao wa Yanga, leo watakuwa wakisaka kuivunja rekodi ya mkongwe Omary Hussein aliyoiweka miaka 32, akiwa ni mchezaji pekee aliyefunga bao dhidi ya Al Ahly.
Hussein aliweka rekodi hiyo mwaka 1982, alipoifungia Yanga bao hilo pekee walipotoka sare 1-1 na kuondolewa na Waarabu kwa jumla ya mabao 6-1, baada ya mchezo wa kwanza kufunga mabao 5-0 jijini Cairo.

Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amejigamba kwamba  atahakikisha anavunja rekodi ya Al Ahly dhidi ya  Yanga kwa kuondoka na ushindi katika mchezo huo.
“Ahly ni timu ngumu na ina uzoefu wa kutosha katika mashindano haya, lakini hatuwaogopi tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunafuzu raundi inayofuata,”alisema Pluijm.

Naye kocha wa Al Ahly, Mohamed Youssef atawakosa viungo Mohamed AbouTrika na Mohamed Barakat daruga mwaka jana, pia amekiri kushtushwa na kasi ya Yanga katika kupachika mabao, lakini amesisitiza kwamba lengo lake ni kupata ushindi na kusonga mbele.
Beki mkongwe Wael Gomaa, (38) amerejea kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Cairo Red Devils, pamoja na kutangaza kujiuzulu mwisho wa msimu huu. Al Ahly ina wachezaji wengine nyota ambao ni Gedo, Ahmed Fathy na Emad Moteab.

Ahly ya Misri ni mabingwa watetezi na kihistoria wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo ni mashindano tajiri zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Klabu hii ya Al Ahly imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mara nane na mara ya mwisho ilitwaa ubingwa huo mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa mujibu wa rekodi, Yanga na Al Ahly zimewahi kukutana mara sita katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Ahly imeshinda mechi nne na mbili zikimalizika kwa sare.
Yanga imekuwa kambini kwa muda wa wiki moja ikijiandaa na mechi hii, ambapo inataka kugeuza kibao cha kukataa kuwa wateja wa Al Ahly.

Pia Yanga inataka kushinda mechi hii ili kujiweka katika mazingira mazuri kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa Jumamosi ijayo mjini Cairo.

Wakati huohuo; Klabu za soka za Ukanda wa Afrika Mashariki zina kibarua kigumu leo zinapowakaribisha wapinzani wao kutoka Afrika Kaskazini na Zambia.
Jijini Nairobi, Gor Mahia watakuwa na kibarua kingine dhidi ya Esperance ya Tunisia, pia katika mchezo wa ligi hiyo.

Wawakilishi wengine wa ukanda huo, KCCA ya Uganda watakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), dhidi ya Nkana Read Devils ya Zambia.
Mechi nyingine ni Zamalek wataivaa Kabuscorp, wakati  Enyimba watakuwa nyumbani kuivaa Real Bamako. Huku Entente Setif watakuwa ugenini kuivaa ASFA Yennenga.
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wataiongoza TP Mazembe kuwavaa Astres Douala, Raja Casablanca watapepetana na Horoya na Vita itakuwa ugenini kuivaa Dynamos ya Zimbabwe.
Powered by Blogger.