CHELSEA YADUNDWA LAKINI YAPENYA NUSU FAINALI.
FERNANDO
TORRES ameendelea kuwa katika kiwango bora wakati Chelsea ilipofanikiwa
kupenya hatua ya nusu fainali ya Europa League (Ulaya ndogo) licha ya
kucheza mchezo wa kujihami na kulala 3-2 dhidi ya Rubin Kazan.
Kufuatia
ushindi wake wa nyumbani (Stamford Bridge) wa 3-1 katika mchezo wa
awali, Chelsea inasonga mbele kwa jumla ya magoli 5-4.
Torres
aliiandikia Chelsea bao la kuongoza dakika ya tano kufuatia pasi murua
ya kiungo Frank Lampard lakini Ivan Marcano akasawazisha muda mfupi
baada ya kuanza kipindi cha pili.
Victor Moses akaipeleka tena mbele Chelsea kabla ya Rubin Kazan kucharuka na kupiga mabao mawili kupitia kwa Gokdeniz Karadeniz na Natcho.
Post a Comment