SAHAU LIONEL MESSI, XAVI NDIYE ALIYEIBEBA BARCELONA DHIDI YA PSG
WENGI
wameelekeza fikira zao kwamba kuingia dimbani kwa Lionel Messi kipindi
cha pili ndiko kumeibeba Barcelona dhidi ya Paris Saint Germain (PSG),
usiku wa Jumatano, lakini ukweli unabaki kuwa ni Xavi ndiye aliyekuwa na
mchango mkubwa, huku akiandika rekodi ya kugawa pasi dimbani.
Barcelona ililazimika kufanya kazi ya ziada kupata nafasi katika nusu fainali ya Champions League.
Iliwekwa
nyuma baada ya dakika 50, lakini ikafanikiwa kupenya kwa sheria ya
mabao ya ugenini pale Pedro aliposawazisha na kufanya sare ya 1-1 dakika
ya 71. Timu hizo zilitoka 2-2 mechi ya kwanza Ufaransa.
Xavi
mwenye miaka 33 alicheza dakika zote 90 za mechi hiyo kwenye dimba la
Nou Camp, na alifanikiwa kwa asilimia 100 kusambaza mipira kwa wachezaji
wenzake dimbani, ambapo alipiga jumla ya pasi 96, ambapo hakuna hata
moja iliyopotea njia.
Kuna
wachezaji wengi waliong’ara kwa kugawa pasi kwa usahihi kwenye
Champions League katika kipindi cha miaka 10 tangu msimu wa 2003/04,
lakini hakuna aliyewahi kufanya hivyo kwa asilimia 100.
Kabla
ya ‘maajabu’ ya Xavi, orodha ya ukamilifu wa pasi ilikuwa ikiongozwa na
Javier Zanetti aliyefanya hivyo kwa asilimia 72 katika mechi kati ya
Inter Milan na Tottenham miaka mitatu iliyopita.
Orodha
kamili ya nyota wanaoongoza kwa kupiga pasi kwa ukamilifu tangu mwaka
2003; asilimia zao, mechi na miaka kwenye mabano ni: Xavi (96% -
Barcelona v PSG, 2013); Javier Zanetti (72% - Inter vs Tottenham, 2010);
Emmanuel Eboue (54% - FC Porto vs Arsenal, 2006); Lilian Thuram (50% -
Barcelona vs Stuttgart, 2007) na Cristiano Ronaldo (50%, Real Madrid vs
Man City, 2012).
Wengine
ni Paulo Vinicius (48% - Braga vs Galatasaray, 2012); Martin Caceres
(48% - Basel vs Barcelona, 2006); John Terry (47% - Chelsea vs Werder
Bremen, 2008); Rolando Jorge Pires da Fonseca (45% - FC Porto vs Dynamo
Kiev, 2006); Ivan Helguera ( 43% - Roma vs Real Madrid, 2004) na Sergio
Ramos (43% - Real Madrid vs Dinamo Zagreb, 2011).
Via saluti5.com
Post a Comment