Kaseja, Dida wawagawa mashabiki Yanga
KITENDO cha mashabiki wa Yanga kugawanyika pande mbili katika kuwasifia makipa Juma Kaseja na Deogratius Munishi ‘Dida’ kwenye mazoezi ya timu hiyo, kimesababisha kocha wa makipa, Juma Pondamali, kushikwa na kigugumizi katika kuamua nani anafaa kuwa kipa namba moja wa timu hiyo.
Kundi kubwa la mashabiki waliofurika kushuhudia mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, lilionekana kunogewa na viwango vya Kaseja na Dida, hali iliyozua mjadala baina yao kuhusu nani anafaa kuwa kipa namba moja.
Kundi la kwanza lilionekana kuukubali uwezo wa mlinda mlango Kaseja namna alivyokuwa akifanya kwa ufasaha mazoezi aliyokuwa akipewa na Pondamali, hali iliyowafanya kumpigia makofi kila mara alipokuwa akifanya mazoezi hayo.
“Kaseja bonge la kipa bwana, uwezo wake bado uko juu sana, alichofanya katika mchezo wa Yanga na Simba ni ‘mistake’ tu za kimchezo. Kaseja atatusaidia sana kwenye mashindano ya kimataifa kwa uzoefu wake,” alisema shabiki aliyekuwa upande wa Kaseja.
Kundi la pili lilionekana kukoshwa zaidi na kiwango cha Dida, namna alivyokuwa makini katika kuyaelewa mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na Pondamali, hali iliyosababisha wawe wanapiga makofi kwa nguvu na kumshangilia.
“Dida anajua sana, sijui kwa nini makocha wetu huwa wanashindwa kumuamini na kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza! Jamaa ni mwepesi sana na anaonekana anayaelewa mazoezi ya mwalimu kwa haraka zaidi,” alisema mmoja wa mashabiki waliokuwa wakimshangilia Dida.
Championi Jumatano lilizungumza na kocha wa makipa wa timu hiyo, Juma Pondamali, kutaka kujua mtazamo wake juu ya mvurugano huo wa mashabiki juu ya makipa hao.
“Siyo Kaseja na Dida pekee, makipa wote hapa Yanga ni wazuri na wote wanaweza wakawa namba moja. Wote wanaonekana kuyaelewa vyema mazoezi ninayowapa, hivyo mimi naona yeyote kati yao anafaa kuwa namba moja,” alisema Pondamali.

Post a Comment