ARSENAL YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND
MSHAMBULIAJI Olivier Giroud amemaliza
ukame wa mabao katika mechi saba baada ya kuifungia Arsenal bao pekee la
ushindi Uwanja wa St James' Park katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Giroud alifunga bao hilo pekee dakika ya 65 akimtungua kipa Tim Krul kufuatia krosi maridadi ya Theo.
Kwa ushindi huo, Arsenal inarejea
kileleni kwa kufikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 19, ikiishusha
Manchester City hadi nafasi ya pili kwa pointi zake 41.

Post a Comment