USIPOWAJIBIKA KAMA MUME, JUA UNA MUME MWENZIO!
TUNAKUTANA tena kupitia ukurasa huu ambao ni namba moja kwa kuandika
makala nzuri zinazogusa maisha yako ya kimapenzi. Ukiwa unaufuatilia
kila wiki, mapenzi hayawezi kukutesa kama yanavyowatesa wengine.
Utajua
mbinu bora za kumpata mwenza sahihi lakini pia jinsi ya kuishi naye kwa
raha mustarehe na kamwe asifikirie kukusaliti wala kukuacha. Mpenzi
msomaji wangu, leo nataka kuzungumza na wanaume walio kwenye ndoa lakini
pia si vibaya na wale wanaotarajia kuingia kwenye maisha hayo wakasoma.
Nimelazimika kuandika juu ya mada hii kutokana na namna ambavyo kasi
ya wanaume kusalitiwa imekuwa kubwa huku wengine wakiombwa talaka na
wake zao waliotokea kuwapenda.
Huwa nakaa na kujiuliza, inakuwaje
mkeo ambaye aliapa kutokusaliti leo aamue kutoka kwenye ndoa na kwenda
kumvulia nguo mwanaume mwingine?
Inakuwaje mwanamke anamuahidi mumewe kuishi naye kwa shida na raha lakini siku ya siku anaomba talaka tena macho yakiwa makavu?
Kwa
hili unaweza kubaki njia panda lakini nilichokibaini ni kwamba,
wanawake wengine wanakuwa na tamaa zao na wanaposhawishiwa, husahau
viapo walivyotoa huko nyuma.
Mbali na hili nimegundua kuwa, baadhi ya wanaume wanasalitiwa na
kuombwa talaka kwa sababu ya kushindwa kuchukua nafasi zao kama wanaume,
na hili ndilo nitakalolizungumzia leo.
Baadhi ya wanaume wanakimbilia kuopoa wake wazuri lakini wakishaingia kwenye ndoa, wanajisahau na kubweteka.
Ifahamike kwamba, mwanaume anayemjali mpenzi wake ndiye anayetimiza
wajibu wake, lakini wengi hujikuta wakitoswa na wapenzi wao kutokana na
ufahamu mdogo ama dharau ya mambo madogomadogo.
Ni vyema ukatambua kuwa uhusiano hauna mambo ‘simpo’. Kila kitu kina
umuhimu mkubwa kulingana na nafasi yake sambamba na utekelezaji wako.
Mwanamke anahitaji mahaba yaliyoshiba na hakika ukijua ‘kumhendo’ kama mke kwa kiwango kitakachomridhisha, hatawaza kukuacha wala kukutafutia mume mweziyo. Unawezaje kulifanikisha hilo?
Mwanamke anahitaji mahaba yaliyoshiba na hakika ukijua ‘kumhendo’ kama mke kwa kiwango kitakachomridhisha, hatawaza kukuacha wala kukutafutia mume mweziyo. Unawezaje kulifanikisha hilo?
Mpende, mheshimu, mjali
Najua unaweza kusema unampenda mkeo na ukawa unawaambia wenzako hivyo lakini je, unaonesha hivyo kwa vitendo? Je, ni kweli umempa nafasi kubwa kwenye moyo wako na kwamba yeye ndiye kila kitu kwako?
Najua unaweza kusema unampenda mkeo na ukawa unawaambia wenzako hivyo lakini je, unaonesha hivyo kwa vitendo? Je, ni kweli umempa nafasi kubwa kwenye moyo wako na kwamba yeye ndiye kila kitu kwako?
Tufahamu kwamba, mwanaume kupitia mapenzi yake ana uwezo mkubwa wa
kumshika vilivyo mkewe na kumfanya asibabaishwe na wanaume wakware.
Ndiyo
maana nasema kama mpenzi wako anakuacha na kwenda kwa mwingine au
anakusubiri unakwenda kazini kisha anachepuka, ujue kuwa umeshindwa
kuchukua nafasi yako kama mume.
Wanawake wanawapenda wanaume ambao huonesha upendo kwa vitendo,
huonesha kujali, jasiri wasioogopa changamoto za kimaisha hivyo anza leo
kutimiza wajibu wako, naamini utamfanya mwenza wako akuone ni wa pekee
unayestahili kupendwa na kuheshimiwa.
Muoneshe kuwa umetulia
Hapa namaanisha kwamba, unatakiwa
kumuonesha mkeo kuwa umetulia na si mtu wa kuchenguliwa akili na hivi
visichana vya kizazi cha dot.com ambavyo haviangalii mume wa mtu wala
nini. Wao wanachotafuta ni pesa hivyo watakutega kwa vivazi na hata
kujilengesha kwako kwa kukupigia simu au kukutumia sms za kimapenzi.
Ili kumfanya mkeo awe na imani na wewe unatakiwa kuwapotezea. Kuwa
makini nao na usiwaruhusu wakuzoee. Ukifanya hivyo na mkeo akajua si mtu
wa kubabaishwa na micharuko, naye atatulia kwani atajua yuko na mtu
makini.
Kumbuka ukiwa ni mtu wa kuendekeza ukaribu na hawa mabinti wasio na
heshima, mkeo naye atajiweka karibu na masharobaro ambao wengi wao
hawana heshima na wanaweza kumfanyia vitendo visivyo vya kistaarabu na
hatimaye kuifanya ndoa yenu kuwa kama shimo la taka.
Mpe haki yake
Labda kama unaumwa au una matatizo yanayofahamika lakini ukweli ni kwamba, kama humpi mkeo haki yake ya ndoa kama inavyostahili, atavumilia sana lakini mwisho atakusaliti kama siyo kuomba talaka yake.

Katika hili naomba niseme kwamba, raha ya ndoa pamoja na mambo
mengine ni pale mnapokutana faragha, ukimchengachenga mkeo wakati
mwenzio anakuhitaji, unajitengenezea mazingira ya kuwapa mwanya wanaume
wengine wakudokolee ‘chakula’ chako.
Mgeuze kuwa mchumba
Kumbuka yale uliyokuwa ukimfanyia mkeo enzi zile mkiwa wachumba mfanyie sasa. Mnunulie zawadi, mtoe ‘out’ siku mojamoja na mambo mengine ambayo unajua yatamfanya aamini bado unampenda licha ya kwamba mmekuwa pamoja kwa muda mrefu, hata kusaliti kamwe.

Post a Comment