JUAN MATA AMETAMBULISHWA RASMI SIKU YA JANA
JUAN Mata ametambulishwa rasmi siku ya jana kama mchezaji mpya wa Manchester United na kukabidhiwa jezi namba 8 na kusema ana kiu kubwa ya kucheza sambamba na Wayne Rooney.
Awali mchezaji huyo wa Hispania alitarajiwa kupewa jezi namba 7 kufuata nyayo za Cristiano Ronaldo, David Beckham, George Best na Eric Cantona lakini kiungo huyo akachagua jezi namba 8 iliyokuwa ikivaliwa na Anderson ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Fiorentina ya Italia.
Akimzunguzia Rooney Mata alisema mshambuliaji huyo ni moja ya sababu iliyomfanya avutike kujiunga na Manchester United.
“Nashindwa kuwa na subira, nina kiu kubwa ya kucheza naye. Ni mmoja wa wachezaji bora kabisa katika historia ya nchi hii – anaweza kuvunga, anaweza kupika magoli pamoja na kusaidia eneo la kiungo na kupoka mipira.
“Si mchezaji wa kawaida. Nitajitahidi kutafuta nafasi na kuwasaidia washambuliaji,” alisema Mata.
Akizungumzia jezi namba saba, Mata alisema anajua ni jezi yenye historia kubwa katika klabu, lakini ameamua kuchagua namba nane.
Mata amesema kitendo cha yeye kuchukuliwa kama mwokozi au msaada wa kurejesha uhai wa
Manchester United haumpi presha na kwamba hiyo ni kama changamoto kwake ya kufanya vizuri.
Akaongeza kuwa Manchster United ni klabu yenye historia ya kupenya kutoka katika nyakati ngumu hadi kwenda kushinda mataji.

Post a Comment