Rais Zuma akubali kujiuzulu Lakini kwa Masharti
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekubali kuachia madaraka ya kuongoza nchi
hiyo, baada ya wito uliotolewa na chama chakle ANC kumtaka kujiuzulu
ndani ya masaa 48.
Makubaliano
hayo ya kujiuzulu yamekuja na sharti kwamba atafanya hivyo baada ya
miezi mitatu mpaka sita kuanzia sasa, na bado uongozi wa ANC haujatoa
jibu kama umeridhia ombi hilo.
Hapo
jana chama cha ANC kikiongozwa na Cyril Ramaphosa ambaye alichukua
wadhifa wa Zuma wa kukiongoza chama hiko, kilituma ujumbe maalum kumtaka
rais huyo kuachia madaraka, kutokana na harakati nyingi za kumtaka
afanye hivyo tangu mwaka jana.
Jacob
Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa, na Bunge la nchi hiyo kujaribu
kupiga kura za maoni ili kumuondoa lakini ilishindikana, na ndipo chama
kuamua kuchukua uamuzi huo mgumu wa kumtaka afanye hivyo, la sivyo
kitamtoa kwa nguvu.
Iwapo
Zuma atafanya hivyo atakuwa amefuata nyayo alizopita rafiki yake mkubwa
Robert Mugabe ambaye alikuwa Rais wa Zimbabwe, aliyetakiwa kufanya
hivyo mwishoni mwa mwaka 2017 na jeshi la nchi hiyo, la sivyo lingetumia
nguvu kumng'oa, na hatimaye kuachia madaraka.
Post a Comment