ad

ad

Kapombe: Naumwa, nipo tu nyumbani Moro


BEKI aliyekuwa akikipiga AS Cannes ya Ufaransa, Shomari Kapombe, amesema ameshindwa kufanya mazoezi kwa kuwa amekuwa akisumbuliwa na malaria mara kwa mara.

Awali beki huyo alikuwa akicheza Simba na alikwenda kuichezea AS Cannes lakini amesema kwa sasa anatumia muda wake mwingi akiwa Morogoro akijiuguza.

Akizungumza beki huyo ambaye inadaiwa yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kutua Azam FC, alisema kwa sasa anashinda tu nyumbani kutokana na kusumbuliwa na malaria kiasi kwamba hajielewi.

“Kwa sasa nipo tu Morogoro nashinda nyumbani kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria, ugonjwa huu umesababisha mimi kushindwa kufanya mazoezi kabisa ili kuweza kuendelea kulinda kiwango changu.
 
“Ndiyo maana sipendi kuzungumzia masuala ya soka kwa sasa, kwa anayetaka kufahamu naelekea timu gani amuulize wakala wangu ndiye atamuelekeza kila kitu anachohitaji, mimi sina cha kuongea kwa sasa,” alisema Kapombe.
Powered by Blogger.