ad

ad

Watu 245 wafariki dunia na 200 kujeruhiwa nchini Brazil

Jeshi la polisi nchini Brazil limesema kuwa, watu 245 wamefariki dunia baada ya kutokea moto katika klabu ya usiku iliyokuwa imejaa watu huko kusini mwa nchi hiyo.
Karibu watu wengine 200 wamejeruhiwa katika moto huo uliotokea kwenye klabu ya Kiss katika mji wa Santa Maria, kusini mwa Brazil.
Mkuu wa kikosi cha Zima Moto cha eneo hilo, Guido de Melo, amesema kuwa, watu waliemewa na kuchanganyikiwa wakati moto huo ulipoanza kuwaka.
Ajali hiyo inakumbushia majanga mengine kama hayo yaliyowahi kuikumba Brazil katika miaka ya huko nyuma ambapo watu 100 walipoteza maisha wakati klabu moja ya usiku ilipowaka moto huko Rhode Island mwaka 2003 na wengine karibu 200 kufariki dunia baada ya moto kuchoma klabu moja ya usiku mjini Buenos Aires mwaka 2004.
Powered by Blogger.