LADY JAYDEE YUPO JUU HATA KITUO CHA REDIO KIKISUSA KUCHEZA NYIMBO ZAKE, WATANZANIA WANAMKUBALI
Na Mahmoud Zubeiry
WATANZANIA wa leo, wengi wao ni waelewa na ndiyo maana wanakosoa mtu au au taasisi bila kujali ukubwa wake, iwapo watabaini mapungufu.
Vyombo vya Habari vinatambulika kama njia ya kufikisha ujumbe kwa jamii, kwa maana ya kuhabarisha, lakini kuelimisha na siku hizi, kuburudisha pia.

Lady
Jaydee
Inapotokea
chombo cha habari kikayumba katika haya, japo kwa maslahi yake
binafasi, basi Watanzania wengi wataelewa na huo utakuwa mwanzo wa
chombo husika kupoteza heshima yake.
Na
Watanzania wanapenda vile vitu ambavyo vinafanya vizuri au kwa namna
moja au nyingine, vinateka hisia za watu. Watanzania wanampenda Lady
Jaydee, ni mwanamuziki mzuri na siku zote yupo juu.
Kazi
zake ni nzuri. Wimbo wake mpya, Joto Hasira ni mzuri, tena nadiriki
kusema sana na unawakuna wengi, kwa ala zake, mpangilio wa sauti,
mtiririko wa mashairi na ujumbe wenyewe.
‘Ameua’
zaidi pale alipomshirikisha MC wa ukweli, Profesa Jay, kijana
aliyefanya mapinduzi makubwa katika muziki wa kizazi kipya, kutoka
kuonekana wa kihuni, hadi wa heshima kiasi fulani.
Jamani,
joto linatia hasira, kwani uongo? Na foleni je? Saluti kwake Jide.
Ajabu leo kituo cha Radio kinagoma kucheza wimbo huo mzuri, yaani
kinajifanya kama kipo Msumbiji hakijui kinachoendelea katika tasniya ya
muziki Tanzania. Hii ni aibu yao wenyewe.
Hicho kituo hicho, lazima kijue kinajishushia heshima kwa jamii ya Watanzania na kupoteza imani kwa wasikilizaji wake.
Kimekwishagombana
na wasanii kibao jamani, tena kwa sababu zile zile. Kama wale wa zamani
walikuwa ‘wanafiki’ na huyu Jide je, ambaye amekitumikia na ametumiwa
na wamiliki wake kama mtambo wa kuwatengenezea fedha, nchi inajua.
Kwani
ile Smooth Vibes ilikuwa ni ya nani? Sina uhakika labda ya Reginald
Mengi au Anthony Diallo. Lakini huko ndiko alikotokea Jide katika
albamu ya Asubuhi ya 2001, iliyoshirikisha na wengine kama akina D. Rob
(marehemu), Terrence, Fina Mango na wengineo.
Watu
wanajua sana, kama msanii gani, gazeti gani, blog gani na ya aina gani
inafanya vizuri- wewe ukiwadanganya wanakujua ni muongo. Na wataacha
kukuheshimu. Utakaa studio unapiga kelele unadhani watu wanakusikiliza
kumbe, muda mrefu tu wamekwishahamia stesheni nyingine baada ya kukuona
wewe na Redio yako ni waongo.
Unawaambia
Watanzania eti Azam FC ni timu ya kwanza ya Tanzania kushinda mechi
Magharibi mwa Afrika baada ya kuifunga Barack Young Controllers 2-1
Liberia, na Simba ilipoifunga Hearts Of Oak ya Ghana 2-0 mabao ya Adam
Sabu (marehemu) na Abdallah Kibadeni, ilikuwa ya Kenya?
Msingi mkubwa wa chombo cha habari ni kutenda haki kwa kuripoti ukweli na kuzingatia usahihi, unapopoteza sifa kama hizi elewa unaelekea kizani na huna heshima tena.
Msingi mkubwa wa chombo cha habari ni kutenda haki kwa kuripoti ukweli na kuzingatia usahihi, unapopoteza sifa kama hizi elewa unaelekea kizani na huna heshima tena.
Kuibeba
chuki kama sera kuu ya mapambano ni kujimaliza mwenyewe- na mbaya zaidi
pale unapoonea wanyonge. Wasanii wa Tanzania ni wanyonge tu na
wanahitaji sana msadaa wa vyombo vya habari, lakini inapotokea chombo
cha habari ndiyo kinakuwa mstari wa mbele kuwanyanyasa, inauma sana.
Mtu
anajipendekeza kwa Mheshimiwa Rais, anajifanya mtetezi wa haki za
wasanii, kumbe ndiye mnyonyaji na mnyanyasaji mkubwa. Huu sasa ndio
unafiki.
Yako wapi yale matamasha ya uzinduzi wa albamu za wasanii wa Bongo Fleva kwa awamu, tena kwa ziara nchi nzima chini ya udhamini mnono wa makampuni makubwa nchini na bado kila sehemu ‘nyomi ya kufa mtu’?

Hizi
sasa ndizo dalili za laana ya kuwanyanyasa wasanii na wanyonge. Na
bado. Lady Jaydee mwanamuziki mzuri tu hata kituo kimoja kisipocheza
nyimbo zake. Yuko juu.
CHANZO CHA HABARI NA BIN ZUBERY BLOG
Post a Comment