Ngassa awaonyesha TFF jeuri ya fedha.
MSHAMBULIAJI Mrisho Ngassa wa Yanga, ameuambia uongozi wake yupo tayari
ulilipe Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kitita cha Sh milioni 45
kutoka kwenye mshahara wake.
Ngassa amekubali kitita hicho cha fedha
kitolewe kwa kuwa ana hamu ya kuanza kuitumikia Yanga baada ya kumaliza
adhabu ya kutocheza mechi sita aliyopewa na TFF.
Imeelezwa Ngassa yupo tayari kukatwa katika mshahara wake na kuna taarifa katika Sh milioni 2 kila mwezi, atakatwa Sh 500,000.
Mshambuliaji huyo alisimamishwa mechi sita pamoja na kutakiwa kurudisha
Sh milioni 30 alizolipwa na Simba pamoja na faini ya Sh milioni 15. TFF
ilishikilia msimamo wake kwamba Ngassa hatacheza hadi atakapolipa fedha
hizo za Simba.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza
kuwa, Ngassa amekubali kuhusiana na hilo na alifikia makubaliano hayo na
mwenyekiti, Yusuf Manji walipofanya kikao walipokutana jijini Mbeya,
hivi karibuni.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo jana, Ngassa alisema:
“Sawa, adhabu yangu ya kutocheza mechi sita za mashindano imemalizika,
lakini siwezi kuongelea lolote, mimi ni mchezaji tu, kazi yangu ni ndani
ya uwanja, hayo mengine ya kiutawala ni vyema yakatolewa ufafanuzi na
viongozi,” alisema Ngassa.
Championi Jumatano lilimtafuta Manji
ambaye alikiri kuzungumza na Ngassa kuhusiana na masuala kadhaa ya klabu
yao likiwemo hilo.
“Mimi ni mwenyekiti, hakuna ubaya kuzungumza na
Ngassa. Tunazungumza kwa ajili ya klabu yetu, hivyo msubiri akicheza
mtamuona,” alisema Manji.
Taarifa nyingine zilieleza kuwa, Yanga
ilikuwa tayari kupeleka fedha hizo leo, lakini ilitaka
TFF wakate Sh
milioni 45 katika Sh milioni 70 inazowadai na walikuwa katika mazungumzo
katika hilo.
Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu, Ernie Brandts,
alisisitiza kwamba ana kila sababu ya kumpanga Ngassa kama atakuwa
amerejea katika kikosi watakapoivaa Ruvu Shooting Jumamosi.
“Tuko
naye kikosini kila siku, tunafanya naye mazoezi na tunashirikiana. Kama
amerejea na yuko katika afya nzuri, nitampanga maana ninamhitaji,”
alisema Brandts.
Wakati hilo la Ngassa linamalizika, taarifa nyingine za uhakika zimeeleza Manji alitarajia kukutana na kikosi kizima cha Yanga, jana usiku.
Wakati hilo la Ngassa linamalizika, taarifa nyingine za uhakika zimeeleza Manji alitarajia kukutana na kikosi kizima cha Yanga, jana usiku.
Mwenyekiti huyo alipanga kukutana na
wachezaji na benchi la ufundi katika hoteli ya Serena jijini Dar ili
kula chakula cha usiku na baadaye kujadili masuala kadhaa kikiwemo
kipigo cha Azam FC na nini cha kufanya baada ya hapo ili kusonga mbele
na ikiwezekana kutetea ubingwa wao. CREDIT GLP.

Post a Comment