ad

ad

MANCHESTER UNITED UTAISOMA!!!! YAPAA KILELENI


Wayne Rooney celebrates
Wayne Rooney makes it 2-1
MANCHESTER UNITED wamevuna pointi 3 muhimu kwa kuichapa Southampton 2-1 na kuzidi kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza.
Manchester United walilazimika kutoka nyuma na hatimaye kupata ushindi huo kupitia kwa Wyane Rooney aliyefunga mabao yote mawili katika dakika ya 8 na 27.
Bao la Southampton lilifungwa na Jay Rodriguez dakika ya 3 kufuatia pasi ya nyuma ya kizembe ya kiungo wa United, Michael Carrick.
Kiungo aliyeng’ara sana, Shinji Kagawa alimtengenezea Rooney pasi nzuri iliyozaa goli la kwanza huku Robin Van Parses na Patrice Evra wakiwa ni wapishi wa bao la pili.

Matokeo mengine ya mechi za jana ni:

Arsenal 2 - 2 Liverpool

Everton 2 - 1 West Bromwich A.

Norwich C. 1 - 1 Tottenham H.

Fulham 3 - 1 West Ham U.

Reading 2 - 2 Chelsea

Via saluti 5

Powered by Blogger.