KANUNI 10 AMBAZO UKIZIFUATA, MAFANIKIO YATAONEKANA
Ndugu wasomaji, kutokana na tatizo sugu la ajira linalosababisha watu wengi, hususan vijana kujikuta katika lindi la umaskini, tumeona ni jambo la busara kuanzisha safu hii, ambayo inaweza kuwasaidia baadhi ya watu kupata mwanga wa mafanikio katika maisha kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujiajiri.
Kwa kuanzia, tunaanza kuwaletea kanuni 10 ambazo kama zitafuatwa kwa umakini na usahihi, upo uwezekano mkubwa kwa mtu kufanikiwa katika harakati zake za kusaka maisha.
1. JIAMINI
Watu wengi duniani ni maskini sababu hawajiamini, wamepoteza nguvu na uwezo wa kupambana na changamoto za maisha sababu walivunjwa mioyo na watu waliowaita wajinga na wasioweza kitu! Kama unataka kufanikiwa, kamwe usiache mtu yeyote akuvunje moyo, siku zote amini wewe ni kiumbe cha kipekee na chenye uwezo wa kubadili maisha yako.
Ukifanya hivi kila siku utaifanya akili yako iwe na uwezo wa kuziona fursa ambazo hutaziona kama hujiamini, kutojiamini kutakufanya kipofu wa fursa!
Mimi Eric Shigongo, nilipuuzwa na kudharauliwa sana kwa sababu mimi na familia yangu tulikuwa maskini, matokeo ya kupuuzwa huko, nilijipuuza pia kama watu walivyosema, hii ilinifanya nisifaulu masomo yangu.
Baadaye nilikutana na mtu aliyenifanya nijiamini, tangu hapo nilianza kuona milango mingi ya mafanikio, nikajua kumbe bila kujiamini huwezi kuziona fursa, hivyo msomaji unapaswa kujiamini!

2. TAFUTA TATIZO ULISHUGHULIKIE
Watu wengi duniani hubaki kulalamika kila siku juu ya matatizo yanayowazunguka bila kuelewa kuwa matatizo hayo ni fursa za kutajirika kama yatashughulikiwa. Mtu mmoja alikwenda mahali ambako watu walilalamika sana kuhusu kuugua malaria, yeye akagundua malaria husababishwa na kuumwa na mbu, alichokifanya ni kuwaleta vyandarua, ugonjwa wa malaria ukaisha sababu watu hawakuumwa na mbu tena.

Lakini alipowapa watu vyandarua wao walimpa fedha kama malipo, akatengeneza utajiri.
Matajiri duniani ni wale wanaotafuta matatizo na kuyafanya fursa, Bill Gates aliona watu wanateseka kuchapa kwa Typewritter akawaleta kompyuta, leo hii ni bilionea.
Wewe pia unaweza kuwa bilionea kama utatafuta tatizo na kulitafutia ufumbuzi, ufumbuzi huo ndiyo uwe ndoto yako, ubunifu wa kitu cha lazima kama unataka kufanikiwa maishani mwako.
3. LAZIMA UWE NA MPANGO
Ukishapata ndoto au kitu unachotaka kukifikia maishani, ni lazima uwe na mpango, jiulize nitafikaje pale? Huwezi kuingia kwenye safari ya maisha bila kujua unakotaka kwenda!
Hata kama upo shuleni, huwezi kila siku kuwa unakwenda shuleni bila kujua unataka kufika wapi?Kwa nani? mtu wa aina hii ni sawa na mtu anayeendesha gari lake amefumba macho, lazima atapinduka.
Hivyo maishani, tengeneza mpango wa kufikia ndoto yako, ujue utaanzia wapi na utamalizia wapi na baada ya muda gani.
4. TEKELEZA
Pamoja na kujiamini, kuwa na ndoto huwezi kufika popote kama huwezi kutekeleza mpango wako, usiwe miongoni mwa watu ambao kila siku hupanga tu lakini hawatekelezi chochote, hawa ni sawa na wanaozungusha tairi la baiskeli wakati wa kunoa kisu, huwa hawasogei mbele!
Ukitaka kufanikiwa maishani ni lazima ufanye, utende, utekeleze mawazo yako, mfano unataka kuwa daktari ni lazima uende shule, uteseke kwa kusoma wakati mwingine kukesha au unataka kuwa na mafanikio kifedha ni lazima uwe tayari kufanya kazi hata kama ni ngumu na chafu ilimradi kesho uwe tajiri. mafanikio yanawezekana tu kwa watu walio tayari kufanya siyo kuongea bila kutenda.
Itaendelea wiki ijayo.

Post a Comment