KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO LA SOKA KUKUTANA MEI 9 KUJADILI UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA FIFA KUHUSU UCHAGUZI WA TFF.

Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana
Mei 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam kupokea na kupanga utekelezaji wa
maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusu
uchaguzi wa shirikisho.
Kikao
hicho cha dharura chini ya Uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga
kitakuwa na ajenda hiyo moja tu katika kuhakikisha utekelezaji wa
maelekezo ya FIFA unafanyika haraka ili uchaguzi ufanyike ndani ya muda
uliopangwa.
FIFA
katika maelekezo yake imetaka kwanza ziundwe Kamati ya Maadili na Kamati
ya Rufani ya Maadili kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wa
Kamati mpya ya Utendaji ya TFF. FIFA imeagiza uchaguzi uwe umefanyika
kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.
Post a Comment