Pluijm: Tutawamaliza Al Ahly kwa dakika 90
JOTO la mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
itakayopigwa Jumamosi hii baina ya Yanga SC na Al Ahly ya Misri linazidi
kuwa kali ambapo Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema
atahakikisha anawafunga mabingwa hao watetezi.
Pluijm ambaye ni raia wa Uholanzi alisema kwamba mipango aliyonayo kwenye mechi hiyo iliyokusanya hisia za wadau wengi wa soka nchini ni kuhakikisha anaifunga timu hiyo kwenye mechi ya kwanza.
Baada ya mechi hiyo, Yanga itapaa na kwenda Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano na miamba hiyo ya Afrika.
Aidha, kocha huyo aliongeza kuwa kikosi chake hakina haja ya kuihofia timu yoyote inayokuja nchini, badala yake kinachotakiwa ni kuhakikisha wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani.
Alisema hatakubali kuzuia na kuiweka timu nyuma kwa kigezo cha kuhofia uwezo wa Al Ahly, badala yake atapambana nao kama ilivyo kwa timu nyingine za Afrika.
“Kikubwa ni ushindi wa hapa nyumbani kwanza, dakika tisini za hapa tunatakiwa kuzitumia vyema, mipango yetu ni kuhakikisha tunaitumia vema nafasi ya uwanja wa nyumbani, hatuwezi kuzuia na kuacha kushambulia, huo utakuwa ni woga. Lazima timu icheze na kushambulia kwa nguvu kwa lengo la kutafuta ushindi mzuri wa hapa nyumbani kwanza,” alisema Pluijm.
Kocha huyo pia alisema aliiona mechi ya fainali ya Super Cup baina ya Al Ahly na Safxien ya Tunisia ambapo alikiri kutosheka kuisoma Al Ahly jinsi inavyocheza na kuzibaini mbinu zao mpya.
“Niliiona ile fainali ya Super Cup halafu pia naifahamu Al Ahly, kwa hiyo ile mechi iliniongezea kitu tu, mara nyingi huwa wanapenda kutumia mawinga kwa ajili ya kutengeneza nafasi zao za kufunga, tayari nimeshaanza kulifanyia kazi hili suala na ninajua nini cha kufanya kutokana na mfumo wao huo,” alisema.

Post a Comment