ad

ad

MIKASA YA MAPENZI: SWALI NA MAJIBU



Nahisi ananichukulia mume wangu
Anko , mimi ni mwanamke nina mtoto na mume. Nina rafiki yangu sina imani naye kwa sababu anapenda sana kuteta na mume wangu. Nimeshawafuma mara nne, wakizungumza   kisiri nahisi anatembea naye, je, nifanyeje?KK.

Jibu: Kwanza kabisa mueleze mumeo kuwa tabia ya kuzungumza na rafiki yako wakiwa sehemu za kificho siyo nzuri. Lakini pia rafiki yako kama kweli ni wa dhati mueleze kero yako bila shaka watajirekenisha. 
Nawashwa sana sehemu nyeti
Anko , naomba msaada wako. Mimi ni msichana nimekuwa nikisumbuliwa sana na kuwashwa sehemu za siri, je huo ni ugonjwa gani? Feibe P.

Jibu: Feibe pole sana kwa matatizo ya kuwashwa sehemu nyeti. Ushauri wangu ni kwamba nenda kwenye hospitali au kituo chochote cha afya wakakupime bila shaka daktari akigundua ugonjwa wako utapewa tiba sahihi. Itakuwa ni kosa kwangu kukuambia huo ni ugonjwa gani kwani kuna maradhi mengi yanayosababisha mtu kuwashwa sehemu hizo.
Powered by Blogger.