AZAM FC KIBARUANI MOROCCO LEO HII MEI, 4 .
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam
katika mechi yake ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika
itakayochezwa Morocco leo (mwaka huu).
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa jijini
Rabat kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Morocco. Timu hizo zilitoka suluhu
katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili
zilizopita.
Azam
iko nchini Morocco kwa karibu wiki nzima sasa ikijiandaa kwa mechi hiyo
chini ya Kocha wake Stewart John Hall. Msafara wa Azam nchini humo
unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella.

Post a Comment