YANGA YAPATA MTIHANI WA PILI UTURUKI
Timu
ya Young Africans Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza na timu
ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uturuki katika mchezo
wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Selen Football -Kalimya
Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.


Young
Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo
huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu hiyo la Denizlispor FC ambayo
imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka jana na hivi sasa inapamabana
kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata
nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina
wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi
na kuwavutia.
Baada
ya kuwa na wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya
Armini Bielefeld ya ujerumani mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine
nzuri ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia
kuona maendeleo ya kikosi changu kutokana na mazoezi ambayo tumekuwa
tukiyafanya tangu tulipofika alisema 'Brandts'
Denizlispor
FC ni miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka sehemu tofauti duniani
ambazo zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya
mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji
wa zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na
Ivernes ya Uholanzi, mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni
miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Young
Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari
kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen
Football - Kalimya complex pemebeni kidogo ya mji wa Antalya.
Kikosi
cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na
hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia
mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Athumani
Idd 'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo
wa juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizrui kabisa kwani
wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini
Antalya.
Kuhusu
hali ya hewa leo haijaonekana kuwa tatizo kwa wachezaji kwani
wanaonekana kuimudu na mda mwingi kwa sasa kumekua na jua linalowaka
kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi mpaka mida ya jioni, kwa leo hali ya
hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya hewa ni nzuri kabisa na jua
linawaka mda wote.
Source: Youngafricans.co.tz
Post a Comment