Pingamizi TFF kujadiliwa leo
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), inakutana leo kupitia pingamizi dhidi ya wagombea
Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo utakaofanyika Februari 24, mwaka huu.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kamati ya uchaguzi imewaonya wagombea wa liowekewa pingamizi kutowenda kusikiliza pingamizi zao wakiwa na wapambe wao.
“Ni marufuku kufika kwenye pingamizi na usaili wakiwa na wapambe wao. Atakayefanya hivyo atakuwa amejitafutia matatizo,” alisema Wambura.
Waliokumbwa na pingamizi nafasi zao wanazowania
kwenye mabano ni Athuman Nyamlani, Jamali Malinzi, (Urais), Michael
Wambura, (Makamu) Eliud Mvela, Epaphra Swai, Athuman Kambi, Mugisha
Galibona na Vedastus Lufano (Ujumbe).
Pingamizi kwenye Bodi ya Ligi Kuu imewakuta wagombea, Hamad Yahaya na Said Mohamed.
“Kikao cha kupitia pingamizi kitafanyika saa 4 asubuhi na wapambe au washabiki wa waombaji uongozi pamoja na waweka pingamizi hawatakiwi kuwepo kwenye eneo la kikao hicho.
“Kikao cha kupitia pingamizi kitafanyika saa 4 asubuhi na wapambe au washabiki wa waombaji uongozi pamoja na waweka pingamizi hawatakiwi kuwepo kwenye eneo la kikao hicho.
Wakati huohuo Wambura alisema kuwa vyombo vingi vya habari vimeonyesha nia ya kuwepo mdahalo wa wa gombea uongozi katika TPL Board na TFF na kwamba Kanuni za Uchaguzi za TFF hazizuii jambo hilo.
Wambura alisema, sura ya mdahalo huo haupaswi kulenga katika kumsaidia mgombe yeyote na kwamba unaweza kufanyika wakati wa kipindi cha kampeni.
“Kanuni hazimlazimishi mgombea kushiriki kwenye
mdahalo. Pia ni vema mdahalo uandaliwe na taasisi inayounganisha vyombo
vingi vya habari au waandishi kama Taswa,” alisema.
“Kamati ya Uchaguzi ya TFF lazima ijulishwe kwa maandishi nia ya kufanyika mdahalo na utaratibu utakaotumika mapema,” aliongeza.

Post a Comment