Bosi wa Man city Roberto Mancini ataendelea kuifundisha kikosi chake chake msimu ujao hata kama hatakosa ubingwa wa Fa.
Kocha wa man city kwa sasa bado ana mahusiano mazuri na mtendaji mkuu wa timu hiyo Ferran Soriano na meneja wake wa michezo Txiki Begiristain.
Kwa sasa Meneja wa man city yupo katika mipango mipya ya msimu ujao baada ya kukosa taji la ligi mwaka huu amesema mwakani ana matumaini ya kunyakua taji hilo.
Kwa sasa kikosi cha man city kinajiandaa vyema kupambana katika fainali ya kombe la Fa na Wigan mwezi ujao tarehe 11 katika uwanja wa Wembley.
Man city siku ya jana imeibuka kifua mbele baada ya kuichapa west ham bao mbili kwa moja,wafungaji wa mechi hiyo ni Sergio Aguero na Yaya Toure.
Post a Comment