NI SERIKALI TATU
MUUNDO wa serikali tatu umeendelea kuwa ndani ya Rasimu ya Katiba
iliyokabidhiwa jana kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na ambacho Tume ya
Mabadiliko ya Katiba imesema ndiyo itakuwa suluhu ya malalamiko juu ya
kero za Muungano.
Akikabidhi Rasimu hiyo jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume, Jaji
Joseph Warioba, alisema baada ya kukaa na kupitia malalamiko juu ya
muundo wa sasa wa Muungano na takwimu za waliotoa maoni, imeona serikali
tatu zinakidhi matakwa ya Watanzania wengi.
Uamuzi wa Tume
umefanyika baada ya kupokea maoni kutoka kwa makundi ya watu zikiwamo
taasisi za serikali, ambao asilimia kubwa ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu,
walionesha kuhitaji muundo huo wa Muungano.
Akiwasilisha taarifa ya Tume kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais Ali
Mohamed Shein, Jaji Warioba alisema katika maoni yaliyotolewa, takwimu
zinaonesha upande wa Tanzania Bara, asilimia 61 walipendekeza serikali
tatu; asilimia 24 mbili na asilimia 13 moja.
Kwa upande wa Zanzibar, asilimia 60 walipendekeza Muungano wa
Mkataba, asilimia 34 serikali mbili na asilimia 0.1 serikali moja.
Aidha, taasisi nyingi kama vile vyama vya siasa, asasi za kiraia na
jumuiya za kidini zilipendekeza muundo wa serikali tatu.
Miongoni mwa taasisi za serikali zilizopendekeza mfumo wa serikali
tatu, ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo katika maoni
yao, zilisema muundo huo utaondoa kero za Muungano.
Kwa upande wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, lilipendekeza kuwapo kwa Mamlaka huru ya
Zanzibar, Mamlaka huru ya Tanganyika na Mamlaka ya Muungano kila moja
ikiwa na mipaka yake.
Jaji Warioba akieleza namna Muungano ulivyoteka mjadala wa Rasimu ya
Awali ya Katiba, alisema kwa Tanzania Bara, wananchi zaidi ya 39,000
walitoa maoni kuhusu eneo hilo.
“Wananchi karibu wote waliotoa maoni, walijikita kwenye suala la
Muungano. Kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa maoni, 19,000 walitoa
maoni kuhusu Muungano,” alisema.
Malalamiko Bara, Zanzibar
Malalamiko Bara, Zanzibar
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, baada ya kuona takwimu za waliotoa maoni
na kuzichanganua, Tume iliamua kufanya utafiti kuhusu muundo wa Muungano
na kubaini malalamiko mengi kuhusu Muungano.
Akitaja malalamiko
waliyobaini, Jaji Warioba alisema kwa upande wa Zanzibar, yapo
malalamiko makubwa matatu ambayo ni Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la
Serikali ya Muungano linalosaidia Tanganyika zaidi kuliko Zanzibar.
“Koti hilo limeifanya Tanganyika kuwa ndiyo Tanzania,” alisema.
Mengine ni kuongezeka kwa mambo ya Muungano na hivyo kuathiri madaraka
ya Zanzibar na kufifisha hadhi yake hivyo kuendelea kumezwa. Wazanzibari
wanalalamikia pia kumwondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano.
Kwa upande wa Bara, malalamiko makubwa yaliyobainishwa na Tume ni
wananchi wa Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati
wenzao wa Zanzibar wana haki hiyo Bara.
Malalamiko mengine ni
Zanzibar kuwa nchi huru, yenye bendera, wimbo wake, serikali na
imebadili Katiba yake ili ijitambue kama nchi, wakati Tanzania Bara
imepoteza utambulisho wake.
Vile vile wanalalamikia Zanzibar kwamba
imebadili Katiba na kuchukua madaraka ya Jamhuri ya Muungano kama vile
kuelekeza sheria za Muungano zilizopitishwa na Bunge zipelekwe kwenye
Baraza la Wawakilishi kujadiliwa.
Tume baada ya kufanya uchambuzi wa malalamiko hayo, ikaona ni vigumu
kuyafanyia ukarabati hivyo ikaona ipendekeze muundo wa serikali tatu ili
pande zote mbili ziwe na hadhi sawa.
“Kila upande utashughulikia
mambo yasiyo ya Muungano na Serikali ya Muungano itabaki na mambo
machache ya msingi na ambayo yanaunganisha Taifa,” alisema.
Uraia
Uraia
Hata hivyo, Jaji Warioba alisema Tume imetambua kuwa muundo huo una
changamoto zake, hivyo ili kujikinga nazo, imependekeza mambo matatu
likiwamo la uraia kubaki kuwa mmoja.
Imependekeza raia wote wa Jamhuri wawe huru na wawe na haki zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi nzima isipokuwa katika mazingira maalumu.
Imependekeza raia wote wa Jamhuri wawe huru na wawe na haki zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi nzima isipokuwa katika mazingira maalumu.
“Haki zao
zikiingiliwa na upande wowote bila sababu maalumu, itasababisha kuibuka
kwa utaifa, utanganyika au uzanzibari na uzalendo utayumba. Uzalendo
ukiyumba, Muungano pia utayumba,” alisema.
Licha ya uraia, lingine ni Serikali ya Muungano kuwa na uhakika wa
mapato kwa ajili ya kulipia gharama za Muungano ambapo Tume imependekeza
ushuru wa bidhaa uwe ni kodi ya Muungano.
Kodi hiyo itakidhi sehemu
kubwa ya matumizi ya Muungano na sehemu iliyobaki itapatikana kutokana
na mapato yasiyo ya kodi yanayotokana na mambo ya Muungano, michango ya
nchi washirika na mikopo.
Tatu ni kuundwa kwa Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali chini ya
uenyekiti wa Makamu wa Rais wa Muungano na ijumuishe viongozi wakuu wa
nchi washirika.
Majukumu ya Tume ni kusimamia mashauriano na
ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano na za nchi washirika ili
kuhakikisha sera zinawiana na pia kusimamia na kuimarisha masuala yenye
maslahi kwa Taifa na pia kutatua migogoro.
Kazi ngumu
Kazi ngumu
Jaji Warioba ambaye alikiri suala la Muungano kuwa moja ya mambo
yaliyojadiliwa kwa hisia kali tangu Rasimu ya awali ilipotolewa, alisema
kazi ya kukusanya maoni na kuibuka na mapendekezo hayo katika Rasimu
hii, haikuwa rahisi ikizingatiwa wajumbe wa Tume wametoka katika makundi
tofauti.
Alisema, “kila mmoja wetu alikuwa na imani yake, maoni
yake, itikadi yake, msimamo wake. Lakini tulikubaliana mapema kabisa,
kwamba wajibu wetu ni kwa Taifa. Kwa hiyo tuliacha imani na misimamo
yetu binafsi na kuamua kusikiliza wananchi kwa makini sana.”
Aliendelea: “Majadiliano yetu yalilenga kupata mwafaka wa kitaifa.
Baadhi ya mapendekezo yetu kwa hakika yatapokewa kwa hamasa kubwa.
Lakini la muhimu ni kupata mwafaka wa kitaifa badala ya kufikia uamuzi
kwa kujipima katika makundi.”
Kulingana na taarifa ya Mwenyekiti huyo, kama ilivyokuwa katika
Rasimu ya Awali, suala la muundo wa Muungano ndilo lililochukua muda
mwingi wa Tume.
CCM yapongeza
CCM yapongeza
Akizungumzia Rasimu hiyo kwa niaba ya CCM, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa Chama hicho Tawala, Nape Nnauye, alisema wanaipongeza Tume kwa
kazi kubwa iliyoifanya kwa utulivu na umakini mkubwa na sasa sehemu
iliyobaki ni ya Bunge Maalumu la Katiba na kura za wananchi.
“CCM
inaitakia kila la heri sehemu muhimu iliyobaki katika mchakato ifanyiwe
kazi kwa busara na umakini mkubwa kama ilivyotangulia kufanywa,” alisema
Nape.
CCM ambayo inaamini katika Serikali mbili, ilisema imesikiliza kwa makini taarifa ya Tume hasa katika suala la Serikali tatu na sababu zilizotolewa na kwamba inazichukua na itaziingiza katika vikao vyake, itatafakari na kutoa uamuzi unaopasa.
Uteuzi, uongozi
CCM ambayo inaamini katika Serikali mbili, ilisema imesikiliza kwa makini taarifa ya Tume hasa katika suala la Serikali tatu na sababu zilizotolewa na kwamba inazichukua na itaziingiza katika vikao vyake, itatafakari na kutoa uamuzi unaopasa.
Uteuzi, uongozi
Katika Rasimu hii ambayo ni ndefu kuliko ya awali, madaraka ya Rais
hasa ya uteuzi yamepunguzwa kwa kuweka vyombo vya kupendekeza majina ya
watu wa kuteuliwa na kwa baadhi ya vyeo kuhitaji kuthibitishwa na Bunge.
Rasimu hiyo yenye ibara 271 ikilinganishwa na ya awali yenye ibara
240, hata hivyo imesisitiza Rais ndiye mwenye hadhi na heshima ya Mkuu
wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu na Kiongozi wa Serikali.
Vile vile
imependekezwa wabunge wasiwe mawaziri, kuwe na ukomo wa uwakilishi
katika Bunge na wapiga kura wawe na madaraka ya kumwajibisha mbunge hata
kabla ya kumalizika kwa muhula wake.
Mengine ni Spika na Naibu Spika wasitokane na wabunge au kiongozi wa
juu wa chama cha siasa. Uraia ni mmoja wa Jamhuri ya Muungano ni mmoja.
Rasimu
inapendekeza kutambuliwa kwa uraia wa kuzaliwa na kujiandikisha ambao
ni wa nchi moja. Aidha, inapendekeza kuwapa hadhi maalumu watu wenye
asili au nasaba ya Tanzania ambao wameacha kuwa raia wa Tanzania kwa
kuchukua uraia wa nchi nyingine.
Marufuku kiongozi wa umma kutumia wadhifa, nafasi au madaraka kwa
manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu, jamaa, marafiki au mtu aliye
na uhusiano naye wa karibu.
Vile vile Tume kwa kuzingatia maoni ya
wananchi, tofauti na ilivyokuwa katika Rasimu ya Awali, sasa
inapendekeza Msajili wa Vyama vya Siasa iwe ni taasisi inayojitegemea na
si kuwa sehemu ya Tume Huru ya Uchaguzi.
Imependekeza pia kuwepo Jeshi la Polisi moja na Idara ya Usalama wa Taifa moja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kipindi cha mpito
Kipindi cha mpito
Rasimu inapendekeza muda wa mpito wa miaka minne, kuanzia tarehe ya
kuanza kutumika kwa Katiba Mpya hadi Desemba 31, 2018; na kwamba sheria
zilizopo sasa zitaendelea kutumika hadi zitakapobadilishwa.
Masuala yaliyopendekezwa yafanyiwe kazi katika kipindi cha mpito ni
pamoja na kutungwa Katiba ya Tanganyika, mgawanyo wa rasilimali baina ya
Serikali ya Muungano na serikali za nchi washirika.
Mengine ni
kufanya maandalizi ya kuendesha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa
kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014.
Kuundwa kwa tume na taasisi za kikatiba zilizoainishwa kwenye Katiba.
Rasimu ya wananchi
Akielezea mchakato wa maandalizi ya Rasimu hiyo,
Jaji Warioba alisema tofauti na wasiwasi uliokuwapo kwa ushiriki wa
wananchi wa kawaida, ungekuwa dhaifu, sura tano za mwanzo za Rasimu
zinatokana na mchango mkubwa kutoka kwa wananchi.
“Tume ilipoanza
kulikuwa na wasiwasi, kwamba ushiriki wa wananchi wa kawaida ungekuwa
dhaifu kwa sababu iliaminika kwamba wananchi kwa ujumla wao hawana ujuzi
wa Katiba,” alisema Jaji Warioba.
Aliendelea kusema: “Lakini Tume
iligundua mapema kwamba wananchi wanajua mambo mengi ambayo ni msingi wa
Katiba yoyote. Sura tano za mwanzo wa Rasimu ya Katiba zinatokana na
mchango mkubwa kutoka kwa wananchi.”
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, maoni ya wananchi yalihusu misingi ya
Taifa, tunu za Taifa, maadili na miiko ya viongozi, dira ya Taifa na
haki za binadamu.
Wananchi pia walitoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala wa nchi, ikiwa ni pamoja na nafasi ya wawakilishi wao bungeni.
Wananchi pia walitoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala wa nchi, ikiwa ni pamoja na nafasi ya wawakilishi wao bungeni.
Ilikotoka Tume Aprili 6 mwaka jana, Rais Kikwete aliteua wajumbe 34
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji Warioba na
kuwaapisha Aprili 13 mwaka huo kabla ya kuanza kazi yao, Mei 2.
Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa miezi 18 kwa Tume kukamilisha kazi yake.
Sheria pia ilitoa nafasi ya Tume kuongezwa muda usiozidi miezi miwili
na iliomba muda huo ikakubaliwa kabla ya kukamilisha kazi yake jana na
kuikabidhi kwa Rais
CHANZO NI HABARI LEO

Post a Comment