CHADEMA, CCM NA CUF WAWASILISHA MAONI YAO TUME YA MABADILIKO YA KATIBA SIKU YA JANA


Mmoja wa Viongozi wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Andrew Chenge akiwasilisha maoni ya
chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Januari 7, 2013 katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam.


Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim
wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.
Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam Januari 7, 2013
Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiwasilisha maoni ya chama chake
kuhusu Katiba Mpya mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba (Jumatatu,
Jan 7, 2013) katika Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kulia kwa Prof. Lipumba ni
Katibu wa Tume Assaa Rashid.


Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba katika picha ya pamoja na
Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Prof.
Ibrahim Lipumba mara baada ya chama hicho kuwasilisha maoni yake kuhusu
Katiba Mpya kwa Tume jijini Dar es Salaam Januari 7, 2013.
(Picha kwa hisani ya WWW.HAKINGOWI.COM)
Post a Comment